Ikulu: Rais hajaidhinisha posho za wabunge!

Status
Not open for further replies.
Wabunge wanaodhani posho ni ndogo na hawawezi kutimiza wajibu wao wajiuzulu! Kwani nafasi ya Ubunge ni nafasi ya uwakilishi na si biashara ambayo madhumuni yake kupata income kubwa au faida kama wanavyotaka ndugu zetu hawa!

Kuna watu kibao ambao wanaweza kutuwakilisha kwa moyo thabiti na kwa nguvu zao zote bila hata kudai kulipwa pesa lukuki kama ilivyo hivi sasa!

Kwa mwenendo wao wa sasa tumewafaham kwamba hawana nia thabit na wala kuguswa na matatizo halisi ya raia wa kawaida na ndio maana hata kwenye tatizo hili kubwa la watu kupoteza maisha kutokana na mgomo wa madaktari, kutoonyesha kuguswa kwa kuwa wao ni wana Appollo na si watu wanaofanana na sisi.

Tunawaomba waachie ngazi ili wakafanye biashara zitakazowalipa Returns kubwa na kuacha hizi nafasi za uwakilishi kwa watu wataoshirikiana na wananchi wa kawaida bila kudai ujira usifanana na shughuri zao!

Hivi tunawafukuzaje kazi hawa waajiriwa wetu sisi wananchi ndio mabosi wao!
Cant we sack them? au ndio inabidi tusubiri miaka yote iliyobaki huku wakituzingua na malalamiko yao juu ya posho? Hivi wanajua kuwa wao ndio chanzo cha migogoro hasa huu wa madaktari? Tutaendelea kuwavumilia huku watu wakifa kila siku?
 
Sheria ya muundo wa mikopo kwa watumishi wa Umma Kama walivyo wabunge haimruhusu mtumishi kukopa zaidi ya asilimia 60 ya kusanyo la Mshahara wake. Sasa iweje wakwetu hawa watungasheria wakope hadi pitilizo la furushi Lao la mwezi? au wanathibitisha kile kimsemo laini kwamba mtunga sheria ndiye mkanyaga sheria hiyo hiyo aliyojitungia.. !!

Salma,

Je, ni kuwa serikali haikuliona hilo? Au serikali imefanya maksudi ili wabunge wakichachamalia jambo iwakumbushe kuwa kumbuka tukivunja bunge deni lako unafilisiwa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom