Prof.Lwaitamwa awasha moto balaa la kina Halima Mdee na wezake 19

ichumu lya

JF-Expert Member
Aug 11, 2016
2,605
2,729
KESI YA MDEE NA WENZAKE: MDHAMINI WA CHADEMA DKT. LWAITAMA AKIHOJIWA LEO MAHAKAMA KUU TAREHE 10 MACHI 2023!

Jaji: Anawauliza mawakili wote kama wapo tayari na wanajibu kuwa wapo tayari

Jaji anamuita Dkt. Lwaitama kizimbani tayari kwa kuendelea kudodoswa (kuhojiwa).

Wakili Panya: Prof! Hebu nikukumbushe jana ulisema wakati taarifa hizi zinatokea kwenye media, ulikuwa huko Bukoba. Unakumbuka?

Dkt. Lwaitama: Ni kweli

Wakili Panya: Unaishi wapi?

Dkt. Lwaitama: Kwa sasa, Kibaha Miembe Saba, ila wakati huo nilikuwa Bukoba nilikozaliwa na nilipokuwa nafanya kazi awali.

Wakili Panya: Mwaka jana, 2022 Mwezi wa 8 ulikuwa wapi?

Dkt. Lwaitama: Siwezi kuwa na kumbukumbu kwa kuwa nipo kwenye Bodi mbalimbali zikiwemo Action Aid inayosafiri nchi mbalimbali. Mwaka jana tu, nilikuwa Bangladesh, nk.

Wakili Panya: Japokuwa unaweza kuwa na safari mbalimbali ila nijibu swali langu. Wiki ya kwanza ya mwezi wa nane mwaka jana.

Dkt. Lwaitama: Nimeshajibu!

Wakili Panya: Unafahamu mtu anaitwa Allen Piter Nanyaro?

Dkt. Lwaitama: Siwezi kujibu, na kwa jina hilo simfahamu!

Wakili Panya: Jana ulisema unaitambua katiba ya JMT, lakini kuna vikundi, kuna saccos na vyenyewe vina katiba zao. Ikitokea katiba zao zikigongana ni katiba ipi ina wajibu wa kuingilia kati?

Dkt. Lwaitama: Katiba ya nchi!

Wakili Panya: Wewe hapa pamoja na kiapo chako kinzani unapinga hawa waleta maombi kuwa siyo Wabunge au unapinga hawakuteuliwa na chama chako?

Dkt. Lwaitama: Sasa hilo swali gani? Hawa siyo Wabunge kwa mujibu wa katiba.

Wakili Panya: Hawa waleta maombi 19 wamekoma kuwa wanachama wa chadema lini?

Dkt. Lwaitama: Pale chama kilipopeleka barua kwa Spika kwa kuwa wamekoma kuwa wanachama

Wakili Panya: Mahakama na sisi tunataka kujua ni lini hiyo barua imepokelewa

Dkt. Lwaitama: Details zilizopo kwenye kiapo changu zinajitolezesha!

Wakili Panya: Anampatia kiapo chake!

Dkt. Panya: Hiyo tarehe ya Barua kufika huijui?

Dkt. Lwaitama: Hiyo Conclusion umeipata wapi? Mimi sijaelewa huyu mwanafunzi wangu! Mimi nilikufundisha kutembea na Details kichwani?

Mahakama inaangua kicheko

Dkt. Lwaitama: Nenda katafute hizo details, mimi siyo Mtendaji Mkuu wa Chama kuwa nahifadhi kila kitu!

Wakili Panya: Hiyo barua iliyokwenda kwa Spika kutoka kwa Chama kwa uelewa wako ilikwenda kwa Spika kabla hawa wahajawa Wabunge au baada ya wao kuwa Wabunge?

Dkt. Lwaitama: Ilikuwa baada ya wao kutenda kitendo hicho cha kuapa! Acha kutafuta ujanja kuwatetea watu.

Wakili Panya: Kwa kipindi hiki kabla ya barua walikuwa Wabunge?

Dkt. Lwaitama: Ndiyo! Ndio maana watu kuna watu wanasema ni Wabunge wa Mchongo!

