Taarifa ya habari ya jana usiku saa 2 ya Radio 5 fm imetangaza kupitia mtangazaji wao aliyepo PEMBA Ndugu Masanja Mabula kuwa watu wasiojulikana wameliteketeza kwa moto kanisa la Pentekoste TAG huko kaskazini Pemba juzi usiku.Lakini amemkariri kiongozi mmoja wa Kanisa hilo akidai wanawahisi baadhi ya watu lakini hawatachukua hatua bali wanamwachia Mungu.
Je, huu sio muendelezo wa kuwabagua wabara na kuwatisha ili wakimbie visiwa hivyo kwa hoja ya kutaka ZNZ kujitenga na Muungano ilihali wa ZNZ wanafanya mambo yao huku bara bila bugudha?
Ivi makanisa zanzibar yanatafuta nini?mbona mnataka kuwachokoza? mmesikia kuna mzanzibar ambaye ni kafiri? acheni chokochoko hazitowafikisha popote. ivi nyinyi mnaochangia zanzibar mmeenda mkaona palivyo na watu wanavyoishi? waacheni jamani msije kutuibulia mengine, nyie komaeni kule Iringa na Mbeya