Mchengerwa ateua Kamati Maalum ya kuratibu Vazi la Taifa

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo ateua kamati maalum kwa ajili ya kuratibu upatikanaji wa vazi la taifa.

Zaidi soma:

1658348783437.png
 
Kumuweka masoud kipanya nadhani Jambo kubwa zuri linakuja

Ingawa hata majina hayo mengine yote NI mazito kazi zao zinaeleweka..

Naomba wasisahau kuhusisha Tehama...means idea zitoke kwa wote na zipigiwe kura baadhi selected Kisha mchakato uende hivyo kupunguza malalamiko wabongo ai wanafahamika.
Maneno mengi kazi Kidogo
 
Kumziba mdomo wasichorwe vikaragosi na kumtengenezea teuzi nyingine.

Hamna mkate mgumu kwenye chai
 
Kitu pekee atachoshauri Mpoto hapo ni kutembea pekupeku...

Tunaacha kuhangaika na vitu vya maana, tunahangaika na mambo yasiyo na tija...

Vazi lolote kwa sisi Waafrika ni zao la Wazungu kwa kuwa nguo zililetwa na watu weupe...
 
Siyo fair, kamati ina upungufu mkubwa, Waziri amteue Kangi Lugola haraka sana,maana alikuwa anapiga Kaunda suti zina bendera ya Taifa kwenye mifuko🤣🤣🤣
 
Hili vazi toka kipindi cha Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na sasa Samia bado halijapatikana tu?
Hivi hilo vazi linatafutwa au linabuniwa?
Lina faida gani kwa taifa?
Litawezaje kukubalika kitaifa?

Kwa maoni yangu hilo jambo lilipaswa litokee automatically kutokea kwenye jamii na serikali inalifanya kuwa kitu rasmi.

Yapo mambo mengi sana kwenye taifa yetu yaliibuka automatically tu na mwisho serikali ikatafuta namna ya kuyarasmisha. Kwa mfano;
Baba wa taifa (Nyerere)
Lugha ya taifa (Kiswahili)
 
Safi sana lazima ukivaa vazi la kitanzania ufeel wewe ni mtanzania, mchengerwa hua ni mbunifu sana na wizara aliyopewa ni ndogo apelekwe hata TAMISEMI maana hua ana kashkash za kueleweka,
 
Kila mtu avae vazi lake, vazi la taifa kwa context gani, huu ni ujinga mkubwa sana.

Hili taifa lina mahitaji ya asili ambayo ni :ardhi, watu, siasa safi na uongozi bora.

Pia lina mahitaji ya kisasa ambayo ni: ubunifu, technology, foreign investment kwenye strategic areas (oil and gas), visibility ( kufunguliwa kwaajili ya utalii na international trade) na amani.

Ata tukivaa vibwaya kama babu zetu hakuna shida
 
Hili vazi toka kipindi cha Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na sasa Samia bado halijapatikana tu?
Hivi hilo vazi linatafutwa au linabuniwa?
Lina faida gani kwa taifa?
Litawezaje kukubalika kitaifa?

Kwa maoni yangu hilo jambo lilipaswa litokee automatically kutokea kwenye jamii na serikali inalifanya kuwa kitu rasmi.

Yapo mambo mengi sana kwenye taifa yetu yaliibuka automatically tu na mwisho serikali ikatafuta namna ya kuyarasmisha. Kwa mfano;
Baba wa taifa (Nyerere)
Lugha ya taifa (Kiswahili)
Magufuli hakushughulika na hiyo kitu. Nakumbuka ilivuma sana enzi za JK. Nahisi viongozi wakikosa kazi za kufanya washauri wao wa pembeni wanawaambia we fanya hivi ili mradi usikike kwa aliyekuteua.

We si unaona makamba anazunguka na majiko ya gesi akigawa. Kajipa uafisa masoko wa taifa gas. Sasa ni nini kile.?
 
... kwa upande wa mavazi ya halaiki wangeomba ushauri toka Chadema. Ni mabingwa sana wa mavazi nadhifu.
 
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo ateua kamati maalum kwa ajili ya kuratibu upatikanaji wa vazi la taifa.

Zaidi soma:

View attachment 2298155
My opinion: Kwa vile hii sii mara ya kwanza kuundwa kwa kamati ya vazi la taifa, kabla ya kuundwa kwa kamati hii, kulitakiwa kufanyike mambo makuu matatu
1. Tuletewe mrejesho wa kilichofanywa na ile kamati ya mwanzo
2. Kama imemaliza muda wake ivunjwe,
3. Ndipo sasa iundwe hii kamati mpya.
Vinginevyo this is duplicity and another wastage of time, money and resources!.
Kama kuna kamati iliundwa, na ipo, haiwezekani kila waziri aunde kamati yake bila kuvunja kamati iliyopo and thank God, wajumbe wawili mtu na mkewe Mustafa na Hadija ni wajumbe wa kama iliyotangulia, ivunjwe halafu kamati mpya ianzie walipoishia,

Mimi pia ni mdau wa vazi la taifa, na niliwahi kuuliza humu kuhusu maendeleo ya ule mchakato wa vazi la taifa

P
 
Back
Top Bottom