Jedwali la Mengi: Nani hayumo?

shalom,

Ndiyo nililipiwa kwa kuwa sikuwa ma uwezo..ila kupewa pesa siyo kosa ziwe za kifisadi ama la...unajuaje pesa ulizosomeshewa na baba yako hazijatokana na Rushwa?

ila nililipiwa na nani?hapo ndipo haujui kabisa....ona unavyopotea,leta ushahidi

siyo hoja..Shaloom na wewe umo kwenye Payroll..Mie nadhani zinachangiwa sana na umasikini wa watanzania...yaani unakuta mzee mzima kama slava anaanza kulia lia apewe fadhila..yaani it totally ashame..

Ukiangalia kabisa ,maneno ya Rostam na Mengi na maelezo yao yote yametoka humu humu JF..

kuna mtu alikuja kuwasaidia ku-compile mambo...Bila JF hakuna kitu

Ndugu Gembe (kamanda wa kutetea mafisadi)

Mimi nimesoma bure mwanzo mwisho siipendi sana hii kwa sababu mimi siyo mjamaa ila sasa nifanyaje

Nina uhakika baba yangu hakuwa fisadi kwani maisha tuliyishi yalikuwa ya furaha lakini ya kawaida ya kuringana kabisa na kipato chake. nakumbuka kabisa njisi majirani wetu wote miaka hiyo walivyokuwa na video na baba yangu akiwa na cheo kuliko wao lakini hakuweza kuafford. sijui hao wengine walizipataje lakini hiyo ni moja tu ya mambo mengi yalionifanya nijue kuwa hatukuishi kwa fedha ya kifisadi. Wewe kama baba yako alionja fedha za kifisadi ndiyo maana amekuachia laana na wewe ya kuopenda ufisadi

Mimi kumtetea mengi akinilipa atakuwa chizi kwani haitaji kufanya hivyo kwani hata asiponilipa nitamtetea. Kwa hiyo kuwa kwenye payroll itakuwa kwangu ni bonus. Na sigopi kujulikana kuwa namtetea mengi hata kidogo maadamu najua kuwa yuko sahihi

Wewe na salve mna tofauti gani wote ni vibaraka wa ufisadi, wote mnalialia ovyo alafu unakuja kumgeuka mwenzio du! nyie mafisadi kwa kugeukana bwana!

Hongera kwa kukiri kuwa umesomeshwa na fisadi na kwa taarifa yako mimi sitaki kujua kama ni nani au alikupa fedha ya currency gani na kwa njia ipi mimi nilichotaka kujua ni dhana nzima ya kuwa wewe umelambishwa fedha za kifisadi.

Unaitajikuombewa kutoa hiyo laana!
 
ambao hawamo kwenye payroll ya Mengi

1.Gembe

Kamanda wa kutetea mafisadi

Mzee toka umemaliza Masters yako uwezo wa kuchanganua mambo umekuishia.....ni wazi uko kwenye payrol ya Rostam, kama kweli huoni anachokifanya kila siku kwenye nchi yetu basi unatatizo kubwa zaidi. Kwanini unabadili majina ya hapa JF kuja mtetea Rostam? staili ya uandishi wako inabaki ile ile......big fonts...
 
I have this Feeling,

Wakati mwingine wakati unahisi mtu akimtetea ROstam au kina Lowassa au Mkuu wa nchi basi huyo yupo kwenye Payroll ya mafisadi.

Kwa ushaihidi ule ule mie nahisi watu hawa watakuwa kwenye payroll ya mengi,haiwezekani watu kumtetea tu mzee huyu wakati huo huo wanpigia chepuo utawala wa kisheria(Mzee kaingilia mahakama)!

Ni utawala gani wa kisheria unaruhusu watu kuzungumia kesi zilizoko mahakamani na kutoa hukumu?

Mie mpaka sasa huwa nasikia Rostam ni Fisadi,ila sijawahi kuona ushahidi wa ufisadi wake!

Aliye nao naomba kwa nia nzuri tu aulete,aje na uthibitisho kama,Rostam alikuja na vithibitisho kwa yale aliyoyafanya mengi.

Ila mpaka sasa mie naona ni tetesi kuwa Rostam ni fisadi ila hakuna vithibi,mpaka nitakapothibitishiwa hayo!

uje na ushihidi wa makaratasi yeye ndiyo mmiliki wa KAGODA,yeye ndiyo miliki wa DOWANS na malipo yaliyowahi kufanywa naye!

watu hawa nimewasoma sana na leo nafikia kusema wako katika payroll,Nahisi ila kuna ukweli,maelezo yao kumtetea mengi ni unbiased

Naomba tuchole Jedwali lingine,mie i have a feeling na siku zote huwa sibahatishi nikihisi,huyu ni mmoja watakaokuwa wanafadhiliwa na Mengi!

1.Mzee Mwanakijiji

2.Kubenea

3...............

Namheshimu sana Mwanakijiji ila naomba aje akanushe tu kwa maneno yake kuwa yeye siyo miongoni mwao!

sitaweza kumhukumu mtu bila ya kuwa na ushahidi ila kama tunavyohisi kina rostam ni mafisadi bais mie nahisi kina Mwanakijiji wanalipwa na Mengi,Period

ambao hawamo kwenye payroll ya Mengi

1.Gembe
2.Invisible
3.Msanii
4.Mfumwa
4.Pasco
5...

Wakati haya mapambano yanaanza hata mengi mwenyewe alikuwa kimya kabisa hakuna hata gazeti lake lililokuwa linaandika haya. Baadaye wakaanza kwanini no body knowz.

Tunachojadili si nani yuko kwenye payroll ya nani bali nani ni fisadi. Evidence zilishatolewa kwa wale wanaosoma magazeti km Mwanahalisi, Tanzania Daima na Raia mwema mambo yalikuwepo mle. Sasa sijui unataka uletewe mlangoni. Pia mfano hapa JF pia iliwahi kuwekwa baadhi ya vitu nafikiri ukifukua kwenye past post uatapata majibu may wasiliana na Mod atakusaidia.

Haya mambo ya nani yuko kwenye payroll nafikiri hatuyataki hapa maana hayajengi bali yanatupotezea muda.
 
Mederator – naomba nitoe ushauri: Wote wale wanaoonekana katika Jf wanapinga jitihada za dhati za wengine kupinga ufisadi na kuliokoa taifa letu katika janga pamoja na pengine vita ya wenywe kwa wenyewe wafutwe uanachama.

Waanzishe Forum yao ya kutetea mafisadi kwani wana uhuru kabisa wa kufanya hivyo, na wawe wanatoa upuuzi wao huko. Kama vile yalivyoanzishwa hapa nchini magazeti ya kutetea mafisadi – e.g. Sauti ya Umma, Nyundo, Taifa Tanzania (la Bagenda), Tazama, Mtanzania na Rai na mengineyo ambayo sasa yamekuwa ya kufungia maandazi.

Waondoke ktk JF yetu – kwani sisi hapa tuna malengo maalum kama nilivyotaja, na wao kama wana malengo yao kinyume na yetu, basi hapa siyo mahala pao tafadhalini sana, waondoke waka-pursue malengo yao huko.

Ni upuzi kabisa kulinganisha ile JEDWALI YA ROSTAM eti na huu ubunifu wa JEDWALI YA MENGI. Hawa akina Gembe, Invisible, Msanii Pasco ni watu gani, wanajulikana hasa mienendo yao kihalisi katika jamii hadi kuwalinganisha na akina Sophia Simba, Nchimbi, Serukamba na Makamba?

Moderator – Waondoke, waondokeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!! Watuache wenyewe.
 
UZURI WA jf ni WE DARE TALK OPENLY...hata kama wengine mtakuwa hampendi mawazo yetu lakini ndio ukweli huo

UFISADI ufisadi..ndio nini ati?

hebu tupishe sie
 
Nchi haiwezi kujengwa kwa kuwa na watu wanao kubaliana kila kitu, hakuna tatizo watu kumtetea RA au Mengi kwa kuwa kila mtu anatetea masirahi yake kwa maana either ya taifa (lakini yakiwa ni yako kwani hakuna anayeongelea matatizo yanayoendelea Siri Lanka kwa kuwa hatuna masirahi nayo) na mwingine masirahi binafsi yanaguswa sana kuliko masirahi ya taifa hivyo anatetea masirahi yake.

Hapa hapakuwa na maana tena kama wote tutakuwa tunakubali post za watu wanaopinga ufisadi peke yao na hakutapendeza watu wote wakiwa wanapenda mafisadi, lazima tuwepo wote tukubaliane kwa kutokubalina ndio masirahi ya nchi yanaweza kujadiliwa vizuri.

Jamii inaundwa na watu wenye kila kitu cha tofauti, hii ndio hajabu ya Mungu kama yupo, kila mtu anakitu cha tofauti na mwenzie, hatuwezi kuwazuia kuongea kile wanachoamini kuwa ni sahihi kwa upande wao, wapewe nafasi ya kuexpress feeling zao bila kutumia lugha za matusi wala wao kutukanwa na wanaopinga ufisadi.

Then mimi nafikiri yote pamoja mafisadi tunayapenda wenyewe, kama CCM ni fisadi kweli kwanini wananchi wa kawaida wanaopata tabu sana hasa vijijini wanawachagua CCM, ndio maana sometimes nikiona mtu wa kijijini anataabika nasema its better kwani lazima wananchi wawe na shida sana kwanza ndio watajua kuwa kuna ulazima wa kubadilisha mfumo mzima wa uongozi

Sio siri alternative ya CCM inaweza isiwepo lakini JK amepwaya mno, nafikiri hata Mrema anaweza kumzidi katika kushugulikia issues zinazolikabili taifa sasa.

Kama angekuwa ameshugulikia matatizo ya mafisadi hawa watu wasingejibishana hata kidogo kwani wote wangekuwa ndani sasa hivi hasa hawawalioforge. Lakini walichangia CCM hawezi kuwashugulikia.
 
Jamani kila unapoenda soga ndo hii hakuna pa kukimbilia hata pale kwenye vichekesho na matani yetu wameanza kuleta habari hizi...hii post nimeinyofoa kwenye blog ya bongo celebrity.....nafikiri inaweza kusaidia kuelezea hisia zangu katika mpambano huu.
...............................................

Vita ya maneno kati ya Reginald Mengi na Rostam Aziz bado inaendelea na ndio kwanza inaanza kushika kasi. Baada ya Rostam kuachia yaliyoonekana kuwa "makombora", Mengi naye kupitia kwa mawakili wake amejibu mashambulizi. Jamii Forums wanazo video nzuri tu za majibu hayo.

Nimeketi na kujiuliza maswali kadhaa. Hivi vita hii ya maneno inamsaidiaje mtanzania wa kawaida? Nini mwisho wake? Je ni kupakana matope tu kwa ajili ya kuuza magazeti,kupotezea watu muda(ukiwamo muda wao wenyewe wahusika) au ni kweli kuna dhamira ya kweli ya kumsaidia Rais JK katika kupambana na ufisadi?

Kitu kimoja ambacho nadhani wote tutakubaliana ni kwamba tayari kuna matumizi mabaya sana ya vyombo vya habari. Vinapokatishwa vipindi vingine ili kuonyeshwa kinachoitwa "kipindi maalumu" ambacho ndani yake ni "mipasho na kujikosha" nachelea kusema kwamba huko siko na serikali kuu lazima iingilie kati.Zipo wapi mahakama? Fulani kakuchafulia jina,una uhakika na ushahidi wa kutosha, kwanini usiende mahakamani kufungua kesi? Lipo pia suala la uzalendo na uraia. Kama unajua kwamba fulani amekuwa akiifisadi nchi kwa muda wote huo,ulikuwa wapi kumfikisha kwenye vyombo vya sheria? Hapa ndipo ninapoona nia ni "kuuza magazeti" na wala sio kumsaidia yeyote. Kuna mzalendo kweli hapa kati ya Rostam na Mengi?
Lakini yawezekana ipo faida ya mchezo huu wa kutajana, kuchongeana, kupigana vijembe. Mwakani watanzania watapiga kura. Mchezo huu ukiendelea, utawapa watanzania nafasi nzuri ya kuchagua viongozi. Nani mkweli kati ya Rostam Aziz na Reginald Mengi? Tizama kwa makini, soma kwa makini, sikiliza kwa makini vita yao ya maneno. Ukweli utaujua.
 
no one is perfect. Mengi na Rostam wote wana lao jambo; haiwezekani wachimbane mikwara mizito namna hiyo bila kupelekana mahakamani. hii inadhihirisha wazi kwamba kampeni za 2009/2010 zimeanza kuweni macho watanzania wenzangu
 
Mkuu Gembe,
Nimeipitia post yako na nimeisoma kwa makini sana. Hata hivyo kabla ya kujibu nimekuta nalazimika kupitia post zako za nyuma kujiridhisha na msimamo wako katika haya mapambano. Pia nimesoma vigezo unavyotumia kuwashutumu watu kuwa wako kwenye payroll ya Mengi. Binafsi simfahamu Mengi, sina undugu naye na sidhani kama anayo hata habari kwamba kuna mwanachama JF anayejiita Mag3.

Hata hivyo, baada ya hiyo tathmini, kwa taadhima natuma maombi kwako na mimi uniorodheshe kwenye hiyo listi kwa sababu naunga mkono bila kificho vita anavyoendesha Mengi kwa sasa. Ila nitakuomba mambo mawili - kwanza, uweze kupata na wewe ujasiri wa kutueleza uko kwenye payroll ya nani. Pili kwa heshima na taadhima naomba uache hiyo avatar kwa sababu you are a disgrace to the face behind it - ni ombi tu.
Nyuma ya kila gabacholi, kuna sura nyeusi ti.
 
Bila shaka wamekupata GAME THEORY. Tuna tatizo kubwa sana Tz. Kuna watu bila aibu wanathubutu kuwatetea mafisadi! Hebu waanzishe Forum yao tujue moja: kwamba wanawatetea mafisadi kwa maslahi yao. Watuachie hii JF tupambane kwa lengo la kuirejesha nchi yetu kwenye mwelekeo sahihi. Magazeti uliyoyataja yanamilikiwa na mafisadi kama ifuatavyo: Sauti Huru (Subash Patel), Nyundo/Tazama (Lowassa), Mtanzania/Rai (Rostam Aziz), Taifa Tanzania (Nazir Karamagi). Na sasa fisadi Tanil Somaiya ameinunua Channel 10. Hebu sikilizeni upuuzi kwenye TV station hii iliyokuwa inaheshimika kabla ya kuangukia mikononi mwa mafisadi. Inasikitisha. Lakini ushindi katika vita hii ngumu dhidi ya ufisadi ni lazima!
 
The fact is we need whistle blowers like Mengi, regardless of his motive for doing what he is doing. If only we could have more of him in our country. I would support anybody with courage like his. You should understand that this is never easy for him. However, if he is found guilty of allegations made by RA, he should be charged for that.

I sometime ask myself, why is he doing this? Is he looking for popularity? Does he have personal conflicts with RA and others, lets’ say business like? As far as I am concerned, these don’t matter very much, let him shout as much as he can since it’s for the good of the country.
Nadhani tusiwe tunaangaliana usoni katika mambo haya.
God bless Tanzania!
 
Mederator – naomba nitoe ushauri: Wote wale wanaoonekana katika Jf wanapinga jitihada za dhati za wengine kupinga ufisadi na kuliokoa taifa letu katika janga pamoja na pengine vita ya wenywe kwa wenyewe wafutwe uanachama.

Waanzishe Forum yao ya kutetea mafisadi kwani wana uhuru kabisa wa kufanya hivyo, na wawe wanatoa upuuzi wao huko. Kama vile yalivyoanzishwa hapa nchini magazeti ya kutetea mafisadi – e.g. Sauti ya Umma, Nyundo, Taifa Tanzania (la Bagenda), Tazama, Mtanzania na Rai na mengineyo ambayo sasa yamekuwa ya kufungia maandazi.

Waondoke ktk JF yetu – kwani sisi hapa tuna malengo maalum kama nilivyotaja, na wao kama wana malengo yao kinyume na yetu, basi hapa siyo mahala pao tafadhalini sana, waondoke waka-pursue malengo yao huko.

Ni upuzi kabisa kulinganisha ile JEDWALI YA ROSTAM eti na huu ubunifu wa JEDWALI YA MENGI. Hawa akina Gembe, Invisible, Msanii Pasco ni watu gani, wanajulikana hasa mienendo yao kihalisi katika jamii hadi kuwalinganisha na akina Sophia Simba, Nchimbi, Serukamba na Makamba?

Moderator – Waondoke, waondokeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!! Watuache wenyewe.

Hatuondoki Ng'o!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom