Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Sipo = hili nililipata wakati nipo Sekondari na hata nilipokuwa UDSM liliendelezwa na washikaji zangu kutokana na tabia yangu ya kuruka matukio pale yanapokuwa magumu kwa kukanusha tu kuwa mie sikuwepo bwana wakati ili linatokea.
 
Sivuti. Lakini napenda kuwa mkali kama vile mwenye hiyo tabia. Nalenga wale mafisadi.
 
kelelee.......napenda kupigia kelele any kind of injustice so when i joined this forum nikaona that should be my name lakini nikakuta tayari kuna mtu anaitwa kelele so i added the xtra e....
 
Renegade, Secret code ya BARAKA HUSSEIN OBAMA, naitumia kama secret name yangu, kwa kuwa hapa siyo lazima kutumia jina HALISI.
 
Richard asili yake ni Ujerumani likimaanisha kiongozi mwenye nguvu au "powerful leader".

Baada ya kuzaliwa nikajikuta naitwa jina hili kwa hio ndio jina nnalotumia.
 
Ab-Titchaz...

Ni corruption ya profession yangu ambayo imenichukua sehemu mbali mbali
ikiwemo Tanzania,Kenya na sasa Marekani. Bado tunaendeleza libeneke la
kufukuza ujinga..hata humu kwa kina Sheikh Baraka Obama.

Asanteni.
 
Geoff=my real name.kirefu kabisa ni geoffrey,sasa ni ngumu sana kwa watu kutamka
 
PakaJimmy.
Nani asiyejua story za zamami za Paka jimi na mbwaTom?

Nilijifunza kusoma na kuandika kwa kupitia story zilizoitwa hivyo wakati huo, nikishikiwa kiboko na babaangu akiwa mwalimu.

So nikaona ni jina ambalo siwezi kulitupa, maana ni kwa vitu kama hivi natesa na kusumbua mtaani sasa! lol!
 
it was in ALASKA,that realities of the world crept in my head,far away from parents,it stuck me that my future/destiny was now in my hands-the days of getting every thing on a plate were over.ALASKA became my dad and mum-the rest is history
 
MmmmmHH!???..watu wakianza na kauli ya "sivuti"...basi najaza papo hapo..LOL..Kwa roho safi mkuu.

Ngambo Ngali upo hapo?

Hajakosea kabisa hata kidogo, usijaze chochote ndio ukweli wenyewe?????? Lakini kuvuta bangi na kuibia maskini kipi afadhali, halafu elewa kuwa wanaovuta bangi wote ni shauri ya umaskini ili kupoteza mawazo ya kuonewa kunyanyaswa na kudhulumiwa. Wengine nanapoteza mawazo kama ifuatavyo Baada ya wavuta bangi wanafuata wanywa gongo na pombe za kienyeji baada ya hao wale wanokunywa bia kwenye kontainer, halafu hivyo hivyo upwards mpaka wale ambao wanatuibia na wakifurahia na kusherehekea kuiba huenda kujitakasa sehemu huku wakicheza gofu, kuvua samaki na maboti yao yenye baa ndani na au kunywa bia ya shs 4000/=, hela ambayo ambao ukimpa mvuta bangi ataenda kununulia watoto utumbo wa kuku ili wanae wasuuze matumbo yao yaliyochoka dagaa , mchunga na mnyavu.Lakini kabla ya wavuta bangi kuna wale wavuta petroli ambao hawana hamu ya kuishi wao wanatafuta njia ya mkato ya kwenda jehanamu na wako wengine wa unga hawa labda nisaidiwe nashindwa kuwaweka kwenye kundi muafaka.
 
Ziondaughter au Binti Sayuni

Sayuni mji mtakatifu wa Mungu ulioteuliwa kwa ajili ya wateule.Waitwao ni wengi lakini wateule ni wachache.
 
Lekanjobe = Hebu niseme
Babu yangu alikuwa msema kweli, akiwa msuluhishi katika jamii yake. Hakuwa na subira kumwambia waziwazi mtu yeyote anayeharibu "Kubinika!" yaani "Unaharibu!" hata kama ni kiongozi. Wakampachika jina la Kubinika kwa utani na ikamkaa hadi kifo chake.
 
Cynic kwa lengo la kuleta cynical flavor JF ( - Yes cynical, but constructive and a little bit off bit opinion). Nilikuwa fun wa JF tangu ianze (bila kujiunga rasmi) and there weren't many such contributors.
 
Back
Top Bottom