Joram Kihango vs Willy Gamba

Hivi inakuaje mnatutia mshawasha wa hivyo Vitabu alafu msitwanbie vinapatikana wapi au tutavipataje?
 
Ni wapi naweza kununua vitabu hv njama,kikosi cha kisasi na kufa na kupona vyote vimeandikwa na Elvis Musiba!
 
walikuwepo ma staring wazuri wengi... Edie Kakhi... Kwenye unyama wa mafia! Na majambazi kama Dr. MOTOWN.. AKA mzungu katili, KABWE MAKANIKA... Aka Jitu kumbuka... Akina jarufu Ram na mzee Helgal ajenti wa MAFIA tanzania... PIA KILIKUWEPO KITABU mbio za jasusi... Nakikumbuka saaaana na staring alikuwa mkali saana! Baadae tukasoma MASHIMO YA MFALME SULEIMAN... tukamuona UMBOPA.. aliefundishwa vita na UMSOLOPOGAAS! NA PIA tukasoma HADITHI YA ALLAN QUATERMAIN.. NIKAMUONA umsolopogaas na shoka lake INKSOKAZ! HAKIKA hivi vitabu vya alan quatermain niliamini ni vya kweli. Na mtunzi aliitwa H. RIDER. HAGARD. ni mwingereza maarufu sana wa karne ya 20!

Daaaaadadaaa!!!! kulaleki!!!! umenikumbusha unyama wa mafia nilisoma series zote tano! halafu hapo kwa Allan Quaterman mama alianza kunihadisia nilipokuwa mkubwa nilivitafuta mwenyewe!! HIVI YAWEZEKANA NCHI YETU INARUDI NYUMA? Mbona wenzetu bado wanao wakina Sedney Sheldon (japo naye amefariki) au wakina James hadley chase?
 
Duh umenikumbusha mbali mdau. Joram kiango alikuwa ni noma hasa kile kitabu cha tutarudi na roho zetu. Ila sikuwahi kujua kwamba ni marehemu. Duuh may his soul rest in peace.
 
Nadhani bado nakumbuka kidogo............
Kufa na Kupona-Wizi wa Karatasi za Siri
Njama-Harakati za Ukombozi Kusini mwa Afrika
Kikosi Cha Kisasi-Mtanange ulikuwa pale DRC Kongo
Kikomo-Wizi wa Almas Mwadui
Hujuma-

I stand to be corrected......Hivi Mkuu wapi ntapati vitabu hivi?
Hujuma mimi sikusoma maana wakati wam mzee mwinyi kilipigwa marufuku. Waliokisoma walinihadithia kwamba alikuwa anazungumzia madawa ya kulevya na kilikuwa kinamuelekeo wa kuisema serikali tukufu na kwamba willy gamba alikufa akiwa kwenye mission. alitoa na cha kinaitwa nitalipa kisasi kwamba mtoto wa willy gamba ndiye alikuja kulipa kisasi cha baba yake kuuwawa nacho pia kilipigwa marufuku (hizi ni hearsay sina uhakika). Lakini cha mwisho ni RUNGU alikuwa anazungumzia mauaji ya rwanda. Kuna kingine nimesahau jina lakini aliweka platform yake arusha nacho pia kilikuwa kinazungumzia majasusi wa Afrika kusini kuja kuua viongozi wa nchi zilizomstari wa mbele wa ukombozi wa Afrika. aaa nimekikumbuka kinaitwa HOFU
 
tutarudi na roho zetu kilikuwa kiboko sana lakini kuna kile najisikia kuua tena kilikuwa moto! Be. R. Mtobwa alianza ku reprint vitabu vyake lakini Msiba nadhani alikuwa busy sana na Chamber of commerce. Wale ambao mlifanya naye kazi hebu tuambieni ELVIS E. Msiba alikuwa mtu wa karakta gani?
 
Tuwa si zama za shigongo? mbona yeye akumbukwi! au ndo nabii akubaliki kwao
Mkuu hakuna mtu wa kumdharau Hussein Tuwa. Yeye hayuko kwenye level ya Shigongo. Ni Mkali sana na kanma umeona kuna comments zinazomkubali. Ukisema nabii hakubaliwi kwao kwani hawa tunaowajadili ni wa wapi? Sema mshawasha wa hawa una mambo mengi sana maana unakumbusha na historia za wakati wetu wa ujima na wakati kila kitu ni analogy!!!!hahahha!! TUWA bado ni kiboko sana kwa kizazi hiki. Shigongo anaandika kitabu kikubwa na anavuta maneno ili kiwe kikubwa na kuna wakati huwa anasahau ameandika nini. Huwezi andika vitabu kwa fujo hivyo ingawa kwa Level za wakina mama wa magazzeti ya udaku anawabamba sana.
 
walikuwepo ma staring wazuri wengi... Edie Kakhi... Kwenye unyama wa mafia! Na majambazi kama Dr. MOTOWN.. AKA mzungu katili, KABWE MAKANIKA... Aka Jitu kumbuka... Akina jarufu Ram na mzee Helgal ajenti wa MAFIA tanzania... PIA KILIKUWEPO KITABU mbio za jasusi... Nakikumbuka saaaana na staring alikuwa mkali saana! Baadae tukasoma MASHIMO YA MFALME SULEIMAN... tukamuona UMBOPA.. aliefundishwa vita na UMSOLOPOGAAS! NA PIA tukasoma HADITHI YA ALLAN QUATERMAIN.. NIKAMUONA umsolopogaas na shoka lake INKSOKAZ! HAKIKA hivi vitabu vya alan quatermain niliamini ni vya kweli. Na mtunzi aliitwa H. RIDER. HAGARD. ni mwingereza maarufu sana wa karne ya 20!

Mama Aliniambia Jina Langu Limetokana Kitabu Hicho..Nilifanikiwa Kukisoma Mwaka Juzi Ingawa Haikuwa Original Version Lakini Nilikubali Kuitwa Allan Quartamain!
 
Tafuta riwaya yake nyingine inaitwa mhanga wa ikulu, nayo ni noma sana.
Tuwa anafuatia baada ya Elvis Musiba na Edwin Semzaba.

Muhanga wa ikulu ni cha BEKA MFAUME na yeye yuko vizuri sana. Edwin Semzaba sikumsoma sana. Mimi alikuwa ni Hammie rajabu na Fred katalambuya (kama sijakosea). Nadhani hawa pia ni marehemu yaaani!!!!
 
walikuwepo ma staring wazuri wengi... Edie Kakhi... Kwenye unyama wa mafia! Na majambazi kama Dr. MOTOWN.. AKA mzungu katili, KABWE MAKANIKA... Aka Jitu kumbuka... Akina jarufu Ram na mzee Helgal ajenti wa MAFIA tanzania... PIA KILIKUWEPO KITABU mbio za jasusi... Nakikumbuka saaaana na staring alikuwa mkali saana! Baadae tukasoma MASHIMO YA MFALME SULEIMAN... tukamuona UMBOPA.. aliefundishwa vita na UMSOLOPOGAAS! NA PIA tukasoma HADITHI YA ALLAN QUATERMAIN.. NIKAMUONA umsolopogaas na shoka lake INKSOKAZ! HAKIKA hivi vitabu vya alan quatermain niliamini ni vya kweli. Na mtunzi aliitwa H. RIDER. HAGARD. ni mwingereza maarufu sana wa karne ya 20!

Umenikumbusha mbali sana ndugu yangu. Rider Hagard ni mwandishi maarufu sana wa zamani. Alifariki mnamo miaka ya 1920. Hadithi ya Allan Quartermain aliiandika mnamo mwaka 1898. Kabla ya hapo aliandika kitabu cha Mashimo ya Mfalme Sulemani. Ni vitabu vizuri sana... Hakika ungedhani ni habari za kweli, kwani zilihusisha baadhi ya maeneo na matukio ya kweli. Loh, sijui kama vijana wa leo wanaweza kupata vitu kama hivyo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom