Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

PAESULTA,nilijijipa hili nikiwa shule ya msingi darasaa la sita mwaka 1993,sababu nilimpenda sana msichana mmoja hivi(amini usiamini mpaka leo hajanitoka moyoni ingawa hatukuwahi kuwa na uhusiano wowote wa kimapenzi kwani sijamuona tena baada ya kumaliza shule ya msingi zaidi ya mawasiliano ya barua kwa muda fulani tulipokwenda sekondari) ,anywa as i was saying nilijipa jina hili baada kuweza kuunganisha herufi ya majina yetu mawili na likatokea jina hili ambalo linatakiwa kurepresent mapenzi yangu kwa msichana yule kwa jinsi yalivyo.sidhani kama nitakuja kumsahau,aliniingia sana moyoni...

pole mdau, hata mimi imeshanitokea miaka ya 1990s, dah nilimpenda sana totoz fulani alikuja jirani yetu! tukawa marafiki sana! lkn siku alipokuwa anarudi kwao weeeeeee wacha nimwage 'chozi'. tangu aondoke siku hiyo sikuwahi muona tena! nimetafuta lkn wapi! jinsi nijisikiavyo kwake sijawahi kujisikia hivyo kwa totoz nyingine!! so, hauko peke yako!
 
Ukweli ni kuwa watu ndani ya JF wanatumia majina ya kubuni kwa kuwa demokrasia ya kweli hapa nchini hakuna, tuwe wakweli, serikali wanaweza kukuweka ndani just sababu unaweka mabaya yao kwenye mtandao, sababu habari nyingi za scandals huwa zinakosa concrete proof sababu mafisadi pia wanaakili wanafanya scandals huku wakijua wakiwa screwed wata unscrew kivipi hivyo wanaficha evidence. Nyote humu mnaogopa kukamatwa that is why we use funny usernames.

Lucky Dube said "Stand for the truth n u will stand alone"
 
Gashle, from sala gashle (origin; zulu) meaning = stay well, safe.
mwisho wa siku napenda kuwepo na amani kwa kila mtu, maelewano na wala sio mafarakano. japo roho inaniuma, maskini Tanzania yetu, mafisadi kila kukicha, uongozi dhaifu, wizi wa kumwaga, nk, lakni ningependa sote tupendane! tuwe kitu kimoja. kimbembe ni kwa namna gani?
 
ni kweli majina mengi huku hayana maana mengine ni matusi tu, mi hili ni jina langu halisi lkn kuna jamaa mmoja anajiita ITETEI LYA KITE hili siyo jina anamaanisha vitu vingine ila kuna majina mengine yenye kubeba ujumbe hayo sawa lkn haya mengine hapana
 
Ukweli ni kuwa watu ndani ya JF wanatumia majina ya kubuni kwa kuwa demokrasia ya kweli hapa nchini hakuna, tuwe wakweli, serikali wanaweza kukuweka ndani just sababu unaweka mabaya yao kwenye mtandao, sababu habari nyingi za scandals huwa zinakosa concrete proof sababu mafisadi pia wanaakili wanafanya scandals huku wakijua wakiwa screwed wata unscrew kivipi hivyo wanaficha evidence. Nyote humu mnaogopa kukamatwa that is why we use funny usernames.

Lucky Dube said "Stand for the truth n u will stand alone"
jina lako zuri linawakilisha uchungu ulio nao mpaka unaamua kulia ila uliyo yasema ni kweli demokrasia hakuna hasa nchi kama zetu ila tuwe na majina ya kistaarabu basi
 
PAESULTA,nilijijipa hili nikiwa shule ya msingi darasaa la sita mwaka 1993,sababu nilimpenda sana msichana mmoja hivi(amini usiamini mpaka leo hajanitoka moyoni ingawa hatukuwahi kuwa na uhusiano wowote wa kimapenzi kwani sijamuona tena baada ya kumaliza shule ya msingi zaidi ya mawasiliano ya barua kwa muda fulani tulipokwenda sekondari) ,anywa as i was saying nilijipa jina hili baada kuweza kuunganisha herufi ya majina yetu mawili na likatokea jina hili ambalo linatakiwa kurepresent mapenzi yangu kwa msichana yule kwa jinsi yalivyo.sidhani kama nitakuja kumsahau,aliniingia sana moyoni...

hahahaaaaa, you should be SULTANI wewe, I know you, dah!.
 
Superman = Extra Ordinary particular in helping people with problems no matter how difficult they are mostly by offering alternative solutions or some support. This happens only in my real life.
 
Chamtumavi
Sina makuu, sitamani cha mtu, nakula jasho langu. Ni bora nibebe mabox nipate rizki yangu, kuliko kutamani cha mtu. Ndiyo nikaamua kujiita Chamtumavi-Nakipenda kilichochangu, cha mwingine nakiona mavi.

i salute you mwaaaaaaaaaaaaaaaaah
 
Alsaidy {formaly al-busaidy} jina la ukoo wangu na najisikia fahari kutambulika hivyo. Ukoo uliyotawala Zanzibar na kuleta maendeleo makubwa na kuifanya Zanzibar kuwa commercial city kwa wakati huo.
 
Wakati niko school A level nilikuwa napenda sana mambo ya diplomasia na nilikuwa na dream kwamba siku moja nami niwe balozi wa Tanzania katika nchi yoyote. Wenzangu walinipachika jina la Ambassador na wakanishauri nisome International Relations. Matokeo yake? Sikuwa hata balozi wa nyumba kumi! I still treasure and honor my friends, and ofcourse my dream...... With due respect....
 
who cares?...very simple name and a serious question kwa watu wote hapa JF mjengoni?..nilikaa na kutafakari jinsi matatizo yooote na hoja zinazotolewa hapa lakini nikagundua hakuna hata mmoja anayejali wala kufuatilia..ndo maana nikauliza who cares?...and i dont care too...ndo maana huwa naongea na kutoa maoni yangu jinsi navyojisikia na sijali lolote na yeyote yule...WHO CARES?
 
Radical - my mind believes in equality and that only revolution can bring a solution, that if we do not for example like the Government we should overthrow it, simply decide your destiny.
 
NGALIKIHINJA
NGALI = ASIYE NA
KIHINJA = JIKO

Nilijipa jina hili kwa kumkumbuka mzee fulani tulikuwa tunaishi naye jirani nikiwa mdogo. Huyu mzee alikuwa ananihamasisha sana nijiunge na kundi lililokuwa linacheza ngoma ya kwetu. Vile vile alikuwa hajibu kitu kama utamsemesha lugha ya kiswahili huku akijuwa kuwa unafahamu lugha ya kijijini kwenu ambayo naye anaifahamu. Hayupo duniani hivyo kwa kumkumbuka yeye nikaamua kutumia jina lake la utani.
 
Shishi.....jina nililitunga kutokana na jina la kitoto nililopewa na mama. nilizaliwa hospitali moja mji wa Embu, Kenya, wakati huo kulikuwa na muziki ukifana sana ukiitwa' shiro murata' kwa kikikuyu inamaanisha 'shiro mpenzi'... 'shiro my love '. sasa pale spitali manurse wakaniita shiro. mama aliporudi nyumbani kawaambia dada na kaka zangu (am the fifth born) kuwa mtoto anaitwa shiro.....basi jina likashika mpaka wa leo naitwa shiro...basi ndio nami nikalifanyia mutation kidogo tu...ikawa shishi!

Hili jina limeshika kabisa ijapokuwa silitumii officially...watu wengine hawajui kuwa nina majina mengine!!! :D
 
Pronounced JETH-roh.
It is of Hebrew origin, and its meaning is "eminent". Moses' father-in-law, a priest of Midian.

Au Kwa watakao penda kutoa jina hili kwa wanao penda kulielewa kwa namna hii
:- Jethro ([ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Hebrew_language"]Hebrew[/ame]: יִתְרוֹ‎, Standard Yitro; "His Excellence/Posterity").
 
Back
Top Bottom