Ikulu: Rais hajaidhinisha posho za wabunge!

Status
Not open for further replies.
Anajaribu kujifanya hakua amekubali ili kupumbaza watu baada ya kuona moto wa madaktari hauelekei kuzimika wala kufifia. Na kwa hilo hawezi kumchukulia MP hatua kwasababu aliyoyasema mapema jana ni kweli, muda tu ndio haukua mzuri kutangaza.

RIP Tanzania!!
 
[h=3]JK abariki posho mpya za wabunge[/h]KILA MMOJA KULIPWA 330,000 KWA SIKU, ZITTO, MAKAMBA, KIGWANGALA WASULUBISHWA KWA KUZIPINGAWaandishi Wetu, Dodoma
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amesema tayari Rais Jakaya Kikwete amesaini kuidhinisha ongezeko la posho za vikao (sitting allowance) kwa wabunge kutoka Sh70,000 hadi Sh200,000 kwa siku. Kupitishwa kwa posho hizo ambazo ziliandikwa kwa mara ya kwanza na gazeti hili, kunafanya sasa mbunge kupokea Sh330,000 kwa siku; Sh200,000 zikiwa ni posho ya kikao, Sh80,000 posho ya kujikimu na Sh50,000 nauli.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya kikao cha utanguzi cha wabunge jana, zilidai kuwa baada ya Pinda kutoa taarifa hiyo, wabunge walishangilia huku Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, akisimama na kudai kuwa taarifa alizonazo ni kwamba Rais Kikwete alikuwa hajasaini kuidhinisha posho hizo.

Hatua hiyo ilisababisha Mbunge wa Kondoa Kaskazini, Juma Nkamia (CCM), kusimama na kuhoji iwapo Zitto ni miongoni mwa wasemaji wa Rais kabla ya Pinda kusimama na kuthibitisha kusainiwa kwa posho hizo akisema siyo ajabu kwani hata watumishi wa Serikali wanalipwa kati ya Sh150,000 na Sh200,000. Hata hivyo, Zitto alitetea msimamo wake kwamba alitarajia baada ya kusainiwa kwa posho hizo na Rais, angepewa masharti mapya ya kazi za ubunge.
 
Gazeti la Mwananchi la leo, Jumanne, Januari 31, 2012 limeandika habari zenye kichwa cha habari – JK abariki posho mpya za Wabunge: Kila mmoja kulipwa sh 330,000 kwa siku.

Habari hizi siyo za kweli na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais inataka kutoa ufafanuzi ufuatao:

Maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuhusu suala hili yako wazi kabisa na hakuna mahali ambako Rais Kikwete amebariki posho hizi.

Maelekezo ya Mheshimiwa Rais kuhusu suala hili ni kama ifuatavyo:

Kwanza, Mheshimiwa Rais Kikwete anakubali haja ya kuangalia upya posho kwa Wabunge lakini amewataka wabunge kutumia hekima na busara katika kulitafakari suala hili.

Pili, Mheshimiwa Rais Kikwete amewataka Wabunge kutumia Kikao cha sasa cha Bunge kulizungumza upya suala hilo.


Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
31 Januari, 2012


Hii serikali kweli imejaa mataahira!!! Hivi Pinda na Kikwete waliwasiliana kwa lugha ipi mpaka Pinda atamke mbele ya Wabunge kwamba Kikwete kaidhinisha posho za Wabunge kuongezwa!? Ni nani kati ya Makinda, Pinda na Kikwete anayesema ukweli kuhusu hili sakata la Kikwete kuidhinisha ongezeko la posho za Wabunge?
Hawa wamezidi kutuchezea akili Watanzania hawastahili kabisa kuendelea kuwepo madarakani wote hawa ni kufukuza kazi mara moja. Duh!!!!! halafu wanajigamba eti wamethubutu, wameweza na sasa wanasonga mbele!!!!!
 
Hawa viongozi wetu sijui walienda kwa mganga mmoja akawapa dawa ya kuwachanganya wao kwao??? hawawi na information zinazofanana.
Ze Comedy wapo wapiiiiiiiiiiiiiiiii??? hii mkiisahau mmefulia
 
​Suala la posho mpya kwa wabunge: JK Makinda wajikaanga:
Jana jioni nilisoma taarif ya Salva Rweyemamu ikikanusha kuwa hakuna baraka za Rais katika posho za wabunge, Makinda anasema rais ametia mkono, hivi ndivyo vwalivopanga kutuchezea akili.

Soma habari hii toka Tanzania daima 01/02/2012
RAIS Jakaya Kikwete na Spika wa Bunge, Anna Makinda, wamejiweka pabaya kwa kutoa kauli zinazopingana kuhusu posho mpya za kikao kwa wabunge.
Huku Makinda akisema Rais Kikwete ndiye aliyebariki posho hizo za shilingi laki mbili kwa siku, Kurugenzi ya Mawasiliano ilisema kwamba Rais hahusiki.
Makinda alitoa kauli hiyo jana mjini hapa mbele ya waandishi wa habari, akisema Rais Kikwete ndiye aliyebariki posho hizo.
Kauli ya Makinda inakuja baada ya Waziri Mkuu naye kubariki posho hizo, baada ya kusema alikabidhiwa faili hilo na Rais Kikwete.
Jana Spika huyo alisema posho hizo, ambazo zimebarikiwa na Rais Kikwete, zilianza kutolewa tangu kikao kilichopita na zinalipwa kwa wabunge waliohudhuria vikao na kusaini.
Hata hivyo, Ikulu ilitoa taarifa jioni ikisema hakuna mahali ambapo Rais Kikwete amebariki posho hizo.
"Maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, kuhusu suala hili yako wazi kabisa na hakuna mahali ambapo Rais Kikwete amebariki posho hizi. Maelekezo ya Rais kuhusu suala hili ni kama ifuatavyo: "Kwanza, Rais Kikwete anakubali haja ya kuangalia upya posho kwa wabunge, lakini amewataka wabunge kutumia hekima na busara katika kulitafakari suala hili," ilisema taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais Kikwete amewataka wabunge kutumia kikao cha sasa cha Bunge kulizungumza upya suala hilo.
Hata hivyo, Ikulu haikuweza kueleza msimamo wa Rais kuhusu posho hizo kama zitolewe au la.
Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wameliambia gazeti hili kuwa kauli ya Ikulu ni ya kipropaganda kwa ajili ya kumlinda Rais baada ya kuona wananchi wanakerwa na posho hizo.
Baadhi ya wachambuzi wanasema kama Rais angekuwa hataki posho hizo zilipwe, kwanza Makinda asingepata ujasiri wa kuzitetea, na pili Rais Kikwete mwenyewe angetoa msimamo wa moja kwa moja badala ya kuzungukazunguka.
Wanasema hata kupeleka suala hilo kwa Waziri Mkuu Pinda, ilikuwa janja ya Kikwete kuwarushia wengine lawama, maana Pinda hawezi kutekeleza au kubariki suala ambalo bosi wake hataki.
Wengine walisema kauli ya Ikulu haiwezi kuaminika kwa kuwa si mara ya kwanza kutoa matamko ya kumtetea Rais katika masuala tata, kama ilivyokuwa sakata la Richmond, ambalo licha ya taarifa ya Ikulu kusema Rais Kikwete hakuhusika, kumbukumbu zinaonyesha kuwa Rais alishiriki kikamilifu katika mchakato mzima wa Richmond na hakuna kilichofanyika kuhusu tenda hiyo ambacho yeye hakujua au hakukubali.
Wiki iliyopita wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alipokuwa na mkutano na wahariri wa vyombo vya habari, alisema Rais Kikwete alilirejesha kwake faili linalohusu posho mpya za wabunge kwake ili azisaini.
Kauli ya Makinda
Katika hatua nyingine, Spika wa Bunge, Anna Makinda, amesema kuwa wabunge hao watalipwa posho za kikao kilichopita na kikao cha sasa.
Alisema mtu akipata mshahara unakuwa wake na familia yake, lakini kwa mbunge si hivyo, kwani ana watu wengi ambao wanahitaji msaada wake, hivyo hawezi kutoa msaada huo kutoka kwenye mshahara wake.
Alisema wabunge wengi wana madeni makubwa, na wengine wanaondoka na mshahara wa sh 45,000 au 100,000 kwa mwezi.
Makinda aliyekuwa ameongozana na Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, na maofisa wengine wa Bunge, alisema wabunge wengine wamekuwa wanakopa hadi mafuta ya kuja bungeni. Alisema wabunge si matajiri kama watu wanavyosema.
Kwa mujibu wa Makinda wapo wanaomaliza muda wao wakiwa hawana kitu kwani hata kiinua mgongo chao, wanakuwa wameshakopa.
Siri ya posho mpya yafichukuka
Hata hivyo, hatua ya serikali ya Kikwete kubariki posho mpya ya sh 200,000 kwa siku imemwokoa Spika Makinda ambaye alikuwa anakabiliwa na tishio la kung'olewa na wabunge.
