Joseph Kusaga ateuliwa Mwenyekiti Kamati ya Kuongoza kamati ya Kupendekeza vazi la Taifa

TUMBIRI

JF-Expert Member
May 7, 2011
1,933
1,199
Kusaga.jpg

WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi ameteua Kamati Maalumu ili kukamilisha mchakato wa kupendekeza vazi la Taifa ambalo litakuwa miongoni mwa vitambulisho mbalimbali vinavyotambulisha utaifa wa Tanzania.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam inasema kuwa kamati hiyo imeanza kazi mara baada ya uteuzi na itatakiwa kukabidhi taarifa yake Februari 28, 2012 kwa Dk. Nchimbi. Alisema hatua inayofuata sasa ni kuwashirikisha wananchi kuhusu mapendekezo yaliyopo na hatimaye kupendekeza vazi mahususi linalotambulisha utaifa wa Watanzania.

Wajumbe waliochaguliwa katika kamati hiyo ni pamoja na Joseph Kusaga ambaye atakuwa Mwenyekiti; Angela Ngowi Katibu; wajumbe ni Habibu Gunze, Joyce Mhaville, Mustafa Hassanali, Absalom Kibanda, Makwaia Kuhenga na Ndesambuka Merinyo.

"Mchakato wa kupata vazi la taifa umeshapiga hatua kubwa, wabunifu wazalendo wa mitindo ya mavazi wameshashirikikishwa na kutoa mapendekezo yao,” alisema Waziri Nchimbi kwenye taarifa hiyo.

Source
HabariLeo | Kamati ya kupendekeza vazi la Taifa yatajwa
 
ANASTAHILI, clouds walianza zamani sana kusapoti vazi la taifa

pamoja na upupu wa kisiasa wa clouds, jamaa pia wanastahili nishani ya kujitolea hasa kwenye maafa ... si mafuriko, mabomu nk

nimemnyonga mnyonge na haki yake nimempa
 
Hivi ni muda gani sasa tangu hii ishu imekuwa inarudiwarudiwa? Vazi la Taifa linabuniwa na wasanii au Lilitakiwa kuchaguliwa kutokana na mavazi yaliyopo sasa?

Naona inakuwa ni ishu ya Ulaji Ulaji sasa!
 
Nadhani c suala la kubuni,mavazi tunayo ilitakiwa tu kuchagua lipi litambuliwe "la kitaifa" tuseme hao jamaa watabuni vazi ambalo wala haliwahi kuvaliwa na jamii/kabila yoyote?
 
Basi tuchukue tu jezi ya Taifa stars, ndo iwe uniform ya taifa.
Hao wote ni kupewa ulaji tuu, mbona kuna mavazi mengi sana yaliyopo? kwanini wasichukue mojawapo badaya ya kuanza kuunda kamati? This country bwana!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kuteuliwa kwenye kamati ya aina yoyote sio sabuni ya kusaficha mtu awaye yoyote dhidi ya ufisadi, unyonyaji na ubadhilifu wa kazi za wasanii wa Tanzania.

Ajisafishe kwanza kwa kurudisha jengo la THT litumike kwa kazi iliyokusudiwa ya kuinua vipaji vya watoto yatima na wale wanaoishi mazingira magumu.

Vilevile arudishe studio iliyotolewa na Rais wa Tanzania. Ile ni studio ya Wasanii wote wa Tanzania sio ya wakina Barnaba na Linnah tu. Media zake zisitumike kama sehemu ya kukomolea wanaomkosoa.

Mia
 
Kusaga.jpg

WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi ameteua Kamati Maalumu ili kukamilisha mchakato wa kupendekeza vazi la Taifa ambalo litakuwa miongoni mwa vitambulisho mbalimbali vinavyotambulisha utaifa wa Tanzania.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam inasema kuwa kamati hiyo imeanza kazi mara baada ya uteuzi na itatakiwa kukabidhi taarifa yake Februari 28, 2012 kwa Dk. Nchimbi. Alisema hatua inayofuata sasa ni kuwashirikisha wananchi kuhusu mapendekezo yaliyopo na hatimaye kupendekeza vazi mahususi linalotambulisha utaifa wa Watanzania.

Wajumbe waliochaguliwa katika kamati hiyo ni pamoja na Joseph Kusaga ambaye atakuwa Mwenyekiti; Angela Ngowi Katibu; wajumbe ni Habibu Gunze, Joyce Mhaville, Mustafa Hassanali, Absalom Kibanda, Makwaia Kuhenga na Ndesambuka Merinyo.

"Mchakato wa kupata vazi la taifa umeshapiga hatua kubwa, wabunifu wazalendo wa mitindo ya mavazi wameshashirikikishwa na kutoa mapendekezo yao," alisema Waziri Nchimbi kwenye taarifa hiyo.

Source
HabariLeo | Kamati ya kupendekeza vazi la Taifa yatajwa

Ufisadi mwingine at work. Watakuja na vazi la ajabu ajabu tu hawa kwa sababu ufisadi umeshawaathiri.
 
Uteuzi mzuri sana huu Joseph amelifanyia mengi hili taifa kimuziki hope siku moja hili taifa ltampa heshima kubwa anayostaili. SALUTE JOE!
kumbe angepewa kutafuta wimbo bora wa kienyeji! Tangia najitambua hii huenda ni kamati ya 20 ya kutafuta vazi la taifa lakini majawabu bado! Mimi nijuavyo vazi la taifa labda litokane na ngozi ama magome ya miti/migomba sasa sijui wanasuti wetu watavaa ngozi kama JZ wa SA?
Hivi na hiyo kamati si italipwa posho ya kazi? Zile kamati zingine nazo zililipwa posho bila matokeo?
 
mmmh!hizi propaganda tumezichoka sasa kila waziri akija anaongelea vazi la taifa then anamaliza muda wake hakuna kinachofanyika!
Aibu nyingine ninayoiona hapa ni kuwa ni miaka mingapi sasa hatuna vazi la taifa?miaka hamsini hatujui vazi linalotutambulisha watanzania.Tuache maneno tuwe serious katika mambo ya muhimu kama haya!!
 
Angalizo kuweni makini msije mkachagua yale Magwanda ndio vazi la taifa!

Yale yatabaki kuwa mavazi ya migambo tu!
 
W. J. Malecela;3027216]Uteuzi mzuri sana huu Joseph amelifanyia mengi hili taifa kimuziki hope siku moja hili taifa ltampa heshima kubwa anayostaili. SALUTE JOE!



Dah.sema yeye mziki ndo umemfanyia mengi.wasanii choka
 
Wapumbavu wote walioteuliwa kwenye hiyo kamati. Wamekosa kazi za kufanya! Vazi la taifa ndio nini? Upuuzi mtupu.
 
Hivi vazi la Taifa linabuniwa kila baada ya miaka mingapi? Kwa kumbukumbu zangu miaka michache iliyopita mashindano ya kubuni vazi la taifa yalifanyika na mshindi alipatikana. Sasa inakuwaje tunarudia kazi hiyo hiyo? Pengine Nchimbi angetueleza watanzania anarudia hili zoezi kwa sababu zipi? Na hizi hela za anatoa wapi wakati kodi inamshinda? Mwaka huu tumeshuhudia NHC wakitoa vyombo nje kwenye ofisi za wizara hii ya Nchimbi kwa sababu ya kutolipa kodi!

Yapo mambo mengine siyaelewi na Nchimbi hajaeleza, Tanzania tuko makabila zaidi ya 100, unawezaje kupata vazi la Taifa very late kwenye uhai wa Taifa huku ukiwa na makabila mengi hivi? Hiki ni kitu kilitakiwa kifanyike wakati wa uhuru (early 1960s) na sio sasa! Na hao watu walioteuliwa wana uelewa mpana kiasi gani kuhusu historia na tamaduni za makabila ya Tanzania?

Yote tisa, kumi, Nchimbi anabuni vazi la taifa lipi? Tanzania au Tanganyika? This whole thing is a waste of money! Tuna kanga na kaunda suti Nchimbi anataka nini zaidi!
 
Back
Top Bottom