Joram Kihango vs Willy Gamba

zingetenezwa movie zao ingekuwa bomba sana, kama allan quartemain, movie zake zipo ni safi sana
 
you guys..long time. Kuna kitabu nlikisoma nliazima library ya arusha mkoa, kinaitwa MBIO ZA JASUSI..dah kilikua nooma. those days..

Mkubwa acha kabisa, nimekitafuta nikaishia kuambiwa Mkapa alivipiga marufuku hivyo vitabu. Kuna cha kwanza kilichotangulia Alex alipoenda mara ya kwanza south sijui kinaitwaje nilichokipata hakukua na jalada wala kurasa za mwanzo hivyo sikufanikiwa kujua jina lake. Ila Stori za hivyo vitabu ni balaa.

Kwa mara ya kwanza nilianza kusikia visiwa vya Roben, CIA n.k
 
Hivi mrembo Zabibu alikuwepo katika simulizi ya kitabu gani...? nadhani ni Njama kama sikosei (nisahihishwe tafadhali). Willy Gamba alipojibarizi naye...alimsifia sana na kumwambia "Yaani, wewe kweli ni mtamu kama zabibu"
 
wote wamekufa na kazi zao zimekufa, Hamie Rajabu nae maskini

Kuna kitabu kimoja cha Hammie Rajabu, kinaitwa Nimekoma Ukuwadi. Ambacho kilikuwa na Riwaya tatu (nisahihishwe kama nimekosea); hiyo ya Nimekoma ukuwadi, na nyingine iliitwa "Si uliringa?"; ya tatu iliitwa "shogayo hasidi" RIP Hammie...Tuli enjoi sana vitabu vyako.
 
Willy Gamba bana mara nyingi akiwa ndio kwanza yuko likizo akila raha na mrembo ndio anapigiwa simu ya kuitwa ghafla Dar! Hapo anajua kimeshanuka,akifika Dar anapokelewa na namba 4 wanaelekea hadi ofisini na kumkuta bosi mkuu amefura kwa hasira kuashiria hali ni tete na ile bosi kumuona tu anamuita "namba moja umefika?" na bosi wake anapomuita kwa namba badala ya jina lake la Willy Gamba ujue kuna jambo zito!!

RIP ELVIS MUSIBA.... Ulikuwa mtu mwingine kwenye uandishi na kutufanya tujisikie salama na kuipenda nchi yetu kwani enzi hizo tuliamini Willy Gamba yupo kweli hivyo hakuna atakayeiweza Tanzania.
 
Hivi mrembo Zabibu alikuwepo katika simulizi ya kitabu gani...? nadhani ni Njama kama sikosei (nisahihishwe tafadhali). Willy Gamba alipojibarizi naye...alimsifia sana na kumwambia "Yaani, wewe kweli ni mtamu kama zabibu"
Yeah ni njama. sasa wakati anaelezea ford mustang gari mimi kijijini hata sijui linaonekanaje maana gari pekee tulikuwa tunaona ni isuzu injection za halmashauri ya wilaya zikileta walimu ama bwana mganga! sasa fikiri nilikuwa na amini ni gari sampli hiyo ndilo msichana kahongwa!!!!!
 
Willy Gamba bana mara nyingi akiwa ndio kwanza yuko likizo akila raha na mrembo ndio anapigiwa simu ya kuitwa ghafla Dar! Hapo anajua kimeshanuka,akifika Dar anapokelewa na namba 4 wanaelekea hadi ofisini na kumkuta bosi mkuu amefura kwa hasira kuashiria hali ni tete na ile bosi kumuona tu anamuita "namba moja umefika?" na bosi wake anapomuita kwa namba badala ya jina lake la Willy Gamba ujue kuna jambo zito!!

RIP ELVIS MUSIBA.... Ulikuwa mtu mwingine kwenye uandishi na kutufanya tujisikie salama na kuipenda nchi yetu kwani enzi hizo tuliamini Willy Gamba yupo kweli hivyo hakuna atakayeiweza Tanzania.

Trust me Image ya Willy Gamba ilifanya tuheshimu sana TISS lakini sasa MI-TISS ya leo inakula rushwa hata mwandishi gani akija akajenga image ya mfano wa Willy Gamba aili zetu zitakataa!!
 
Watabaki kuwa watu muhimu katika uandishi hapa duniani. Mungu awarehemu

Mkuu ni kweli nimesoma riwaya nyingi kwa mfano Tutarudi na Roho Zetu kwa kingereza kinaitwa"Zero Hour" cha Ben R. Mtobwa na njama ya Msiba ni balaa. Vitabu hivi ni vizuri sana.
 
msimsahau mzee Zahir Ally Zoro baba yake banana kwenya Mafia Mob

ha ha ha! Hapo kuna Kabwe Makanika aka Jitu Kumbuka. Huyu aliwasumbua aana Mafia mob wakiwa na wakubwa wao kina Don Fredrique Gaetano, Lucy Luciano na Giovani Pambieri. Kuporana almasi kule Maganzo Shinyanga na michezo ya mashine ya Magnum 357!
 
hapa unapoongea narudia 24hrs kwa mara ya sita!!!!

hiyo muvi uwa haichoshi, hata ukiangalia mara mia, hivi haikuendelea season 12? maana niliishia 11, kitu cha jack baur federal agent from ctu, ethan, madam president. ila tafuta nyingine ya kikorea IRIS nalo bonge 1 la muvi. wacha hao wazamani waadithiane kwa vitabu, sisi kwa muvi.
 
daaah umekumbushia mbali nilikuwa na vitabu vya Msiba njama, kikomo, kikosi cha kisasi nk nikamwazima rafiki yangu baada ya wiki moja akapata ajali akafari ikawa ndio mwisho wa kuwa navyo
 
Ulikuwa unajisikiaje unapomuona mwenzako ameshika KUFA NA KUPONA, NJAMA, KIKOSI CHA KISASI, KIKOMO ama SALAMU TOKA KUZIMU, TUTARUDI NA ROHO ZETU?, LAZIMA UFE JORAM, MIKONONI MWA NUNDA, NAJISIKIA KUUA TENA!!!HEBU KUMBUKA ULIPOKUWA UNASUBURI ZAMU YAKO NA WEWE UAZIME!!!
Nimeshangazwa kujua kwamba karibia kila mwandishi bora wa nyakati hizi amefariki. Nataka tuwakumbuke na kuwaombea. Lakini ni lazima nimpongeze mwandishi bora wa nyakati hizi HUSSEIN TUWA. kwa kweli ni mkali sana hebu kwa wale wapenzi wa riwaya tutafute riwaya zake MKIMBIZI, UTATA WA 9/12 NA MDUNGUAJU

Nakukubali mkuu, hussein tuwa ni kiboko wa sasa, ukweli wa dhati kwangu shigongo si mwana riwaya za kusisimua.
 
Duh,umenikumbusha mbali sana.Willy Gamba alikua bingwa wa kuvunja watu shindo
 
Huku wakichombeza kwa lugha ya kiitaliano

"cappi de tutti cappi" boss of the boss

"Cossa nostra"
 
mkuu IRIS nayo ni kiboko,ni kama wameiga baadhi ya vitu vya 24!

hiyo muvi uwa haichoshi, hata ukiangalia mara mia, hivi haikuendelea season 12? maana niliishia 11, kitu cha jack baur federal agent from ctu, ethan, madam president. ila tafuta nyingine ya kikorea IRIS nalo bonge 1 la muvi. wacha hao wazamani waadithiane kwa vitabu, sisi kwa muvi.
 
hiyo muvi uwa haichoshi, hata ukiangalia mara mia, hivi haikuendelea season 12? maana niliishia 11, kitu cha jack baur federal agent from ctu, ethan, madam president. ila tafuta nyingine ya kikorea IRIS nalo bonge 1 la muvi. wacha hao wazamani waadithiane kwa vitabu, sisi kwa muvi.
Mimi pia ni wazamani. Combination ya kutoka analog mpaka digital ni kali kuliko digital pekeyake. Mimi nimeanzia vitabu na hiyo IRIS nasubiri season 5. Kuna city hunter,Athena, swallow the sun na sasa namalizia A man called God hapa nasubiri wakorea watakuja na nini tena. Umeona kijana wa kidijitali?
 
nimeona kijana wa zamani, aya mkuu, hivi sinti bint kasri ilikuwa miaka gani vile? athena nimeicheki, nami pia naisubiria IRIS no 5.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom