Ikulu: Rais hajaidhinisha posho za wabunge!

Status
Not open for further replies.
Hivi kwa nini asiseme tu kuwa hakubaliani nalo hilo jambo?

Halafu yeye malipo yake ni shi'ngapi?

Thubutu!? Iliwampigie kura ya kutokuwa na imani naye aachie ngazi? Never ! Aliponea chupuchupu lile suala la Jairo kwa hiyo wabunge lazima awaheshimu sana.
 
Haya sasa. Serikali inashindwa hata kutoa maelezo yanayoeleweka kuhusu posho ya wabunge ndiyo tuitegemee itatue tatizo la mgomo wa madaktari? Iinue uchumi? Tusiilaumu bure serikali ya Jk. Tujue kuwa hatuna serikali bali ni msukule tu. Hivi Jk anaposema kuwa wabunge waliangalie tena suala la posho anataka kusema nini wakati walipendekeza kiwango na yeye ndiye aliyebaki aidhinishe?

Jk anapolirudisha kwa wabunge suala ambalo limepelekwa kwake anakaa ikulu kule kufanya ninii? Amekwenda ikulu kutalii? Lazima afanye kazi kama rais siyo kutuletea usharobaro.
 
Hii aibu kwa Pinda na Makinda!

Sidhani kama hao watu wanajua kuna 'AIBU'. Walikuwa wanatetea posho za wabunge wakidhani zitapita kimya kimya kama walivyozoea! Wakapigana vijembe kuhusu posho. Haya sasa kila mtu ataibuka na kudai malipo zaidi bila hivyo watu wanagoma sijui nani atatoa huduma! au kufanyakazi za uzalishaji.
 
Haya sasa. Serikali inashindwa hata kutoa maelezo yanayoeleweka kuhusu posho ya wabunge ndiyo tuitegemee itatue tatizo la mgomo wa madaktari? Iinue uchumi? Tusiilaumu bure serikali ya Jk. Tujue kuwa hatuna serikali bali ni msukule tu. Hivi Jk anaposema kuwa wabunge waliangalie tena suala la posho anataka kusema nini wakati walipendekeza kiwango na yeye ndiye aliyebaki aidhinishe?

Jk anapolirudisha kwa wabunge suala ambalo limepelekwa kwake anakaa ikulu kule kufanya ninii? Amekwenda ikulu kutalii? Lazima afanye kazi kama rais siyo kutuletea usharobaro.

Anawarudishia waliangalie upya baada ya kuona maji ya shingo. Kukubali anashindwa na kukataa anashindwa pia. Kwa vile wabunge wa ccm na binamu yao shibuda ndio walikuwa wanadai posho kwa nguvu huenda watamhurumia na kuamua kupunguza kiwango! Aibu juu ya aibu! Nikimkumbuka shibuda alivyokuwa akitoa maelezo kuhusu ujira wa mwiha huku binamu zake wanashangilia nahisi kicheko!
 
Screw them! Hivi kuna vyama vingapi vinatawala Tanzania? Hivi waziri mkuu na rais wana matatizo ya mawasiliano?

Ama hii ni Kama serikali ya Mugabe na Tvsangirai, Kibaki na Odinga? Same team, same objective fighting other to achieve it = poor management!!!
 
Ukweli nilikuwa siamini kama Jakaya angeweza kukubali na kuruhusu posho za wabunge kupandishwa. Pole sana Jakaya, kila lawama unapewa wewe. Kweli ukubwa ni jaa.
 
Siku chache zilizopita Sumaye alipinga nyongeza ya posho kwa wabunge na akasema itaiweka ktk wakati mgumu serikali na rais maana makundi mengine ktk jamii nao watadai kuongezewa mishahara na posho . Akaibuka naibu spika Ndugai akamsimanga PM wetu wa zamani,sasa alichosema Sumaye kinajionyesha wazi.
 
Ukweli nilikuwa siamini kama Jakaya angeweza kukubali na kuruhusu posho za wabunge kupandishwa. Pole sana Jakaya, kila lawama unapewa wewe. Kweli ukubwa ni jaa.

Kidatu, sasa hapa unataka katika huu mkanganyiko lawama apewe nani? Kwani hii ya posho imeanza kujadiliwa leo? Kidatu, hii movie yote ni usanii tu katika kutafuta ahueni kwenye damage control. Mtu yeyote yule, ambaye hadi leo mwaka wa nane toka Kikwete aukwae Uraisi, hajamwelewa Raisi wetu ni mtu wa aina gani, hatakaa amwelewe, si jana, si leo wala kesho. Kikwete si kiongozi kwa sababu yeye mwenyewe anaongozwa na matukio na muda mwingi yanamkuta hajajipanga na hivyo kujikuta hana majibu yanayoeleweka kwa wakati muafaka.

Kidatu, hebu nieleweshe japo kidogo kwa sababu naona unampa pole, je Raisi amekubali ama hajakubali kuruhusu posho za wabunge kupandishwa?
 
Siku chache zilizopita Sumaye alipinga nyongeza ya posho kwa wabunge na akasema itaiweka ktk wakati mgumu serikali na rais maana makundi mengine ktk jamii nao watadai kuongezewa mishahara na posho . Akaibuka naibu spika Ndugai akamsimanga PM wetu wa zamani,sasa alichosema Sumaye kinajionyesha wazi.

Sumaye could make good Presidents far much better than Jakaya ...
 
Jamani great thinkers wa JF, lets be serious! WHAT IS GOING ON WITH OUR COUNTRY?!!! MBONA NI KAMA TUMELAANIWA NA ALIYETULAANI KESHA KUFA! TUMGEUKIE NANI SASA! SO SAD!
 
Ni hii mambo ya madokta hawezi thubutu, sasa sijui atakaa kimya hadi lini, hii ni a black and white issue.

Na kama anategemea "timing", kwenye situation hii it doesnt work kwasababu eventually ni lazima a pick either side ama asolve both sides...
 
​Suala la posho mpya kwa wabunge: JK Makinda wajikaanga:
Jana jioni nilisoma taarif ya Salva Rweyemamu ikikanusha kuwa hakuna baraka za Rais katika posho za wabunge, Makinda anasema rais ametia mkono, hivi ndivyo vwalivopanga kutuchezea akili.

Soma habari hii toka Tanzania daima 01/02/2012
RAIS Jakaya Kikwete na Spika wa Bunge, Anna Makinda, wamejiweka pabaya kwa kutoa kauli zinazopingana kuhusu posho mpya za kikao kwa wabunge.
Huku Makinda akisema Rais Kikwete ndiye aliyebariki posho hizo za shilingi laki mbili kwa siku, Kurugenzi ya Mawasiliano ilisema kwamba Rais hahusiki.
Makinda alitoa kauli hiyo jana mjini hapa mbele ya waandishi wa habari, akisema Rais Kikwete ndiye aliyebariki posho hizo.
Kauli ya Makinda inakuja baada ya Waziri Mkuu naye kubariki posho hizo, baada ya kusema alikabidhiwa faili hilo na Rais Kikwete.
Jana Spika huyo alisema posho hizo, ambazo zimebarikiwa na Rais Kikwete, zilianza kutolewa tangu kikao kilichopita na zinalipwa kwa wabunge waliohudhuria vikao na kusaini.
Hata hivyo, Ikulu ilitoa taarifa jioni ikisema hakuna mahali ambapo Rais Kikwete amebariki posho hizo.
“Maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, kuhusu suala hili yako wazi kabisa na hakuna mahali ambapo Rais Kikwete amebariki posho hizi. Maelekezo ya Rais kuhusu suala hili ni kama ifuatavyo: “Kwanza, Rais Kikwete anakubali haja ya kuangalia upya posho kwa wabunge, lakini amewataka wabunge kutumia hekima na busara katika kulitafakari suala hili,” ilisema taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais Kikwete amewataka wabunge kutumia kikao cha sasa cha Bunge kulizungumza upya suala hilo.
Hata hivyo, Ikulu haikuweza kueleza msimamo wa Rais kuhusu posho hizo kama zitolewe au la.
Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wameliambia gazeti hili kuwa kauli ya Ikulu ni ya kipropaganda kwa ajili ya kumlinda Rais baada ya kuona wananchi wanakerwa na posho hizo.
Baadhi ya wachambuzi wanasema kama Rais angekuwa hataki posho hizo zilipwe, kwanza Makinda asingepata ujasiri wa kuzitetea, na pili Rais Kikwete mwenyewe angetoa msimamo wa moja kwa moja badala ya kuzungukazunguka.
Wanasema hata kupeleka suala hilo kwa Waziri Mkuu Pinda, ilikuwa janja ya Kikwete kuwarushia wengine lawama, maana Pinda hawezi kutekeleza au kubariki suala ambalo bosi wake hataki.
Wengine walisema kauli ya Ikulu haiwezi kuaminika kwa kuwa si mara ya kwanza kutoa matamko ya kumtetea Rais katika masuala tata, kama ilivyokuwa sakata la Richmond, ambalo licha ya taarifa ya Ikulu kusema Rais Kikwete hakuhusika, kumbukumbu zinaonyesha kuwa Rais alishiriki kikamilifu katika mchakato mzima wa Richmond na hakuna kilichofanyika kuhusu tenda hiyo ambacho yeye hakujua au hakukubali.
Wiki iliyopita wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alipokuwa na mkutano na wahariri wa vyombo vya habari, alisema Rais Kikwete alilirejesha kwake faili linalohusu posho mpya za wabunge kwake ili azisaini.
Kauli ya Makinda
Katika hatua nyingine, Spika wa Bunge, Anna Makinda, amesema kuwa wabunge hao watalipwa posho za kikao kilichopita na kikao cha sasa.
Alisema mtu akipata mshahara unakuwa wake na familia yake, lakini kwa mbunge si hivyo, kwani ana watu wengi ambao wanahitaji msaada wake, hivyo hawezi kutoa msaada huo kutoka kwenye mshahara wake.
Alisema wabunge wengi wana madeni makubwa, na wengine wanaondoka na mshahara wa sh 45,000 au 100,000 kwa mwezi.
Makinda aliyekuwa ameongozana na Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, na maofisa wengine wa Bunge, alisema wabunge wengine wamekuwa wanakopa hadi mafuta ya kuja bungeni. Alisema wabunge si matajiri kama watu wanavyosema.
Kwa mujibu wa Makinda wapo wanaomaliza muda wao wakiwa hawana kitu kwani hata kiinua mgongo chao, wanakuwa wameshakopa.
Siri ya posho mpya yafichukuka
Hata hivyo, hatua ya serikali ya Kikwete kubariki posho mpya ya sh 200,000 kwa siku imemwokoa Spika Makinda ambaye alikuwa anakabiliwa na tishio la kung’olewa na wabunge.
Habari ambazo gazeti hili limezipata zilisema kuwa baada ya Makinda kuonekana kama vile ameshindwa kutimiza ahadi yake ya mara kwa mara kwa wabunge kwamba angeongeza posho, baadhi ya wabunge, tena kutoka ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM),walipanga kuibuka na hoja ya kutokuwa na imani na Spika.
Inaelezwa kuwa hoja hiyo ilipangwa kuibuliwa na mmoja wa wabunge machachari wanawake wa CCM na kuungwa mkono na wengi ambao walionekana kukerwa na Makinda kushindwa kusimamia maslahi ya wabunge kama alivyoahidi.
Mmoja wa wajumbe kutoka Kamati ya Bunge aliliambia gazeti hili kwamba tayari Spika alishawapa matumaini kwamba posho zimeongezwa, hivyo asingeeleweka kama angesema posho hazijaongezwa kwa sababu Rais hajasaini.
“Unakumbuka Spika alipokurupuka na kupingana na katibu wake kuhusu posho, CCM ilitoa taarifa kupinga nyongeza hiyo kama makundi mengine yalivyofanya. Mama alilalamika kwamba chama kimemtosa.
“Hata hivyo aliahidiwa kwamba serikali ingemlinda. Ndiyo maana Rais amebariki posho mpya kabla ya kuanza kikao hiki cha sita, hivyo amezima mpango wa mahasimu wa Makinda,” alisema mjumbe huyo ambaye ni mmoja wa wabunge machachari wa CCM.
Wabunge: JK amejikaanga
Hata hivyo, wakati duru za siasa zikisema hatua hiyo imemwokoa Makinda, duru za siasa zinasema kuwa hatua hiyo inazidi kumweka pabaya Rais Kikwete.
Hali hiyo inaeleza inaweza kusababisha makundi mengine ya kijamii kujitokeza kwa nguvu kutaka walipwe madai yao haraka kama walivyofanyiwa wabunge.
Baadhi ya wabunge waliozungumza na gazeti hili na kuomba majina yao yahifadhiwe, walisema licha ya ukweli kwamba wao wamenufaika na posho hiyo, hatua hiyo itawajengea wananchi chuki dhidi ya makundi mengine yanayodai kutaka yaongezewe posho.
Baadhi ya makundi yaliyochochewa kutaka yatimiziwe madai yao ni pamoja na madaktari walioko kwenye mafunzo kwa vitendo ambao hadi leo wako kwenye mgomo wakitaka serikali iwaongezee posho na madai mengine mbalimbali.
Mbunge mmoja wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka moja ya majimbo ya mkoa wa Tabora, alisema Rais Kikwete amekosea kubariki posho hizo sasa wakati kuna makundi mengine yamekuwa yakidai kuongezewa mishahara kwa muda mrefu bila mafanikio.
“Wengine tumetishiwa kunyang’anywa kadi za CCM kutokana na kupinga posho, lakini ukweli unabaki kuwa tatizo la mikopo ni la wabunge wenyewe.
Kama mbunge amekopa milioni 300, halafu mwisho wa mwezi anatoka na sh 100,000, ni tatizo lake; na dawa si kumwongezea posho,” alisema mbunge huyo.
Mbunge mwingine wa CCM alisema tatizo si posho za wabunge bali mfumo mzima wa posho serikalini kwani nyingine hazina tija.
Kauli ya mbunge huyu inafanana na msimamo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambacho kimekuwa kinaishawishi serikali iondoe posho na badala yake iboreshe mapato ya watumishi.
“Hapa bungeni tumetofautiana, walioacha kukopa wanaishi vizuri na hawana matatizo. Lakini wapo waliokopa mikopo yote iliyojitokeza. Kuna wabunge wana mihula mitatu hadi minne na kila mwaka wanachukua mikopo ya magari. Mbunge wa aina hii, akitoka na mshahara wa sh 100,000 hapaswi kulalamikia maisha magumu, na dawa yake sio kuongeza posho,” alisema.
Mbunge Kasulu Mjini, Moses Machali (NCCR- Mageuzi), alisema Rais Kikwete amejikaanga kwa mafuta yake kwani wafanyakazi na watumishi wengine wanaolalamikia maisha magumu na kutaka waongezewe mishahara, hawatamuelewa.
“Wafanyakazi waliomba na hadi sasa wanataka kima cha chini kiwe sh 315,000 wamenyimwa, lakini leo wanasikia mbunge kila anaposaini hata kama hasemi wala kuchangia kitu, analipwa sh 200,000; hiyo ni mbali na per diem (posho ya kujikimu). Hawawezi kukuelewa,” alisema.
Akikubaliana na hoja ya CHADEMA, Machali alisema ni vema serikali ipitie upya mfumo wa ulipaji posho badala ya kuwaangalia wabunge tu, kwani maisha magumu yako kwa wote.
Naye David Kafulila, Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi) alisisitiza kuwa kuna umuhimu wa kufumua mfumo mzima wa posho na kwamba madai ya nyongeza ya posho na mishahara, hayawezi kushughulikiwa vipande vipande.
“Leo utawalipa wabunge, kesho madaktari, walimu nao wakigoma, nao uwalipe kwa wakati wao. Hii haiwezekani,” alisema.
Alisema mfumo wa malipo kwa sasa ni mbaya kwani wakati daktari anayefanya kazi nzito ya kutibu wagonjwa analipwa sh milioni moja, ofisa wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) analipwa sh milioni sita kwa kukusanya kodi.
 