Habari ambazo gazeti hili limezipata zilisema kuwa baada ya Makinda kuonekana kama vile ameshindwa kutimiza ahadi yake ya mara kwa mara kwa wabunge kwamba angeongeza posho, baadhi ya wabunge, tena kutoka ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM),walipanga kuibuka na hoja ya kutokuwa na imani na Spika.
Inaelezwa kuwa hoja hiyo ilipangwa kuibuliwa na mmoja wa wabunge machachari wanawake wa CCM na kuungwa mkono na wengi ambao walionekana kukerwa na Makinda kushindwa kusimamia maslahi ya wabunge kama alivyoahidi.
Mmoja wa wajumbe kutoka Kamati ya Bunge aliliambia gazeti hili kwamba tayari Spika alishawapa matumaini kwamba posho zimeongezwa, hivyo asingeeleweka kama angesema posho hazijaongezwa kwa sababu Rais hajasaini.
"Unakumbuka Spika alipokurupuka na kupingana na katibu wake kuhusu posho, CCM ilitoa taarifa kupinga nyongeza hiyo kama makundi mengine yalivyofanya. Mama alilalamika kwamba chama kimemtosa.
"Hata hivyo aliahidiwa kwamba serikali ingemlinda. Ndiyo maana Rais amebariki posho mpya kabla ya kuanza kikao hiki cha sita, hivyo amezima mpango wa mahasimu wa Makinda," alisema mjumbe huyo ambaye ni mmoja wa wabunge machachari wa CCM.
Wabunge: JK amejikaanga
Hata hivyo, wakati duru za siasa zikisema hatua hiyo imemwokoa Makinda, duru za siasa zinasema kuwa hatua hiyo inazidi kumweka pabaya Rais Kikwete.
Hali hiyo inaeleza inaweza kusababisha makundi mengine ya kijamii kujitokeza kwa nguvu kutaka walipwe madai yao haraka kama walivyofanyiwa wabunge.
Baadhi ya wabunge waliozungumza na gazeti hili na kuomba majina yao yahifadhiwe, walisema licha ya ukweli kwamba wao wamenufaika na posho hiyo, hatua hiyo itawajengea wananchi chuki dhidi ya makundi mengine yanayodai kutaka yaongezewe posho.
Baadhi ya makundi yaliyochochewa kutaka yatimiziwe madai yao ni pamoja na madaktari walioko kwenye mafunzo kwa vitendo ambao hadi leo wako kwenye mgomo wakitaka serikali iwaongezee posho na madai mengine mbalimbali.
Mbunge mmoja wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka moja ya majimbo ya mkoa wa Tabora, alisema Rais Kikwete amekosea kubariki posho hizo sasa wakati kuna makundi mengine yamekuwa yakidai kuongezewa mishahara kwa muda mrefu bila mafanikio.
"Wengine tumetishiwa kunyang'anywa kadi za CCM kutokana na kupinga posho, lakini ukweli unabaki kuwa tatizo la mikopo ni la wabunge wenyewe.
Kama mbunge amekopa milioni 300, halafu mwisho wa mwezi anatoka na sh 100,000, ni tatizo lake; na dawa si kumwongezea posho," alisema mbunge huyo.
Mbunge mwingine wa CCM alisema tatizo si posho za wabunge bali mfumo mzima wa posho serikalini kwani nyingine hazina tija.
Kauli ya mbunge huyu inafanana na msimamo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambacho kimekuwa kinaishawishi serikali iondoe posho na badala yake iboreshe mapato ya watumishi.
"Hapa bungeni tumetofautiana, walioacha kukopa wanaishi vizuri na hawana matatizo. Lakini wapo waliokopa mikopo yote iliyojitokeza. Kuna wabunge wana mihula mitatu hadi minne na kila mwaka wanachukua mikopo ya magari. Mbunge wa aina hii, akitoka na mshahara wa sh 100,000 hapaswi kulalamikia maisha magumu, na dawa yake sio kuongeza posho," alisema.
Mbunge Kasulu Mjini, Moses Machali (NCCR- Mageuzi), alisema Rais Kikwete amejikaanga kwa mafuta yake kwani wafanyakazi na watumishi wengine wanaolalamikia maisha magumu na kutaka waongezewe mishahara, hawatamuelewa.
"Wafanyakazi waliomba na hadi sasa wanataka kima cha chini kiwe sh 315,000 wamenyimwa, lakini leo wanasikia mbunge kila anaposaini hata kama hasemi wala kuchangia kitu, analipwa sh 200,000; hiyo ni mbali na per diem (posho ya kujikimu). Hawawezi kukuelewa," alisema.
Akikubaliana na hoja ya CHADEMA, Machali alisema ni vema serikali ipitie upya mfumo wa ulipaji posho badala ya kuwaangalia wabunge tu, kwani maisha magumu yako kwa wote.
Naye David Kafulila, Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi) alisisitiza kuwa kuna umuhimu wa kufumua mfumo mzima wa posho na kwamba madai ya nyongeza ya posho na mishahara, hayawezi kushughulikiwa vipande vipande.
"Leo utawalipa wabunge, kesho madaktari, walimu nao wakigoma, nao uwalipe kwa wakati wao. Hii haiwezekani," alisema.
Alisema mfumo wa malipo kwa sasa ni mbaya kwani wakati daktari anayefanya kazi nzito ya kutibu wagonjwa analipwa sh milioni moja, ofisa wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) analipwa sh milioni sita kwa kukusanya kodi.

Chukua maneno ya Kafulila yana Mantiki yana walinda wote Rais, na Spika. tatizo ni mfumo si Rais wala Spika.
 
Pengine wale walionifunza kuogopa uongo sikuwaelewa...ngoja tuone nani mkweli na nani muongo. Ngoja tuone nani uongo utamsitiri this time. Kweli kuna watu wamejichimbia shimoni
 
Hivi kweli kwenye leadership kuna mtu anastahili kuitwa muheshimiwa? Mbona kama hamna heshima miongoni mwao?
 
Naye David Kafulila, Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi) alisisitiza kuwa kuna umuhimu wa kufumua mfumo mzima wa posho na kwamba madai ya nyongeza ya posho na mishahara, hayawezi kushughulikiwa vipande vipande.
"Leo utawalipa wabunge, kesho madaktari, walimu nao wakigoma, nao uwalipe kwa wakati wao. Hii haiwezekani," alisema.
Alisema mfumo wa malipo kwa sasa ni mbaya kwani wakati daktari anayefanya kazi nzito ya kutibu wagonjwa analipwa sh milioni moja, ofisa wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) analipwa sh milioni sita kwa kukusanya kodi.


 
Naye David Kafulila, Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi) alisisitiza kuwa kuna umuhimu wa kufumua mfumo mzima wa posho na kwamba madai ya nyongeza ya posho na mishahara, hayawezi kushughulikiwa vipande vipande.
"Leo utawalipa wabunge, kesho madaktari, walimu nao wakigoma, nao uwalipe kwa wakati wao. Hii haiwezekani," alisema.
Alisema mfumo wa malipo kwa sasa ni mbaya kwani wakati daktari anayefanya kazi nzito ya kutibu wagonjwa analipwa sh milioni moja, ofisa wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) analipwa sh milioni sita kwa kukusanya kodi.



