Joseph Kusaga ateuliwa Mwenyekiti Kamati ya Kuongoza kamati ya Kupendekeza vazi la Taifa

Aghrrrr yaani
baada ya kuona
hii redio inampa
maujiko ya ndivyo
sivyo, Ameamua
kumtengenezea
ulaji! Ila kila lenye
mwanzo lina ukomo
endeleeni kulipana
fadhila kishkaji

cku yaja!!!
 
kuliwahi kuwa na kabifu ka chini chini kati ya Salma kikwete na Regina Lowasa kuhusu hili vazi
 
Vazi la taifa! So what? Waziri anakaa anaamua kuunda kamati ya kutafuta upuuzi! Tumekosa ya kufanya? Tusimjadili Kusaga bali umuhimu wa hilo vazi! Subiri msikie mabilioni yatakayotumika while Sewahaji panatisha!

hayo si ya Wizara ya Afya? Hii ni Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo..
 
hayo si ya Wizara ya Afya? Hii ni Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo..
Hahahaha! Priorities mkuu,haingii akilini Hali ya wodi ya Sewahaji tu pale Muhimbili pengine inasubiri wafadhili(sijui lini maana hata mpango rasmi hakuna!) lakini tunachota mabilioni kutafuta vazi la taifa! Kwanza vazi la taifa halina faida ya msingi kama unajua manufaa yake ku uplift uchumi wetu tuambie hapa,tuna matatizo mengi tena ya msingi ya kutatua tena kwenye sector hiyo hiyo ya michezo na utamaduni mfano haki miliki za wasanii na program za kueleweka kwa vijana kuinua michezo na si vazi la taifa! Kwanza spirit ya uzalendo inazidi kupotea kwa watanzania sababu za ufisadi alafu unawaletea nguo eti waipende nchi yao! Kama nguvu hiyo Nchimbi angeiweka kusaidia wasanii unajua angeokoa kodi kiasi gani na kuongeza ajira pia? Narudia tuupinge huu UPUUZI ni ulaji tu!
 
Vazi la taifa! So what? Waziri anakaa anaamua kuunda kamati ya kutafuta upuuzi! Tumekosa ya kufanya? Tusimjadili Kusaga bali umuhimu wa hilo vazi! Subiri msikie mabilioni yatakayotumika while Sewahaji panatisha!
Viongozi wa Tanganyika ni walevi wa chang'aa mpaka akili pia zimedumaa. Hata viwanda vya nguo hawana then wanawaza ujinga huu,ivi wale wamasai wa kilosa watafaidika nn na upuuzi huu. Kwa taarifa yao,hilo vazi lao hata chumbe lisifike kwani huku zenj naona watu wanavaa mavazi ya staha sana na sjackia kamati yyte kuundwa! By the way mbona vazi la taifa c vimini+vitop na jeans za maraprap, kamati ya nn tena jamani? Shame on all viongozi wa Tanganyika.
 
Joseph Kusaga,hebu tengeneza heshima ya karne! Kataa uteuzi with facts (najua hili Joe hawezi kabisaaaa!) lakini ni ushauri wa bure tu kaka Joe!
 
What for?

This leadership is so controversial. Huku wanadai hatuna pesa simamisheni ajira kwa 50%. huku tume ya vazi la taifa na mabilioni ya kusherehekea uhuru na hawataki kufuta posho, infact bila aibu wanajadili kuziongeza zizidi hata kima cha chini cha mishahara yetu. Pole nchi yangu na Watz wenzangu. Sijui kama uongozi huu nao umetoka kwa Mungu?
 
Hahahaha! Priorities mkuu,haingii akilini Hali ya wodi ya Sewahaji tu pale Muhimbili pengine inasubiri wafadhili(sijui lini maana hata mpango rasmi hakuna!) lakini tunachota mabilioni kutafuta vazi la taifa! Kwanza vazi la taifa halina faida ya msingi kama unajua manufaa yake ku uplift uchumi wetu tuambie hapa,tuna matatizo mengi tena ya msingi ya kutatua tena kwenye sector hiyo hiyo ya michezo na utamaduni mfano haki miliki za wasanii na program za kueleweka kwa vijana kuinua michezo na si vazi la taifa! Kwanza spirit ya uzalendo inazidi kupotea kwa watanzania sababu za ufisadi alafu unawaletea nguo eti waipende nchi yao! Kama nguvu hiyo Nchimbi angeiweka kusaidia wasanii unajua angeokoa kodi kiasi gani na kuongeza ajira pia? Narudia tuupinge huu UPUUZI ni ulaji tu!
Uwezo wako wa kuelewa ni mdogo sana mpaka inakuwa kazi kukuelimisha.cha kwanza swala la uanzishaji wa vazi la taifa ni uamuzi ulioanzishwa miaka mingi ila kwa sasa limepata uamasishaji mpya chini ya Nchimbi.....Vazi la taifa linaleta umoja kwa jamii ambayo ina makabila mengi na kuendelea kuonyesha sisi ni jamii moja kama ilivyo lugha ya kiswahili.umoja na ushirikiano unajenga jamii iliotulia na inakuwa kivutio cha utalii duniani na inasaidia kuongeza kipato cha nchi.Kamati haijaundwa kudesigne vazi kama mnavyozani kwani kazi hio ilifanywa na wasanii mbalimbali kwa sasa kamati inatoa maoni ya jumla kama watanzania wangependa vazi lipi kati ya hayo ndio ije hatua nyingine......nani leo hajui nguo ya kinigeria kwa mfano!nani hataki nguo ya kitanzania
 
Ili kuepuka Cost na muda, wangepitisha tu MAGWANDA ya CHADEMA kuwa Vazi la Taifa
 
Uwezo wako wa kuelewa ni mdogo sana mpaka inakuwa kazi kukuelimisha.cha kwanza swala la uanzishaji wa vazi la taifa ni uamuzi ulioanzishwa miaka mingi ila kwa sasa limepata uamasishaji mpya chini ya Nchimbi.....Vazi la taifa linaleta umoja kwa jamii ambayo ina makabila mengi na kuendelea kuonyesha sisi ni jamii moja kama ilivyo lugha ya kiswahili.umoja na ushirikiano unajenga jamii iliotulia na inakuwa kivutio cha utalii duniani na inasaidia kuongeza kipato cha nchi.Kamati haijaundwa kudesigne vazi kama mnavyozani kwani kazi hio ilifanywa na wasanii mbalimbali kwa sasa kamati inatoa maoni ya jumla kama watanzania wangependa vazi lipi kati ya hayo ndio ije hatua nyingine......nani leo hajui nguo ya kinigeria kwa mfano!nani hataki nguo ya kitanzania
Hakuna kisicho na faida ndugu lakini uzito wa faida unategemea sana priorities kama Taifa.wote tunaijenga taifa moja kwanini tunashindwa kuboresha kwa mfano wodi ya Sewahaji iliyo ktk hali mbaya kwa kisingizio cha ukosefu wa fedha alafu tunakwenda kuunga bilions kwenye huu upuuzi? Umeitaja Nigeria unafikiri Mavazi yao yamewaletea umoja? Wao waliunda kamati kama hizi la sijui mavazi? Hujui usemalo ndugu.nimebahatika kuzunguka nchi hii hasa vijijini najua hali ilivyo nchi hii,nimetembelea shule za msingi na vituo vya afya,unaweza kulia!ninavyoona upuuzi kama huu tena nikijua pesa nyingi tu zitaungua inauma sana,unajua hata jeshi letu limeshindwa kuokoa wenzetu juzi kwa wakati mafuriko yalipotokea sababu ya vifaa? Hawa hawa wanajeshi walikuwa wanavunja matofali kwa vichwa juzi! Kama akili yangu ndogo kwa haya sawa mkuu!
 
Kusaga.jpg

WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi ameteua Kamati Maalumu ili kukamilisha mchakato wa kupendekeza vazi la Taifa ambalo litakuwa miongoni mwa vitambulisho mbalimbali vinavyotambulisha utaifa wa Tanzania.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam inasema kuwa kamati hiyo imeanza kazi mara baada ya uteuzi na itatakiwa kukabidhi taarifa yake Februari 28, 2012 kwa Dk. Nchimbi. Alisema hatua inayofuata sasa ni kuwashirikisha wananchi kuhusu mapendekezo yaliyopo na hatimaye kupendekeza vazi mahususi linalotambulisha utaifa wa Watanzania.

Wajumbe waliochaguliwa katika kamati hiyo ni pamoja na Joseph Kusaga ambaye atakuwa Mwenyekiti; Angela Ngowi Katibu; wajumbe ni Habibu Gunze, Joyce Mhaville, Mustafa Hassanali, Absalom Kibanda, Makwaia Kuhenga na Ndesambuka Merinyo.

"Mchakato wa kupata vazi la taifa umeshapiga hatua kubwa, wabunifu wazalendo wa mitindo ya mavazi wameshashirikikishwa na kutoa mapendekezo yao,” alisema Waziri Nchimbi kwenye taarifa hiyo.

Source
HabariLeo | Kamati ya kupendekeza vazi la Taifa yatajwa
nilisha sahau kuhusu hilo swala.kumbe bado mpaka leo halijapatikana!!?
 
Nimeipotezea nyororo hii mara kadhaa nikiona upuuzi gani huu, tunaacha mambo ya msingi ya kitaifa twashughulikia mabazee, lililonistua ni hili Jina kuwamo "Makwaia" namtambua Kama mtu
 
Sor ckumalizia....makwaia.....namtambua Kama mtini makini....kaingiaje hapa?
 
kwanza tujiulize,leo wamasai waache lubega wavae hayo ya akina kusaga? Tunaiga kutoka wapi haya na kwa faida gani mpaka tutumie miguvu yote hii?
 
ANASTAHILI, clouds walianza zamani sana kusapoti vazi la taifa

pamoja na upupu wa kisiasa wa clouds, jamaa pia wanastahili nishani ya kujitolea hasa kwenye maafa ... si mafuriko, mabomu nk

nimemnyonga mnyonge na haki yake nimempa

A real gentleman! I salute you mkuu!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom