Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Hili swali linawahusu wale ambao hawatumii majina yao ya kweli hapa ukumbini. Je, jina lako lina maana yoyote? Kuna sababu yoyote ile iliyokufanya uamue kutumia jina hilo!?

Nilikuwa nimeamua kutosema lolote kuhusiana na hali ya kisiasa ndani ya nchi yetu (kuwa bubu) pamoja na kwamba nilikuwa siridhiki na mambo mengi sana niliyokuwa nayasikia kwa Watanzania wenzetu, kuyashuhudia kwa macho au kuyasoma kwenye magazeti yetu mbali mbali. Niliamua kuwa kimya kwa sababu nilijua sauti yangu kama zilivyo sauti za Watanzania wengi ambazo hazisikilizwi na walio madarakani, haitafika kokote.

Mpaka nilipoanza kutembelea hapa miezi ya mwisho wa mwaka 2006 nikafurahishwa sana na michango ya baadhi ya wanachama na kuona hapa kuna sauti ya umma ambayo kama itaendelea na kushamiri basi itasaidia sana kuleta mabadiliko ya kweli ndani ya nchi yetu.

Nilibahatika kuwa Bongo kipindi cha kuapishwa Kikwete, pamoja na kuwa hakuwa amenigusa kama kiongozi mpya wa nchi yetu nilitiwa hamasa kubwa kuwaona Watanzania wenzangu wakiwa na shauku kubwa ya kumpata Kikwete kama Rais mpya wa Tanzania na weng walikuwa na matumaini makubwa toka kwake na wengine kumuita "Mkombozi wetu". Watu walipoanza kulalamika kuhusu utendaji wake kama Rais wa nchi, mimi nilikuwa nawaambia ni mapema mno kuanza kumlaumu. Niliomba apewe angalau kipindi cha mwaka mzima tangu aingie madarakani na hapo ndipo anastahili kuanza kutupiwa lawama mbali mbali kuhusu utendaji wake.

Basi nilipoamua kujiunga nikaamua jina la Bubu maana nilikuwa nimeamua kunyamaza kimya kwa miaka mingi pamoja na kutoridhishwa na mengi. Nikaukumbuka na ule wimbo wa 'Nginde ngoma ya ukae" Bubu ataka kusema mambo yanapomzidia. Ndipo baada ya mwaka na ushee tangu Kikwete aingie madarakani nikaamua rasmi kujiunga ili niungane na Watanzania wenzangu katika mijadala mbali mbali inayohusu hatima ya nchi yetu maana ile miezi 12 ilikuwa imekatika na kuvurunda kwa srikali ya Kikwete kulikuwa kunazidi kushamiri.

Hivi ndivyo jina BAK lilivyozaliwa rasmi na mnamo February 2007 nikajiunga rasmi na ukubi huu wakati huo ukiitwa Jambo Forums.

Kama kuna baadhi mtapenda kuchangia kuhusu maana ya majina yenu na kama kuna sababu rasmi za kuamua kuyatumia majina hayo basi mnakaribishwa.

Sijui kwanini sijawahi kuisahau stori yako brother "BUBU ATAKA KUSEMA" .....
Ulinikaribishaga vizuri sana hapa jamvini,
sure sitaki kusahau kitu lol...
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hili swali linawahusu wale ambao hawatumii
[FONT=B
[FONT=Book Antiqua]

BAK, seven years down the line lazima itakuwa umepewa karama ya kusema, funguka, bubujika sema.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hongera B kwa thread nzuri
nilikuwa sijasoma daaah nimesoma mwanzo mwisho nimefurahi kujua/kupata maana ya majina hapa JF

Jina langu ndivyo nilivyo
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Sijui kwanini sijawahi kuisahau stori yako brother "BUBU ATAKA KUSEMA" .....
Ulinikaribishaga vizuri sana hapa jamvini,
sure sitaki kusahau kitu lol...

Ahsante sana Mkuu JG kwa maneno mazuri ulistahili makaribisho ya kuwekewa red carpet :):)...msalimie binti yetu :)
 
Hongera B kwa thread nzuri
nilikuwa sijasoma daaah nimesoma mwanzo mwisho nimefurahi kujua/kupata maana ya majina hapa JF

Jina langu ndivyo nilivyo

Hongera zako B, uendelee hivyo hivyo kucheza mbali na mkorogo :):)....Black is beautiful. Hongera kwa kuusoma uzi wote :):)
 
Kama inavyojieleza yenyewe, am a person likes to be happy and make others happy in and for the GLORY OF GOD. it is also kind of a prayer as i smile or make others smile i want also to be among of the Saints that GOD can count on them here down on earth
 
Happiness is always good for your health.
 
Hiyo NN haiko patented kweli? Manake nikiiona tu nakoki binduki yangu,lol!

Naongea na wanazuoni wanifanyie grafting ya mbeya ichanganywe na ya afghanistan, maana hii imekuwa diluted na matatizo ya Tanzania, watotot hawana mikopo, wagonjwa wanalala chini, madaktari wa kuwatibu hakuna, mafuta yamepanda bei, mgonjwa toka kijijini mpaka kituo cha afya anapanda bajaj ( kiluxury) vinginevyo Bodaboda, maji vijijini hakuna, dolari ianapanda siku hadi siku.

Kilo sukari, unga na mchele usiguse, bila NN maisha hayaendi hata kidogo.
 
Back
Top Bottom