Mwawado
JF-Expert Member
- Nov 2, 2006
- 993
- 252
Watanzania tumekuwa wepesi mno kurithika na Ahadi zisizotekelezeka za hawa viongozi wetu wasio makini.
Mwezi July/2010 nilibahatika kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Pili wa "Tanzanian Diaspora in Ameica (DICOTA) uliofanyika Jijini Minneapolis - Minnesota,Pamoja na mambo mengine kulikuwa na Mada iliyozungumzia kirefu kuhusu Tatizo hili la Usafiri katika Jiji la Dar-Es-Salaam ,Athari zake Kiuchumi na namna ya kupunguza na hatimaye kuondoa kabisa tatizo hilo,Mada hiyo iliyokuwa na ushawishi mkubwa iliendeshwa na Pro.L.Meekisho (professor of Mechanical Engineering,Portland State University) na Prof.Primus Mtenga (Civil Engineering,Florida A&M University).Katika Majadiliano ya kuona kiini cha cha tatizo na namna gani serikali kwa kutumia mipango ya muda mfupi na mrefu kuondoa Tatizo hilo ilibidi Katibu Mkuu ofisi ya Rais Bwana Philemon Luhanjo kutolea maelezo.Katika maelezo ya Katibu Mkuu ambaye pia ni Msaidizi wa kwanza wa Rais na Katibu wa Baraza la Mawaziri,alisema njia za muda za kutatua Tatizo hilo ni pamoja na kufunga baadhi ya barabara wakati wa kazi na kufikiri kuzuia Private Public Transport kama Dalala na Bajaji kuingia Mjini.
Baadhi ya Washiriki wa Kongamano hilo walionyesha kutoridhishwa na njia hizo. Mapendekezo ya prof.Meekisho ilikuwa ni pamoja na kuhamisha baadhi ya huduma nyingine za mawizara na kuzipeleka katika miji midogo ya Kibaha,Bagamoyo na Kisarawe,hali hiyo itakuza Miji hiyo ya karibu kwa kuongeza Ajira,kuboresha hali ya maisha ya watu na kuboresha Miundombinu....Utatuzi wa Muda wa hali hiyo Jijini Prof alipendekeza kuwepo na usafiri wa Treni kwa kutumia Reli ya kati na Tazara ambazo kwa sasa zote hazitumiki ipasavyo. 1);Tazara itasaidia kupunguza Mlundikano wa watu wa Gombo la Mboto,Tabata,Temeke,Tandika na Uwanja wa Ndege,Kukiwepo na utaratibu Mzuri Reli ya Tazara inayoishia Kurasini itapunguza sana Mlundikano wa magari kwa njia za Uhuru,Kilwa na Nyerere. 2);Reli ya kati pia itatumika ktk mpango huo,Reli hiyo itaunganisha Jiji na maeneo mengi,kwa sababu kuna sehemu Reli hiyo imepelekwa kwenye Viwanda vya Urafiki (zamani) na saruji Wazo,kwa maana hiyo ikikarabatiwa vyema itasaidia idadi kubwa ya watu wa Ubungo,Kawe,Mwenge,Kimara na Magomeni na kwa hali hiyo itapunguza mlundikano wa magari ktk barabara za Morogoro,Ali Hassan Mwinyi,na Bagamoyo na kwa ziada kuwepo na Usafiri rahisi wa majini kutoka Ferry mpaka Jangwani Beach,ambao utatoa huduma kwa watu wa Jangwani Beach,Mbezi,Masaki na hatimaye Oysterbay.
Kwa maelezo ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais ni kwamba World Bank wapo tayari kutoa pesa,wanachoihitaji wao ni mipango makini ya kuondoka Mlundikano huo ambao mahali pa dk 30 inachukua masaa 3 - 4 kwa muda wa asubuhi na bada ya masaa ya kazi.
Katibu Luhanjo alisisitiza wazi kuwa tusiwasikilize sana wanasiasa kwa madai kwamba kipindi hichi cha Uchaguzi Ndugu zetu wanasiasa wanasema chochote wanachoona kitawapa kura....alisema hayo baada ya kuambiwa kuwa "Waziri Membe ameahidi Serikali itaamua suala la Dualcitizen kabla ya November".Bwana Luhanjo alidai kuwa mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi,na hiyo Novemba aliyoisema Mh.Membe ni Wakati ambao Rais Mteuliwa atakuwa anaunda Serikali yake,Bw.Luhanjo alisema msitegemee suala la Dual Citizenship kujadiliwa na Baraza la Mawaziri mwaka huu,kwa sababu sio priority kwa wakati huu baada ya uchaguzi.
Sasa Tunapaswa kuangalia maneno ya Bwana Kikwete ktk wakati huu karibu na Uchaguzi,Hii miradi ya magari ya kutumia mawese (mafuta nafuu),na flyovers za fire,Chang'ombe,Magomeni na Ubungo ni maneno ya kutafutia Kura!