Prof. Mbarawa: Treni za SGR ni za mwendo wa kawaida (siyo mwendokasi)

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
21,563
50,415
Mkurugenzi wa shirika la reli nchini, Masanja Kadogosa amesema treni ya SGR itatumia saa moja na nusu kutoka DAR mpk Moro na itatumia msaa 3 kutoka DAR mpk Dodoma.

Ndipo waziri wa uchukuzi prof. Makame Mbarawa akasema "naomba wananchi waelewe hii treni siyo ya high speed kama zile za China na South Korea. Na hata ujenzi wa reli yake ni tofauti na hii ya kwetu ".

Source: ITV habari.

My take; Naona kama tumebadllishiwa gia angani. Mbona mwanzo tuliambiwa itakuwa treni ya mwendo kasi? Kama Dar mpk Moro ni saa moja na nusu, kuna haja gani ya kuitumia? Si ni bora watu waendelee kutumia IST ama Vitz zao tu?

...........................................................................

UPDATES.
Shirika la reli limeandika kuwa umbali kutoka DAR mpk Moro ni km 300 na speed ya treni ni 160 kmph. Kimahesabu ni kwamba treni hiyo itatumia saa 1 na dk 52 (~2 hrs), ukiongeza na saa 1 la kuisimamia na kupakia unapata masaa 3. Huu ni muda sawa na wa mabasi.
 
Hiyo tofauti ya ujenzi kati ya reli za China na Korea na hii reli yetu ya SGR ni ipi?

Nina wasiwasi Mbarawa asijekutumia udhaifu wao wa kununua vichwa chakavu vya treni ya SGR, vilivyosababisha spidi iwe ndogo, akahamishia kwenye ujenzi wa reli.

Maana naona siku hizi ni kama kuna mchezo huko serikalini wa kumtupia lawama The late Magufuli kwenye kila kitu.

Wajanja wamekula pesa kwenye ununuzi wa vichwa vya treni, wameachwa hawafanywi chochote na bosi wao, wapo tu wanatamba kwa ukwasi..

Leo malengo ya utengenezaji wa reli ya SGR ili kurahisisha usafiri yameshindwa kufikiwa, lawama inatupiwa njia ya treni!.

Mbona hili jambo halikuwahi kusemwa kabla? sasa kuna maana gani ya kuwa na hiyo reli ya SGR?

Prof. Mbarawa ameonesha incompetence muda mrefu sana kwenye hiyo wizara, ajabu anaachwa tu, na haya ndio matokeo yake.

Kwa kauli hii ya Prof. Mbarawa, sasa hata ujenzi wa JNHPP nao hauna maana, lile bwawa sasa limegeuzwa la kutuondolea ile migao yao ya umeme wanayoitengeneza, yale malengo mahususi ya kuzalisha umeme wa kuendesha treni ya SGR yamekufa.

I doubt kama yupo atakayekuwa tayari kupoteza muda wake atoke Dsm kwenda Morogoro kwa masaa matatu, wamechezea pesa nyingi, wamepoteza muda, wameshindwa kufikia malengo.
 
Kama itaoperate kwa speed ya kwaida huo uwekezaji mkubwa uliofanyika kwa gharama kubwa hauta akisi tija inayopatikana

Tafsiri ya uwekezaji huo mkubwa imebebwa na dhana ya mwendo kasi ili kuokoa muda na kuchochea ukuaji kwa uchumi
 
Mkurugenzi wa shirika la reli nchini, Masanja Kadogosa amesema treni ya SGR itatumia saa moja na nusu kutoka DAR mpk Moro na itatumia msaa 3 kutoka DAR mpk Dodoma...
Hata iwapo utatumia vitz ndege sasa moja na nusu utaishia mbezi na hapo umeserereka barabarani hakuna foleni na hujakutana na wale nyonya damu wa road a.k.a kunguru weupe😁
 
Mkurugenzi wa shirika la reli nchini, Masanja Kadogosa amesema treni ya SGR itatumia saa moja na nusu kutoka DAR mpk Moro na itatumia msaa 3 kutoka DAR mpk Dodoma...
Uamuzi ni wako ukiamua kupanda au kutopanda na kwenda na IST yako. Hautolazimishwa mkuu. Hii ni hatua ya kwanza. Ipo siku tutafika kwenye mwendokasi kama Morocco.
 
Mkurugenzi wa shirika la reli nchini, Masanja Kadogosa amesema treni ya SGR itatumia saa moja na nusu kutoka DAR mpk Moro na itatumia msaa 3 kutoka DAR mpk Dodoma...
Kwani toka ujenzi unaanza uliambiwa speed yake ni ngapi nje ya 160? Kwamba hujui tofauti neno speed train na high speed train.Tusitengeneze strory zetu wakati jambo lenyewe linajulikana .Ingekuwa high speed usingeona kona au single phase.
 
Back
Top Bottom