Machifu na Mashujaa wa Iringa wampa Paul Makonda jina la Wigombikanana lenye maana ya Mlinzi wa Taifa

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,301
9,729
Ndugu zangu Watanzania,

Habari ndio hiyo kuwa machifu na mashujaa wa mkoa wa Iringa kwa pamoja na umoja wao wamempatia Mwamba Mwenyewe na kijana jasiri kusini mwa jangwa la Sahara Mheshimiwa Paul Makonda jina la WIGOMBIKANANA lenye maana ya Mlinzi wa Taifa letu.

Hii ni kwa kutambua jitihada zake kubwa katika kuwasemea ,kuwapigania na kuwatetea wananchi wanyonge na kumwambia ukweli na kufanya kazi vyema na kutekeleza vyema maagizo ya Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hasssan.

lakini pia Mheshimiwa Makonda alipewa mkuki kama ishara ya kumpatia nguvu ya kupambana na wote wanaotaka kudhoofisha uongozi wa Taifa letu chini ya uongozi shupavu na madhubuti wa Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hasssan,mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita,nyota ya matumaini,nuru ya wanyonge na mama wa upendo .

Mheshimiwa Makonda Anaendelea kuteka mioyo ya makundi yote , Anaendelea kugusa hisia za wengi, Anaendelea kuwa shujaa katika mapambano ya kumtetea mtanzania, amejitoa na kujitolea kwa ujasiri mkubwa sana kuwa msitari wa mbele kabisa katika kuona mtanzania anatendewa na kupata haki kwa haki bila kujali kipato chake wali hali yake.

Kinywa cha Mheshimiwa Makonda kimegeuka kuwa kinywa cha mamilioni ya watanzania ambao walikuwa hawana mahali pa kuzungumzia kero zao ,sasa Makonda komandoo amegeuka kuwa msemaji wao na sauti yao.ndio maana anagusa wengi na kuteka hisia za wengi kwa kuwa anazungumza yale yaliyojaza vifua na mioyo ya mamilioni ya watanzania.

Kwa hali inayoendelea huku mitaani na namna Mheshimiwa Makonda anavyokubalika na kupendwa na watanzania, naamini kwa dhati ya moyo wangu kuwa lipo kusudi la Mungu kumuinua na kumleta Mheshimiwa Makonda wakati huu ili amsaidie Mheshimiwa Rais kusikiliza sauti za watanzania na kuzipatia ufumbuzi. Moyo wa Mheshimiwa Makonda upo kwa watanzania kama ilivyo kwa Mh Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania mama samia suluhu Hasssan ambaye muda wote mawazo yake na upendo wake upo kwa watanzania.

ndio maana amekuwa akichukizwa sana na kuwa mkali anapoona kuna mtanzania anaonewa mahali fulani iwe na vyombo vya dola au watumishi wa umma au viongozi au watu binafsi.

Kazi iendelee mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Utakuta malevi fulani yamekusanywa hapo na kuitwa machifu kumbe ni upumbavu mtupu
Wivu tu umekushika mdogo wangu mvuta bangi.acha bangi na ufanye kazi kwa bidii uone kama jamii haitatambua mchango wako. Mheshimiwa Makonda ni tumaini jipya la watanzania wanyonge.
 
Mwamba Mwenyewe na kijana jasiri kusini mwa jangwa la Sahara Mheshimiwa Paul Makonda jina la WIGOMBIKANANA lenye maana ya Mlinzi wa Taifa letu.
Hahahaaaa........Nafikiri Watz waliokiuwa serious na hili Taifa ni wale waliofanikisha Uhuru tu, baada ya hapo tumegeuka Comedian au tuna matatizo ya akili lakini hatujitambui.
 
Hahahaaaa........Nafikiri Watz waliokiuwa serious na hili Taifa ni wale waliofanikisha Uhuru tu, baada ya hapo tumegeuka Comedian au tuna matatizo ya akili lakini hatujitambui.
Labda wewe ndiye mwenye matatizo lakini Watanzania wanajitambua vyema kabisa.
 
Back
Top Bottom