JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 626
- 938
Taarifa Binafsi ni taarifa zozote zinazohusiana na namna ya kumtambulisha au anavyotambulika mtu.
Mfano wa Taarifa Binafsi unaweza kujumuisha Jina, Anwani, Barua pepe, Nambari ya Kitambulisho Binafsi, Nambari ya Usajili, Picha, Alama za Vidole, Nyenzo za Kibaolojia, au taarifa nyingine zozote zinazoweza kumtambulisha mtu, zenyewe au kwa kuunganisha na taarifa nyingine.
Siku hizi baadhi ya Wakusanya taarifa wamekuwa wakibadilisha taarifa za kuhusu jina au anwani kwa kuweka ‘code’ (pseudonymize information), kama vile AB123, lakini hiyo bado ni Taarifa Binafsi ikiwa tu ‘code’ hiyo inaweza kufuatiliwa na kuonesha taarifa halisi za mtu.
Utazitambuaje taarifa binafsi za Watu?
Sheria ya Tanzania ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya mwaka 2022 imeanisha kuwa Taarifa binafsi maana yake ni taarifa kuhusu mtu anayetambulika ambazo zimetunzwa kwa namna yoyote, ikiwa ni pamoja na;
Lakini pia kwa Mujibu wa Sheria hiyo ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya mwaka 2022, Baadhi ya Taarifa Binafsi ni nyeti zaidi na zinahitaji kiwanngo cha juu cha ulinzi. Taarifa hizo ni Pamoja na zile zinazohusiana na;

- Taarifa binafsi zinazohusu rangi, asili ya kitaifa au kikabila, dini, umri au hali ya ndoa ya mtu binafsi;
- Taarifa binafsi zinazohusu elimu, historia ya matibabu, jinai au ajira;
- Namba yoyote ya utambulisho, alama au namna nyingine maalum inayomtambulisha mtu binafsi;
- Anwani, alama za vidole au kundi la damu la mtu binafsi;
- Jina la mtu binafsi linaloonekana katika taarifa binafsi za mtu mwingine anayehusiana naye au pale ambapo ufichuzi wa jina hilo utadhihirisha taarifa binafsi za mtu;
- Taarifa iliyotumwa kwa mkusanyaji wa taarifa binafsi na mtu, ambayo ni wazi kuwa taarifa hiyo ni binafsi au ya siri, na majibu kwa taarifa hiyo yanaweza kufichua maudhui ya taarifa ya awali, na mtazamo au maoni ya mtu mwingine yeyote kuhusu mhusika wa taarifa;
Lakini pia kwa Mujibu wa Sheria hiyo ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya mwaka 2022, Baadhi ya Taarifa Binafsi ni nyeti zaidi na zinahitaji kiwanngo cha juu cha ulinzi. Taarifa hizo ni Pamoja na zile zinazohusiana na;
- Taarifa ya vinasaba, taarifa inayohusu watoto, taarifa inayohusu makosa, miamala ya kifedha ya mtu binafsi au hatua za kiusalama, taarifa za kibayometriki;
- Ikiwa imechakatwa, ni taarifa binafsi inayoonesha asili ya rangi au kabila, itikadi za kisiasa, imani za kidini au kifalsafa, ushirika, uanachama wa vyama vya wafanyakazi, jinsia na taarifa za kiafya au mahusiano ya kingono; na
- Taarifa binafsi yoyote ambayo kwa mujibu wa sheria za nchi inachukuliwa kuwa ina athari kubwa kwa haki na maslahi ya mhusika wa taarifa