Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 74,871
- 155,840
Ulikuwa unavutiwa zaidi na yupi kati ya wakali hao?
Ulikuwa unavutiwa zaidi na yupi kati ya wakali hao?
Joram Kiango malaika wa Shetani..lakini wote kwa ujumla Riwaya zao zilikuwa nzuri sana .
Hivi mbona sasa hazipatikani?anayejua zunzuzwa waoi tafadhari tuwasiliane
Zawadi ya ushindi mtunzi alikuwa nani nimesahau?
Tena Musiba aliandika vitabu vyote hivyo kipindi alichokuwa anatumikia kifungo kirefu jela. Baada ya kifungo, alirudi uraiani, biashara imemchanganyia uandishi ndio basi tena.Ninavyofahamu mimi willy Gamba hakuwa mwandishi wa vitabu vya hadithi isipokuwa ni jina lililotumiwa na mwandishi wa vitabu maarufu wakati huo ambaye sasa ni mfanyabiashara maarufu vilevile anayeitwa A.MUSIBA. Nakumbuka KITABU CHAKE CHENYE HADITHI YA KUSISIMUA YA KIPELELEZI KATIKA JIJILA KINSHASA ( KUFA NA KUPONA )cha A.MUSIBA aliyetumia jina la Wily Gamba Kama Muhusika mkuu.
Kwa kweli umenikumbusha mbali enzi hizo kusoma vitabu vya hadithi ilikuwa ni mojawapo ya starehe kama si kwenda cinema.Nimesoma karibu vitabu vyote vya willy gamba,kuanzia kikomo,kikosi cha kisasi,hofu,njama,tutarudi na roho zetu,na vile vile vya joram kiango kama najisikia kuua tena,pesa zako zinanuka,dar es salaam usiku na vingine.Naweza kusema kila mmoja alikuwa na uzuri wake ila pointi nyingi atachukua willy gamba ambaye alikuwa anacheza kama mtu wa usalama wa taifa tofauti na joram kiango ambaye alikuwa anacheza kama mpelelezi wa kujitegemea.
Tena Musiba aliandika vitabu vyote hivyo kipindi alichokuwa anatumikia kifungo kirefu jela. Baada ya kifungo, alirudi uraiani, biashara imemchanganyia uandishi ndio basi tena.
Ulikuwa unavutiwa zaidi na yupi kati ya wakali hao?
Mkuu hapo kwenye red muhusika mkuu hakuwa Willy Gamba alikuwa Joram Kiango
Joram Kiango malaika wa Shetani..lakini wote kwa ujumla Riwaya zao zilikuwa nzuri sana .
Hivi mbona sasa hazipatikani?anayejua zunzuzwa waoi tafadhari tuwasiliane
Zawadi ya ushindi mtunzi alikuwa nani nimesahau?[/QUOTE]
Ni Ben Mtobwa,amefariki mwaka huu mwanzoni,Mungu amrehemu.
Enzi za Nyerere, sometime hata bila sababu, mtu anakunywa mvua nyingi tuu hata bila sababu ya msingi. Hata mimi Mzee wangu ni mhanga wa enzi hizo na walikuwa wote huko.Kumbe jamaa alitupwa lupango, nini ilikuwa sababu hasa ya kifungo hicho kirefu?