Mahakama inaangua kicheko

Wakili Panya: Wakati hawa wanakwenda kuapa walikuwa wanachama wa CHADEMA?

Dkt. Lwaitama: Bila shaka!

Wakili Panya: Kale ka mchakato ka ndani ka kuwapata watu wanaokwenda kuwa Wabunge kalifuatwa au hakakufutwa?

Dkt. Lwaitama: Kuteua na kukokotoa na baadaye kuwaeleza kuwa ninyi ni Wabunge ni vitu tofauti. Na hii inakuja baada ya Uchaguzi, kuwa wananchi wanapigia Wagombea labda wa CHADEMA kura na Tume inachakata kura na kuleta Orodha!

Wakili Panya: Swali langu, ule mchakato wa ndani ya Chama ulifuatwa au haukufuatwa

Dkt. Lwaitama: Ulifuatwa

Wakili Panya: Wewe ni miongoni mwa Wadhamini wa CHADEMA, ni nini majukumu ya Udhamini wa Chama?

Dkt. Lwaitama: Kama Mdhamini pamoja na mambo mengine yahusuyo masuala ya kifedha na hata haya yaliyonileta hapa. Haiwezekani wanachama wote kuwa hapa. Nakuwa sura ya kisheria ya Chama.

Wakili Panya: Kwenye masuala ya utendaji ya chama, chama kina mfumo wake na wewe hujishughulishi moja kwa moja day to day!

Dkt. Lwiatama: Kama mwanachama naweza kuwa najishughulisha kufuatilia

Wakili Panya: Nauliza kama majukumu yako ya day to day!

Dkt. Lwaitama: Mimi sihusiki moja kwa moja ila kuhusu kufiatilia, nafuatilia!

Wakili Panya: Kuna dhana ambayo waleta maombi 19 wanasema kwenye Application yao kuwa wanashangaa na jinsi Katibu Mkuu alionesha kuhusu viapo vyao kuwa wao wanasema walifuata utaratibu na kuna shahidi anaitwa Nusrat Hanje aliwahi kusema hilo!

Wakili Mtobesya: Mh Jaji, hilo swali lina matatizo, linamtaka shahidi atoe maoni kwenye ushahidi wa shahidi mwingine!

Jaji: Hebu rudia swali

Wakili Panya: Anarudia swali

Dkt. Lwaitama: Utaratibu wanaosema ulifanyika ni ule wa mchakato wa kupata majina ya Viti Maalum wa Chama ngazi zote na utaratibu walikiuka kupeleka hayo majina kwa Tume kinyume na utaratibu wa Chama.

Wakili Panya: wewe ulipata wapi hayo kuwa hao walipeleka majina bila baraka za Kamati Kuu?

Dkt. Lwaitama: Niliyajulia kwenye Kikao cha Baraza Kuu lililosikiliza rufaa zao, na hayo yapo pia kwenye huo Muhutasari wa Kikao cha Kamati Kuu!

Wakili Panya: Wewe ulikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu?

Dkt. Lwaitama: Kwani kujua kitu mpaka uwe Mjumbe wa Kamati Kuu?

Wakili Panya: Kwa hiyo ulipewa Muhutasari na kuelezewa hayo yote! Ni nani aliyekuita?

Dkt. Lwaitama: Chama kina watendaji wa Chama anaitwa Mashuve, Mndeme ndo waliniita wakanieleza na nikajiridhisha nikasaini.

Wakili Panya: Wakati unaitwa ulikuwa na mtu mwingine kuelezewa hayo, ulikuwa peke yako au ulikuwa na wakili wako?

Dkt. Lwaitama: Nilikuwa peke yangu niliitwa nikaenda ofisini.

Dkt. Panya: hawa waleta maombi 19 walivyoitwa na Kamati Kuu walijibu wito na kutoa sababu kuwa wapewe nafasi. Hii fact unaizungumziaje?

Dkt. Lwaitama: Hiyo fact niliikataa kwa kuwa kwa mfano mimi nimeitwa kuja hapa nikatoka Moshi na kutii kufika. Wao walishindwa hata mmoja wao kufika?

Dkt. Panya: Umewahi kuona barua hiyo ya waleta maombi wakiomba Kamati Kuu kuwapa muda kidogo wa kufika mbele ya Kamati Kuu?

Dkt. Lwaitama: Niliiona na niliiona na sababu niliziona walisema sababu ya kwanza ni usalama na Chama kiliwajibu!

Wakili Panya: Anasoma barua mojawapo, inayosema mleta maombi anaomba kuongezewa muda wa kufika kwenye Kikao cha Kamati Kuu.

Wakili Panya: Hizi sababu unazizungumziaje?

Dkt. Lwaitama: Kwa kweli sababu ya kwanza ya kuwa wapewe muda wa kutafakari juu ya Chama chao naichukulia ni kama walishindwa kukitazama Chama kwanza kwa kuwa watu walikuwa kwenye taharuki ya Chama. Hivyo walipaswa kufika kutoa ufafanuzi wa hilo. Sababu ya pili ya usalama ilikuwa ya kitoto kwa kuwa hakukuwa na watu wanaweza kuandamana ukizingatia kuwa wakati huo ulikuwa ni Utawala wa Hayati Magufuli. Na hata hivyo baadaye Kikao kilihamishiwa eneo ambalo pengine pangekuwa salama zaidi lakini walipuuza.

Wakili Panya: Uliwahi kuona barua ya Katibu Mkuu ya wito wa hawa waleta maombi?

Dkt. Lwaitama: Ndiyo naijua.

Wakili Panya: Anasoma barua hiyo.

Wakili Panya : Unamfahamu Tunza Malapo?

Dkt. Lwaitama: Huyu namfahamu.

Wakili Panya: Huyu siyo mwanasheria na hivyo alielezwa afike yeye mwenyewe.

Wakili Panya: Kwa hiyo suala la usalama ni sensitive ndio maana kilihamisha venue?

Dkt. Lwaitama: Chama kiliwapa benefit of doubt!

Wakili Panya: Sababu iliyopelekea CHADEMA kutoa maamuzi bila kuwasikiliza ni nini?

Dkt. Lwaitama: Waliitwa na hawakutokea, na kwa kuwa walikuwa wanufaika walipaswa kufika na ikabidi Chama kiamue jambo hilo, na kwa kuwa kulikuwa na taharuki, hivyo kusingekuwa na nafasi ya kuchelewesha michakato hiyo.

Wakili Panya: Hivi wangepewa hiyo wiki moja kungeathiri nini?

Dkt. Lwaitama: Kulikuwa na mazingira ambayo ilikuwa lazima michakato husika ilichukue muda huo, na isingewezekana wao kupewa muda zaidi.

Wakili Panya: Je, Chama kilichukua uamuzi wa haraka ili viongozi wasionekane wamelamba asali?

Dkt. Lwaitama: Hapana! Nimesema Chama kilihitaji kujinusuru kugawanyika kutokana na jambo hilo.

Wakili Panya: Mheshimiwa tunaomba Kielelezo Tal 6 Kichezwe hapo tuone

Jaji: Anatoa maelekezo kielelezo hicho kichezwe kwenye TV. Mahakama iko kimya Mtaalamu wa IT amekwenda kutafutwa nje ili aje aweke flash Disc kwenye tv

Inachezesha Video ya Mwenyekiti wa CHADEMA wakiwa kwenye Kikao cha Baraza Kuu la 2022.

Wakili Panya: Video hii iliyochezwa umeleta wewe mahakamani inatwa Tal 6, uniafahamu

Dkt. Lwiatama: Ndiyo na mimi nilikuwepo.

Wakili Panya: Ulikuwepo kama nani?

Dkt. Rwiatama: Kama mgeni mwalikwa kama unavyomuona Sisty Nyahoza (Naibu Msajili wa Vyama vya siasa)

Wakili Panya: Naomba uiambie Mahakama, nini ulitaka kuachieve kwa kuleta hiki kielelezo TL 6?

Dkt. Lwaiitama: Ni ili kuonesha namna Chama kilikuwa na huruma dhidi yao na jinsi kilitamani wao watubu wasamehewe.

Wakili Panya: Video inaonesha akimuelezea Halima Mdee tu, je hao wengine 18 aliwaeleza?

Dkt. Rwiatama: Alihangaika na Halima kwa kuwa yeye ndio alikuwa na ushawishi kwa wenzake.

Wakili Panya: Ulijuaje kuwa alikuwa na ushawishi?

Dkt. Lwaitama: Mimi najua kutoka kwenye akili yangu na nina hakika wewe unajua pia.

Wakili Panya: Mkutano Mkuu mzima wa Baraza Kuu ulichukua muda gani kwenye video.

Dkt. Lwaitama: Mheshimiwa Jaji, mimi siyo mtaalamu wa masuala hayo siwezi kujua Intered procces zilichukua muda gani!

Wakili Panya: unasema Mwenyekiti alizungumza kabla ya Baraza Kuu kufanya maamuzi. Ni kweli ulisema pia kwenye maelezo yako? Swali: Mwenyekiti alijua vipi kuwa Baraza Kuu litaamua

Dkt. Lwaitama: Kwa kuwa alikuwa ameletewa rufaa na alijua baada ya Baraza Kuu likishaamua pengine atapoteza majembe kama hayo. Ni kama alikuwa anawashawishi Wajumbe wawasamehe

Wakili Panya: Mr. Mbowe alizungumza kwa capacity yake kama Mwenyekiti wa Taifa?

Dkt. Lwaitama: Ni kweli ila ukisikiliza kwa umakini kuna mahali alisema ngoja nitoe ya moyoni, hilo haliwezi kuwa jambo la kitaasisi!

Wakili Panya: Jana tulizungumza kuhusu kura ya siri au ya wazi! Swali: Baraza Kuu lilifanya maamuzi ya kupiga kura ya wazi au siri?

Dkt. Lwaitama: Mbele ya Kikao cha Baraza Kuu Wajumbe walihojiwa na kukubaliana kuwa kura iwe ya wazi! Na pamoja na mambo mengine waliamua pia kuwa Naibu Msajili abaki ukumbini

Wakili Panya: Wakati kura zinapigwa walikuwepo watu wengine kama wewe na Sisty?

Dkt. Lwaitama: Kura zilipigwa mbili, ya kwanza Baraza Kuu lilipiga kura ya kutaka Wajumbe waalikwa wawepo akiwemo Sisty, na Kura zote zilikuwa za wazi kwa makubalino ya Baraza Kuu.

Wakili Panya: Kuna watu walioshiriki kwenye Kikao kama wewe, Omary Othman, Jenerali Ulimwengu, Juma Dun Haji, Bobe Wine, Askofu Mwamakula, nk.

Dkt. Lwaitama: Wakati wa kura ya pili ya Baraza Kuu hao hawakuwepo tena. Walibaki mimi Lwaitama na Sisty Nyahoza (Naibu Msajili).

Wakili Panya: Wakati kura ya pili inafanyika ulikuwa umeshakuwa Mjumbe wa Bodi au la!

Dkt. Lwaitama: Ilikuwa baada ya mimi kuwa Mjumbe.

Wakili Panya: Wewe kama Mdhamini wa CHADEMA na CHADEMA ina katiba; moja ya jukumu ulilonalo ni kama Mjumbe wa Bodi ya Udhamini kuiheshimu katiba.

Dkt. Lwaitama: Naiheshimu na ndio maana ni mwanachama.

Wakili Panaya: Unafuata vifungu vyote vilivyopo au kuna vifungu huvifuati?

Dkt. Lwaitama: Sasa navifuataje sasa mimi nimekaa hapa muda huu!

Wakili Panya: Kwenye Katiba ya Chadema Toleo la 2019 Sura ya 7 Ibara ya 7:7:11

Wajumbe wa Baraza Kuu la Taifa litakuwa kama ifiatavyo!

