Iwaay

Member
May 21, 2016
36
55
Kuna mambo yanayoendelea kwa wananchi wa jimbo la babati mjini kama tu CCM watafanya makosa na kurudisha jina la Pauline Gekul. Wananchi wengi wanasema wamemchoka Paulina nakusema bora hata Esta Mahawe au achukukiwe mtia nia aliyeshika nafasi ya nne Mwalimu Darabe.

Kuna taarifa za chichi chini kuwa kamati ya Wikaya haimtaki Esta ambaye aliongeza kura za wajumbe na kwa upande wa kamati ya mkoa imempa Esta alama B ambayo inaonyesha kuwa anakubalika kwa maaana waliona mchango wake kimkoa katika bunge lililopita akiwa Mbunge wa viti maaalum kupitia mkoa wa manyara.

Kinachotakiwa ni CCM kuangalia kati ya wale watia nia 32 yupi anakubalika kwa wananchi ili apite mapema na kwa kishindo katika uchaguzi wa mwezi wa kumi.
 
Back
Top Bottom