Zitto
Former MP Kigoma Urban
- Mar 2, 2007
- 1,562
- 10,880
Uamuzi wa wanafunzi kugoma ni uamuzi wa sahihi kabisa. Pia ninaunga mkono kwa wao kuweza kuhusisha mateso wanayopata na kero kadhaa mfano matumizi mabovu yaliyoripotiwa na mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali.
Si sahihi kwa watu kusema wanafunzi wamekosea. Dhana ya mgomo ni wao kushitaki kwa jamii kwa kero zao ambazo serikali haitaki kuzisikia.
Ifahamike kuwa toka sheria namba 9 ya mwaka 2004 itungwe serikali imekuwa ikiikiuka sheria hii makusudi kabisa. Kwa mafano sheria haisemi na wala haitoa mamalka kwa bodi ya HESLB au chombo kingine chochote kusema ni madaraja gani ya watu watasomeshwa kutokana na mkopo wa serikali. Serikali ilikaa na kuamua tu.
Sasa ndio yakaja haya mambo ya asilimia 40 ambayo ni kinyume kabisa na sheria na 9 ya mwaka 2004.
Mimi binafsi nadhani ilikuwa sahihi kwa wanafunzi kugoma. Vilevie ni makosa kwa utawala wa chuo kuwafukuza. Kanuni za chuo (by-laws) zinasema kuwa wanafunzi watatimuliwa, au chuo kufungwa iwapo tu watagoma kwa siku tatu mfululuzo. Hazikufika.
Kwa mimi ambae nimewahi kuwa Kiongozi wa wanafunzi, naanza kuona kuwa ni afadhali ya Prof. Luhanga kuliko huyu wa sasa. Nakumbuka mimi jinsi Luhanga alivyokuwa makini kumaliza migogoro ya wanafunzi. Prof wangu Mukandara nadhani has to learn kutoka aliyemtangulia. Kufukuza wanafunzi haijawahi kuwa sulhisho miaka nenda rudi. Hatujifunzi?
Nadhani katika mijadala ya kitaifa mingi tunayohitaji ni pamoja na huu wa elimu ya juu.