7.7.11Wajumbe wa Baraza Kuu la Taifa watakuwa kama ifuatavyo;
(a) Wajumbe wote wa Kamati Kuu
(b) Makamu Mwenyekiti wa Kanda
(c) Makatibu wa Kanda
(d) Watunza Hazina wa Kanda
(e) Wenyeviti wa Baraza la Uongozi, Mkoa.
(f) Makatibu wa Mkoa
(g) Wajumbe wateule wasiozidi sita
watakaoteuliwa na Mwenyekiti wa Taifa
kwa kushauriana na Katibu Mkuu na
kudhinishwa na Baraza Kuu. Wajumbe
wateule hawa watateuliwa kwa uwiano
wa wajumbe wanne; wanaume na
wanawake wawili.
(h) Wajumbe watano watakaochaguliwa
na Mkutano Mkuu wa kila Baraza la
Chama, kwa uwiano wa wajumbe
wanne toka Bara na mmoja toka
Zanzibar kwa kila Baraza.
(i) Wenyeviti wa Wilaya za Chama
(j) Makatibu wa Wilaya za Chama.

Wakili Panya: Kwenye Katiba wajumbe wa Bodi ya Wadhamini siyo wajumbe wa Baraza Kuu!

Dkt. Lwaitama: Ndiyo siyo Wajumbe!

Wakili Panya: Naomba Mheshimiwa Jaji ichezwe kielekezo HDM

Video Imechezwa! Inachezwa video ambayo Mheshimiwa Mbowe akieleza msimamo wa Chama kuwa hatujawahi kuteua Wabunge wa viti maalum. Iko kwenye Kielelezo HDM 08

Wakili Panya: Baada ya kuona hiyo Kielelezo HDM 08 Video bado unataka kusema huyo ndo Mwenyekiti aliyekuwa anataka kuwasamehe?

Dkt. Lwaitama: kabisa.

Wakili Panya: Wabunge 19 malalamiko yao ni kuwa viongozi wakuu wa Chama na wakiwemo wapiga kura, Mwenyekiti Mbowe alikuwa ni mmoja wa wapiga kura?

Dkt. Rwaitama: Ni sahihi alikuwa ni miongoni.

Wakili Panya: Kwa sababu ulipata bahati ya kuwepo kwenye kwenye Baraza Kuu na kura ilikuwa kura ya wazi, Mwenyekiti alipiga kura gani?

Dkt.wiatama: Kwa kuwa kura zilikuwa zinapigwa kwa makundi kwa Kanda na nilikuwa tu naona watu wanasimama kwa kundi sikuweza kuona kila mmoja mmoja kuwa nani alipiga ipi au ipi.

Wakili Panya: Unakumbuka matokeo ya kura?

Dkt. Lwaitama: Ndiyo na nimeyaandika

Wakili Panya: Matokeo yakoje nisomee hapo

Dkt. Lwaitama: Jumla ya waliopinga, wasiokuwa na Upande (5) 1.2%; Wasiokubalina na Kamati Kuu 5 1.2%; Waliokubalina na maamuzi ya Kamati Kuu 413.

Wakili Panya: Kwa hiyo Mbowe alipiga kura gani?

Dkt. Lwaitama: Ukiangalia kwenye Kamati Kuu, Wajumbe wote walipiga kura ya kuunga mkono maamuzi yao ya awali

Wakili Panya: Kwa hiyo walipewa nafasi ya kujitetea?

Dkt. Lwaitama: Walipewa nafasi ya kujitetea kwenye Baraza Kuu

Wakili Panya: Kwa njia gani?

Dkt. Lwaitama: Walipewa nafasi kwa njia ya maandishi na baadaye wakaulizwa iwapo wana cha kusema, na hawakusema.

Wakili Panya: Waliokuwa wanathibitisha nakala kama ni zao ni nani alithibisha kuwa zile zilikuwa sawa na zile za Wajumbe?

Jaki Mkeha: Uliza swali lingine hilo siyo swali

Wakili Panya: Kura zilipokuwa zinapigwa ni kwa nini kura zilipigwa kwa wanaokubaliana na maamuzi ya Kamati Kuu na kwa nini ilisomeka kuwa wanaopinga maamuzi? Kwa nini usiseme kuwa wanaokubaliana na warufani?

Dkt. Lwaitama: Maswali yalikuwa matatu na yalikuwa ni wanaopinga au wanaokubaliana na wasiounga mkono upande wo wote.

Wakili Panya: Anasoma hoja za Kamati Kuu kwa Baraza Kuu ambazo lilikuwa hitimisho yaliyoletwa na Katibu Mkuu!

Swali: Je! Warufani walipewa nafasi ya kutoa maneno ya hitimisho?

Dkt. Lwaitama: Walihitimisha kwa njia za maandishi

Wakili Panya: Mh Jaji tunaomba tuahirishe kwa muda kidogo kisha tukirudi wenzangu wataendelea

Jaji: Tunaahirisha mpaka saa 7:46 mchana.

MAHAKAMA IMEREJEA.

Jaji Mkeha Ameingia!

Kesi inatajwa na Wakili wa Jamhuri anawatambulisha Mawakili waliongezeka ni EMANUEL UKASHU na ADV MALENGA

Wakili Panya: Mh Jaji namkabidhi Wakili Aliko Mwamalenge aendelee na Maswali ya Dodoso

Wakili Mwalenge: Kwenye Chama cha CHADEMA siyo kila mwanachama ni kiongozi.

Dkt. Lwaitama: Ni sahihi

Wakili Mwamalenge: Na siyo kila mwanachama ni Mbunge.

Wakili Mwamalenge: Kwa hiyo utakubalina na mimi kuwa pale katiba inapomuongelea mwanachama inazungumzia wote haijalishi ni Mbunge au ni nani

Dkt. Lwaitama: Ni sahihi

Jaji: Uliza swali la msingi mpaka muda huu sijaandika cho chote kwa kuwa siyo mambo yanayoweza kuisaidia Mahakama.

Wakili Mwamalenge: Kuna barua mliiandika kielelezo (Kwa Wabunge 19) barua ya wito wa kufika mbele ya Kamati Kuu. Kwenye hiyo barua Mmmemwandikia Nagenjwa Kaboyoka (HJ2).

Dkt. Lwaitama: Ni sahihi.

Wakili Mwamalenge: Kwenye hao Wabunge 19 ukiacha mbali Ubunge, wapo ambao walikuwa ni viongozi wa Chama wa ngazi mbalimbali.

Dkt. Lwaitama: waliandikiwa kama wanachama

Wakili Mwamalenge: Halima Mdee mlipomuandikia alikuwa Mwenyekiti wa BAWACHA.

Dkt. Lwaitama: Ndiyo.

Wakili Mwamalenge: Tendega alikuwa Katibu Mkuu BAWACHA Taifa, Kishoa alikuwa Naibu Katibu Mkuu BAWACHA Taifa, Ester Matiko alikuwa Mwenyekiti wa Chama wa Kanda ya Serengeti ni kweli au si kweli?

Dkt. Lwaitama: Ni kweli. Ila waliandikiwa kama wanachama na siyo viongozi

Wakili Mwamalenge: Barua hizi mliziandika na mkasema ni kwa mujibu wa kanuni ya 6.5.1 Ibara ya (5.4.4) Swali: Kwenye Barua yenu mlikuwa mnamuandikia kamawanachama huyu Halima Mdee?

Dkt. Lwaitama: Bila shaka.

Wakili Mwamalenge: Katiba ya CHADEMA 6.5.5 inasema kiongozi yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu bila ...........

Wakili Mwamalenge; kwa nini hamkumpa huyu kiongozi haki yake ana Exception au hana?

Dkt.waitama: Mh Jaji sina makabrasha hapa nijiridhishe kama kiongozi anayo au hana Exception.

Wakili Mwamalenge: Kwa barua mliyowaandikia na mambo mliyoyaandika hapa ndio makosa yao au kuna mengine?

Dkt. Lwaitama: Mimi siyo mwanasheria siwezi kujua kuwa Hati ya Mashataka iweje! Ila unaweza kuitwa kwa makosa fulani ndani ya maelezo au majibu yakapatikana pia makosa zaidi.

Wakili Mwamalenge: Wakati wanaitwa kwa makosa hayo yalikuwa yameandikwa kwenye barua makosa gani yaliyoongezeka?

Dkt. Lwaitama: Kama yalivyo kwenye kiapo hicho.

Wakili Mwamalenge: Kwa mujibu wa Tal 5, makosa yalikuwa manne, na yalijadiliwa wakiwa hawapo hawa Wabunge 19.

Dkt. Lwaitama: Wangejuaje kuwa ni makosa kama hawakufika?

Wakili Mwamalenge: Lini mara ya mwisho umetembelea nyumbani kwa Conjesta Rwamlaza?

Dkt. Lwaitama: Nyumbani kwake wapi? Nyumbani kwake hata sikujui

Wakili Mwamalenge: Vipi hawa wengine?

Dkt. Lwaitama: Sijawahi kuwatembelea au labda niliwahi kutembelea bila kujua kuwa ni nyumbani kwao!

Mahakama : Inaangua kicheko

Wakili Mwamalenge: Accountant wa Chama ni lini mara ya mwisho kukaa naye kuzungumzia masuala ya fedha?

Dkt. Lwaitama: Kwa hiyo ukiwa Mjumbe wa Bodi unakaa na Accountant wa Bodi hiyo? Au Taasisi hiyo? Mimi ni Mjumbe wa Bodi nyingi duniani sijawahi kuona hilo.

Wakili Mwamalenge: Ulijuaje gharama zilizotumika kwenye Baraza Kuu la 11 Mei?

Dkt. Lwaitama: Nilijua kwenye vikao na siyo kuwa kwa kuwa sijakaa na Accountant ndio ujue mahesabu yaliyotumika?

Wakili Mwamalenge: Kuna sehemu uliulizwa kuwa wakati Kamati Kuu imekaa kuwavua, whether hawa walikuwa ni Wabunge au siyo Wabunge?

Dkt. Rwaitama: Ni sahihi

Wakili Mwamalenge: Kwenye katiba ya CHADEMA, muongozo Sehemu E, jatua za kinidhamu za Wabunge na Mameya,

Anasoma

Wakili Mwamalenge: Kwa nini hawakushughulikiwa kwa kufuata utaratibu huu?

Dkt. Lwaitama: Kwa upande wa CHADEMA hawakuwa Wabunge. Walishughulikiwa kama wanachama.

Wakili Mwamalenge: Kwa mujibu wa Katiba yenu chombo cha mwisho cha maamuzi ni kipi?

Dkt. Lwaitama: Baraza Kuu

Wakili Mwamalenge: Kuna mtu anaitwa Matha Mtiko! Unamfahamu? Kama unamfahamu vipi?

Dkt. Lwaitama: Simfahamu

Wakili Mwamalenge: Uliulizwa kuhusu suala la Udharura, Je? ulikoma lini? Udharura huo ulikoma?

Dkt. Lwaitama: Dharura kwenye vyama vya siasa ni jambo la papo kwa papo! Na chama kilisharidhisha wanachama kwa kuwanyang'anya uanachama

Wakili Mwamalenge: Unamfahamu Fabia Nyangoro

Dkt. Lwaitama: Katika muktadha huo simfajamu unless ungenionesha picha.

Wakili Mwamalenge: Mhe Jaji! Naomba nimlete Edson Kilatu aendelee.

Wakili Kilatu: Unamfahamu Aida Kenan?

Dkt. Lwaitama: Namjua nilimuona mtu ameapishwa tu huko kwenye media

Wakili Kilatu: Juzi kule Moshi, Mwenyekiti wa BAWACHA alisema moja kati ya mafanikio waliyoyapata ni pamoja na kumpata Mbunge Aida.

Dkt. Lwaitama: Sikupei Antention kwenye hilo

Wakili Kilatu: Je hivi viapo vyote vya waleta maombi 19 ulisoma na kujiridhisha?

Dkt. Lwaitama: Ndiyo

Wakili Kilatu: Nikiangalia counter Affidavit ya kwako Para 34 Umejibu Counter Affidavit zote, na kwenye hiyo 39 uliyotaja ulimaanisha unajibu ya wote au ya nani?

Dkt. Lwaitama: mpaka nijiridhishe.

Wakili Kilatu: Anasoma content zilizopo kwenye Paragraph hizo kwa kila Para hizo, Na amesoma mbili ya Kaboyoka,

Wakili Kilatu: Kwa hiyo ulimaanisha hivyo?

Dkt. Lwaitama: Mh Jaji inawezekana Content ikawa imehama Paragraph kwa kila Affidavit, hivyo tuangalie kila moja kwa content

Wakili Kilatu: Unauelewa kidogo wa mambo ya Sheria?

Dkt. Lwaitama: Mimi siyo Mwanasheria ila siyo mbumbumbu kihivyo.

Wakili Kilatu: Kwenye Verification yako Affidavit kuna mahali umetaja kuwa ulipata kuwa mwanasheria?

Dkt. Lwaitama: Kama ningekuwa nafanya hivyo kwa kila kitu kuwa nimeshauriwa au nimefunzwa

Wakili Kilatu: Kuna mtu anaitwa Shaban Othman unamfahamu?

Dkt. Lwaitama: Kwa Context hiyo nitakuwa simfahamu

Wakili Kilatu: Kwenye Verification yako umesema kuwa hizi taarifa umesema kuhusu hizi taarifa ulizopata kuwa ni za kweli ila hizi za watu ambao hujawataja na zenyewe zilikuwa za ukweli? Kuna Sehemu umeeleza hapa kwenye Documents hii!

Dkt. Lwaitama: Mh Sijaelewa!

KIBATALA ANAINGIA NA KUULIZA SWALI MOJA TU.

Wakili Kilatu: Mh JAJI, Narudisha kwa Panya

Wakili Panya: Mh Jaji tunamshukuru Prof Lwaitama na tunahitimisha maswali yetu ya Dodoso

Jaji: Upande wa serikali mna cho chote

Wakili Kalokola: Mh Jaji hatuna.

Jaji: Kibatala

Wakili Kibatala: Mh Jaji nina swali moja tu

Wakili Kibatala: Wakati unailizwa na Wakili Panya, uliulizwa iwapo kwenye Baraza Kuu kuwa iwapo warufani walipata nafasi ya kusikilizwa, naomba nikusomee Muhutasari wa Kikao cha Baraza Kuu.

Kibatala: Anasoma

Wakili Panya: Mh Jaji kama ataniruhusu niongelee hicho kipengele baadaye na mimi kwa kuwa sikukizungumzia kabisa nilijikita kwenye kusikiliza rufaa tu.

Jaji: Hivi Mnaamini kuwa hata kama majibu yakiwa tofauti kwenye kilichopo kwenye Affidavit

Kibatala: Hakuna Objection ni maoni binafsi,

Jaji; Uliza swali

Kibatala Anarudia swali:

Dkt. Lwaitama: Kama ningeulizwa hivyo ningejibu kwa ufasaha kama sasa kuwa baada ya maelezo ya Katibu Mkuu na muda mfupi kabla ya Baraza Kuu kupiga kura walipewa nafasi ya kuomba msamaha.

Wakili Kibatala: Mh Jaji sisi tulikuwa na swali moja tu!

Jaji Mkeha: Anaandika

Jaji Mkeha: Prof Tunakushukuru sana na tunakudischarge.

Jaji Mkeha: Tarehe ya kuendelea na Maswali ya Dodoso ni tarehe 18 na 19 Aprili 2023, Saa 3 Asubuhi na Mdodoswaji Madam Ruth Mollel utafika bila kukosa!
IMG-20230310-WA0103.jpg
 
Jaji Mkeha: Tarehe ya kuendelea na Maswali ya Dodoso ni tarehe 18 na 19 Aprili 2023, Saa 3 Asubuhi na Mdodoswaji Madam Ruth Mollel utafika bila kukosa!View attachment 2544732
Aione Erythrocyte
 
Hakuna kitu kigumu mahakamani kama cross examination ... Kikifika hicho kipindi kuna watu wataikimbia mahakama
 
Dah! Huyu Wakili Panya ana busara sana kumzidi Mwalimu wake. Licha ya Mwalimu wake kumkejeli yeye kamvumilia, lakini kamshindilia makonde ya maswali Hadi Mwalimu kaipata fresh!
 
,
 
Hadi maamuzi yanakuja tolewa na mahakama, muhula wa ubunge wa kina Mdee utakuwa umefikia ukingoni...
 
Back
Top Bottom