ignas kinunda
Member
- Sep 2, 2013
- 22
- 2
Gud dud
Inaitwa mshindi f1 na unayoisemea inaitwa sukari f1 ndio 100g sh.50,000, 250g sh 100,000 -500g 200,000 kg. 380000
Nimejaribu kufuatilia kuanzia mwanzo michango ya watu mbalimbali ili kuwona namna naweza kuchangia katika kuboresha. Nikiri mapema kuwa mimi ni mtaalamu wa kilimo kwa ujumla na matunda na mbogamboga hasa na pia nimexcel kwenye maswala ya mbolea na udongo hivyo nitakuwa nachangia kwa kadiri muda utavokuwa unaniruhusu na kumoderate baadhi ya zana nitaugawa mchango wangu sehemu tatu kwanza ni ushauri wa ujumla, kisha utaalamu wa uoteshaji na magonjwa na mwisho mbolea na utunzaji.
Mkuu wangu kilimo cha bustani ni changamoto! Faida ipo tena nzuri ya kuridhisha kabisa.
Binafsi nina uzoefu wa kutosha juu ya kilimo cha tikiti maji.
Mathalani unataka kulima ekari1 ya tikiti, huu ni mchanganuo mfupi kabisa;
kawaida ekari1=sqm4000
Kwa spacing ya 1m shimo hadi shimo na 2m mstari kwa mstari na kila shimo huwa naacha miche 2 na kuruhusu matunda3.
Na kama utapata mbegu ya hybrid itakuwa vizuri zaidi maana MATUNDA yake yanajiuza yenyewe, shambani ni sh1500.
So ukishusha hesabu hapo juu:
Jumla ya mashina ktk ekari1 ni
Sqm4000÷(1m×2m)×2=4000
Idadi ya MATUNDA =(4000×3)=12000
Mauzo shambani ni 12000×1500=Tshs18,000,000/=
Tatizo ni usimamizi, ila kilimo hiki kinalipa sana!
Ndiyo zipo zinakua na uwezo Wa kuhimili mikikimikiki ya masika.hizi nyingine zinaoza.mi mwenyewe ninampango Wa kulima tikiti la masika kwsbb linalipa.kuna jamaa ni mzoefu zaidi Wa mambo haya ndiye aliyeniwekea oda kiwandani.km utapenda nitakutumia no.yake
habari bwana mkubwa,samahan naomba unieleweshe juu ya tatzo hlo la matikit kupasuka naweza kuepukana nalo vp?sababu lmenikumba had nachanganyikiwa nimelima ekari mbl na nusu yale makubwa makubwa yamepasuka sana had nahs kukata tamaa ,plz msaada wako ni muhimu bw.kisima
Habari zenu wadau.
Wakuu mimi nataka kujaribu kulima tikiti maji kipindi hiki cha masika. Nitafanya kilimo cha kisasa. Mbegu ni Sukari F1 hybrid.
Tatizo nimekuwa nikipata ushauri tofauti kuhusu kipindi hiki ambacho masika inakaribia kuanza (Takribani mwezi mmoja baadaye) Wengine wanasema Matikiti hayapendi mvua nyingi, wengine wanasema kama nitayahudumia kwa madawa hakutakuwa na tatizo.
Wakuu naombeni mawazo yenu, je inawezekana nikafanikiwa kuvuna kipindi hiki cha masika?
Natanguliza Shukrani.
march to may ndio masika kwa ukanda wa pwani,nyanda za juu kusini masika huanza november mwishoni mpaka may. Kwa hiyo utaona kwamba,november mpaka february kwa ukanda wa pwani si masika. Sasa tikiti maji lenye soko la kufa mtu ni hili la january,february, tikiti la kuanzia may mpaka july huwa ni majanga sababu wakulima wengi huwa wanamudu changamoto za maji mashambani.
Hiyo ndiyo hali halisi lakini wewe unaiona ni "too theoretical" nadhani ni kwa sababu ya wingi wa mahela kwa ekari moja! Lakini huo ndio ukweli na ndio maana unaambiwa KILIMO KINALIPA hasa ukiwa serious nacho, ukijitoa, ukikifanya ndio AJIRA YAKO na ukikifanya KISAYANSI.Too theoretical
sukari F1 ni bora na inafaa ina tunda kubwa na lenye rangi iliyokoa na kujaa utamu.
ni mara mbili. mpaka tatu inategemea, kama ulikata kichwa lisiendelee kuzaa.na mimi nataka nijaribu.
sorry hivi hzo mbegu zinakuwa zimewekwa kwny makopo au na je shamba la ekari 1 ni kiasi gan cha ujazo wa mbegu kitahtajka?
Kwa ekari moja gharama zake za uendeshaji zikoje kwa mkoa kama morogoro?