Kikwete kafanya mengi kipindi chake cha uongozi, tutamkumbuka...

Pia tutamkumbuka kwa kua rais wakwanza tz kuwaumbua mafisadi wanaoiba mali za tz nakuwapeleka mahakamani,pia kuvunja serikaliyake na kumtimua waziri mkuu kwa tuhuma tu zakushiriki ufisadi,hakuna hata rais 1 ktk east africa aliewahi kuwaumbua nakuwatimua mawaziri wake kwa kujihusisha na ufisadi.mnyonge mnyongeni hakiyake mpeni.

Ndugu hii sio kweli....Huu ulikuwa ni usanii tuu... kama sio mchanga wa macho..ni nani ameshashafungwa mpaka sasa pamoja na ufisadi wa kutisha uliopo hata sasa????????
 
Ndugu hii sio kweli....Huu ulikuwa ni usanii tuu... kama sio mchanga wa macho..ni nani ameshashafungwa mpaka sasa pamoja na ufisadi wa kutisha uliopo hata sasa????????

Kufunga au kutokufunga mtu hiyo sio kazi ya Rais, ni kazi ya mahakama.
 
stop kidding people. hayo yote ni ***** tu. usome ulichoandika then ujisahihishe mwenyewe. nitarejea bdae kukagua marekebisho.
 
Kila Rais hukumbukwa kwa jambo au mambo kadhaa mazito wakati wa muongo wa uongozi wake. Kwa upande wa JK, wa-TZ watamkumbuka sana kwa mambo makubwa matatu: 1. Vituko vya RA/EL na zengwe la Richmond/Dowans 2. Milipuko ya mabomu huko mbagala na g'mboto 3. Kashfa ya mabilioni ya fedha za EPA. Una lingine la kuongezea hata kama zuri, asije akasema wa-TZ hawajamtendea haki?

EPA ilianzia kwa JK ? soma ripoti vizuri ya Ernest & Young juu ya sakata la EPA ndio utajua lilianzia wapi, acha uvivu wa mawazo na kufuatilia mambo
 
Mkuu hii umemaliza yaani funga kazi mwenye macho haambiwi tazama kwa wana JF ambao ni mabubusa ! atakae bishia na haya basi huyo mchicha mwiba
 
Nitamkumbuka kwa semina elekezi zisizo na effect kule Ngurdoto na kukarabati magereza ili kuwaandalia makao jamaa zake wenye kesi za kuchovya.
pia kwa kukalia majina ya wauza unga, kuwapa muda wala rushwa ili wajirekebishe, kuwaomba wezi warudishe fedha walizoiba na bila kuchukua hatua zozote- mwisho kwa hotuba ya mbwembwe na bashasha akiwahutubia wazee wa disim ambapo aliwatukana wafanyakazi wote.


Amani yetu inatumiwa vibaya.
 
tutamkumbuka kwa machungu ya maisha aliyotuongezea,kweli ameacha mark!

Tutamkumbuka alivyoenda Cuba kubembea na mkewe pamoja na wapambe wake!
Tehe tehe, kwanini asinunue bembea moja kama ile then ailete nchini awe anabembea kila siku?
 
a.jpg
mimi nitamkumbuka kama raisi wa kwanza wa tanzania kukutana na kupiga picha na boyz 2 men-viongozi wote waliopita hawakuweza kufanya hivi
 
Tutamkumbuka kama bingwa wa safari na asieweza kuongoza hata kata lakini akafanya fitna na kupewa madaraka asiyoyaweza
 
Nitamkumbuka kwa mambo manne.

1. Uvumilivu, amekuwa akivumilia kila aina ya kejeli na majina mabaya anayoitwa especial hapa JF majina hayo ni kama mkwere, msanii, mchachuaji na mengine mengi.

2. Uhuru wa kujielezea, ni katika kipindi cha JK vyombo vya habari asasi za kiraia na raia wamekuwa na uhuru zaidi wa kuelezea mambo ya siasa.

3. Usikivu, hili sina uhakika sana lakini nimeshawishika kuliamini baada ya mwenyekiti wa taifa wa CDM mhe Mbowe kusema Rais JK ni "msikivu"

4. Nitamkumbuka kama Rais alietawala vipindi viwili ambavyo tatizo la umeme alishindwa kulifuatilia kwa karibu na kulimaliza especial kipindi cha kwanza. Sote tunakumbuka alipoingia tu madarakani alikaribishwa na mgao wa umeme. Nina imani kama angeamua na watendaji wake wangeamua basi katika kipindi cha miaka mitano ya mwanzo angelishughulikia kwa umakini tatizo la umeme na kulipunguza kama sio kulimaliza kabisa. Hili litakumbukwa kwa wenye vyama na wasiokuwa na vyama kwa maana linamgusa kila mmoja wetu especial tunaoishi uswahilini ambapo hata kama kuna ratiba ya mgao huwa haufuatwi. Umeme maranyingi uswahilini huwa unakatwa masaa mawili kabla ya muda wake na kurudishwa masaa mawili baada ya muda wake ushahidi ni jana wilaya ya temeke umeme ulikatika saa kumi alasiri badala ya kumi na mbili na nusu na kurudi saa saba na dakika 25 badala ya saa tano!
 
Ntamkumbuka kwa kumpa mkewe kampuni ya WAMA ili kuwanyonya wote wenye jinsia ya kike,2. kwa kukataa kura za wafanyakazi wake. 3. Kutangaza rasmi tarehe ya kuleta udini,tangu pale bungen, 4. Kwa kuwadhibiti majambazi wa kuteka benki na kule k.koo. Leo unaweza kupita na mil.100,lakn enzi za mkapa du!mara nmb,nbc ,k.koo,duka za wafua madini ila leo shwari. 5. Kwa kumleta Al alidaiwi kutuuzia umeme wa kisanii. 6. Kwa kumlinda jambaz/fisad kwa kusema muache mzee apumzike. 7. Kwa kuleta udkteta na utawala wa kibabe. 8. Kwa kuwachagua washkaj waongoze wizara 9. Kumteua mwanachuo wa kike awe Dc. 10. Kwa kuleta umasiki mkubwa tz.mwisho kutajwa ktk list ya majambaz na matapeli asichukue hatua ya kujiuzulu/list of shame.
 
Tutamkumbuka kama Rais wa kwanza kupata ulinzi wa majini, kama Toothless dog president, Mdesaji mkubwa, msani na anayecheka cheka tu katika mambo ya muhimu bila kufanya decision na aliyeleta USULTANI NA UFAMILIA kwenye taasisi ya urais.
 
Pia tutamkumbuka kwa kua rais wakwanza tz kuwaumbua mafisadi wanaoiba mali za tz nakuwapeleka mahakamani,pia kuvunja serikaliyake na kumtimua waziri mkuu kwa tuhuma tu zakushiriki ufisadi,hakuna hata rais 1 ktk east africa aliewahi kuwaumbua nakuwatimua mawaziri wake kwa kujihusisha na ufisadi.mnyonge mnyongeni hakiyake mpeni.

Tutamkumbuka kama Rais aliewahi kuwaumbua nakuwatimua mawaziri wake kwa kujihusisha na ufisadi na baadae kuwakampenia kama mapanga ya zamani yenye makali yaleyale na kuwashika mikono ili wachaguliwe tena na wananchi, what a paradox?
 
Kila Rais hukumbukwa kwa jambo au mambo kadhaa mazito wakati wa muongo wa uongozi wake. Kwa upande wa JK, wa-TZ watamkumbuka sana kwa mambo makubwa matatu: 1. Vituko vya RA/EL na zengwe la Richmond/Dowans 2. Milipuko ya mabomu huko mbagala na g'mboto 3. Kashfa ya mabilioni ya fedha za EPA. Una lingine la kuongezea hata kama zuri, asije akasema wa-TZ hawajamtendea haki?
Binafsi, nitamkumbuka kwa mabaya zaidi kuliko mema. Hakuna kitu kinakera kama kuona kiongozi anapeleka taifa lako motoni akishangiliwa na baadhi ya watu (kutokana na maslahi binafsi, chama chao au kukosa uelewa) halafu ukashindwa kuchukua hatua yoyote kuzuia uovu huo.
Naweza kusema katika marais wanaoua matumaini ya watu waliowachagua JK anaongoza. Watanzania walipomchagua walidhani yeye ndo atawaongoza kumbe RA ndo kashika remote Controler na ndiye kiongozi. Mungu atulinde hawa Vimeo watalipa siku moja na God knows they will pay dearly!
 
ntamkumbuka kwa kuwa mstari wa mbele kufungua shule za primary, kusema hamjui mmiliki wa dowans wakati alialikwa ikulu,ntamkumbuka kwa ahadi ya kujenga wiwanja vikubwa vya kimataifa BUkoba, KIgoma na Mbeya wkt wananchi hawana huduma za msingi kama hospitali,maji nk, na pia ntamkubuka kwa kulamwaga vibajaji vya kubebea wajawazito badala ya ambulance vijijini siji vitapita barabara zipi huko nk nk nk.ohhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh bila kusahau our president is handsome jamani
 
Yaelekea wafahamu vizuri serikali naomba uniambie hao wezi wa epa waliorejesha billion walisamehewa kwa sheria gani na uwizi walifanya akiwemo manji(Fisadi PAPA) Siogopi kumtaja kwani akinipeleka mahakamani atanidai shilling moja tu. Hivyo vyuo vikuu 11 ni vya serikali?

-Mgogoro wa zanzibar hadi kesho waulize wanasema wamejiamulia wenyewe japo kuna wamarekani ndio wamepewa tuzo ya Martin Luther King Award ya Mwaka 2010 kikwete wapi na wapi hajumo kwenye hiyo tuzo hatuwezi kumkumbuka kwa hilo samahani ndugu enh!!. yeye ndio anahitaji usuruhishi amuachie DR. Slaa Kiti chake bila hivyo yanazidi kumuandama malaana aliambiwa ikulu sio pahari pa kukimbiliwa kwani kuna biashara gani ajiondokee mapema kama Rasi wa tunisia.

Tanzania Mortgage Refinance Company ni wizi mtupu nyumba unapata mkopo wa milion 100 kurejesha hadi vitukuu wako watakuwa wanakulipia deni ni sawa na mikopo hiyo ni sawa na mkataba wa Richmond au iptl na nyumba ya kawaida tu. Kuchunguzwa Mikataba ya Madini tutamkumbuka Speaker Sitta, Milipuko ya mabomu sio hujuma ni uzembe kazini.

Lami barabara nyingi ni fedha za wahisani haziusiani na road licence na parking fees zetu anazila tu Upinzani lazima waongee ndio kazi yao kuikosoa na hawezi kuwaachisha kuongea japo keshajaribu hadi kachoka kawatengenezea mabomu ya scud anawarushia masikini hajui wenzake wana patroit yaani wanazuia kilainiiii ila wapo imara na wasafi anamwambia dr.slaa anamke wa kuazima wakati yeye mh! tuyaache haya mkwewe kampa ubunge na shemeji yake kampa do1s. tutamkumbuka kwa mengi mabaya ila mazuri pia yapo. Hivi ni kweli Huwa hamnukuu na kutaja jina nyerere ni baba wa Taifa? hata siamini husema mzee nyerere?mh!
 
Back
Top Bottom