Joshua Nassari Kumwoa Halima Mdee?

EMT udaku haufanani na wewe aisee

Mie nimeikuta tovuti ya Habari Leo. Bonyeza hapa habari ya pili: HabariLeo | Gwiji la Habari Tanzania

attachment.php
 
kwani Halima Mdee hayupo hapa JF? atuweke wazi basi kwani akiendelea kunyamaza ndio ccm wanapata mwanya wa kumchafua
 
Inaonyesha mapenzi ya Hon Josh yamekuwa hot cake, maana watu wanashobokea mwacheni basi afanye kazi atabemendwa bure!
 
Mhe. Josh atapata wachumba mwaka huu na ndo za uvumi zitakuwa nyingi mpaka atakoma....
 
hilo litayasaidia magazeti ya udaku kama habari leo, jambo leo pamoja na uhuru kuthibitisha kwamba CHADEMA ni chama cha kifamilia. Mtu na mkewe, mtu na dadake, mtu na mkwewe etc. Maana kila siku wanajaribu kutafuta kibaya cha kuandika dhidi ya chadema hawapati, hili likitokea watachonga sana.
 
Mmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh !!!!!!!!!!
 
Nilikuwepo kweli pale alipotakiwa na WanaCDM Halima Mdee awasalimie WanaCDM waliofurika pale na ndipo akasema akiwafurahisha wanainchi lakini hakuwa na ukweli ktk msemo wake!

Na hata ingekuwa hivyo ingependeza sana kwn ni kila kitu na wakati wake!!
Ingependeza sanaaaaaaaaa!!
 
Nilikuwepo kweli pale alipotakiwa na WanaCDM Halima Mdee awasalimie WanaCDM waliofurika pale na ndipo akasema akiwafurahisha wanainchi lakini hakuwa na ukweli ktk msemo wake!

Na hata ingekuwa hivyo ingependeza sana kwn ni kila kitu na wakati wake!!
Ingependeza sanaaaaaaaaa!!

Huyu anadai alikuwepo na hukusikia hayo

Mie nilikuwepo, mbona sijamsikia akitangaza?
 
Huyu anadai alikuwepo na hukusikia hayo



Labda hakusikia kutokana na shamrashamra nyingi iliyokuwa imetanda anga ile,Ila hakika H. Mdee alifurahisha halaiki ile kwa neno hilo but hakuwa serias!
 
Kwa maelezo yako hakuna kitu kama hicho-kuolewa na Nassari. Kwanini kuzua na kutunga wakati wahusika wapo? Kufurahi na kuolewa mbona ni vitu viwili tofauti na wazi? It is the matter of using just common sense even sense commonly if you cannot use common sense.
 
Labda hakusikia kutokana na shamrashamra nyingi iliyokuwa imetanda anga ile,Ila hakika H. Mdee alifurahisha halaiki ile kwa neno hilo but hakuwa serias!

Kwa maelezo yako hakuna kitu kama hicho-kuolewa na Nassari. Kwanini kuzua na kutunga wakati wahusika wapo? Kufurahi na kuolewa mbona ni vitu viwili tofauti na wazi? It is the matter of using just common sense even sense commonly if you cannot use common sense.

Basi Habarileo imekuwa ni ya habari za utani. Huwezi amini hii ndio habari kuu Habarileo siku ya leo: HabariLeo | Gwiji la Habari Tanzania
 
Mi naona poa tu, au mnataka akaolewe na LucyNde aka kibajaj aka kudadadeki!!!
 
Kwa mujibu wa tovuti ya Habari Leo mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) amesema sasa yuko tayari kufunga ndoa na Mbunge mteule wa chama hicho wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari. “Nafurahi kwamba Nassari hatimaye ameshinda ubunge katika uchaguzi mdogo,” alisema Mdee wakati akihutubia maelfu ya wakazi wa Arusha na Meru.

Mdee alifafanua, kwamba yeye na chama chake walikuwa wamebanwa na kampeni za kuhakikisha Chadema inatwaa jimbo la Arumeru Mashariki na ndiyo sababu hakujibu mara moja maombi ya Nassari ya kumwoa aliyoyatoa katika moja ya mikutano yake ya kampeni.

“Naondoka kwenda Dar es Salaam kujiandaa kwa Mkutano ujao wa Bunge, kisha nitakwenda Dodoma ambako nitamsubiri Nassari na kwa pamoja tutafanya maandalizi,” alisema Mdee huku akishangiliwa na hadhira hiyo huku wakiimba na kucheza katikati ya mvua iliyokuwa ikinyesha.

Mdee alisema ndoa kati ya wabunge hao wawili wa Chadema ni wazo zuri na itatangazwa sana na kuandika historia. Alipoona anashambuliwa sana na wapinzani wake juu ya useja wake katika kampeni hizo, Nassari hatimaye alitangaza kumwoa Mdee ambaye pia hajaolewa.

Na katika moja ya mikutano ya hadhara, alisimama naye jukwaani kukampeni. “Kuna viongozi wengi wa kidini Dodoma, ikiwa ni pamoja na ndani ya Bunge ambao watatushauri jinsi ya kulitimiza hili,” alisema Mdee na kuongeza kwamba baba yake Joshua, Mchungaji Samuel Nassari alipata kusema, ‘mwanamke mzuri ni zawadi kutoka kwa Mungu’.

Chadema ina idadi kubwa ya wabunge vijana ambao hawajaoa, ikiwa ni pamoja na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Mr Sugu’; wa Ubungo, John Mnyika; wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na sasa Nassari.

Source: Habaroleo: HabariLeo | Halima Mdee atangaza kuolewa na Nassari

Mwanzoni nilidhani ni habari ya April fool lakini imeandikwa tarehe 3 Machi baada ya uchaguzi.

attachment.php

Magazeti ya Tz siyo ya kuamini hata kidogo yamejawa uzushi na fitna ili tu wapate kuuza magazeti yao
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom