Mafisadi walia baada ya kukiri wizi uliotokea Wilaya ya Kinondoni

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,047
20,411


Sijui, ila mie naliona hili katika sura tofauti, naliona kama ni dhana tu ya kutafuta vidagaa vidogo dogo kuvitoa kafara ili kuficha mambo makubwa maovu ambayo yanafanywa na watendaji pamoja na viongozi ktk sekta ya umma.

Kweli kabisa kama kweli ipo ndani mwetu, na utu unatawala nafsi zetu, hiyo milioni 67 kwa hao watu zaidi ya 20 kwa kipindi cha mwaka mzima, ndio hela ya kuwahukumu hao vidagaa hivyo mbele ya umma na media?

Hao wa kina mama kuna ambao wamechukua au wamesababisha upotevu wa laki 2, laki 5, 1mil, wengine 2mil, ni kweli kisheria wanakosa na wanastahili kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria, lakini ninachojiuliza kwanini hizi taratibu za kuhukumiwa hivi zinawagusa hawa vidagaa tu kwa hizi hela za ada wanazotafuta na haziwagusi wanaojilimbikizia mali ambazo hata kazi nazo hawana - ufisadi mkubwa?

Kama tunaamua kuhukumi hivi kwa hawa wadogo basi na hao mafisadi wakubwa pia wahukumiwe kwa stahili hii hii kama wanavyohukumiwa nayo hawa wakinamama wanaotafuta kwa njia isiyo halali hela ya ada na chakula kwa ajili ya familia zao.

Kinyume na hapo mimi naona ni uonevu kwa hawa kina mama na na hawa vijana, kinyume na hapo mie naona kama ni njia tuu inatumika kuwatoa kafara hawa vidagaa ili kupata popularity “tumechukua hatua”.

Kama sheria haifanyi kazi kwa usawa, hata mwenye kosa anapohukumiwa kwa sheria hiyo anakuwa ameonewa, haki na sheria lazima vionekane vikitendeka na kupatikana kwa usawa kwa watu wote bila kujali nafasi ya mtu.​
 
ded.jpeg

ATHUMANI MSABILA amerudishwa kutoka Igunga alipokuwa amehamishiwa kujibu tuhuma za wizi, Naona Uteuzi wake utenguliwe na apewe yule Dada anayefundisha IFM, ambaye alikuwa DC na juzi juzi ndio karudishwa chuo.
 
Back
Top Bottom