vCTRMA
JF-Expert Member
- Jan 12, 2016
- 306
- 102
ediMimi nalima aina ya Sugar baby inachukua siku 60 tu kuvuna tangu plus siku 3-5 za kukaa ardhini, kwa hiyo kwa mwaka nalima mara 4 tu nina ekari 5 na kila eka napata kuanzia 2M-3M.
Spacing ni 2mx2m na kila shimo naweka mbegu 2 ambazo zinazaa matunda 2-3 kwa maana kila shimo napata matunda 4-6 ( wastani matunda 5).
Hivyo kwa spacing hiyo napata mashimo 1000-1200
Idadi ya matunda: Mashimo x Matunda kwa shimo x ekari [1,000 x 5 x 5 = 25,000]
Mapato: wastani wa shilingi 500 kwa tikiti x idadi ya matikiti kwa eneo la ekari 5 [25,000 x 500 = 12,500,000]
Mapato kwa mwaka: 12,500,000 x 4= 50,000,000
Gharama za uendeshaji wa shamba ni Tsh 25,000,000
Faida Kuu ni Tshs 25,000,000 M.
Tujenge taifa letu kwa kilimo
mkuu naomba nitumie wasaa huu kukujulisha mimi nataka nianze hicho kilimo cha matikiti mkuu, ila sina knowledge, shamba lipo kisarawe (3acres) mkuu naweza kuanza kwa kipi na kipi?
na mtaji unaeza ukawa kias gani? na huwa msimu gani ndo kilimo kinaanza
naomba msaada pliz