Elections 2010 Kikwete aahidi usafiri wa treni Dar

tunaomba watuwekee ufafanuzi wa hiyo njia itapita wapi kuwezesha hayo mabasi kwenda mbio toka feri hadi Kimara.Na wakati huo huo siye wa madongo kuinama mbagala, tabata,kawe,mwenge,tegeta tunapita wapi kufika katika mijengo yetu ya kazi na dala dala zetu?
Hapa wanatafutia njia ya kutokea muungwana hapo 31oct.
 
Trillion 7.3! OMG...

Sijaona layout ya huo mradi lakini naamini ni usanii mtupu...
 
Barabara ya Mwenge,Mandela,Bandari inamiaka zaidi ya mitano haijaisha hiyo reli na barabaraya ya kasi atamaliza lini apumzishwe tuu ili wenake waje wasimamie hiyo miradi period
 
mitanzania inaniboa mwanzo mwisho...yani haya mawazo ya kutumia treni for local transportation in dsm mie ninayo tangu rais mkapa eti wao leo wamelijua hili...plus kutumia njia ya bahari na kutengeneza touristic trips along the ocean na vijisiwa vidogodogo kama bongoyo na mbunde etc....haya ndio matatizo ya kujaza mizee yenye mawazo mgando kwenye sehemu za kufanya maamuzi magumu na sahihi..a genious ..a person who think ahead of time...kweli mie genious uki-compare na hii mizee ya huko serikalini....

kwa lugha ingine, kidhungu, wanaitwa USEFUL ******!
 
This guy whatever he say he mean it, and infarct he does it. And if he doesn't do it, is just because of time limitation. Give him more time u gonna prove my words.

Are you another version of Malaria Sugu?? MS anatutosha sana, where the hell are you coming from? we dont need another MS
 
Hii sawa na yule aliye sema anataka kuwaletea wananchi wa Karenga bahari wavue samaki.
Uchaguzi huu tutasikia mengi. Tunaomba kwa miezi michache atekeleze ahadi viporo zile kwanza.
 
This guy whatever he say he mean it, and infarct he does it. And if he doesn't do it, is just because of time limitation. Give him more time u gonna prove my words.

Naona jamaa wanauliza ati njia ni wapi? Reli kuanzia Central Police katikati ya jiji mpaka Ubungo ipo siku nyingi tu. Ni namna ya kuanza kuitumia. Siyo kwamba itajengwa mpya.
 
SERIKALI inatarajia kuanza kutumia njia ya reli kwa ajili ya kusafirisha abiria kwa mkoa wa Dar es Salaam ili kuondokana na adha ya foleni ambayo inazidi kila kukicha.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Rais Jakaya Kikwete wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa miundombinu kwa mabasi yaendayo kasi.

Rais Kikwete alisema kuwa suala hilo lilikubaliwa katika vikao vya Baraza la Mawaziri hivyo kinachosubiriwa ni Wizara ya Miundombinu kuangalia namna ya kuanza kulifanyia utekelezaji.

Alisema kuanza kutumia njia ya reli kutaleta manufaa na kupunguza foleni kwa wakazi wa jiji kwa kuwa kwa safari moja zaidi ya abiria ambao si chini ya elfu nne wataweza kusafirishwa.

“Mpango wa sasa tulionao ni kutumia njia ya reli kwa ajili ya kusafirisha abiria maana njia hiyo itasaidia kupunguza foleni na kwa wakati mmoja zaidi ya abiria elfu nne watasafirishwa, jambo hilo tulishakubaliana na Baraza la Mawaziri hivyo wizara husika tunaamini itakuwa imeanza kufanyia utekelezaji,” alisema.

Haya ngoja tuone..! hahahahahahaha

Katika hatua hiyo Rais Kikwete alizindua awamu ya kwanza ya ujenzi wa Miundombinu ya Mradi wa Mabasi yaendayo kasi (DART) katika jiji la Dar es Salaam ambao utanatarajiwa kukamilika mwaka 2012.

Ujenzi huo unaoanzia eneo la feri na kuishia Kimara ambapo aliwataka wamiliki wa mabasi hayo makubwa kutumia gesi asilia ili kuondokana na uharibifu wa mazingira.

Mradi huo unaotekelezwa katika awamu sita, umefadhiliwa na Benki ya Dunia (WB) hadi kukamilika kwake utagharimu kiasi cha sh trilioni 7.3.
Source: Tanzania Daima

Kama hajadanganywa huyu sijui...! Mzee wa uzinduzi, alizindua feri, gari la wagonjwa, hoteli ya kitalii kule Arusha hahahahaha! Jamaa wasanii sana


Alikuwa wapi miaka mitano iliyopita asifanye hivyo?.

Au anasubiri kuja kusema haitekelezeki kama zilivyokuwa ahadi zake za 2005.

Huyu jamaa anakumbuka shuka wakati kumeshakucha.
 
Pesimistic! I am not blaming u, because you born that way.

Haya mwenzetu optimist tupe hoja zako maana ni rahisi kukosoa kuliko kutoa hoja.Hivi ulikuwa wapi wakati JK anajigamba kuwa foleni hizohizo ambazo sasa anaziita ADHA ni dalili za maisha bora kwa kila Mtanzania?Labda hukumsikia,au kama ulimsikia pengine uko too optimistic to understand that unamwagiwa changa la macho.

We can't blame you,there are people who were born to be taken for the ride for their entire lives.
 
Ujenzi huo unaoanzia eneo la feri na kuishia Kimara ambapo aliwataka wamiliki wa mabasi hayo makubwa kutumia gesi asilia ili kuondokana na uharibifu wa mazingira.

Kuna na gesi asilia? Wizi mtupu
 
You guyz dont be myopic, yaani mnadhani sisiem especially kikwete ndo wanahaki na uwezo wa kuleta maendeleo ndani ya nchi hii!!

I tell you these, and please note not to forget what am gonna say at the point real development in tatnzania gonna come.
1. lazioma sisiemi isitawale vyama vingine vipewe nafasi kusimamamia rasilimali za watanzania
2. Kama sisiemi isipoachia madaraka kwa kuona kwamba imeshindwa kufanya mipango na kutengeneza fulsa kuondoa umasikini ambao unaonekana kukua kila kukicha, basi lazima tuingie kwenye machafuko ile kuwe na nidhamu katika utawala. nisingependa tufike uko though history teach us that for and developed nation that we see to day once passed in a hard time of sacrificing the blood of its citizens.
 
Kwanini atoe ahadi wakati huu?if really jf is the home of great thinkers,tuwaambie watu ukweli hakuna kitu kama hicho ni kuomba kura tu huko
 
Aulizwe huyu katika ahadi zako ulizozitoa kwenye kampeni yako ya 2005 ni ngapi umeshatimiza hadi sasa? Jibu ni ZERO! na hili halina ubishi sasa kisharukia kutoa ahadi nyingine!
 
Back
Top Bottom