Kilimo cha matikiti maji (watermelon): Ushauri na Masoko

Habarini wadau,wajasiriamali wenzangu;...nilifaidika na elimu iliyotolewa hapa juu ya ulimaji wa tikiti maji na sasa niko mbioni kukianza mapema mwanzoni mwa mwezi wa kumi kwa malengo ya kuvuna december,nilienda duka la pembejeo wakaniambia mbegu zilizopo na ambayo wananishauri;kuna sukari F1,Juliana F1 na Sugarbaby, wakanishauri Sukari F1 ndio mbegu nzuri.

Sasa wadau nimekuja hapa jukwaani kupata ushauri wenu nikiamin wengi mmelima na mmeona matokeo ya kati ya hizo mbegu hapo juu,lakini pia nataka kuchanganya na zao lingine katika ulimaji wa hayo matikiti,na zao kama viazi, nyanya, pilipili hoho, tango, ama green beans je wadau linawezekana hilo, je ipi no mbolea sahihi kwa kupandia hizo tikiti(mean kuchanganya kwenye udongo)

Natanguliza shukrani zangu nikiamini mtaniahauri vyema mjasiriamali mwenzenu!!
 
Inaitwa mshindi f1 na unayoisemea inaitwa sukari f1 ndio 100g sh.50,000, 250g sh 100,000 -500g 200,000 kg. 380000

sorry hivi hzo mbegu zinakuwa zimewekwa kwny makopo au na je shamba la ekari 1 ni kiasi gan cha ujazo wa mbegu kitahtajka?
 
Nimejaribu kufuatilia kuanzia mwanzo michango ya watu mbalimbali ili kuwona namna naweza kuchangia katika kuboresha. Nikiri mapema kuwa mimi ni mtaalamu wa kilimo kwa ujumla na matunda na mbogamboga hasa na pia nimexcel kwenye maswala ya mbolea na udongo hivyo nitakuwa nachangia kwa kadiri muda utavokuwa unaniruhusu na kumoderate baadhi ya zana nitaugawa mchango wangu sehemu tatu kwanza ni ushauri wa ujumla, kisha utaalamu wa uoteshaji na magonjwa na mwisho mbolea na utunzaji.

kama utaweza nipm namba yako ndugu ili nikutumie kwa ushauri kwani utakuwa wa msaada mkubwa sana kwangu
 
Mkuu wangu kilimo cha bustani ni changamoto! Faida ipo tena nzuri ya kuridhisha kabisa.
Binafsi nina uzoefu wa kutosha juu ya kilimo cha tikiti maji.
Mathalani unataka kulima ekari1 ya tikiti, huu ni mchanganuo mfupi kabisa;
kawaida ekari1=sqm4000
Kwa spacing ya 1m shimo hadi shimo na 2m mstari kwa mstari na kila shimo huwa naacha miche 2 na kuruhusu matunda3.
Na kama utapata mbegu ya hybrid itakuwa vizuri zaidi maana MATUNDA yake yanajiuza yenyewe, shambani ni sh1500.
So ukishusha hesabu hapo juu:
Jumla ya mashina ktk ekari1 ni
Sqm4000÷(1m×2m)×2=4000
Idadi ya MATUNDA =(4000×3)=12000
Mauzo shambani ni 12000×1500=Tshs18,000,000/=
Tatizo ni usimamizi, ila kilimo hiki kinalipa sana!

habari bwana mkubwa,samahan naomba unieleweshe juu ya tatzo hlo la matikit kupasuka naweza kuepukana nalo vp?sababu lmenikumba had nachanganyikiwa nimelima ekari mbl na nusu yale makubwa makubwa yamepasuka sana had nahs kukata tamaa ,plz msaada wako ni muhimu bw.kisima
 
Ndiyo zipo zinakua na uwezo Wa kuhimili mikikimikiki ya masika.hizi nyingine zinaoza.mi mwenyewe ninampango Wa kulima tikiti la masika kwsbb linalipa.kuna jamaa ni mzoefu zaidi Wa mambo haya ndiye aliyeniwekea oda kiwandani.km utapenda nitakutumia no.yake

na mimi naomba connection nimelima tayari natarajia kupanda juma nne au tano
 
Kuna sababu nyingi za tunda kupasuka, lakini Sababu kuu za tunda lolote kupasuka (Fruit Cracking) huwa ni

1. Water stress-Upungufu wa maji wakati mmea unaanza kutengeneza matunda

2. Tatizo la lishe hasa Calcium-Kama udongo ulikuwa hauna Calcium ya kutosha, na hukuweka mbolea ya kutosha yenye calcium (Mfano wa mbolea zenye Calcium Contents ni CAN, Yarra Nitrabor etc.. Calcium huimarisha ganda kuwa gumu,na kuleta rangi ya kuvutia


habari bwana mkubwa,samahan naomba unieleweshe juu ya tatzo hlo la matikit kupasuka naweza kuepukana nalo vp?sababu lmenikumba had nachanganyikiwa nimelima ekari mbl na nusu yale makubwa makubwa yamepasuka sana had nahs kukata tamaa ,plz msaada wako ni muhimu bw.kisima
 
Jambo la msingi katika kilimo cha tikiti ni kuwa unapaswa kutime ule mwezi wa mwisho wa kukomaa kwa matunda, inabidi lisikutane na maji mengi, maana maji yakiwa mengi sukari inapungua, saizi ya tunda inakuwa ndogo, lakini pia linapasuka.

