Ikulu: Rais hajaidhinisha posho za wabunge!

Status
Not open for further replies.
Katika taarifa ya habari ya saa mbili usiku kurugenzi ya habari yasema kuwa rais kikwete hajabariki posho za wabunge.hivi mtoto wa mkulima ni nani alimtuma kusema kuwa rais kabariki posho za wabunge.pole mtoto wa mkulíma umekuwa mbuzi wa kafara.bora tu urudi katavi ukafuge kuku.jamani hii iko vp?

Wamegeuka Samaki walana wao kwa wao.
 
sasa nimebahatika kuiona hiyo press release, aixee! hivi Salva ana elimu gani? anadhalilisha tasnia ya habari, yani anaandika kipeperushi mavi kabisa hakina hata details

nikama memo toka kwa mtu fulani kwenda kwa mshirika wake ambao wamezoeana kupitia vikao vya bar..crap kabisa
 
Katika taarifa ya habari ya saa mbili usiku kurugenzi ya habari yasema kuwa rais kikwete hajabariki posho za wabunge.hivi mtoto wa mkulima ni nani alimtuma kusema kuwa rais kabariki posho za wabunge.pole mtoto wa mkulíma umekuwa mbuzi wa kafara.bora tu urudi katavi ukafuge kuku.jamani hii iko vp?

Wamegeuka Samaki walana wao kwa wao.
 
Nadhani hawa jamaa sio wajinga wanajua wanachofanya,nikikumbuka maneno ya naibu spika wakati anahojiwa ITV,dk 45,alisema watu wanalalamikia posho za wabunge lakini hawajui posho za mihimili mingine ya serikali.Nahisi Kikwete anashindwa kuwa na msimamo na posho hizi sababu anajua basis wabunge wanazotumia kudai hizi posho(inawezekana wameangalia wenzao kwenye mihimili mingine na kuona viwango vya posho wanazolipana).Na hapo ndo tulichukulie swali la NN kwa umakini hivi huyu raisi na maofisa wake wanalipana kiasi gani cha posho?.Nna hakika tukichunguza posho wanazolipwa majaji,mawaziri na makatibu wakuu na kulinganisha hizi wanazodai wabunge tutajua ni kiasi gani tunatafunwa.
 
SECONDED! I hate the word itself - "posho" halina element ya kitumwa kweli nyie wajuaji wa kiswahili sanifu?
Hivi nchi nyingine wanafanyaje? Naambiwa huu ni utamaduni wa nchi za Kiafrika zaidi,Ni kweli ? kama ndio kwanini?

Teh teh teh teh teh! Ha ha ha ha!

Mkuu; Mh. Shibuda alitoa mbadala mzuri sana wa hilo neno. Badala yake alishauri litumike "
ujira wa mwia". Nadhani, kwa "busara" kibao lilizojaliwa Bunge letu, wangesikiliza ushauri huo leo hii kichefuchefu tunachokipata kwa kusikia neno "posho" kingeepukwa. Waheshimiwa Wabunge na Spika wenu, dakeni ushauri huo.
 
ametoka kuongea spika makinda kwenye habari tbc kuwa posho hiyo haitoki kila siku ni kipindi cha bunge tu...ngoja kesho aumbuke sasa sijui atajiudhuru na pinda wake? au watanzania tunapigwa changa la macho
 
Yani kikwete Mpuuzi kweli, badala ya kutoa msimamo kama Kiongozi anavyopasa Kuwa eti na Yeye anatoa maoni kama raia wa kawaida asiye na madaraka.! Halafu na wale waliotoa taarifa kwa Umma kwamba Huyu jamaa anayeitwa Rais kabariki posho mpya alizitoa wapi...na kwanini bunge linataharuki kubwa...Nahisi Jk amesharuhusu tayari anajikosha tu kwa wananchi wakati yeye ndio nyoka anaewaangamiza Watanzania huku akijichekeshachekesha utadhani
 
Kwa mawazo yangu Rais amesaini ila anakwepa lawama, haiwezekani watunga sheria wakaanza kujilipa kabla Rais kusaini vinginevyo ni kukiuka taratibu za pesa za nchi kitu ambacho wabunge hawawezi kukifanya.

Swali la msingi hapa ni uhalali wa taharifa ya kurugenzi ya mawasiliano ya Ikulu, hawajasema wazi mambo muhimu hapa kama vile

Je posho zimesainiwa au hazijasainiwa?

Nini msimamo wa serikali kuhusiana na posho hizo?

Je budget intoka wapi na haikuwepo?
 
inaonyesha Kikwete hataki kabisa kupewa lawana ya hizi posho. hataki kusaini ila anashindwa kuongea ama anaangaliia upepo kwanza.

Siyo kwamba hataki kusign huyu bwana atakuwa amekwisha sign posho za wabunge ila anataka iwe siri. Kama bunge lingekuwa na 100% ya wachumia tumbo (I mean CCM MPs) hii issue ingekwenda kimyakimya. Ila kwa kuwa kuna wristle browers wanashindwa. Wasiwasi wangu ni kuwa Bunge linaweza kufanya profiling ya kuweka mkakati kuwa wabunge wa CCM wanaotaka posho zinongezeke wajiorodheshe kwa siri na ka ikitokea wote wamefanya hivyo basi wanaambiwa kuwa watalipwa hicho kiasi ila habari ikivuja tu wanarusha kiasi chote cha ziada hata kama ni baada ya miaka miwili. Hii itawafanya wapokee posho mpya bila vyama kero kwa ongezeko la posho kujua.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom