Just in: UDSM wafukuzwa

Watawala kuweni serious na ishu za kitaifa, historia ni mwalimu mzuri sana, kama mtakumbuka wakati wa wimbi la vibaka hasa mjini Dar es Salaam, kila kibaka akikamatwa na kufikishwa polisi kesho unamkuta mtaani akiendelea kupora watu, wnanhi wakachoka kila kibaka alipokamatwa hakupewa fursa ya kufikishwa polisi anahukumiwa kwa kupigwa mawe na kuchumwa moto.

kwa maamuzi ya Vilaza kama Pro-confuser mkandara, msistaajabu kuona watanzania kuchoshwa na kuanza kuwapiga mawe na kuwachoma moto, hili linawezekana msiseme mimi ni mchochezi.
 
Inauma jamani...hivi tumemkosea nini Mungu sisi mpaka anatupa viongozi wa namna hii...??

Tumewachagua wenyewe, tusimsingizie Mungu. Ni sawa na mtu kuacha kutumia kondomu, akipata UKimwi anaanza kumlaumu shetani. Ni sisi wenyewe. Unakumbuka tulivyobishana kule bcs. Tuliokuwa tunamtetea SAS tukaambiwa sio wazalendo kwa kutetea waarabu! Haya sasa huyu mzalendo wenu vipi na mauzauza yake!

Wakati mwingine inakuwa vigumu hata kuwahurumia hawa vijana wa vyuo vyetu. Wao walipata nafasi nzuri ya kuitwa kuongea na JK pale Diamond Jubilee. Badala kuandaa ajenda na hoja za maana, wakajiandaa kwa kupiga pasi magwanda ya kijani na kofia za njano za CCM. Matokeo yake wakaishia kummiminia JK misifa. Naye kama kawaida yake, akawapa tabasamu zito, kisha akawaambia "matatizo yenu nimeyasikia, yatafanyiwa kazi"! Walivyo mazuzu, wakacheka hadi gego la mwisho, wakabambikizwa mikadi ya kijani hao! Sasa nasema wakati mwingine, matatizo yetu ni makubwa kuliko yanavyoonekana nje. Kuna shida kwenye mfumo wa elimu. Elimu tunayoipata katika mfumo wetu ni elimu inayozalisha woga na comformist wa ajabu sana. Ndio maana hata maprofesa wetu wanaishia kutoa vitisho badala hoja za kiprofesa! Tuna shida kubwa sana, Mungu tu ndio anayejua!
 
Hao wafanyakazi wanaendelea kufanya kazi na kulipwa for whose benefit while in the real sense chuo hakifanyi kazi? Kweli sasa naanza kuamini maneno ya Jeikei to the extent that hasara nyingine tunazipata kwa "kutokuwa na wataalam"

Kazi za walimu wa chuo kikuu ni: kufanya utafiti, kutoa ushauri wa kitaalamu na kufundisha. Kutokuwepo wanafunzi haina maana kazi zimekwisha, ni kazi moja tu hiyo!
 
Mwanasiasa:

Nakubaliana nawe. Wanachuo wanausaliti wa aina nyingi. Lakini hatupaswi kuutumia udhaifu wao kuhalalisha maamuzi mabovu ya serikali yenye athari kwa wanachuo wa kesho(watoto wetu) na maslahi ya taifa(yatakayotokana na madhara ya wanachuo wa sasa kuathirika).

Maswali ya kujiuliza:

1. Serikali ilikuwa wapi toka mwaka jana malalamiko haya yalipoanza? Toka Kikwete atoe ahadi Feb 3 hatua gani zimechuliwa? Leo wanafunzi wanalalamika kama wamekurupuka!

2. Kwa nini chuo kimefungwa kwa ghafla(less than twelve hours wanafunzi watawanyike hata wale wa mikoani) wakati ambapo hakukuwa na uvunjaji wowote wa amani? Kwa nini subira ya siku tatu kama utaratibu unavyohitaji haijazingatiwa?

3. Wanasema 40% inawahusu 1st years pekee, kivipi wakati 2nd years wameshapewa posho yao ya field badala ya 6,000 wamepewa 3600? Je wataweza kwenda kwenye mafunzo ya vitendo kwa utaratibu huu.

4. Wanasema serikali iliahidi mwezi wa nane ingeshughulikia. Another lie. kauli ya Msola ilihusu grades za kudhamini na si 40%. Hata kama ingekuwa kweli ni mwezi wa nane, vipi hawa wanapaswa kwenda field kabla ya mwezi wa nane?


Likini kinachonisikitisha ni kwamba Chuo kimeingia katika bandwagon ya kuwa tool ya serikali ya kufanya propaganda kuwa madai ya wanafunzi hayana msingi na kwamba wamekurupuka. Hii ndio huduma ya kufunisha, consultancy na utafiti inayotolewa na chuo.

Kinachonisikitisha ni kwamba madai haya yameanza kupewa picha kuwa ni ya wanafunzi pekee wakati ni yake mzazi mwenye mtoto udsm, ni yako mtanzania mwenye mtoto anayetaka afike UDSM, ni yako mwananchi unayetaka mtalaamu etc etc....i expected more voice.....more action.....

Kwa kifupi suala hili lina muhusu zaidi mtanzani yoyote mwenye kipato cha chini ya laki 5 kwa mwezi kuliko viongozi wa serikali

JJ
 
Labda serikali itueleze instead(na hii ndio problem yangu na wanafunzi wa vyuo-wanashindwa kutoka nje ya box na ku-widen demands!)- kama hakuna hela:

1. Vipi serikali imetumia bilioni 900 mpaka sasa ziada ya bajeti?

2. Vipi ikulu imetumia bilioni 54?

3. Pesa ya RADA bilioni 24(sio 12) ziko wapi?

4. Mbona tumesamehe kodi billioni 400 kwa muda mfupi?

5. Kwa nini mkataba wa richmond wa bilioni 272 bila umeme? (Tayari tumealipa dowans takribani bilioni 123).

Na hawa wote tumewalipa. Hatujawakopesha. Kwa nini tushindwe KUKOPESHA wanafunzi 40%?

JJ
 
Maoni ya Mhariri wa Habari leo yalinishangaza zaidi. Gazeti hili pamoja na kuwa ni la serikali lilianza vizuri. Lakini kwa maoni ya hivi karibuni kuhusu Mgomo wa UDSM yamenifanya nihoji kama kweli litakuwa ni chomo cha kuhudumia wananchi au ni mdomo tu wa serikali! Maoni yalibeba kichwa Migomo ya nini zama hizi za uchangiaji?

The fact they missed ni kuwa tulichonacho Tanzania hivi sasa kwenye elimu ya juu kwa mtindo huu si cost sharing(uchangiaji) ni ubebaji(cost bearing) wa gharama za elimu.

Kama mwanafunzi anakopeshwa 60% halafu anatakiwa kulipa mwenyewe 40%, kitu gani hapa ambacho serikali ina-share?

Binafsi sipingi dhana ya serikali kukopesha: ila kama hakuna utaratibu wa ku-assess needs then u-assess the capacity to repay, ukishafanya hivi(which they do kwa dhamana ya barua mbalimbali) then mkopeshwaji akopeshwe 100% atimize mahitaji yake.

In any case, hii ni revolving fund. Kama wakopeshaji watarudisha eventually, So kinachotakiwa ni initial major investment from the government or even banks.(ingawa hii hai-appply Tanzania kwa kuwa hakuna interest)!

Na mtizamo wangu ni kuwa wenye daraja la kwanza na best perfomers vyuoni wasikopeshwe 100%. Wakopeshwe only 60 or 40% percent. Zingine ziwe government grant. Ni njia moja ya kuthamini talents to kutoa motivation!

JJ
 
Inasikitisha kuwa maamuzi yanayohusu hatima ya elimu ya watoto wetu yanafanywa kisiasa. Tatizo la mikopo kwa wanafunzi sio gumu kama wanavyotaka tuamini. Binafsi ni suala la sera zisizo na kipaumbele. Ilani ya Uchaguzi ya CCM (2005-2010) inasema hivi kuhusu suala hili:

63: Katika kipindi cha 2005-2010, CCM itazielekeza Serikali kuchukua hatua zifuatazo:-
.....

(d) Kuweka utaratibu wa kutumia Mfuko wa Mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu ili wanafunzi wengi zaidi waweze kufaidika na Mfuko huo.


Sasa hadi hii leo, ni utaratibu gani unaoelewekwa uliowekwa ambao unahakikisha "wanafunzi wengi zaidi" wanafaidika na mfuko huo? Kwanini tusije na sera inayoeleweka kuhusu mikopo ya elimu ya juu?

Hatuwezi hata kidogo kuendelea kwa haraka kama tunaikwaza sekta ya elimu ya juu. Viongozi ambao wameiongoza Wizara ya Elimu ya juu wameshindwa kabisa kutatua matatizo ya wanafunzi hadi Rais kuingilia kati. Leo hii, bado tunakimbilia Ikulu, hawa kina Msolla, Mama Katunzi, na wengineo kama wameshindwa wakiri na kuandika barua za kujiuzulu. Haiwezekani chini ya uongozi wao matatizo ambayo tulidhani yameisha miaka ya 90 bado yanaendelea!

Kama hii inayotolewa ni mikopo na si hisani na wanafunzi wako tayari kukopa, kwanini wasikopeshwe? Hata kama serikali haina nia (najua inao uwezo) wa kukopesha kwa asilimia mia moja, basi ijaribu angalau asilimia 85. Tuliofanya kazi kwenye mabenki hasa yanahusiana na mikopo ya nyumba tunajua kuwa mkopo mzuri ambao mtu mwenye credit history nzuri (najua Bongo hatuna utaratibu wa kufuatilia historia ya ukopaji) ni hadi asilimia 80 bila adhabu na wachache wanaweza kupatiwa hadi asilimia 95!

Badala ya kutegemea mikopo tu ni lazima pia tuje na unataratibu mwingine wa kuwasaidia vijana kulipia masomo badala ya kulipiwa na serikali. Walioenda kwenye vyuo vya Marekani (sijui nchi nyingine) watagundua kuwa wanafunzi wanapewa scholarships mbalimbali na mojawapo ambayo ni most common ni ile ya kufanya kazi shuleni na kulipwa. Kuna ubaya gani wa kuwaajiri wanafunzi hawa kwa kazi mbalimbali hapo vyuoni na kuwalipa kiasi kidogo badala ya kuwapa fedha za dezo? Nani anafyeka, kusafisha vyoo, madirisha n.k Kwanini kuajiri watu wa nje wakati kuna wanafunzi ambao wanaweza kufanya mambo hayo kwa kulipwa? Of course, wabongo hawatataka kusafisha vyoo kwa kuwa wao "wasomi"!

Wakati umefika kwa jumuiya za wananchi kuitisha kujiuzulu kwa Dr. Msolla na mama Katunzi ili mtanzania mwingine mwenye uwezo, mawazo mapana, na nia ya kutatua matatizo ya elimu ya juu achukue nafasi hiyo. Mlolongo wa matukio ya kukatisha tamaa elimu ya juu unachosha!!!

-Matatizo ya wanafunzi Ukraine
-Matatizo ya wanafunzi Cuba
-Mgogoro wa mikopo TZ
-Migomo ya wanafunzi
-Kubadilika badilika kwa taratibu za mikopo
-Ubadhirifu wa fedha za wizara hiyo

Hii inatosha!!
 
Kuna jamaa wa BBC London anayo majina lukuki sasa ngojea aje na yeye aeleze msimamo wako maana siku zote nimekuwa namuona anaitetea serikali ama balozi wakiguswa yeye anakuja na kufanya uchambuzi yakinifu na hili nalo njoo basi utusaidie mwana wa BBC wewe na mwana CCM mahili .
 
Mnyika: Mambo mawili ya msingi kwa maoni yangu. Mosi, Mimi naamini mgomo ni hatua ya mwisho katika kudai haki ikimaanisha kuwa hatua za kawaida za majadiliano zimeshindikana. Unapofanya mgomo unakuwa umesha-exhaust silaha zingine zote na umebaki nayo hiyo tu ya mgomo. Sina uhakika kama vijana wetu walisha-exhaust njia zote za majadiliano. Zaidi ya yote sina uhakika kama hata uwezo wa kujadiliana wanao! Ndio maana nikatoa mfano wa Diamond Jubilee. Ni wazi vijana walipoteza nafasi muhimu walipokutana na rRais Kikwete. Badala ya kuimba ngonjera za kumsifia Kikwete na CCM yake, walipaswa kumwambia ukweli kuwa sera ya CCM ya elimu ya juu ni mbovu na wangempa alternatives. In short, we expected them to address broaders issues about our higher education policy than the mere mkopo.

Pili, naamini kuwa lengo la mgomo kwa hali ya wanafunzi ni kutafuta huruma ya wananchi. Hakuna maana kama mtagoma au kuandama mkaishia kuzomewa na wananchi. Sasa, ili upate huruma ya wananchi katika mazingira ya Tanzania ambayo wananchi wengi wamelishwa limbwata la CCM na Kikwete, lazima kujipanga vizuri. Kwa maoni yangu kwa mgomo huu serikali itashinda na wanafunzi wataishia kuzomewa. Sio kwamba madai yao hayana msingi, yana msingi sana. Mimi nikisoma pale mlimani niliamini na ninaendelea kuamini hata sasa kuwa ili madai yenu yapate nguvu, lazima myape sura ya kiwananchi. Yaani muoneshe kwamba mnaandamana kwa kuguswa na jambo fulani la kijamii. Kwa mfano, mgomo kama huu unaoendelea pale mlimani ungekuwa wa maana zaidi kama wanafunzi wangekuwa wanapinga sera ya kuchangia gharama za elimu ya juu au kutaka serikali iongeze bajeti ya elimu. Lakini ilivyo leo kwa macho ya wananchi wengi ni kuwa haya madai yao yataonekena ya kibinafsi zaidi. Mnyika naomba uniambiwa, kwa njaa ya pesa iliyopo Tanzania leo hii ukimwambia mwananchi wa Kiteto, Gumanga, Kibondo, Chalinze, Keko Magurumbasi, Manzese kwa mfuga mbwa, etc, kwamba wanafunzi wanasema eti 3,600 kwa siku haitoshi, unafikiri watakusikiliza wewe au serikali? Tena RTD wataitungia mazungumzo baada ya habari utaona jinsi vijana watakavyosutwa! Huoni kwamba inabidi wanafunzi wabadili strategy za kudai mikopo yao, vinginevyo wataendelea kuonekana ni wabinafsi na serikali itaibuka mshindi tu?

That said, serikali yetu haina sera thabiti na muda mrefu ya elimu ya juu. Serikali ya CCM huwa haina uwezo wa kufikri zaidi ya kushinda uchaguzo ujao. Ili upate sera endelevu ya elimu ya juu lazima ufikirie beyond the next 5, 10,15 years. Ukweli unaouma pia ni kwamba hata sisi wapinzani hatuna sera inayoshikika kuhusu elimu ya juu. Pengine ndio maana kina mwanakijiji wana wasiwasi kama tungefanya tofauti kama tungepewa serikali kesho. Lazima sasa migomo hii ya wanafunzi itupe fursa ya kuchanganya bongo ili tuibuke na sera mbadala ya elimu ya juu. Ni vizuri sana kuwahurumia wanafunzi, lakini tukumbuke huruma pekee haisaidii sana maana haitatui tatizo.
 
mzeewa siasa nangoja yule kijana amnbaye ana majina mengi hapa yuko kule BBC Uingereza aje atueleze hapa , kesha acha kutumia jina lake kamili hapa japokuwa analo na nimegundua huwa analitumia kwa msimu sana .
 
Kuna Kitu Tuna Miss Hatutaki Kuangalia Vizuri Au Kwa Makusudi Tunapenda Kulaumu,

Hawa Vijana Kwa Maelezo Ya Mkuu Wao Wa Chuo Mh Mkandara Alisema Walinasihiwa Sana Warejee Madarasani Na Suala Lao Linashughulikiwa, Pia Huo Muda Wa Kutumika Hizo Pesa Bado Haujafika Hadi Julai Kama Sijakosea.

Sasa Huku Kugoma Ndio Suluhisho.

Mie Nilikataa Kusoma Udsm Kwa Hofu Hii Ya Migomo Baada Ya Kusoma Degree Miaka Minne Au Mitatu Unaweza Ukasoma Hadi Kumi(jokes)

Tuwe Wa Kweli Haya Mambo Yameshapita Na Wakati.

Tuwe Wa Kweli Na Serikali Pamoja Na Wizara Na Bodi Bado Haijasema Wapi Wamefika Wao Wanaanza Mgomo.

Au Ndo Wakati Ushafika Mtoto Kumkemea Baba Yake Na Kumpiga Bakora?

Tuangalie Na Upande Wa Shilingi, Ukweli 40% Kwa Mtanzania Kuchangia Wengi Wao Hawawezi, Lkn Mazungumzo Yanaendelea.

Hii Ya Kuipa Serikali Mashindikizo Si Sahihi, Na Nnaamini Jk Mpole Sana Maana Bado Anachukua Hatua Za Kishkaji Kuwahurumia Hao Wakosa Fadhila.
Tukumbuke Jkn Vipi Alishughulikia Migomo Na Waliopita?????????????????????????????????????
 
mtumwitu, hivi haya matatizo ya wanafunzi chuo kikuu yameanza lini? Kwanini unafikiri kuwa baada ya serikali "kuangalia" basi matatizo yatatoweka. Isn't this like deja vu?
 
Mkjj

Wewe Ni Mjuzi, Hivi Unahisi Walivyofanya Hawa Wanafunzi Ndio Suluhu? Baba Yako Ukimuomba Kitu Na Akakwambia Jioni Nitakuletea, Ikifika Saa Saba Wakati Wa Kul A Unagoma Na Kuanza Kumuamuru Baba Yako Baba Mie Sili Hadi Kile Kitu Nilichokuomba Unipe, Tena Hata Ile Jioni Ulioahidiwa Haijafika? Jee Ni Suluhu Hio, Ningekuwa Mzazi Mie Ningecharaza Bakora Kwa Watoto Walitozwa Vichwa.

Tunahitaji Wasomi Tena Saana, Lkn Wasomi Wenye Kujua Nyakati.
 
mtumwitu, serikali siyo baba ya watanzania! ila nikitumia mfano wako wa ubaba, kama baba anaendelea kutoa ahadi kila kukicha kushughulikia matatizo yenu na anakuja na kusema "hana pesa" halafu umemuona amepitia kilabuni na kumwaga bia, watoto wana sababu ya kuuliza "baba, mbona unatudanganya?" Halafu baba anaamua kushika bakora kuwachapa "how dare you"! na kuwatimua nyumbani!
 
Duuhh sasa na mimi naanza kuamini JK had a point ya kuomba wataalamu wa ushauri toka Norway.

Just imagine mtumwitu ndio mshauri wa rais.............kwanza kakimbia tatizo halafu anakuja na ushauri eti..............bakora tuu!!
 
Ogah,
Yaani Watanzania wooote wana mtizamo wa Mtumwitu?
Basi heri twende Norway!
 
Kazi za walimu wa chuo kikuu ni: kufanya utafiti, kutoa ushauri wa kitaalamu na kufundisha. Kutokuwepo wanafunzi haina maana kazi zimekwisha, ni kazi moja tu hiyo!

Aaa wapi! Labda kwenye makaratasi tu! Ni utafiti gani huo wanaoufanya? Je kuna matokeo gani yoyote utafiti huo yaliyonufaisha taifa na wananchi? Wameshindwa hata kubuni au kuvumbua vyanzo vingine ya nishati na kuzalisha umeme. Kila umeme unakatika tu. Wahandisi wa umeme wako wapi? Na ni ushauri gani wa kitaalamu wanaoutoa na ni kwa nani....? Kazi yao ni kufundisha tu....na kama wanafunzi wamefukuzwa basi na wao mishahara yao isitishwe kwa sababu hawana kazi ingine zaidi ya hiyo
 
MWANASIASA

Ni kweli hawa vijana wamewahi sana kugoma kama chuo kilivyochukua hatua ya kuwataka waondoke 'ghafla'...

Hatua nilizoshauri awali ni ile waombe ushauri,audience na rais,barua ya wazi,lobbying in the parliament[ hii naongeza sasa] na mwisho kutishia kwa kuweka deadline kuwa ikifika siku fulani tunagoma...mimi binafsi ingawa nina interest sana kujua mambo ya bongo na husoma takriban magazeti kumi mtandaoni kwa siku sikuona hata kidogo mgogoro huu ukitabirika...matokeo yake wameathirika sana vijana hawa PR wise kwani kila mtu anawaona wamekurupuka...migomo mingine itawawia vigumu kujustify.


Kwa upande wa serikali narejea sio kweli kulikuwa na tamko kuwa watapewa hiyo nyongeza,bali waliahidi kushughulikiwa, wangeuliza wajibiwe kwanza kabla ya kugoma....


Kwa upande mwingine vyama vyetu vya siasa za upinzani,walivyo wababaishaji basi huu mgomo ishakuwa dili! ati nao wametoa ultimatum kuwa warejeshwe watoto hawa!

Kwanza wao walikuwa wapi ilipotolewa agizo la 40% contribution? Ni chama kipi kilichotoa alternative to mikopo au mtazamo tofauti na ule wa serikali? kuibuka huku ni kutaka umaarufu wa kulazimisha!

Ni wakati sasa tukawa na misuguano ya hoja badala ya siasa za cheap popularity...
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom