Just in: UDSM wafukuzwa

The government should not pay or provide free university education. When university students graduate they all want to go overseas to look for greener pastures so to speak. They do not want to stay and help build or serve the country. So in effect if Tanzanian taxpayers are subsidizing the economies in other countries like Botswana, South Africa, Europe and USA where these graduates eventually end up. This is particularly true for Medical students. I know the salaries in Tanzania are low but if you stick around eventually you will end up making a good living in maybe 10 years or even less if you have your education.

Manji Supporter aka Raj Patel aka Ukweli aka Ngrh8tr
 
Jamani mimi kwa maneno machache naweza kusema ni kuwa hakuna kitu kikubwa serikali inaweza kuwafanyia watu wake kama kuwapatia Elimu. Na hakuna nchi ambayo inaweza kundelea bila kuwa na human capital. Human capital sio elimu ya msingi bali ni elimu ya juu hapa si maanishi kuwa elimu ya msingi sio muhimu bali ni haki ya kila mmoja. Na wala siamini kama kweli serikali inashindwa kuwapatia hiyo asilimia 100% ya mkopo. Cha msingi ni serikali iandae mikakati mashuhuri ya ukusanyaji wa hii mikopo na naamini hii inawezekana kwa asilimia 70 au hata zaidi.

Kitendo cha serikali kushindwa kukaa na vijana na kujadili ni aibu kubwa na ni utumiaji wa mabavu usio na maana. kama sisiemu (CCM) waliweza kaa na CUF na kufikia muafaka wanashindwa je kujadili na hawa vijana? mimi nauhakika kabisa watanzania wengi hawawezi kulipa hiyo 40% ambayo ni sawa na 500,000. Kama hawa wazazi walishindwa kuwalipia ada ya msingi na Sh 70,000 za sekondari je wataweza kulipa laki tano? Huu ni mzaha. Sisi kila siku tunaona pesazetu walipa kodi zinatumia vibaya kwa ubadhilifu. Tumeona masemina, maritrit, maworkshop yasio na msingi yanafanyika kwenye Mahoteli ya kifahari. Mf maandalizi ya Budget maofisa wa Hazina wanakaa Kunduchi beachi zaidi ya mwezi mmoja je haya ni matumizi muhimu kuliko kuwapatia vijana wetu elimu?

Sasa wanafunzi wamefukuzwa lakini bado pesa ya mlipakodi masikini aliyebana mkanda kwenye tumbo yake yene njaa inaendelea kugharamia uendeshaji wa shughuli za chuo kama utawala, mishahara, umeme nk. Je hii ni kwa manufaa ya nani. Sisi wengi tulikumbwa na haya lakini mimi namalizia kwa kusema tunahitaji kuwapatia wananchi wetu elimu, tunahitaji wasomi ili tuweze kuondoa umasikini, tunahitaji wasomi ili tufikie MDG, tunahitaji wasomi ili tupunguza wimbi la uhalifu. Ni jukumu la serikali kuwapatia wananchi wake elimu. Tunatumia pesa ngapi kwa mashangingi ya serikali? tunatumia pesa ngapi kwa safari za viongozi na maofisa wa serikali safari zisizo na manufaa? tunatumia pesa ngapi kwa alowace za wabunge? Mimi na sema serikali ina uwezo kabisa hii ni kukwepa majukumu.

Wadogo zangu wanachuo walio vaa mashati ya CCM yenye nembo ya jembe na nyundo kule diamond jublee sasa ndio wanaona kuwa walidanganywa. Anywa siku hizi cuo kikuu ni kambi ya CCM tunajua malecturer wanagombana kwa sababu ya UCCM, baadhi ya wanafunzi walipata scholarsip za MA especialy Economics kwasababu ni wana CCM. Cha msingi kama kweli JK aliwaahidi kwanini aiswatimizie ahadi alizotoa? KUWAFUKUZA SIO KUTATUA TATIZO BALI NI KUAHIRISHA TATIZO.


Hoja hujibiwa kwa hoja.
 