Katibu wa Bunge - posho hazijalipwa!

Spika - zimelipwa na zimeshaidhinishwa (na nani)?

Pinda - Rais amesafiri kwenda Davos ameniachia suala la posho kuwa nisaini au kutokusaini

Zitto - PInda hana mamlaka ya kusaini

Pinda na Spika - zimeshapitishwa na hela zipo tayari zimetayarishwa ili mlipwe

Wabunge - Applause!

Madaktari - mnajipendelea basi mgomo unaendelea

Wananchi - Tuandamane au tusiandamane?

Kurugenzi ya Ikulu - Rais hajasaini kamwe. Anataka wabunge watumie busara.

Kama mambo ya kusoma ramli vile.......

Utadhani nchi inajiongoza yenye na haina kiongozi. Kila mtu ni msemaji.
 
Nini source ya taarifa hii ya Invisible na ile ya gazeti la Mwananchi? Haiwezekani kuwa mojawapo ya taarifa hizi sio ya kweli? Kwa akili ya kawaida sioni ni vipi mkanganyiko kama huu unaweza kutokea (pamoja na utendaji mbovu wa serikali uliopo!).

Wewe upo tanzania kweli. Hapa chochote kinatokea mkuu! Kwani ni mara ya kwanza.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Interesting and confusing. Rais, WM, Spika chama hicho hicho, serikali hiyo hiyo. Na leo hii wamemzotoa Zitto aliyesema kwamba Rais hajaidhinisha posho. Kwa hiyo Zitto anajua zaidi habari za ikulu kuliko WM na Spika. Pwechepweche!!

Ndo swali la kujiuliza sasa.
 
Waziri mkuu Mizengo Pinda na Spika wa bunge Anna Makinda waliuambia umma kuwa rais Jakaya Kikwete ameidhinisha kuongezwa kwa posho ya wabunge. Siku moja baadaye ikulu imekanusha.Je kwa kumsingizia rais, kudanganya umma, na kupinga na rais watanusurika kuwajibishwa? Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA
 
Kikwete mwenyewe hana ubavu wa kushindana na safu ya waandamizi wake aliowateua mwenyewe. Kama angeweza kuwa na uamuzi thabiti na kutoridhia posho hizo ana nguvu kubwa ya kuweza kukataa kutia sahihi na si kurudisha wakajadili eti watumie wenyewe busara kuamua, huu ni ulegelege.
 
kwa serikali hakuna cha ajabu labda wewe ndiyo utachashangaa hakuna mtu wala sisimzi atakae chukuliwa hatua...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom