Kikwete kafanya mengi kipindi chake cha uongozi, tutamkumbuka...

Kila Rais hukumbukwa kwa jambo au mambo kadhaa mazito wakati wa muongo wa uongozi wake. Kwa upande wa JK, wa-TZ watamkumbuka sana kwa mambo makubwa matatu: 1. Vituko vya RA/EL na zengwe la Richmond/Dowans 2. Milipuko ya mabomu huko mbagala na g'mboto 3. Kashfa ya mabilioni ya fedha za EPA. Una lingine la kuongezea hata kama zuri, asije akasema wa-TZ hawajamtendea haki?

ATAKUMBUKWA KWA JAMBO MOJA MUHIMU SANA KULIKO HAYO ULOYATAJA AMBALO NI:-
Rais wa Kwanza Duniani kuongoza nchi Maskini SAANA kwa 10 Bila kujua Chanzo cha Umaskini wake!
 
Ndugu zangu; maxence, invisible, katavi, pakajimmy, rev, 1st lady, preta na wengine wengi, nyie mtamkumbuka kwa lipi JK? Kweli kila rais ana mengi ya kukumbukwa nayo, lakini yale yanayokujia hata ukiamshwa usingizini unajiachia bila hofu kuyasema maana ndio ukweli wenyewe bila kumuonea wala kumbeba au kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa. May be it'll save as a challenge for our future president!
 
Pia tutamkumbuka kwa kua rais wakwanza tz kuwaumbua mafisadi wanaoiba mali za tz nakuwapeleka mahakamani,pia kuvunja serikaliyake na kumtimua waziri mkuu kwa tuhuma tu zakushiriki ufisadi,hakuna hata rais 1 ktk east africa aliewahi kuwaumbua nakuwatimua mawaziri wake kwa kujihusisha na ufisadi.mnyonge mnyongeni hakiyake mpeni.
No no no no!! hapa nisaidieni, kwani ALIMTIMUA au akinaMwaki-embe walimtaka huyo PM "APIME" MWENYEWE na alipopima akaona tatizo ni u-PM akaamua ku-stp down kwa prssre ya bunge!!! ebo!!
 
Kila Rais hukumbukwa kwa jambo au mambo kadhaa mazito wakati wa muongo wa uongozi wake. Kwa upande wa JK, wa-TZ watamkumbuka sana kwa mambo makubwa matatu: 1. Vituko vya RA/EL na zengwe la Richmond/Dowans 2. Milipuko ya mabomu huko mbagala na g'mboto 3. Kashfa ya mabilioni ya fedha za EPA. Una lingine la kuongezea hata kama zuri, asije akasema wa-TZ hawajamtendea haki?

atakumbukwa kwa kumuwezesha FANCY*NKUHI teh teh teh
 
Kila Rais hukumbukwa kwa jambo au mambo kadhaa mazito wakati wa muongo wa uongozi wake. Kwa upande wa JK, wa-TZ watamkumbuka sana kwa mambo makubwa matatu: 1. Vituko vya RA/EL na zengwe la Richmond/Dowans 2. Milipuko ya mabomu huko mbagala na g'mboto 3. Kashfa ya mabilioni ya fedha za EPA. Una lingine la kuongezea hata kama zuri, asije akasema wa-TZ hawajamtendea haki?

uteuzi wa MKUU WA WILAYA MANYONI utakumbukwa milele :)
 
1) RA/EL wanamakosa gani katika sakata la Dowans?

2) Milipuko ya mabomu imetokea kipindi cha JK lakini inawezekana kabisa kuwa ni hujuma za watu kama wewe mnaomchukia JK bila sababu.

3) Kashfa ya EPA ni JK aliyoiibua na ni JK aliyehakikisha japo baadhi ya hizo pesa zinarudi. Kumbuka EPA ilianza na fedha ziliibiwa kabla ya Kikwete kuwa madarakani.

Tutayomkubuka nayo Kikwete ni mema yote na kujituma kweke.

1) Kwa kipindi kifupi vyuo vikuu 11 na bado hajamaliza muda wake. VYUO VYOTE KUWA HAVINA WALIMU, NA VINGINE KEAJIRI VIHIYO - UDOM. HILI SI JEMA HATA!!!

2) Mashule ya sekondari zaidi ya awamu zote zilizopita ukijumlisha na tulizorithi kwa mkoloni. MATOKEO YA MITIHANI YA FORM 4 THIS TIME NI KIELELEZO TOSHA KUTHIBITISHA KUSHINDWA KWAKE!!! HILI SI JEMA HATA!!!!

3) Zahanati kila kata. NA AMBULANCE ZA BAJAJ KWA WAJAWAZITO, ZAHANATI HAZINA MADAKATARI. HAKUNA WEMA HAPA!!!!

4) Muhimbili kwa kipindi chake kifupi ameiwezesha kwenye upasuaji wa moyo na mishipa midogo ya fahamu. Na kuwapeleka masposhilisti kibao kusomea fani hizo. BADO HAWAJAANZA, SERIKALOI HAINA FEDHA HATA!!! KAZI WIZI TU...

5) Barabara kwa kiwango cha lami ni zaidi ya awamu zote zilizopita na bado. HII NI HANG OVER PROJECTS ZA BWM, YEYE HANA HATA MOJA, LABDA TUSUBIRI "FLY OVERS" ALIZOAHIDI KWENYE KAMPENI, HAYA YOTE YANAMDHALILISHA TU. HAKUNA JEMA

6) Mortgage kuwawezesha wananchi kupata nyumba kwa mikopo nafuu. Tayari, sijui kama umesikia kitu inaitwa Tanzania Mortgage Refinance Company? Kama bado, subiri utaiona ikiyawezesha mabenki kuwapa watu mikopo. PERHAPS...WE ARE WAITING

7) Benki za wakulima? Au na hili hulijuwi? PERHAPS...WE ARE WAITING

8) Kuwekeza kwenye pembejeo za kilimo na kuzigawa nchi nzima. PEMEBEJEO ZOTE ZINAUZWA NJE, MALAWI NA CONGO, MFANO MZURI NI SUMBAWANGA....HAKUNA JEMA HATA...

10) Kuweza kuibadili mikataba na makampuni ya uchimbaji Madini na kumchaguwa mbunge wa upinzani kuendesha shughuli za hiyo tume. ALICHOFANYA NI SAWA NA KUBADILI MZIKI WA BONGO FLAVA KWENDA KWENYE TAARABU... HAKUNA JEMA!!!!

11) Kutatua mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar na sasa Zanzibar ni njema. HAKUTATUA...NI SHADA TU, TUSUBIRI, MAANA SISI HUWA TUNAJIFUNZA KWA UHALISIA. MFANO NI MABOMU YA GONGO LA MBOTO... HAKUNA JEMA HATA!!!

12) Kufungua midomo ya wapinzani mpaka sasa wanaweza kusikika. Subutu, wakati wa awamu zilizopita! HILI SI LA KUJIVUNIA NI WAJIBU WAKE KIKATIBA...INGAWA KATIBA INAJICHANGANYA YENYEWE!!!!

Na mengine mengi tu.

nITAMKUMBUKA KWA KUCHEKA CHEKA NA KUTOKUWA SERIOUS, PLUS SAFARI ZA NJE.....
 
Bye bye JK, we'll definately remember you always for the bad and for the good. Though so far the bad outweighs the good, and the bad memory lasts longer! Mmh, poor JK can't we do without you? Surely, we can!
 
Kipindi cha pili cha muhula wa utawala wa JK pia kitakumbukwa kwa kuibuka mchungaji wa loliondo anayetibu magonjwa sugu kwa sh.500 tu. Big up, JK!
 
1)

3) Zahanati kila kata.

5) Barabara kwa kiwango cha lami ni zaidi ya awamu zote zilizopita na bado.

Samahani bradha, kata yetu haina zahanati hata ya kusingiziwa. Lakini pia hatuna lami tangu nchi hii ipate uhuru, na nilipo ni makao makuu ya kata yetu. Shule unayoita 'ya kata' tumeijenga wenyewe mwaka jana na bado haijakamilika. Mbunge aliahidi kuleta mabati ya kuezekea shule, tangu ashinde uchaguzi hajaonekana.
 
Pia tutamkumbuka kwa kua rais wakwanza tz kuwaumbua mafisadi wanaoiba mali za tz nakuwapeleka mahakamani,pia kuvunja serikaliyake na kumtimua waziri mkuu kwa tuhuma tu zakushiriki ufisadi,hakuna hata rais 1 ktk east africa aliewahi kuwaumbua nakuwatimua mawaziri wake kwa kujihusisha na ufisadi.mnyonge mnyongeni hakiyake mpeni.

Ndezi wewe! Low Ass hakufukuzwa, alijiuzulu mwenyewe. Tena Bungeni Dodoma. Mi namkumbuka JK kwa kwenda Jamaica kumuona Beenie Man baada ya kuikosa show yake pale viwanja vya CoET Kijitonyama(zamani TTCL), kwa kuwa show ile iligongana na safari yake ya Copenhagen kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Kupunguza uzalishaji wa hewwer ukaa.
 
808.jpg

TANGANYIKA BWANA HIVI VITUKO TUTAACHA LINI?
 
Jambo jema kwa JK so far ni pamoja na kujali watoto yatima na kuwapa zawadi wakati wa sikukuu. Huwa naona mbuzi wa zawadi na viroba vya mchele katika viwanja vya ikulu kupitia luninga. Tumpigie makofi prezda wetu kwa kujali yatima, kama vitabu vitakatifu vinavyotuasa.
 
Ndugu zangu; maxence, invisible, katavi, pakajimmy, rev, 1st lady, preta na wengine wengi, nyie mtamkumbuka kwa lipi JK? Kweli kila rais ana mengi ya kukumbukwa nayo, lakini yale yanayokujia hata ukiamshwa usingizini unajiachia bila hofu kuyasema maana ndio ukweli wenyewe bila kumuonea wala kumbeba au kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa. May be it'll save as a challenge for our future president!
Nitamkumbuka huyu jamaa kama rais wa kwanza duniani kununua vyombo fulani mfano wa bajaji eti zitumike kuwabebea WAJAWAZITO!...
Lakini zaidi, chombo hicho ni cha ajabu sana, maana hakijawahi kutumika popote duniani, majaribio ya kwanza ni kwa wajawazito wa TANZANIA... maana mjamzito akipandishwa humo, anapigwa jua, anapigwa vumbi, na kama kuna mvua basi yote itamuishia!...kwa assessment yangu, wajawazito wote wakithubutu kupanda kifaa hicho(cha aina yake), wote watajifungulia njiani!
Kwa hilo sitamsahau!

Back
Top Bottom