Joseph Kusaga ateuliwa Mwenyekiti Kamati ya Kuongoza kamati ya Kupendekeza vazi la Taifa

Vazi la Taifa maana yake nini hasa?na je linatachukua sura ipi,maana makabila ni zaidi ya 120,je litachukua suta ya lugha ya kiswahili inayotuunganisha sote au litakuwaje kwanza,na je kuna haja ya kupoteza rasilimali zetu kwa jambo hilo sasa?hivi kudumisha mila na tamaduni zetu na kubuni vazi hili zikoje?na hata hivyo vazi hili litabuniwa au kuchaguliwa kwa vigezo vipi maana naona sura nyingi zilizoko kwenye kamati hiyo ni pamoja na za bongo fleva.wizi mtupu,
 
Mi ningeona ni busara kuwa na kamati japo tuhoji hiyo studio iko wapi,ili iwanufaishe vijana wanaotaka kutoka kupitia muziki,sasa leo malipo ya kuandaa birth day ya JEI KEI tunayashuhudia,kwa dhuluma za studio na dhuluma kwa wanamziki alizofanya mteuliwa huyu,mimi binafsi sitolivaa vazi hili,nitavaa jinsi na magwanda tu.sitaki,big NO
 
Hivi watawala wetu wako makini kweli? Tuna matatizo mangapi TZ yanayohotaji ufumbuzi sasa na sio maamuzi haya ya kizimamoto. Vazi la taifa lina faida gani, na kwa nani? Ni watanzania wangapi watavaa vazi hilo wakati zaidi ya nusu hawana hata cha kutia mdomoni?

Hebu nyinyi watawala wa nchi hii, (hamstahiki kuitwa viongozi), kuweni makini, tafuteni njia za kuwasaidia Watanzania wajikwamue toka katika llindi la umasikini uliokithiri kabla ya kutoa mawazo-upupu kama haya. Hivi hamuoni haya baada ya kufanya maamuzi kama haya badae mnaenda kupitisha bakuli kwa wafadhili kuomba misaada ya elimu, afya, maji....? Kusema kweli nimeshaanza kujisikia aibu kujitangaza kuwa mimi ni Mtanzania kwa sababu yenu.

Mnatia kinyaa. Aaaaaggggghhhhhrrrrrrr!
 
Well said!

Mkuu, katika siku nimehamaki moja leo baada ya kusoma upuuzi huu. Naamini tupo wengi, na tungeweza kutoa hasira zetu kwenye visanduku vya kura, lakini hata huko wanachakachua.
Miafrika Ndivyo tulivyo [Source: Nyani Ngabu].
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom