Elections 2010 Kikwete aahidi usafiri wa treni Dar

Mkimbizi

JF-Expert Member
Aug 23, 2008
222
34
SERIKALI inatarajia kuanza kutumia njia ya reli kwa ajili ya kusafirisha abiria kwa mkoa wa Dar es Salaam ili kuondokana na adha ya foleni ambayo inazidi kila kukicha.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Rais Jakaya Kikwete wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa miundombinu kwa mabasi yaendayo kasi.

Rais Kikwete alisema kuwa suala hilo lilikubaliwa katika vikao vya Baraza la Mawaziri hivyo kinachosubiriwa ni Wizara ya Miundombinu kuangalia namna ya kuanza kulifanyia utekelezaji.

Alisema kuanza kutumia njia ya reli kutaleta manufaa na kupunguza foleni kwa wakazi wa jiji kwa kuwa kwa safari moja zaidi ya abiria ambao si chini ya elfu nne wataweza kusafirishwa.

"Mpango wa sasa tulionao ni kutumia njia ya reli kwa ajili ya kusafirisha abiria maana njia hiyo itasaidia kupunguza foleni na kwa wakati mmoja zaidi ya abiria elfu nne watasafirishwa, jambo hilo tulishakubaliana na Baraza la Mawaziri hivyo wizara husika tunaamini itakuwa imeanza kufanyia utekelezaji," alisema.

Haya ngoja tuone..! hahahahahahaha

Katika hatua hiyo Rais Kikwete alizindua awamu ya kwanza ya ujenzi wa Miundombinu ya Mradi wa Mabasi yaendayo kasi (DART) katika jiji la Dar es Salaam ambao utanatarajiwa kukamilika mwaka 2012.

Ujenzi huo unaoanzia eneo la feri na kuishia Kimara ambapo aliwataka wamiliki wa mabasi hayo makubwa kutumia gesi asilia ili kuondokana na uharibifu wa mazingira.

Mradi huo unaotekelezwa katika awamu sita, umefadhiliwa na Benki ya Dunia (WB) hadi kukamilika kwake utagharimu kiasi cha sh trilioni 7.3.

Source: Tanzania Daima

Kama hajadanganywa huyu sijui...! Mzee wa uzinduzi, alizindua feri, gari la wagonjwa, hoteli ya kitalii kule Arusha hahahahaha! Jamaa wasanii sana
 
Muungwana ana ahadi ngumu sana. Ila kama city wakiwa serious wanaweza, chukulia mfano zile reli zinazoenda viwandani mfano kutoka stesheni kuja ubungo ipo reli, kutoka stesheni kwenda tabata hadi vingunguti ipo reli, kwa hizo chache wanaweza wakafanya kama india, bali ahadi hii itatekekelezela 2020 or so.
 
mitanzania inaniboa mwanzo mwisho...yani haya mawazo ya kutumia treni for local transportation in dsm mie ninayo tangu rais mkapa eti wao leo wamelijua hili...plus kutumia njia ya bahari na kutengeneza touristic trips along the ocean na vijisiwa vidogodogo kama bongoyo na mbunde etc.

...haya ndio matatizo ya kujaza mizee yenye mawazo mgando kwenye sehemu za kufanya maamuzi magumu na sahihi..a genious ..a person who think ahead of time...kweli mie genious uki-compare na hii mizee ya huko serikalini....
 
Ofcourse inakera and to them watakwambia serikali haina hela, wakati hii ni miradi inayoweza kuwa promoted na ikajiendesha yenyewe!
 
Mkuu huwezi kuamini, kuna ramani ya jiji inaonyesha hizo njia lakini kote kulishauzwa na kuna nyumba juu yake.

Watanzania inabidi sasa tuamke. M2 anapotoa ahadi kama hizi ili kupata kura inabidi tuhoji kabla ya kupiga kura. Kwa mfano mtu anapokwamia nipe kura halafu kutukua na maishabora kwa kila mtanzania. Inabidi umuulize hayo maisha bora yatakujaje? Akikwambia kwa kasi mpya na ari mpya ujue bado hajakujibu!
 
Mkuu huwezi kuamini, kuna ramani ya jiji inaonyesha hizo njia lakini kote kulishauzwa na kuna nyumba juu yake.

Ramani ya jiji la Dar inaonyesha hadi bara bara za angani(flying over) lakini wajuaji wakayauza maeneo yote na huwezi tena kuzijenga kwakuwa msongamano wa majengo umekuwa ni kikwazo.
 
mitanzania inaniboa mwanzo mwisho...yani haya mawazo ya kutumia treni for local transportation in dsm mie ninayo tangu rais mkapa eti wao leo wamelijua hili...plus kutumia njia ya bahari na kutengeneza touristic trips along the ocean na vijisiwa vidogodogo kama bongoyo na mbunde etc.

...haya ndio matatizo ya kujaza mizee yenye mawazo mgando kwenye sehemu za kufanya maamuzi magumu na sahihi..a genious ..a person who think ahead of time...kweli mie genious uki-compare na hii mizee ya huko serikalini....

Pesimistic! I am not blaming u, because you born that way.
 
Kama hajadanganywa huyu sijui...! Mzee wa uzinduzi, alizindua feri, gari la wagonjwa, hoteli ya kitalii kule Arusha hahahahaha! Jamaa wasanii sana

This guy whatever he say he mean it, and infarct he does it. And if he doesn't do it, is just because of time limitation. Give him more time u gonna prove my words.
 
Huu mradi umeanza kuuimbwa toka mwaka gani sijui. Na kuna watu wanakula mishahara tayari. Hii miradi ambayo bado wanachi hatujaona dalili za kuanza kwake bora rais awaachie watendaji wake waizungumzie.

Kuna mradi mwingine wa kuumia feri Posta- tegeta msaada Mbezi. Kuna waziri aliuzindua kwa maneno miaka ya nyuma. Hope nado wanatafuta wafadhili.
 
This guy whatever he say he mean it, and infarct he does it. And if he doesn't do it, is just because of time limitation. Give him more time u gonna prove my words.
I'm not crazy, to give him another chance!
 
This guy whatever he say he mean it, and infarct he does it. And if he doesn't do it, is just because of time limitation. Give him more time u gonna prove my words.

Alisema ataifanya Dar es Salaam iwe kama California...na ameweza 100% yaani tumeizidi pia hiyo California....dadaangu
 
Mkuu huwezi kuamini, kuna ramani ya jiji inaonyesha hizo njia lakini kote kulishauzwa na kuna nyumba juu yake.

Mkuu tuwekee hapa tuwadai kabla ya hawaja pewa kura hasa pale watakpo kuja kuziomba.
Jamaa wana zingua sana hawa.
 
Zawadi maybe he fulfils his promises when he is dreaming at nite next to his wife.
Kwahio mipango ni miwili sio? Wa reli na DART?
Unajua kuna njia za mbadala ambazo ni less expensive and more sustainable than hayo maflyovers! HongKong,NY,Shanghai zina ma fly overs ya kufa mtu je hakuna traffic jams? Hawajui kua cost hio ya trilions haiishi hapo bali kuna billions tutalipa kila mwaka kwa foreign companies kwa ajili ya maintenance and repair!!?
Nilichukua ka course ka city planin as general education university ila mbona nakumbuka more sustainable solutions than hizi. E.g. SATTELITE TOWNS! Jengeni satelite town with all facilites including govment officer at 100 km radius of city center. Mkiweka full biznes parks outside city center mimi kama mfanyabiashara wa mkoani sitakua na haja ya kuingia CBD! And now is when we have a chance. Sema watu wesha chukua 20% zao.
 
Back
Top Bottom