Vitabu vya Ben R Mtobwa vinapatikana kwenye maduka ya vitabu yaliyopo DSM na vimetolewa tena na Mkuki na Nyota

Vp vya willy Gamba vinapatikana wapi ili nasi ambao hatukuvisoma tuvifaidi manake tittle tu inaonyesha vimekamilika.

Nataka nicheze movie nikitumia script ya vitabu hivi. Je nani ana haki ya hakimiliki kwa mujibu wa sheria?
Ninavyofahamu mimi willy Gamba hakuwa mwandishi wa vitabu vya hadithi isipokuwa ni jina lililotumiwa na mwandishi wa vitabu maarufu wakati huo ambaye sasa ni mfanyabiashara maarufu vilevile anayeitwa A.MUSIBA. Nakumbuka KITABU CHAKE CHENYE HADITHI YA KUSISIMUA YA KIPELELEZI KATIKA JIJILA KINSHASA ( KUFA NA KUPONA )cha A.MUSIBA aliyetumia jina la Wily Gamba Kama Muhusika mkuu.
Kwa kweli umenikumbusha mbali! Nakumbuka kitabu cha NJAMA, mwanafunzi mmoja alikiiba nyumbani kwao na kuja nacho shuleni. Ilikuwa kukipata kwa kuazima lazima ufanye booking ya moja week mbili. Baadae ikawepo booking ya mchana na ya usiku. Ukiamua kusoma mchana maana yake ukose vipindi, ukibahatika kupewa uende nacho nyumbani basi kama hujamaliza kesho yake unajifanya kuugua ili usije shule. Ila jamaa walivyokuwa na usongo unashutukia wamekufuata huko huko.