Huyo wa TRA mil 6 na ya rushwa nguvu juu. wala rushwa wakubwa. Nchi hii afadhali iangamie iumbwa upya kama kuna uumbaji!!!!
 
Wachangiaji wengi kwenye uzi huu hawako makini. Yaani ni kujiachia kwenye matani kwa wiiingi.
 
Kwa ujumla katika suala hili failure kubwa inaonekana kwa Pinda na Makinda. Hawa watu wameshindwa kumsaidia rais na kiongozi wa nchi kuondokana na jambo hili. Ninachoona mimi ni kuwa rais hataki posho hizi ambazo zimepigiwa kelele sana si tu na wananchi (kupitia kwa wabunge wa Chadema na vijana wachache wa CCM) zinapigiwa kelele vile vile na Donor community.

Sitting allowance ni jina baya kabisa! Sasa cha ajabu, wakati hali ya hewa ikiwa chafu hivyo, Mizengo na Anna na magenge yao ya wabunge wa CCM (wasiojali nini kinazungumzwa huko nje) wanazuka na mapendekezo ya kuongeza posho. Tena posho inayoongezwa ni hiyo hiyo Sitting allowance; si subsistence, wala mishahara. Hapa ni wazi hawa watu wawili (Mizengo na Anna) wanataka kumfanya rais aonekane kituko mbele ya wananchi na donor community ndo maana anachomoa!!

Kwa maneno hayo anayotumia kuwa watumie busara, ninaelewa kuwa rais hataki suala hili tena kwa wakati huu. Anajua hawajatumia busara hata kidogo na ni kama wanamkaanga. Rais hataki kutunishiana misuli moja kwa moja na hilo genge la wabunge linalopendekeza na kushangilia kuongezeka kwa posho hizo. Anajua kuwa genge hilo linamkaanga, ila hataki kupambana nao moja kwa moja. Alichohitaji ni Kiongozi wa shughuli za serikali bungeni na Spika wabunge waweze kusoma hali watumie uongozi wao bungeni kuzima hoja hiyo au kuichelewesha hadi hapo muda muafaka utakapofika.

Bahati mbaya Mizengo na Anna wanaonekana kukosa muono wa kumuelewa kiongozi wa nchi. Kwa hiyo ameamua sasa kuwatandika za usoni moja kwa moja hadharani kwa kukataa yale wanayoyasema.

Kusema kweli hapa ni failure kubwa kwa waziri mkuu Pinda na Spika Makinda. Wamemuanika na kumkaanga rais mbele ya wananchi na watoa misaada wanaopinga posho ya kukaa. Wao wameamua kuongeza hiyo hiyo posho inayolalamikiwa. Hilo genge la wabunge wa CCM lilokaa na kuamua kuwa waongeze Sitting allowance kwa asilimia nyingi sana bila kugusa allowance zingine wakati wanajua jinsi allowance hiyo ili 'unpopular' kwa wananchi na 'Donors' ni genge ambalo mheshimiwa rais anataka Mizengo na Anna wamsaidie kuli-control. Wameshindwa vibaya.

Hayo ndo madhara ya kuweka viongozi wasiokuwa smart kuwa wasaidizi wako hata kama ni loyalilsts kiasi gani. Spika smart na waziri mkuu smart wasingemuanika rais wazi wazi namna hiyo kwa kupandisha sitting allowance kwa asilimia nyingi (karibia 200%) wakati kila mtu anaiona ni POSHO YA KIZUSHI.

Hapa ilihitajika 'smart maneuver' kuisambaratisha hoja hiyo hata kama ilitoka kwa wabunge wengi kivipi. Waliokuwa na uwezo wa kufanya hiyo maneuver ni waziri mkuu na Spika huko bungeni.
 
Hivi, hili suala la posho mnalizungumziaje jamani??? Nadhani, tunahitaji nguvu ya ziada kulipinga kabisa!!!
Hali ya uchumi ni mbaya; then "wapuuzi" wachache wanaamua mambo kwa kufuata matumbo yao!!! HATUWEZI KUKUBALI hili.....
 
Kwamba mbunge anaweza kukwepa kikao cha bungeni ili akahudhurie semina (semina nzuri pembeni mahudhurio hafifu bungeni) ambako atakusanya posho ya kikao. Anahudhuria kama mbunge na kwa siku anaweza kuonekana kwenye semina mbili tatu. Viwango vya posho wanavyolipwa viko pegged na viwango rasmi vya bunge. Je hii ni halali alipwe akisaini bungeni na siku hiyohiyo alipwe kwa kuhudhria warsha pembeni?

Taasisi moja ya kimataifa wamesema kwa viwango hivi vipya Dodoma watasikia kwenye radio.
 
JK abariki posho mpya za wabunge

KILA MMOJA KULIPWA 330,000 KWA SIKU, ZITTO, MAKAMBA, KIGWANGALA WASULUBISHWA KWA KUZIPINGAWaandishi Wetu, Dodoma
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amesema tayari Rais Jakaya Kikwete amesaini kuidhinisha ongezeko la posho za vikao (sitting allowance) kwa wabunge kutoka Sh70,000 hadi Sh200,000 kwa siku. Kupitishwa kwa posho hizo ambazo ziliandikwa kwa mara ya kwanza na gazeti hili, kunafanya sasa mbunge kupokea Sh330,000 kwa siku; Sh200,000 zikiwa ni posho ya kikao, Sh80,000 posho ya kujikimu na Sh50,000 nauli.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya kikao cha utanguzi cha wabunge jana, zilidai kuwa baada ya Pinda kutoa taarifa hiyo, wabunge walishangilia huku Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, akisimama na kudai kuwa taarifa alizonazo ni kwamba Rais Kikwete alikuwa hajasaini kuidhinisha posho hizo.

Hatua hiyo ilisababisha Mbunge wa Kondoa Kaskazini, Juma Nkamia (CCM), kusimama na kuhoji iwapo Zitto ni miongoni mwa wasemaji wa Rais kabla ya Pinda kusimama na kuthibitisha kusainiwa kwa posho hizo akisema siyo ajabu kwani hata watumishi wa Serikali wanalipwa kati ya Sh150,000 na Sh200,000. Hata hivyo, Zitto alitetea msimamo wake kwamba alitarajia baada ya kusainiwa kwa posho hizo na Rais, angepewa masharti mapya ya kazi za ubunge.
Kuna mbunge alishasema pinda ni muongo kuliko shetani...
 
Wapinzani wa rais ndani ya CCM wanatumia Bunge kumfanya rais aonekane ze comedy kwa kupandisha posho ambayo inalalamikiwa na kila mtu. Kwa nini hawakufikiria kuongeza subsistence allowance kwa mfano? kwa nini waongeze tena kwa asilimia kubwa posho ambayo kila mtu anaona ni posho kituko? Mambo kama haya viongozi inatakiwa wayaone ndo maana rais anawashauli watumie busara, ameshapaona hapo kuwa yeye ndo anakaangwa!!

Akiridhia, ataonekana kituko mbele ya wananchi na wahisani; asiporidhia atakuwa amewaudhi wabunge wa chama chake!! Hoja hii (ya kupandisha sitting allowance) ilitakiwa Pinda na Makinda waizike kwa kutumia madaraka yao!!
 
MKJJ siamini maneno yako, hebu leta ushahidi angalau wa mbunge mmoja aliyewahi kusaini kihivyo... ila kwa mtu kama Msindai huyo nina hakika anaweza kwani kwenye pesa ana roho ngumu kama drill bit, Niliwahi kumwona aki demand pesa pale REDET miaka ya nyuma nilipigwa na butwaa ya kufa mtu wakati yeye wala hakuwa anajistukia
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom