Kinachouangusha upinzani Tanzania ni nidhamu

Abdalah Abdulrahman

JF-Expert Member
Aug 29, 2019
222
201
Nidhamu ndio msingi wa maendeleo ya kila kitu duniani, ukitaka kuwa tajiri ni lazima uwe na nidhamu ya fedha, ukitaka kuishi vema kwenye ndoa yako ni lazima uwe na nidhamu katika mahusiano yako, ukitaka kuwa na chama chenye ushawishi mkubwa na chenye uwezo wa kukamata dola ni lazima viongozi na wafuasi wa chama wawe na nidhamu. Ukosefu wa nidhamu kwa viongozi na wafuasi wa vyama vya upinzani umepoteza matumaini kwa wapiga kura na watanzania wa rika zote kwa jumla.

Vyama vya upinzani Tanzania vilianza kwa matumaini makubwa ya kushika dola,rejea matokeo ya mwaka 1995 ambapo Marehemu Lyatonga Mrema alipata ushindi wa asilimia 27.9% dhidi ya mpinzani wake marehemu Rais mstaafu Benjamin Mkapa ambae alipata ushindi wa asilimia 61.8%. Kutokana na kaida ya siasa, ushawishi mara nyingi hukua kwa chama pinzani na hupungua kwa chama tawala hasa kwenye jamii ambayo imekua na chama kimoja kwa muda mrefu,na jamii ambayo idadi kubwa ya watu ni vijana. Jambo la kushangaza ni kuwa ushawishi kwa vyama pinzani nchini unapungua kila kukicha kutokana na sababu nyingi. Sababu hizo ni pamoja na nidhamu, uchu wa madaraka kwa viongozi wa vyama vya upinzani, kukosa ajenda, kukosa umoja, kukosekana kwa demokrasia ndani ya vyama vya upinzani, na kuwa na sera kinzani na maadili ya Watanzania. Katika makala hii, nitaeleza kwa kina juu ya sabababu moja ya ukosefu wa nidhamu kwa vyama vya upinzani na athari zake.

Vyama vya upinzani vinajukumu kubwa la kukosoa serikali na kushauri serikali kwa kuonesha sera mbadala juu ya uendeshaji wa nchi. Jambo hili lapaswa kufanywa kwa nidhamu na ueledi mkubwa. Yapo mambo mengi mazuri ambayo vyama vya upinzani vimefanya na hivyo kujenga imani kwa baadhi ya wananchi. Baadhi ya mambo hayo ni kama vile kuibua ufisadi katika nyanja mbalimbali, kuhamasisha chama tawala kufanya kazi zake sawa sawa nakadhalika.

Juhudi hizi zimekua zikikwamishwa na ukosefu wa nidhamu ndani ya vyama hivi, miongoni mwa matukio ya kuonesha ukosefu wa nidhamu katika vyama vya upinzani ni pamoja na wabunge wa upinzani kutukana hadharani, wafuasi kuwatukana na kutumia lugha chafu katika mitandao, ugomvi kati ya vyama vya upinzani na uwepo wa makundi ndani ya vyama hivi.

  • Wabunge wa Upinzani kutukana hadharani.
Mwaka 2016 aliyekua mbunge wa Mbeya mjini kwa tiketi ya Chadema Mr 2 alinyanyua kidole cha kati bungeni akiashiria kuwatukana wabunge. Kitendo hiki ambacho kiliwachukiza Watanzania na bunge kilipelekea kusimamishwa kwa vikao kumi vya bunge vya msimu huo. Kukosekana kwa mbunge huyu kuliwakosesha fursa wananchi wa Mbeya mjini kusikiliziwa changamoto zinazohusu jimbo lao.

  • Wafuasi wa Upinzani kutoa lugha chafu
Idadi kubwa ya wafuasi wa vyama vya upinzani ni vijana wasio na maadili mema ya kitanzania. Hili linathibitishwa kutokana na aina ya maneno ambayo wanayatumia katika ushawishi wao. Licha ya kukosa staha ya maneo vijana wengi wamejengwa juu ya msingi wa kutafuta haki kwa vitisho na kudhuru au kuharibu mali za uma. Wafuasi wa Chadema wamekua wakiwatukana viongozi wa juu wa serikali akiwemo Raisi, spika na mawaziri bila viongozi wao kukemea tabia hizi ambazo zinaathiri mustakabali mwema wa Taifa.

  • Kampeni chafu
Marehemu Lyatonga Mrema aliwahi kutukanwa hadharani na kuvunjiwa heshima yake na viongozi na wafuasi wa Chadema katika kampeni za Uchaguzi 2020 alipokua akigombea ubunge wa jimbo la Vunjo. Kwa kauli yake mwenyewe Marehemu Lyatonga Mrema alisema

“Siwalaumu wanachama wa CHADEMA, viongozi wao ndio wenye fujo na mimi, sasa najiuliza tatizo ni nini ,uzee wangu? kama ndio hivyo wawaachie wananchi, kama kuumwa mbona tangu 1984 naugua kisukari, kwa nini wananitendea haya?”

Kampeni hizi chafu na za fujo na lugha chafu pia zilitokea huko ndanda ambapo mbunge wa Ndanda Chadema ndugu Cecil Mwambe aliamua kujiondoa katika chama hicho. Na hapa ninanukuu alichokisema.

“Niliitwa majina yote mabayo mnayoyajua, lakini nilivumilia nikiwa najua na matusi yote yaliyotukanwa, mbaya zaidi mimi ni mwenyekiti wa Chama, vipi kwa mwanachama wa kawaida?”

Kwa ujumla kampeni za fujo, kuharibu mali za wananchi na kupora ni sehemu ya mkakati wa vyama vya upinzani. Baadhi ya njama hizi huratibiwa na viongozi wa ndani ya chama katika ngazi mbalimbali.

  • Kutoaminiana na kutohurumina na kuthaminiana.
Vyama vya upinzani vimekua na tabia ya kuhukumiana bila kupeana nafasi ya anayehukumiwa kujitetea. Matokeo ya adhabu hizi kwa wananchama wengi ambao wamevuja jasho na damu kufikisha vyama hivi mahala vilipo yamezaa dhana ya kutoaminiana na kuhurumiana. Chadema iliwahi kuwafukuza vijana waliovuja jasho na damu kama vile kina Zitto Kabwe, Halima Mdee, Ester Bulaya na wengine wengi kwa dhana ya usaliti.

Madhara ya matusi, lugha chafu na fujo kwa vyama vya upinzani ni pamoja na kupoteza watu mahiri na wastaarabu ndani ya vyama vya upinzani wenye nyazifa kubwa ndani ya vyama vya upinzani na wabunge, kuondoa imani kwenye vyombo vya ulinzi, kupoteza kundi kubwa la wafuasi wastaarabu, kupoteza kundi kubwa la wapiga kura.

Hivi sasa vyama vya upinzani vinaokoteza vijana ambao ukitizama katika matamshi yao, ni vijana wasio na uzalendo na wanaotaka kuidumbukiza nchi katika matatizo.

Kupoteza Watu Makini.

Katika awamu ya tano viongozi wengi wa vyama vya upinzani ambao walikua nguzo katika vyama hivyo waliamua kuhamia chama tawala kutokana na sera nzuri za chama na utekelezaji wa sera zake. Viongozi hawa kwa uzalendo wao waliamua kuunga juhudi za Chama cha Mapinduzi ili kuwahudumia wananchi. Kutokana na sera nzuri za CCM viongozi hawa hawakubaguliwa na walikaribishwa na kupewa nafasi mbalimbali ili wawahudumie wananchi. Ni katika kipindi hki zaidi ya wabunge na madiwani wapatao 150 walijiuzulu nafasi zao na kuhamia CCM ili kuchangia katika maendeleo ya nchi. Viongozi haw ani pamoja na aliyekua mgombea wa nafasi ya Urais Mh. Edward Lowasa, David Silinde, Mwita Waitara, Julias Kalanga Laizer, Maulid Mtulia, Dr Mashinji ambae alikua katibu mkuu wa Chadema, na wengine wengi.

CCM INA UHAKIKA WA KUTAWALA AWAMU 5 MBELE
 
MaCHADEMA ni wizi na uzinzi tu wanajua. Hakuna Chama pale bora ACT. CCM hoyee
 
Upinzani Tanzania upo chadema peke yake. Na chadema inaangushwa kwa wizi wa kura wa ccm.
Kuna viongozi tuliwaamini kama Halima Mdee,Kina Nasari,Wilbraod Slaa,Mh Lowassa,nakadhalika.Wapo wapi leo hii.Tanznaia hakuna upinzani kabisa,kuna watu wenye akili kubwa wanaowadanganya wananchi wenye akili ndogo kuwa kuna upinzani.
 
Chama Cha Mbowe kimeshapotea. Kimekosa agenda... hata akiibuka Amber Ruti na tukio watalidandia na kulifanya agenda. Kumbukeni walivyodandia suala la Diamond Platinumz kwenye tuzo za muziki.
 
Kuna viongozi tuliwaamini kama Halima Mdee,Kina Nasari,Wilbraod Slaa,Mh Lowassa,nakadhalika.Wapo wapi leo hii.Tanznaia hakuna upinzani kabisa,kuna watu wenye akili kubwa wanaowadanganya wananchi wenye akili ndogo kuwa kuna upinzani.
Mtu kuhama kutoka chama kimoja kwenda kingine sio ishu kubwa, ni mambo ya kawaida. Tuache kuleta uadui pale mtu anapohama.

Mtu anayesaliti ni kesi tofauti na hao wapo kila sehemu hata ccm hivyo huwezi kuwaepuka bali kuwashughulikia inapotokea.
 
  • Wabunge wa Upinzani kutukana hadharani.

  • Wafuasi wa Upinzani kutoa lugha chafu
Weka unafiki pembeni kwanza halafu urudi hapa utajua kati ya wapinzani na ccm wepi Wana matusi na lugha chafu zaidi.
Nani alisema kama umekula pesa ya umma utaitolea kwenye matundu yote yaliyoko mwilini mwako?
Nani aliyesema unataka tumtie mimba mkeo ndio ujue tunafanyakazi?
Katika awamu ya tano viongozi wengi wa vyama vya upinzani ambao walikua nguzo katika vyama hivyo waliamua kuhamia chama tawala kutokana na sera nzuri za chama na utekelezaji wa sera zake.
Ile biashara ya kununua wafunge na madiwani wa upinzani iliyofanywa na magufuli na polepole nani asiyeijua?
Kampeni chafu
Chama kipi kinaongoza kuwahonga wananchi wassiojielewa vyakula, vinywaji, mashati na kofia za kijani wakati WA kampeni?
sasa najiuliza tatizo ni nini ,uzee wangu? kama ndio hivyo wawaachie wananchi, kama kuumwa mbona tangu 1984 naugua kisukari,
Kama umezeeka na una kisukari, umekaribia kufa! (by default). Kuwa mkweli uwe huru umrudie Mungu wako, atakupokea utakaporudi kwake. Acha unafiki ktk siku zako za mwisho.
 
Nakupinga
Uchaguzi wenyewe upo huru na haki? Tuanzie hapo

Kwa nini ccm hawaitaki Tume huru ya uchaguzi ikiwa wanatambua kwamba upinzani unajimaliza wenyewe
 
MaCHADEMA ni wizi na uzinzi tu wanajua. Hakuna Chama pale bora ACT. CCM hoyee
1666887023896.png

Wasaliti tupu kama hili
 
We subiri waje hapa kucomment usome matusi na mihemuko yao.

CCM sio chama cha kizazi hiki, kama mlifanikiwa kutawala nchi hii kwa hizi propaganda mfu, basi mjue siku zenu zinahesabika. Na bila machafuko hamtatoka mahadarakani. Hizo siasa chafu, na chaguzi za kihayawani mnazoendesha kwa kushirikiana na vyombo vya dola zinafikia mwisho. Jiandaeni kukaa pembeni kwa amani, hii kulazimisha kukaa madarakani kwa shuruti tutafikia pabaya lazima.
 
Kinachouangusha Upinzani Tanzania ni:-
1.CCM
2.POLISI
3.USALAMA WA TAIFA
4.TUME YA UCHAGUZI
5.WAKURUGENZI
6.WALIMU
7.UJINGA WA WATANZANIA.

Uko sahihi kabisa, huyu mleta uzi anafikiri kila mtu humu ndani ni mzee, hivyo hajui tunajua ni wapi upinzani unafanyiwa hujuma. Anajaribu kutuletea porojo za kiccm akidhani atatupoteza maboya hajui kuwa huwa tunaona chama la majizi ccm likiagiza vyombo vya dola kunajisi chaguzi. Na anatagemea kuna mpinzani atafanya siasa za kujikomba kwa CCM ili apate mlo.
 
Mtu kuhama kutoka chama kimoja kwenda kingine sio ishu kubwa, ni mambo ya kawaida. Tuache kuleta uadui pale mtu anapohama.

Mtu anayesaliti ni kesi tofauti na hao wapo kila sehemu hata ccm hivyo huwezi kuwaepuka bali kuwashughulikia inapotokea.
Hoja niliyokua najibu ni suala la kusema eti Chadema ndio chama cha upinzani peke yake.Sio kweli kila mtu pale anataka maslahi yake na hakuna mtu hafikiki,ni kiwango cha kufikika tu.Siasa ni biashara ya istagram au facebook account,unakusanya follower kisha unauza account.
 
Weka unafiki pembeni kwanza halafu urudi hapa utajua kati ya wapinzani na ccm wepi Wana matusi na lugha chafu zaidi.
Nani alisema kama umekula pesa ya umma utaitolea kwenye matundu yote yaliyoko mwilini mwako?
Nani aliyesema unataka tumtie mimba mkeo ndio ujue tunafanyakazi?

Ile biashara ya kununua wafunge na madiwani wa upinzani iliyofanywa na magufuli na polepole nani asiyeijua?

Chama kipi kinaongoza kuwahonga wananchi wassiojielewa vyakula, vinywaji, mashati na kofia za kijani wakati WA kampeni?

Kama umezeeka na una kisukari, umekaribia kufa! (by default). Kuwa mkweli uwe huru umrudie Mungu wako, atakupokea utakaporudi kwake. Acha unafiki ktk siku zako za mwisho.
Endelea kufuatilia huu uzi kisha uone nani atatoa matusi,au fuatilia kwenye mitandao ya kijamii uone nani atatoa matusi.
 
Back
Top Bottom