SUA nao watimuliwa
Hosteli Mabibo 'walizwa' mizigo yao
NA LATIFA GANZEL, MOROGORO

HATIMAYE wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) wa mwaka wa kwanza na wa pili wamesimamishwa masomo yao kwa muda usiojulikana kutokana na mgomo uliofikia siku tatu tangu Aprili 16, mwaka huu.
Wakati hayo yanatokea, baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, wanaoishi katika hosteli za Mabibo, wameripotiwa kuibiwa mali zao na wenye mikokoteni, wakiwa katika pilikapilika za kuondoka baada ya kusimamishwa masomo.
Kwa upande wa wanafunzi wa SUA, walikutana na majibu hayo baada ya kuandamana kwa kutembea kwa miguu umbali wa kilomita 10 kutoka kampasi yao ya Solomoni iliyopo Mazimbu hadi eneo la utawala la chuo hicho lililopo kata ya Mbuyuni.
Kutokana na hali hiyo, wanafunzi hao walipofika eneo la utawala saa 9 alasiri huku wakiwa wamebeba mabango, walikuta Baraza la chuo hicho limeamua wawe wameondoka chuoni hapo jana saa 12 jioni huku chuo hicho kikiwa chini ya ulinzi wa polisi kuhakikisha kuwa amani haivunjwi.
Baadhi ya mabango waliyokuwa wamebeba wanafunzi hao, yalikuwa na ujumbe wa kutaka wazazi wawaunge mkono, pia kudai uchaguzi wa mwaka 2010 utakuwa mgumu, mwingine ulikuwa ukidai wazazi wao hawana uwezo wa kuwalipia asilimia 40 ya gharama.
Wanafunzi hao wakati wakitoka Mazimbu kuelekea SUA, walikuwa wapatao 2,000, lakini cha kushangaza walikuwa wakipungua kadri walivyokuwa wakikaribia eneo hilo la utawala kwa kuhofia polisi waliokuwa wametawanywa kila eneo la chuo hicho.
Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo hicho, Omari Ali, alisema uongozi wa wanafunzi uliamua kufanya maandamano kutokana na kwamba chuo hicho kilitoa tamko kuwa ifikapo Aprili 27, kila mwanafunzi awe amamaliza asilimia 40 kama ilivyotakiwa.
Mgomo huo wa wanafunzi ulianza Aprili 16, mwaka huu ambapo wanafunzi hao walidai sio mgomo bali ni majadiliano kuhusu maslahi yao jambo ambalo lilifanya uongozi wa chuo hicho kuona kama ni hali ya kawaida.
Juzi, wanafunzi hao walipotakiwa kuingia darasani walidai hawawezi kuingia hadi wajue hatma yao kuhusu asilimia 40 ya gharama za uchangiaji na kuongezwa kiwango cha posho za matumizi ya siku wakiwa katika mazoezi ya vitendo ambayo ni sh. 6,000 hadi ifikie sh. 10,000 kama ilivyoongezwa ya matumizi ya kila siku wakiwa chuoni kutoka sh. 2,500 hadi kufikia sh. 3,600.
Wakati huohuo, baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, wanaoishi hosteli za Mabibo, wameripotiwa kuibiwa mali zao na wenye mikokoteni, wakiwa katika pilikapilika za kuondoka baada ya kusimamishwa masomo.
Uamuzi wa kuwasimamisha masomo ulifikiwa juzi na Baraza la chuo hicho, kufuatia mgomo wa wanafunzi hao uliodumu kwa siku mbili mfululizo wakitaka kuondolewa uchangiaji wa gharama za masomo.
Habari zilizopatikana katika hosteli ya Mabibo zilidai kwamba wizi huo, ulisababishwa na kutokuwepo kwa umakini wa ufuatiliaji wa mizigo hasa kwa wanafunzi waliokuwa wakitumia mikokoteni ya kukodi kuondoa vifaa vyao.
Mmoja wa walinzi wa kampuni ya Full Time Security, ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema wengi wa wanafunzi hao, walikuwa wakihaha kusaka mizigo yao, baada ya wenye mikokoteni kutoweka nayo.
Alisema wengi wao walikuwa wakifika katika eneo la lango kuu na kuulizia iwapo wamewaona vijana waliowakodisha kuchukua mizigo, hali iliyowawia vigumu askari hao kuwatambua.
Kwa mujibu wa askari huyo, pia hali ya msongamano na giza ilichangia kujitokeza kwa upotevu wa mali za wanafunzi hao.
"Kwa kweli ilikuwa inatuwia vigumu kuwasaidia maana utakuta mtu anakuuliza umemuona mtu mwenye mzigo wangu?, alisema askari huyo na kuongeza kuwa ugumu huo ulitokana na msongamano wa wanafunzi waliokuwa wakitoka na mizigo yao.
Katika eneo la kampasi ya Mlimani, Ofisa Uhusiano wa Chuo Kikuu, Julius Saule, alisema hali ni shwari na kwamba wanafunzi walengwa waliondoka kama walivyoamriwa.
Hata hivyo, hakutaka kuzungumzia zaidi hatua zinazofuatia baada ya wanafunzi hao kuondoka kwa maelezo kwamba siyo msemaji.
Wanafunzi hao pamoja na vyuo vishiriki vya Ardhi na Usanifu Majengo (UCLAS), Elimu Mkwawa (MUCE), Elimu Dar es Salaam (DUCE) na Taasisi ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (IJMC), waliamrishwa kuondoka juzi ifikapo saa 12 jioni baada kukaa kuingia madarani licha ya uongozi wa chuo kuwasihi kufanya hivyo.
Katika madai yao wanafunzi hao wanalalamikia malipo ya sh. 3,600 badala ya sh. 6,000 kwa siku kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo ambayo wanadai hailingani na mahitaji halisi.
Pia wanataka kuondolewa kwa sera ya uchangia wa asilimia 40 ya gharama za masomo ya elimu ya juu, wakidai kwamba wanafunzi wengi ni masikini na hivyo itawawia vigumu kuchangia gharama hizo.

Source: Uhuru
Hii ni aibu kabisa,

Inaonekana kama elimu ya juu siyo moja ya priorities za nchi. Kwa ushauri wangu ni afadhali majengo ya vyuo vikuu yauzwe kwa "wawekezaji" yabadilishwe kuwa Hoteli za Kisasa. Uwezo wetu wa kuendesha elimu ya juu kwa raia wetu bado ni mdogo sana na hasa kwa vile elimu ya juu kwa raia wetu haijawa kitu cha muhimu kutokana na kuwa tunaweza kupata wataalamu kutoka Norway.
 
Ndugu Zangu Napata Presha ,sijui Kama Wanangu Watasoma Tena.....just In: Mmesikia Masharti Yaliyotolewa Na Prof Rwekaza Ya Watoto Kurudi Chuoni.........moja Ya Sharti Ni Waje Na Barua Iliyoambatana Na Bank Slipi Watakayokuwa Wamelipia Bank Ile 40% Ya Cost Sharing...including Laki Moja Ya Matibabu....out Of That Au Kama Mtu Hana Hizo Asiweke Mguu Chuoni..

Mbona Muungwana Amefanya U Turn Na Kutusahau Namna Hii ,masharti Gani....wangapi Watamudu???
 
Mbona Muungwana Amefanya U Turn Na Kutusahau Namna Hii ,masharti Gani....wangapi Watamudu???

Wahenga walisema mtoto akililia wembe mpe. Mwezi wa kumi na mbili mwaka 2005 tulilia wembe tukaupata. Sasa umeanza kutukata vidole vyetu wenyewe: tutakoma.
 
Wahenga walisema mtoto akililia wembe mpe. Mwezi wa kumi na mbili mwaka 2005 tulilia wembe tukaupata. Sasa umeanza kutukata vidole vyetu wenyewe: tutakoma.

Miezi mitatu iliyopita alisema angelishughulikia hili swala na wanafunzi wakiwa na magwanda ya Chama Tawala wakipiga vigelegele walichoshau ni kuuliza atalishughulikiaje?Kichuguu hiyo ndiyo jeuri ya Ushindi wa kishindo aka tsunami 80%.
 
Jamani hii inasikitisha sana kweli tuanajenga taifa la aina gani? Hivi kweli Mzazi wa kule kwetu Nkasi anaweza kupata wapi 640,000 kwa ajili ya kijana wake? wengine hiki kiasi huwa wanakiona kwenye maandishi tuu sasa kweli elimu ni kwa matajiri tuuu. Mimi nadhani hawa waliotoa huu uamuzi wamefilisika kiungwana na hawana uzalendo. Hapa no doubt kuwa watoto wa wakubwa tuu ndio wataenda university. Mimi naone msemo wa ELIMU KWA WOTE si sahihi inabidi iwe ELIMU KWA WATOTO WA WAKUBWA.
 
Jamani hii inasikitisha sana kweli tuanajenga taifa la aina gani? Hivi kweli Mzazi wa kule kwetu Nkasi anaweza kupata wapi 640,000 kwa ajili ya kijana wake? wengine hiki kiasi huwa wanakiona kwenye maandishi tuu sasa kweli elimu ni kwa matajiri tuuu. Mimi nadhani hawa waliotoa huu uamuzi wamefilisika kiungwana na hawana uzalendo. Hapa no doubt kuwa watoto wa wakubwa tuu ndio wataenda university. Mimi naone msemo wa ELIMU KWA WOTE si sahihi inabidi iwe ELIMU KWA WATOTO WA WAKUBWA.
Ninawapa pole walalahoi wenzangu Kama kweli serikali itashikilia msimamo wake kwamba atakayelipa ndiye atakayerudi chuoni basi wasionazo watakuwa wamewafukuzisha Chuo na Hii inauma sana hasa kwa wale masikini wenye uwezo Kiakili waliokuwa na ndoto ya kusoma kwa bidii ili kesho wawasaidie waliowazunguka na hata taifa,Umasikini wao ndiyo itakayoua ndoto yao hiyo kwasasa.Eeh Mungu Muumba wasaidie waja wako wanaohitaji msaada wako kwani wewe ndiye uwajuwao vyema!
 
The government should not pay or provide free university education. When university students graduate they all want to go overseas to look for greener pastures so to speak. They do not want to stay and help build or serve the country. So in effect if Tanzanian taxpayers are subsidizing the economies in other countries like Botswana, South Africa, Europe and USA where these graduates eventually end up. This is particularly true for Medical students. I know the salaries in Tanzania are low but if you stick around eventually you will end up making a good living in maybe 10 years or even less if you have your education.

Ndugu yangu, are you serious? That one should wait around for 10 solid years to have a decent living? Umeangalia life expectancy ya Mtanzania kweli..mtu anamaliza chuo akiwa mtu mzima mwenye watoto kutokana na usomi wa ki-ukulima ukulima..yaani huanzi shule hadi baba adundulize vihela vya pamba/korosho/kahawa..By the time unakwenda shule u mtu mzima kabisa , ndo maana wanafunzi wengi katika vyou vya Tz wako married. Now, a graduate has responsibilities kwake yeye mwenyewe, kwa mke/mme na watoto, kwa wazazi, kwa the extended family you can think of; and you expect him to stick around like a nun waiting for a miracle...Please, tuwe realistc... Our people are looking for greener pastures outside the country not because they like, they are forced to: Katika wooote walio nje ya nchi, kwa upeo wangu mdogo nadhani hakuna ambaye akipewa nafasi kama aliyonayo huko pamoja na mazingira ya kuishi sawa na hayo hapa nyumbani atakataa kurudi..some of them are doing donkey work..its not like they enjoy it, they enjoy the pay and everything that goes with it. Inakuwa afadhali mtu kwenda kufanya kazi za ajabu ajabu nje upate unachotaka kuliko kukaa hapa bongo na kazi iwe ya ajabu iwe ya maana hupati..na maji huna, na umeme huna, na wanao wanakutole macho, na wazazi nao wanasema ya nini alisoma kama hawezi kutusaidia na kusaidia ndugu zake...I tell you, given an opportunity I will ran like crazy..niachane na hii shida ya bongo...Siamini kama ni sahihi kuwalaumu wasomi kutafuta kazi nje; na wala siamini kama hicho kitakuwa ni kigezo cha haki cha kufanya serikali isiwalipie. Istead, serikali inatakiwa ijenge mazingira mazuri ambayo yatawavutia watu/wasomi wabaki hapa nchini.

Hebu jaribu kukumbuka enzi zile serikali for some reasons iliamua kujaza the so called TX hapa nchini; wakaja ma-tx ambao hawajawahi kuona darasa kwao, bado wakapewa vyeo kuwaongoza wasomi kweli wa TZ, wakati hao wasomi wetu wanalipwa about 50 thousand or so Tshs, hao ma -tx walikuwa wanalipwa thousands of dollars plus a helluva allowances..usisahau gari lililoandikwa "TX"..I mean, hii tabia ya kudharau wasomi wetu ndo inawakimbiza,
hakuna mtu ana-enjoy kuishi kwenye nchi za watu..hebu soma ile shairi ya MKJJ inayosema 'Nilidhani peponi'..this is what we find there, but we stick around cos the end justifies the means..at least ukiwa nje utakusanya tu-dollar au tu-pound ukiwatumia home wanakuona Mungu, wakienda kusali wanakuombea..wakati uking'ang'ania bongo wanakuona msomi-chizi

Kwanza mimi nitawashangaa wasomi walioko vyuoni ambao visheni yao imeishia within the four corners of TZ..let the go out and see the other side of the moonlight! Hata Jeikei alisema '..mnataka tukae wote hapa tukiangalia umaskini wetu tugawane mihogo!.."
 
Mimi naunga kabisa mkono wasomi wanaoenda kufanya kazi nje. Kuna nchi kama Philipine large % of their GDP inatokana na remitance kutoka kwa watu wanaoishi na kufanya kazi nje ya nchi. Pesa nyingi za kigeni za nchi ya India na Philipine zinatoka kwa wananchi wanao fanya kazi nje. Hata wawekezaji wengi wa Kichina nchini mwao walikuwa nje ya nchi. Tofauti na pesa lakini pia wasomi hawa wanapata ujuzi kutoka huku nchi za watu. So, serikali ni jukumu lake isomeshe watu wake hata kama wengine wanaenda nje ya nchi. After all kipato cha wasomi wa Tanzania ni cha chini sana kulinganisha na huko wanakoenda kufanya kazi kama Botswana.
 
mnaonaje tukamrejesha mjerumani?

maana kuna mshauri mmoja alisema

mjerumani katili lakini hakutuhini
chai ilo na sukari tena sabuni laini
leo iweje kwa shari foleni kila dukani?

kama nitakuwa nimequote vibaya nisamehewe ni masiku mengi toka nilipousoma shule, huyu aliona mjerumani alikuwa bora kuliko huu uhuru na nyie mnasemaje?//////////////////
 
Yeah, Thats a cowardly way of handling the situation, though
its much easier to use someone's brain and when the going gets tough you bear no blame..ni hao wakoloni...
 
Nawapa pole sana vijana wetu. Lakini nafikiri ni vizuri wakatumia walkati huu kutafakari nafasi na mchango wao katika jamii ya watanzania. Vyuo vyetu lazima viwe chachu na changamoto katika kuchambua namna nchi yetu inavyoendeshwa.Lazima waongoze katika kujenga jamii ya KITANZANIA isiyo na woga, na yenye kujikomba kwa viongozi wa serikali. Mie kwa sasa sioni tofauti kati Vyuo vikuu vyetu na wanafunzi wa shule za msingi.Mambo mengi ndani ya nchi yanakwenda mrama lakini wao wako kimya kama vile hawapo.Wanakuwa wakali pale wanapoona posho zao zinabana kiasi cha kutowawezesha kwenda kulamba bia na kujirusha viwanja.
Kuna mjumbe alisema kweli kuwa "wamejitenga sana na jamii" Wamekuwa wabinafsi.
Sasa hiyo 100,000/- na 40% wanatakiwa wawaombe wazazi wao ambao wanaendelea kuishi katika umasikini mkali unaosababishwa na uendeshwaji mbaya wa serikali ya JK.
Siku walipovaa majani ya mgomba walifanya hivyo ili kujikomba kwa JK ili aweze kuwapatia pesa wanaliokuwa wanahitaji.
 
The government should not pay or provide free university education. When university students graduate they all want to go overseas to look for greener pastures so to speak. They do not want to stay and help build or serve the country. So in effect if Tanzanian taxpayers are subsidizing the economies in other countries like Botswana, South Africa, Europe and USA where these graduates eventually end up. This is particularly true for Medical students. I know the salaries in Tanzania are low but if you stick around eventually you will end up making a good living in maybe 10 years or even less if you have your education.



Your name suggests a lot ..............................

Wherever a Tanzanian go he will continue to contribute immensely in the economy of Tanzania, may be you are still in a box to understand.
 
Bwana Manji Supporter wewe upo kwenye dunia ipii? Hivi kweli watanzania wanafanya kazi nje ya nchi ni hasara?

Mimi naunga kabisa mkono wasomi wanaoenda kufanya kazi nje. Kuna nchi kama Philipine large % of their GDP inatokana na remitance kutoka kwa watu wanaoishi na kufanya kazi nje ya nchi. Pesa nyingi za kigeni za nchi ya India na Philipine zinatoka kwa wananchi wanao fanya kazi nje.

Hata wawekezaji wengi wa Kichina nchini mwao walikuwa nje ya nchi. Tofauti na pesa lakini pia wasomi hawa wanapata ujuzi kutoka huku nchi za watu. So, serikali ni jukumu lake isomeshe watu wake hata kama wengine wanaenda nje ya nchi. After all kipato cha wasomi wa Tanzania ni cha chini sana kulinganisha na huko wanakoenda kufanya kazi kama Botswana. Pia watu wetu wakienda kufanya kazi nje ya nnchi ni kupunguza tatizo la ajira nnchi. Nchi nyingi wanatoa hata ruzuku kwa watu wao wende nje kufanya kazi na China ni mfano.
 
Chancellor wa UDSM ni nani kwa sasa?

Nini kazi za Chancellor?

Mara nyingi anakuwepo chuo kikuu wakati wa sherehe za kutunuku shahada na stashahada, lakini wakati wa matatizo [migomo] huyu jamaa hasikiki kabisa, kama analipwa mshahara kwa pesa ya walipa kodi kwa maoni yangu sioni kama tunatendewa haki sisi walipa kodi.

Tunamuomba atoe tamko
 
The government should not pay or provide free university education. When university students graduate they all want to go overseas to look for greener pastures so to speak. They do not want to stay and help build or serve the country. So in effect if Tanzanian taxpayers are subsidizing the economies in other countries like Botswana, South Africa, Europe and USA where these graduates eventually end up. This is particularly true for Medical students. I know the salaries in Tanzania are low but if you stick around eventually you will end up making a good living in maybe 10 years or even less if you have your education.

Ninafahamau watu wengi wa WTZ walioko ughaibuni wanaopeleka pesa nyingi sana huko nyumbani kusaidia ndugu zao kukabiliana na maisha magumu. Nina imani kuwa huo ni mchango mkubwa sana wa WTZ walioko nje. Wengine wanatumia mapato yao ya nje kuwekeza pale nyumbani. Hii Kasumba ya kuchukulia kuwa kila aliyeko nje ni mbaya ndiyo inayopelekea watu kupinga uraia wa nchi mbili na vile vile kuzuia raia wenye haki ya kikatiba wasipige kura eti kutokana na mahali wanapokaa. Ni kasumba iliyopitwa na wakati.

hebu fikiria watanzania wote walioko nchi za nje wakirudi pale Tanzania, serikali itawapa kazi gani kulingana na utaalamu wao. Kama madakitari wachache tu wa Muhimbili serikali iliamua kuwafukuza na kuona kuwa hawana umuhimu, je itakuwaje kame madakitari wote walioko nchi za nje wakirudi?

Nadhani kuwa furaha ya watu wa kasumba kama yako ni kuona kuwa watanzania wote wanarudi TZ ili muweze kuwadhihaki kama Dr. Massau aliyeamua kurudi Tanzania kutumia ujuzi wake kwa watanzania baada ya kuwa amekaa nchi za nje lakini leo hii serikali inamdhihaki.
 
Wabunge wataka mabadiliko katika sheria ya mikopo
*Wataka wanafunzi wote wapewe
source mwananchi
Na Midraji Ibrahim, Dodoma

KUFUTIA mgomo wa wanafunzi wa vyuo vikuu, Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, imependekeza sheria ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kupelekwa bungeni kwa ajili ya kufanyiwa marekebisho kwenye maeneo yaliyoonyesha udhaifu.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Omar Kwaang' alisema ili kuleta ufanisi katika kusimamia, kutoa na kurejesha mikopo ni bora sheria hiyo ichambuliwe na kuainisha maeneo yenye utata, upungufu au udhaifu yaweze kufanyiwa marekebisho.

"Serikali ilete marekebisho ya sheria namba 9 ya 2004 ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ambayo yatazingatia hoja zilizoainishwa na kamati na kuzingatia maoni ya wadau wa elimu," alisema Kwaang' na kuongeza:

"Kwa kuzingatia maoni ya wadau hasa wazazi na wanafunzi na hatimaye kuleta ufanisi katika kutoa mikopo na kuondoa matatizo yaliyojitokeza tangu utekelezaji wa sheria hiyo kuanza."

Pia, kamati hiyo ilipendekeza serikali kufanya utafiti wa kina kwa takwimu na kupata maoni ya wananchi kwenye maeneo ya watoto wengi ambao wazazi wao hawana uwezo, sio rahisi kupata daraja la kwanza au pili ambayo yanapata ufadhili wa serikali.

Kwaang' alikuwa akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo bungeni juzi.

"Kawaida ambako kuna miundombinu duni ikiwa ni pamoja na walimu wachache, kutokuwapo maabara, vitabu, samani wanafunzi wanaoandaliwa katika mazingira hayo si rahisi kufaulu mtihani katika daraja la kwanza na la pili na wale wanaofaulu ni wachache sana na hao watakuwa wale wenye vipaji maalum. Wadau wanadai kuwa utaratibu huu unawaondoa moja kwa moja kupata mikopo," alisema.

Alisema mwelekeo wa serikali kutoa mikopo kwa waliofaulu kwa madaraja hayo, utawafanya wanafunzi kuacha masomo ya sayansi ambayo kwa kawaida ni magumu kupata madaraja hayo na kukimbilia mengine ya sanaa, hali itakayozua tatizo la uwiano wa wataalam na sekta ya sayansi na teknolojia itaathirika.

Kwaang' alisema, kuchanganya vigezo vya umaskini na kufaulu ni kuleta matabaka na madaraja katika jamii kwa sababu, wananchi wengi wa vijijini ni maskini na matajiri wako mijini ambako mazingira ni mazuri kumsaidia mtoto.

"Hali hii itawagawa wazazi waanze kutafuta shule nzuri zaidi popote ili hatimaye watoto wao wapate daraja la kwanza na pili kuwawezesha kupata mikopo. Serikali itafute motisha nyingine kwa wanafunzi watakaofanya vizuri katika masomo," alisema na kuongeza:

"Maoni ya wadau yafanyiwe utafiti wa kina kwa takwimu za motisha ili kuepuka hali ya kutoelewana katika jamii tukizingatia tofauti iliyowahi kutokea kati ya maamuzi ya serikali na maoni ya wadau pale serikali ilipofuta baadhi ya masomo na serikali baadaye kukubaliana na maoni ya wananchi."

Kuhusu mikopo ambayo haijarejeshwa, Kwaang' alisema, baadhi ya wakopaji wanafunzi wanaona mikopo ni sehemu ya misaada au chanzo cha mapato kutoa serikalini kwa ajili ya masomo yao.

Kamati hiyo imebaini uwezo mdogo wa utendaji wa bodi na taarifa zisizo sahihi zilizotolewa na wanafunzi, umechangia bodi kushindwa kufanya tathmini wa wanaostahili na wenye uwezo.

"Taarifa ya bodi inadhihirisha kuwa wanafunzi wanaotoka kwenye familia zenye uwezo walipewa mikopo na baadhi ya wanafunzi walipewa mkopo mara mbili," alisema Kwaang'.

Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Prof Rwekaza Mkandala alisema Februari 3, mwaka huu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Rais Jakaya Kikwete, alieleza wazi kuwa Serikali inatafuta namna ya kutatua tatizo hilo, lakini wasitegemee kutatuliwa katika kipindi cha mwaka huu wa fedha.

Hata hivyo, ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ya Machi inaonyesha kuwa serikali mpaka Februari mwaka huu ilitumia zaidi ya bajeti yake Sh900 bilioni.

Kama kilio cha wanafunzi wanaosoma katika vyuo vikuu cha mikopo ya elimu ya juu kuwa asilimia 100 kingesikilizwa, serikali ilitakiwa kuongeza kiasi cha Sh93 bilioni kwenye fedha zilizoombwa na Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi.

Kwa mujibu wa taarifa za Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu, Prof. Peter Msolla, Bodi ya mikopo ilomba Sh140 bilioni kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi, lakini ikapewa Sh63.5bilioni na kisha ikaongezewa Sh47.8bilioni ambazo serikali ilikopa katika mabenki ya ndani na hivyo kufanya kiasi cha fedha zilizotolewa kwa ajili hiyo kufikia Sh111.3 ambazo ni karibu asilimia 80 ya maombi ya bodi hiyo.

Serikali iliongeza mikopo kwa wajasiriamali kutoka Sh500 milioni kwa kila mkoa zilizotangazwa bungeni mwaka jana na Waziri Mkuu Edward Lowassa kufikia Sh1bilioni baada ya Rais Jakaya Kikwete kutangaza nyongeza ya Sh500 milioni akiwa mkoani Mara.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom