Joseph Kusaga ateuliwa Mwenyekiti Kamati ya Kuongoza kamati ya Kupendekeza vazi la Taifa

Tuna changamoto nyingi sana zinazotukabili. Sidhani kama vazi la taifa nikapaumbele kwasasa.

Kwa wizara ya Nchimbi hicho ni kipaumbele.. Na akifanikisha,atakuwa na cha kujivunia siku za usoni. Maana ni Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo.
 
Nashauri kamati husika iwaone Bakwata na taasis nyingine za dizaini hiyo haraka. Huenda tukapata vazi la taifa mara moja bila usumbufu wala gharama kubwa na itungwe sheria haraka ku-enforce atakayekwenda kinyume na vazi hilo akatwe kichwa hadharani na azikwe kabla ya swalat alasiri. Ya nini kupoteza muda?

Mkuu, labda nikuambie ukweli tu wewe ni Futuhi wa JF..wewe JF kwako ni sehemu ya mapambano ya udini tu hakuna cha ziada!
 
kunaitwa kutapanya mali. Vazi la taifa halibuniwi, ni kitu cha asili tu. Tuna variety kubwa sana Tanzania kuweza kuwa na vazi moja. Kwa nini mtu akiwa nje asijitambulishe kwa vazi la kabila lake? Yes Kikwete anavaa la kikwere, pinda anavaa ki posuta posuta!
 
Hivi ni muda gani sasa tangu hii ishu imekuwa inarudiwarudiwa? Vazi la Taifa linabuniwa na wasanii au Lilitakiwa kuchaguliwa kutokana na mavazi yaliyopo sasa?

Naona inakuwa ni ishu ya Ulaji Ulaji sasa!

ndiyo maana kachaguliwa Kusaga sasa.. Sasa hivi vazi kuna uhakika wa kulipata,mwanzo mwisho!
 
Mkuu mbona unashambulia wateuliwa?

Hata kama umuhimu wa vazi la kitaifa ungekuwepo si Joseph anaepaswa kuiongoza hiyo kamati.Joyce is smarter, clean and hardworker more than him.Si hivo tu bali ninaamini kuna watu wengi sana ambao wana uelewa mkubwa katika mambo haya...... Kusaga tayari ana kashfa za wizi wa kazi za wasanii ati anasema kaupeleka muziki wa bongo fleva mbali ???(crap). Tanzania nchi ya ajabu sana ukishakua mwizi na ukafahamika viongozi badala ya kukemea,, watakutengenezea mazingira ya kuiba tena na tena.
 
kunaitwa kutapanya mali. Vazi la taifa halibuniwi, ni kitu cha asili tu. Tuna variety kubwa sana Tanzania kuweza kuwa na vazi moja. Kwa nini mtu akiwa nje asijitambulishe kwa vazi la kabila lake? Yes Kikwete anavaa la kikwere, pinda anavaa ki posuta posuta!

wahaya wana vitambaa vya magome ya migomba nadhani,safi sana ile... Au wazunguke mikoani watafiti kwa makabila mbalimbali na Hassanali achukue sample kisha 'apewe' fursa na kamati atengeneze,labda kanzu,na nguo ya kike,ama shati la mikono mirefu na suruali kisha waje na vazi la couples. Kisha liwe linauzwa kwenye maduka mbalimbali kama watakavyoona inafaa. Lakini ziwe readymade sio kitambaa eti kila mtu akashone mwenyewe!
 
Vazi gani tena wanataka zaidi ya KANIKI KITENGE NA KHANGA??
 
Angalizo kuweni makini msije mkachagua yale Magwanda ndio vazi la taifa!

Yale yatabaki kuwa mavazi ya migambo tu!
mwambie Nape na Beno Malisa walioanza kuiga kuvaa hizo nguo za kikamanda.
 
Ufisadi mwingine at work. Watakuja na vazi la ajabu ajabu tu hawa kwa sababu ufisadi umeshawaathiri.

Lakini unaonaje tukiwasubiri kwanza wamalize kazi waliyopewe ndio tuwahukumu? Maana tukiwahukumu mapema hivi tutakuwa hatujawatendea haki.
 
Hata kama umuhimu wa vazi la kitaifa ungekuwepo si Joseph anaepaswa kuiongoza hiyo kamati.Joyce is smarter, clean and hardworker more than him.Si hivo tu bali ninaamini kuna watu wengi sana ambao wana uelewa mkubwa katika mambo haya...... Kusaga tayari ana kashfa za wizi wa kazi za wasanii ati anasema kaupeleka muziki wa bongo fleva mbali ???(crap). Tanzania nchi ya ajabu sana ukishakua mwizi na ukafahamika viongozi badala ya kukemea,, watakutengenezea mazingira ya kuiba tena na tena.

Joyce is smarter,yes... But she will deliver on the post she has more than the chairmanship.. She has that patronizing kind of attitude..
 
hiyo ni kupoteza muda kiswahili wameshindwa kukiendeleza na kukilinda sasa wameamia kwenye mavazi yamsaidie nini mtanzania, leo hii vijana wanakosa ajira kisa interview zinafanywa kwa english hivi kuwa na vazi na kitaifa ndo kupata maendeleo. Nitarudi baadae
 
Tanzania hebu tuache upuuzi....
Eti vazi la Taifa!!!
Kiswahili chenyewe tu tumeshindwa kukishamirisha.
Hivi tuna utamaduni mmoja hapa Tz??
Hivi tuna kabila moja hapa Tz??
sasa itawezekana vipi kwa namna ya nchi yetu ilivyo kuwa na Vazi moja??
hizi ni porojo tu kama zile za muziki wa Taifa.....!!!!

Mkuu, labda nikuambie ukweli tu wewe ni Futuhi wa JF..wewe JF kwako ni sehemu ya mapambano ya udini tu hakuna cha ziada!

hapam mkuu yupo sahihi kabisa wale jamaa huwa hawachelewi kulalamika. utasikia wataandamana kupinga vazi la taifa ati linaharufu ya ukristo ndani yake.
 
Lakini unaonaje tukiwasubiri kwanza wamalize kazi waliyopewe ndio tuwahukumu? Maana tukiwahukumu mapema hivi tutakuwa hatujawatendea haki.

Tumbiri ndugu yangu hamna kitu kama hicho, tuwe na vitu vya msingi vya kusubiri kuliko kitu kama hicho eti vazi la taifa!
Hebu jipe tafakari utekelezaji wake utakuwaje??
Katika namna kiswahili tu kinaelekea kutushinda katika kuwa na msimamo wa kukisimami kama kweli "Lugha ya Taifa"
Ah hebu turudini kwenye mjadala wa KATIBA hawa mapoyoyo wasituyumbishe kwa mambo ya kijingajinga haya
 
hivi hiyo kamati niyakujitolea au watalipwa posho za vikao na safari???? Kama ni ya posho basi kodi imeumia,na tunaomba viongozi wetu wawahurumie wananchi wengi wa tanzania hususani vijijini wenye matatizo mengi ya kimsingi kama ukosefu wa huduma za afya,elimu bora na walimu, ukosefu wa maji safi, na miundo mbinu kama barabara etc, vazi la kitaifa kwa wakati huu sio priority. Ila kama ni kamati ya kujitolea itakuwa siyo mbaya
 
Uteuzi mzuri sana huu Joseph amelifanyia mengi hili taifa kimuziki hope siku moja hili taifa ltampa heshima kubwa anayostaili. SALUTE JOE!

Labda ungeyataja hayo 'mengi' yaliyofanyika katika nyanja ya muziki,ndo ningekubaliana na wewe mkuu.
Halafu uteuzi sio mahali pa kulipa fadhila kaka ni mahali anapowekwa mtu kutokana na utendaji usio na shaka katika nyanja husika.

Lakini unaonaje tukiwasubiri kwanza wamalize kazi waliyopewe ndio tuwahukumu? Maana tukiwahukumu mapema hivi tutakuwa hatujawatendea haki.
Mkuu, hii s verdict kwa hao wajumbe, ni maoni kuhusu umuhimu wa hiyo nadharia ya kwua na vazi la taifa... tumechelewa sana, hili lilitakiwa liwepo tangu 1960s ndio lingekuwa relevant. Sasa hivi ni kutafita kuanzisha malumbano yasiyo na kichwa wala miguu na kupoteza fedha zetu bila sababu ya msingi
 
Back
Top Bottom