Kamati ya Bunge yapongeza utekelezaji Wizara ya Utamaduni

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
738
478
Kamati ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imepongeza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo kulingana na Bajeti iliyotengewa kwa mwaka wa fedha 2022/23.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo ametoa pongezi hizo leo Machi 23, 2023 jijini Dodoma, wakati Kamati hiyo ilipopokea taarifa ya Utekelezaji wa Wizara kwa mwaka wa Fedha 2022/23, ambapo amesema Wizara imendeleea kutekeleza majukumu yake ikiwemo kusaidia wadau kunufaika na kazi zao pamoja na kutatua migogoro inayoibuka miongoni mwa wadau wa Sekta zake.

"Wizara hii ndiyo inayotoa furaha kwa Watanzania, sisi kama Wabunge tunataka kuona utulivu kwenye Sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, tuendelee kuwatia moyo vijana wetu wafanye kazi ili tuwe tunasikia mambo mazuri" Amesisitiza Mhe. Mkumbo.

Awali akiwasilisha taarifa ya Wizara, Waziri Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema kwa mwaka wa Fedha 2022/23 wizara imefanikiwa kuanzisha upya mchakato wa Vazi la Taifa, kuendelea kubidhaisha kiswahili pamoja na Kuratibu na kuandaa Tamasha la Utamaduni na Siku ya Kiswahili.

Mhe. Pindi Chana ameeleza kuwa, Wizara imefanikiwa kuratibu ushiriki wa Timu za Taifa katika mashindano ya Kombe la Dunia ikiwemo Serengeti Girls na Tembo Warriors ambazo zote zilifika hatua ya Robo fainali, huku akiongeza kuwa tayari Serikali inamlipa Kocha wa Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Star)

Aidha, Wajumbe wa Kamati hiyo wamechambua taarifa hiyo kwa nyakati fofauti ambapo wamesisitiza Wizara kuendelea kusimamia sekta hizo ambazo zimeajiri vijana wengi zaidi.

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na baadhi ya Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakiongozwa na Rais Ndg. Wallace Karia.View attachment 2563147View attachment 2563148View attachment 2563149View attachment 2563150View attachment 2563154View attachment 2563151View attachment 2563152View attachment 2563153
IMG-20230323-WA0002.jpg
IMG-20230323-WA0014.jpg
IMG-20230323-WA0011.jpg
IMG-20230323-WA0012.jpg


Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kamati hizi kazi yake huwa ni kupongeza na kisha kuvuta posho .

Na wakati mwingine huwa wanapongeza tu hata bila kukagua mradi ili mradi posho washapewa.
 
Back
Top Bottom