Hivyo unapaswa kufanya timingi kwa kujua eneo ulilopo, mvua zinaanza lini na kuisha lini,

Mfano Njombe/iringa mvua zinaanza November na kuisha May, hivyo unaweza panda tikiti mwezi April wakati bado mvua zipo, kufika may wakati mvua zinaishia tikiti huku zinatoa matunda.

Kilimo ni timingi-Lazima ujue muda sahihi wa kupanda, na utime pia katika upande wa soko.

Kilimo ni maarifa.


Habari zenu wadau.

Wakuu mimi nataka kujaribu kulima tikiti maji kipindi hiki cha masika. Nitafanya kilimo cha kisasa. Mbegu ni Sukari F1 hybrid.
Tatizo nimekuwa nikipata ushauri tofauti kuhusu kipindi hiki ambacho masika inakaribia kuanza (Takribani mwezi mmoja baadaye) Wengine wanasema Matikiti hayapendi mvua nyingi, wengine wanasema kama nitayahudumia kwa madawa hakutakuwa na tatizo.

Wakuu naombeni mawazo yenu, je inawezekana nikafanikiwa kuvuna kipindi hiki cha masika?

Natanguliza Shukrani.
 
huwezi kupata mbegu ya tikiti ambayo haipasuki msimu wa mvua nyingi, ila tu mbegu aina ya mshindi (ni hybrid) hua haipasuki sana kama nyingine.., ila kupungua ladha haikwepeki., kikubwa fanya timing kama ilivyoelekezwa hapo juu..
 
march to may ndio masika kwa ukanda wa pwani,nyanda za juu kusini masika huanza november mwishoni mpaka may. Kwa hiyo utaona kwamba,november mpaka february kwa ukanda wa pwani si masika. Sasa tikiti maji lenye soko la kufa mtu ni hili la january,february, tikiti la kuanzia may mpaka july huwa ni majanga sababu wakulima wengi huwa wanamudu changamoto za maji mashambani.

je mkuu malila naweza kulama tikiti njombe msimu huu wa masika
 
jamani naombeni kujua mbegu ya tikiti ya Sukari FI inayotengenezwa Kenya,hii ikoje?
 
Too theoretical
Hiyo ndiyo hali halisi lakini wewe unaiona ni "too theoretical" nadhani ni kwa sababu ya wingi wa mahela kwa ekari moja! Lakini huo ndio ukweli na ndio maana unaambiwa KILIMO KINALIPA hasa ukiwa serious nacho, ukijitoa, ukikifanya ndio AJIRA YAKO na ukikifanya KISAYANSI.

Kinallipa tusikatishane tamaa ndugu zangu.
 
Ningefurahi sana pia kama tungepata majibu ya hili swali, pia kujua kati ya mbegu zote zilizotajwa ni ipi bora zaidi kwa utamu na ukubwa, ipi isiyoshambuliwa sana na magonjwa, ipi ya muda mfupi zaidi n.k Cc: Asprin Malila riltz Mama Joe na wengine
sukari F1 ni bora na inafaa ina tunda kubwa na lenye rangi iliyokoa na kujaa utamu.
 
MBEGU ZINAKUWA KWENYE MAKOPO, KIASI CHA MBEGU GRAM 250-300 HUTOSHA KWA EKA 1 (SQUARE METRE 4000), NAFASI YA UPANDAJI NI MITA 1 MMEA MPAKA MMEA, NA MITA 1.5 KUTOAKA KATIKATI YA TUTA MOJA HADI LINGINE.

sorry hivi hzo mbegu zinakuwa zimewekwa kwny makopo au na je shamba la ekari 1 ni kiasi gan cha ujazo wa mbegu kitahtajka?
 
GHARAMA KUBWA IKO KWENYE MBEGU, GRAM 250 ZA KUTOSHA EKA 1 ITAKUGHARIMU KATI YA 1110,000-250,000, GHARAMA NYINGINE NI YA MAJI (KAMA UTATUMIA PUMP, SO GHARAMA YA MAFUTA) KUTEGEMEA NA PUMP UTAKAYOKUWA NAYO UNAWEZA JIKUTA KWA SIKU UNATUMIA MPAKA LITA 7-10, SASA ZDISHA KWA BEI YA FUEL YA SASA MARA SIKU 70 ZA KUKAA SHAMBANI, SAMBAMBA NA HILO JE PUMP YA KUMWAGILIA NI YAKO.. KAMA NI YA KUNUNUA SI CHINI YA LAKI3 PUMP NZURI, YA KUKODI KWA MUDA WA MIEZI 3 HIYO SI CHINI YA LAKI 2. KUTEGEMEA NA MSIMU ULIOLIMA (JE NI WA JUA AU MVUA??) KAMA NI WA MVUA GHARAMA NYINGINE ITAKUWA KATIKA MADAWA YA UKUNGU NA WADUDU. KWA UCHACHE KABISA GHARAMA YA EKA 1 YA TIKITI MPAKA UNAVUNA ITAKUGALIMU SI CHINI YA MILIONI 2, GHARAMA NYINGINE NI MBOLEA UTAHITAJI MIFUKO MIWILI YA DAP=180,000, UTAHITAJI UREA MIFUKO MIWILI 140,000TSH, UTAHITAJI NA CAN YA KUMALIZIA MIFUKO 3 TSH 210,000 ETC...... KILIMO NI GHARAMA HIVYO NI VYEMA KUJIPANGA VIZURI, ANDAA 2.5 MILIONI NDIO UINGIE SHAMBA.

Kwa ekari moja gharama zake za uendeshaji zikoje kwa mkoa kama morogoro?
 

Similar Discussions

99 Reactions
Reply
Back
Top Bottom