Joshua Nassari Kumwoa Halima Mdee?

Kuoana ni jambo la sifa.

Kuoana sio sawa na kuzini. Waache waowane...!!!!!!!!!!!!! Usiwatie rabsha.
 
Watu hawatokeani kwenye mikutano ya kampeni, hiyo ilikuwa changamsha genge. Ule ulikuwa uwanja wa mapambano na sio mapenzi.
naona kama Madame Halima ana kapete kakurembeshea mambo kidoleni au ni geresha mapambo? Dogo janja atakuwa kama Dr Love Pimbi itabidi avae viatu virefu halafu HM avae flat shoes.Wakicheza blues dogo janja atakuwa anakamata nyonga bibie anabamba mabenga. Je pair imekubali? Kwa rangi sina shaka, elimu pia sina matatizo. Ushauri wa bure dogo janja akaoane na ama Esther Bulaya au mdogo wake Zitto Kabwe(muhonga ??) tutengeneze royal family fulani hivi. MANENO YANAUMBA MSIFANYE MZAHA.bulaya anampenda sana dogojanja. fanyeni uchunguzi bunge litakapoanza tarehe 10 next week after easter.
 
Itakuwa couple moja matata sana! God bless them and make it a reality O Lord!
 
Dogo janja alikosea,angesama hivi 'kwa kuwa wanasema sijaoa basi mimi ntamuoa bi kiroboto' hapo vipi? Pangechimbika mjengoni?
 
huyu joshua inaelekea kila mtu anamtaka...
ngoja na mie niongeze speed...
tuone nani atamnyakua...lol
 
mjadala wa siasa Arumeru tumeshaufunga, tupo kwenye mkakati wa maendeleo ya wanaarumeru.
 
suala la uchumba wa Joshua na Halima haituhusu kwani ni la wao wenyewe sisi kazi tayari ya kumchagua joshua kutuwakisha bungeni au siyo wana JF?
 
naona kama Madame Halima ana kapete kakurembeshea mambo kidoleni au ni geresha mapambo? Dogo janja atakuwa kama Dr Love Pimbi itabidi avae viatu virefu halafu HM avae flat shoes.Wakicheza blues dogo janja atakuwa anakamata nyonga bibie anabamba mabenga. Je pair imekubali? Kwa rangi sina shaka, elimu pia sina matatizo. Ushauri wa bure dogo janja akaoane na ama Esther Bulaya au mdogo wake Zitto Kabwe(muhonga ??) tutengeneze royal family fulani hivi. MANENO YANAUMBA MSIFANYE MZAHA.bulaya anampenda sana dogojanja. fanyeni uchunguzi bunge litakapoanza tarehe 10 next week after easter.


Ipogolo wee mmbaya weewe....halafu unaufahamu kwa yale yanayo endelea.....Mliumbwa kwa mfano wa Mungu....kwahiyo uumbaji upo kwa vinywa vyenu.....ni kama utani hivi lakini chunga sana
 
Kwa mujibu wa tovuti ya Habari Leo mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) amesema sasa yuko tayari kufunga ndoa na Mbunge mteule wa chama hicho wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari. "Nafurahi kwamba Nassari hatimaye ameshinda ubunge katika uchaguzi mdogo," alisema Mdee wakati akihutubia maelfu ya wakazi wa Arusha na Meru.

Mdee alifafanua, kwamba yeye na chama chake walikuwa wamebanwa na kampeni za kuhakikisha Chadema inatwaa jimbo la Arumeru Mashariki na ndiyo sababu hakujibu mara moja maombi ya Nassari ya kumwoa aliyoyatoa katika moja ya mikutano yake ya kampeni.

"Naondoka kwenda Dar es Salaam kujiandaa kwa Mkutano ujao wa Bunge, kisha nitakwenda Dodoma ambako nitamsubiri Nassari na kwa pamoja tutafanya maandalizi," alisema Mdee huku akishangiliwa na hadhira hiyo huku wakiimba na kucheza katikati ya mvua iliyokuwa ikinyesha.

Mdee alisema ndoa kati ya wabunge hao wawili wa Chadema ni wazo zuri na itatangazwa sana na kuandika historia. Alipoona anashambuliwa sana na wapinzani wake juu ya useja wake katika kampeni hizo, Nassari hatimaye alitangaza kumwoa Mdee ambaye pia hajaolewa.

Na katika moja ya mikutano ya hadhara, alisimama naye jukwaani kukampeni. "Kuna viongozi wengi wa kidini Dodoma, ikiwa ni pamoja na ndani ya Bunge ambao watatushauri jinsi ya kulitimiza hili," alisema Mdee na kuongeza kwamba baba yake Joshua, Mchungaji Samuel Nassari alipata kusema, ‘mwanamke mzuri ni zawadi kutoka kwa Mungu'.

Chadema ina idadi kubwa ya wabunge vijana ambao hawajaoa, ikiwa ni pamoja na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Mr Sugu'; wa Ubungo, John Mnyika; wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na sasa Nassari.

Source: Habaroleo: http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=28596

Mwanzoni nilidhani ni habari ya April fool lakini imeandikwa tarehe 3 Machi baada ya uchaguzi.

attachment.php
 

Attachments

  • Halima mdee.PNG
    Halima mdee.PNG
    42.8 KB · Views: 2,098

Similar Discussions

Back
Top Bottom