Kamati zinazoundwa kufanya Mchakato wa Vazi la Taifa mbona hazimalizagi Kazi?

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,280
Mchakato wa kutafuta vazi la Taifa ulianza Mwaka 2004 ambapo kuliundwa Kamati Maalum na aliyekuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo wakati huo, Dkt. Emmanuel Nchimbi

Julai 2022, iliundwa Kamati mpya ya kusaka vazi la Taifa ambapo ilielezwa ingeendelea ilipoishia Kamati ya awali iliyoundwa Mwaka 2014

Hata hivyo, kumekuwa na Sintofahamu nyingi kuhusu Kamati hizi ambazo hutumia Fedha za Serikali kwenye kazi hiyo huku mchakato ukiishia njiani kila wakati
 
Hizo kamati haziwezi kubuni vazi la taifa katika nyakati hizi za utandawazi. Watu wa dini watabaki kuvaa mavazi ya maadili ya dini zao. Wahuni watabaki kuvaa mavazi ya kihuni, makahaba watavaa mavazi ya kikahaba na waungwana watavaa mavazi ya kiungwana. Siku hizi wanawake wengi hawajifungi kanga wanatembea na visuruali vya kubana huku wengine ni wamama watu wazima na wameolewa na wana watoto. Unakuta mama mtu mzima kavaa sare kama mtoto wake mdogo wa kike wote wamevaa visuruali vya kubana na wanatembea mitaani bila aibu. Wanaiga mavazi ya fasheni toka nje ya nchi
 
Back
Top Bottom