Kikwete kafanya mengi kipindi chake cha uongozi, tutamkumbuka...

Yote mliyoorodhesha hapa ni muendelezo wa Kazi za BEN MKAPA. Nafikiri huyu jamaa hana lolote la kujisifia zaidi ya kuharibu hata kile wenzie walichofanya.

Nafikiri tungefuata kauli za Nyerere tusingeburuzwa to this extend!
 
weweeee

daraja si lake (nkapa)
mpango wa shule si wake ( nkapa)
bara bara (nkapa)

hayo mengine yasiyo na tija kwa taifa ndo yake
MMES ya Mkapa haikuwa na mpango wa kujenga shule mpya. Walitaka kuboresha zilizokuwepo tu. Na MMES yenyewe sio wazo la Mkapa. Barabara mipango ilikuwepo tangu enzi za Mwalimu hata hilo daraja la Mkapa, la Msumbiji. Mkapa naye alifanya kuyaendeleza tu haya kama anavyofanya JK.
 
Ameongeza wake wa3 ndani ya kipindi cha miaka mi5 akiwa ikulu, wa2 mashombe wa kiarabu na m1 shombe wa kihindi. Hatujawahi kuwa na rai aliyeoa mke akiwa ikulu sasa yeye wa3 si mchezo kajitahidi.
 
Kikwete amefanya mambo mengi nataka niwakumbushe tuu watanzania wenzangu.

Tutamkumbuka kwa mengi sana hasa hili la kukemea mgomo wa wafanyakazi na kucheka na mafisadi amejitahidi kwa kweli tumpongeze kwa hilo.:becky:
Tumpongeze mwezi Oktoba kama waingereza walivyompongeza Gordon Brown na chama chake cha Labour!
 
Thanks kwa kunichagulia katusi haka. Mnyonge mnyongeni lakini HAKI yake mpeni.
Tatizo lenu mkizidiwa hoja mnafikiri ni tusi, nimekuambia wewe piga ua ni pro Kikwete, ukiniambia mimi ni pro Chadema sintachukulia tusi ni kama changamoto kwangu.
 
Siamini kama hili ni kweli. Mfutieni Mkapa dhambi zake chache alizofanya basi! Halafu, angalau JK ameyafanyia kazi haya ambayo yote mnamlundikia mtangulizi wake. Unakumbuka mradi wa maghorofa ya Michenzani kule Zanzibar alooyaacha Mzee Abeid Amani Karume? Walipita Marais wanne pale na hawakuyafanyia kitu hadi Rais wa sasa ambaye ni mwanae ndiye amekuja kuyamalizia. JK anafanyakazi bwana.


Wild ndugu yangu hata JK mwenyewe anajua yeye sio jasiri wa kufanya maamuzi mazito kama Chemkapa, na nukuu maneno machache yaliyo kwenye gazeti la Mwananchi la leo "RAIS Jakaya Kikwete amemsifu Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa kuwa ni jasiri kutokana na maamuzi aliyoyafanya kuiingiza nchi maskini kama Tanzania katika mtihani mzito wa kutekeleza ujenzi wa daraja la Umoja, ambalo limezinduliwa jana". Je? kwa hilo dogo tu unakubali kuwa JK si mfanyakazi bora ila ni msafiriji bora? We acha bwana sema tu kama unagombea ubunge kwa tiketi ya CCM ndio maana unampamba chairman wako.
 
Tatizo lenu mkizidiwa hoja mnafikiri ni tusi, nimekuambia wewe piga ua ni pro Kikwete, ukiniambia mimi ni pro Chadema sintachukulia tusi ni kama changamoto kwangu.
Mimi sio pro-Kikwete. Najitahidi tu kuwa mkweli. Sitaki kuisaliti nafsi yangu. Itanisuta. Si unaijua tabia ya ukweli? Ukweli huwa hautaki kupindishwa. Yapo mazuri anayoyafanya JK.
 
Wild ndugu yangu hata JK mwenyewe anajua yeye sio jasiri wa kufanya maamuzi mazito kama Chemkapa, na nukuu maneno machache yaliyo kwenye gazeti la Mwananchi la leo "RAIS Jakaya Kikwete amemsifu Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa kuwa ni jasiri kutokana na maamuzi aliyoyafanya kuiingiza nchi maskini kama Tanzania katika mtihani mzito wa kutekeleza ujenzi wa daraja la Umoja, ambalo limezinduliwa jana". Je? kwa hilo dogo tu unakubali kuwa JK si mfanyakazi bora ila ni msafiriji bora? We acha bwana sema tu kama unagombea ubunge kwa tiketi ya CCM ndio maana unampamba chairman wako.

Mkapa alikuwa mzuri sana kwenye kutafuta fedha za miradi kama hii na hasa daraja kama hili ambalo liko nyumbani kwao, litawasaidia jamaa na ndugu zake. Hebu tujiulize kidogo, daraja linahitajika sasa?
 
Tatizo ninavyoliona ni kuwa hapa JF kuna watu walikuwa hawampendi huko nyuma, hawampendi hivi sasa na hawatampenda daima.

Hizi ni hulka za binadamu unapokichukia kitu basi, hata kama kuna kauzuri ndani mja hujifanya haoni wala hasiki. Lakini Ada ya mja kunena muungwana vitendo.

Kama kweli JK hafai kiasi hicho basi October ndiyo kipimo kizuri sana ila wananchi wakimrudisha tena ndiyo mfahamu kuwa anakubalika na kuna watu wengi zaidi yetu sisi ambao wanaona mambo anayoyafanya ni kwa faida ya nchi yetu.
 
Kama kweli JK hafai kiasi hicho basi October ndiyo kipimo kizuri sana ila wananchi wakimrudisha tena ndiyo mfahamu kuwa anakubalika na kuna watu wengi zaidi yetu sisi ambao wanaona mambo anayoyafanya ni kwa faida ya nchi yetu.

Uchaguzi upi wa October? Ule wa chini ya uneven playing field? Ule utakaoendeshwa na ile Tume (NEC) ya CCM? Ule utakaoshirikisha mamilioni ya waliojifunika mablanketi mazito? Ule ambao CCm wakupue tena BoT kupata hela za kumshindisha mtu wao? uchaguzi gani huo unaousema?
 
Great thinkers always view things in three dimension.

Mimi kama binafsi ninaona kuwa japo JK kuna mambo yanamshinda kwa sababu ambazo zipo nje ya uwezo wake ila ninampa credit kama kiongozi kwa mambo yafuatayo.

1. Uvumilivu: Nina uhakika kabisa kuwa JK ana uwezo wa kutumia mkono wa chuma katika kuiongoza nchi kwa kunyamazisha kila mpiga kelele, lakini ameacha wazi watu waseme yanayowakera (at least kwa hili kuna advancement of freedom of expression)

2(a). Transparency: Kuna mambo ya funika funika mengi sana yamekuwa yakifanyika kabla ya JK kuwa madarakani laiti kama yangefunuliwa nafikiri tungemuona JK ni shujaa kwa sasa. Tulikuwa tunazisikia reports za CAG, lakini hivi sasa zipo open japo kupitia mtandaoni.

2(b). Kama angeamua kuizima issue ya EPA angeweza kwani nina uhakika kabisa kuwa kabla ya uamuzi wa kumteua Auditor serikali ilikuwa inajua madudu yaliyofanywa katika kutafuta pesa za uchaguzi 2005 na baadhi ya watu ku-take advantage, angeminya information zote kutoka, hakuna ambaye angejua nini kilifanyika, Ila sasa tunajua na Manyang'au wote wanajiuliza mara mbilimbili kufanya anything of that nature again.

2(c). Mauaji ya wafanya-biashara wa mahenge akina Chigumbi, uchunguzi wa tume aliounda uliwekwa hadharani na hatua kuchukuliwa tofauti ilivyokuwa ikifanywa na wa kabla yake mambo yote yalikuwa yanaishia kwenye makablasha. hatua hii pia inaleta nidhamu kwa polisi waliobaki kuwa ukiharibu utafunuliwa tu.

UBAYA WA JK TUNAUONA NI KWA KUSHINDWA KUWACHUKULIA HATUA WATUHUMIWA, LAKINI NCHI YOYOTE YA SHERIA RAIS SI MAHAKAMA AU POLISI KUWA KILA KITU LAZIMA ATOE AMRI YEYE. WATENDAJI WA CHINI WANAOGOPA NA HATA WANAFIKIA KUSEMA NCHI ITACHAFUKA WATU FULANI WAKIGUSWA(KUMBUKA KAULI YA IGP-MWEMA) SASA UNATARAJIA JK AFANYE NINI?.

NINA UHAKIKA KABISA KUWA JK NAE KAMA BINADAMU BADO ANAHITAJI KUISHI (UNAKUMBUKA KAULI YA MKAPA?) SASA KAMA NCHI HAIJAFIKIA KIWANGO CHA KUMHAKIKISHIA ULINZI 100% NI LAZIMA AWE MWANGALIFU NA GENGE LA MAFIA WANAOITAFUNA NCHI.

LAWAMA ZANGU KUU KWA JK NI KUNG'ANG'ANIA KAZI AMBAYO INATAKA MAAMUZI MAGUMU NA MAKUBWA WAKATI AKIWA AMEZUNGUUKWA NA WATUHUMIWA AMBAO ANATAKIWA KUCHUKUA HATUA DHIDI YAO, ANGETANGAZA KUWA PEMBENI NA KUMTAFUTA MTU JASIRI AMUUNGE MKONO KUONDOA UOZO HUO HATA KAMA ATATOKA UPINZANI KAMA DR. SLAA. ANGEFANYA HIVYO BASI NI KWELI TUNGEMLILIA SANA BAADA YA MIAKA MITANO IJAYO KUWA NI RAIS ALIYEIOKOA TANZANIA TOKA KWENYE MIDOMO YA SHARK (MAFISADI) LAKINI NA HUU NAO NI UAMUZI MGUMU AMBAO PIA HAUWEZI.
 
Huyu jamaa nahisi ana matatizo.

Hivi anamjuwa J. K au ni bendera kufuwata upepo. J. K anavilio vya mamilion ya watanzania, J. K nikamba ilio lika and at any tm itakatika.

Ni Rais alie kuwa na kejel nying ktk vikao kuliko msimamo. J. K.

Ni rais aliyeanguka mara nyingi ktk jukwaa na hii inamanisha kuanguka kwa utawala wake, hatumpondi, wala hatumchukii ila anayo kazi kubwa na ngumu kuuhakikishia umma au kuuthibitishia kile amefanya.

Ni rais ambaye amekuwa na vitisho vingi kwa wananchi wakati nchi ikiliwa na wajanja. Ameshindwa hata tu kujenga kituo cha kimataifa cha kuuza, kukata na ku design Tanzanite.

Hivi kweli nani atalia? Take it from me huyu ndie rais wa kwanza ambaye if hatokuwa makini atasimamishwa kortini kujibu mashitaka.

Haya ni maoni ila kwa zaidi subiri uyaone.
 
JK hata akifanikiwa kuchakachua matokeo ya kura zetu Mwenyezi Mungu kwenye utukufu wake hatamfikisha huko 2015. Atamharakisha kumpeleka kwenye hukumu ya kiyama ili kunusuru haki yetu ya Maisha bora kwa kila mtanzania.

Eeeehhhhhhhhhh Mwenyezi Mungu kwenye Utukufu wako epusha balaa hizi za matakwa ya akina Malaria Sugu kwani tutaumia sana na tumekwisha kuumia mno tuonee huruma Amen.

Nimesikia Malaria Sugu naye akiitikia Amen. Huo ndiyo mwisho wa purukushani za JK na siasa zake za kitapeli tapeli.
 
Hakuna shule za msingi za Kata,
Binafsi nitamkumbuka kwa kulinganisha data za Mwinyi VS Mkapa (aliachiwa nini na amefanya nini) Mkapa VS Kikwete (aliachiwa nini na nini kafanya). But for sure mpaka sasa suala la inflation limejenga negative performance.
 
Wengi wa watanzania, Tutalia, tutasikitika, tutaumia na tutakumbuka Jk atapotuaga rasmi 2015.
hapa pakiwa uwanja wa kimataifa wa mpira wa miguu wa Dar.
Hapo jk atamaliza muhula wake wa 2 wa urais na kukabidhi kijiti kwa mtu mwengine.
sababu za kulia kwa watz tunazo .
1) kufanya siasa bila ya vurugu
2)Uchumi kukuwa kwa kasi
3)Kuwapa wapinzani uwanja mkubwa wa siasa.
4)Kuinua elimu hasa ya msingi kwa kuanzisha shule za kata
5) kuwajali walimu

TUMPE KURA JK ATIMIZE NDOTO ZETU

Ni kweli tutamkumbuka sana! Binafsi namkumbuka kwa haya:

1. Kwa wastani ni mtu mzuri (reasonable).
2. 'Maisha bora kwa Watanzania ifikapo 2010' siyaoni:
a. Ili kupata huduma muhimu za kijamii bila rushwa haiwezekani au ikiwezekana si kwa kiwango kinachoridhisha.
b. Utawala wa sheria (usimamizi na utekelezaji wake bado sana) - kujichukulia sheria mkononi kuanzia kwa polisi wenyewe na askari wengine na hata wananchi ni mifano tosha ya kukosekana kwa utawala wa sheria.
c. Watu wenye kipato hawabanwi sana na sheria kama zinavyowabana watu wa kawaida na ndiyo maana wenye fedha tunaona wananeemeka na wasio na fedha wanaendelea kuwa maskini na kufa mara nyingi hata kabla ya siku ya kifo chenyewe.
3. Kuwadhalilisha wafanyakazi kwa kupuuza madai yao ya muda mrefu na kutumia lugha isiyo ya kistaraabu kujibu hoja zao. Kiongozi anayewajali watu wake hasa wenye matatizo ya muda mrefu kama wafanyakazi na pia Watanzania kwa ujumla asingehutubia kibabe namna ile!
Kwa haya yote, naukumbuka uongozi wa Dr Kikwete na ikitokea kuna uwezekano wa kuwa na kiongozi mwingine ni bora zaidi ili hata kama Dr Kikwete ataomba tena kujachaguliwa baadaye. Kwa hiyo, siwezi kumwona Dr Kikwete kama indispensable.
 
Tutamkumbuka kikwete kwa kuendesha nchi kiujanjaujanja, kuhunikihuni, kienyejikienyeji na kipropaganda. Ukweli jk hana uwezo kwani pamoja na kulelewa na Mzee Mkapa kwa miaka 10 akiwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje lakini bado kichwa chake kigumu kwelikweli. Mimi sishangai sana maana hiyo ndiyo hulka ya waswahili kubabaishababaisha, kupenda starehe badala ya kazi, kujisikia mbele ya jamii n.k. Yote hayo ndiyo anayofanya jk. kwa namna nchi inavyokwneda, ninamwone huruma rais ajaye.
 
Kweli beauty is in th eyes of the beholder! kwangu mimi bado hajanishawishi kma ni tegemeo la vijana wala wazee. ni tegemeo la wana mtandao na familia yake na maswahiba
 
Kila Rais hukumbukwa kwa jambo au mambo kadhaa mazito wakati wa muongo wa uongozi wake. Kwa upande wa JK, wa-TZ watamkumbuka sana kwa mambo makubwa matatu: 1. Vituko vya RA/EL na zengwe la Richmond/Dowans 2. Milipuko ya mabomu huko mbagala na g'mboto 3. Kashfa ya mabilioni ya fedha za EPA. Una lingine la kuongezea hata kama zuri, asije akasema wa-TZ hawajamtendea haki?
 
Kila Rais hukumbukwa kwa jambo au mambo kadhaa mazito wakati wa muongo wa uongozi wake. Kwa upande wa JK, wa-TZ watamkumbuka sana kwa mambo makubwa matatu: 1. Vituko vya RA/EL na zengwe la Richmond/Dowans 2. Milipuko ya mabomu huko mbagala na g'mboto 3. Kashfa ya mabilioni ya fedha za EPA. Una lingine la kuongezea hata kama zuri, asije akasema wa-TZ hawajamtendea haki?


Haki gani atadai zaidi ya kuchaguliwa kwa kishindo mwaka 2005, hii ya 2010 sio haki yake ni Wizi tu ambao aliusuka na kuufanikisha. Tutamkumbuka sana kama rais mwizi.
 
Back
Top Bottom