Ikulu: Rais hajaidhinisha posho za wabunge!

Status
Not open for further replies.

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Gazeti la Mwananchi la leo, Jumanne, Januari 31, 2012 limeandika habari zenye kichwa cha habari – JK abariki posho mpya za Wabunge: Kila mmoja kulipwa sh 330,000 kwa siku.

Habari hizi siyo za kweli na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais inataka kutoa ufafanuzi ufuatao:

Maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuhusu suala hili yako wazi kabisa na hakuna mahali ambako Rais Kikwete amebariki posho hizi.

Maelekezo ya Mheshimiwa Rais kuhusu suala hili ni kama ifuatavyo:

Kwanza, Mheshimiwa Rais Kikwete anakubali haja ya kuangalia upya posho kwa Wabunge lakini amewataka wabunge kutumia hekima na busara katika kulitafakari suala hili.

Pili, Mheshimiwa Rais Kikwete amewataka Wabunge kutumia Kikao cha sasa cha Bunge kulizungumza upya suala hilo.


Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
31 Januari, 2012
 
wameanza kujikana ee!!hadanganywi mtu hapa.ina maana wabunge watakataa posho?tunasubiri tuone.
 
Mhhh haya yetu macho
maelezo zaidi ya kujichanganya maana Waziri wake Mkuu anasema yake na Spika anasema yake na huku wabunge washaanza kulipwa na wanazitaka kwa kila njia
Wanaopinga wanaonekana wasaliti
Sasa tuelewe lipi
 
Kwa hiyo Pinda amewachuuza wabunge yaani amewaingiza vichakani wazima wazima.
 
wameanza kujikana ee!!hadanganywi mtu hapa.ina maana wabunge watakataa posho?tunasubiri tuone.

Hapa wote wanajikanyaga tu hawaeleweki wanaogopa hasira za wananchi huyu anasema hili yule nae anasema lake muda si mrefu wataanza kupopolewa mawe wanavyo pita mitaani buku 330 nyingi sana kwa siku ukiangalia mlalahoi anasotea buku 2.5 nayo hapati mpaka agonge mawe au abebe zege dah.
 
inabiid tujue kuwa hawa wabunge wanalipwa hizi pesa?? isije ikawa wanapewa mshiko huku wanatupaka mafuta kwa mgongo wa chupa
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Du! Hii Kali yaani wameanza kukanusha tena? Sasa hapa hatu mihimili sio bunge wala serikali. Ni upuuzi mtupu.
 
Well hapo sasa ndio tunajua nchi hii watu wapo makini kiasi gani kuokoa ngozi zao wenyewe lakini matokeo yake ni kama wanajikaanga kwa mafuta yao wenyewe.

Sasa hiyo taarifa ya Ikulu mbona inalenga zaidi kumuaibisha Rais na Utawala wake mbovu. Kweli watu wanatoa taarifa kama hiyo na kusema kwamba ni taarifa toka ofisi muhimu kuliko zote nchini? Ina maana hakuna mawasiliano kati ya Waziri Mkuu na Rais na Spika wa bunge? Ikiwa ni hivyo tunaelekea wapi kama nchi?

Dah inauma sana hii. Kuzaliwa Mtanzania sio laana ni baraka sasa kwa nini tuwaache wachache wachezee baraka tulizopewa na mwenyezi Mungu katika hii nchi yake?
 
badala ya kutolea kauli la madaktari kugoma hili wamejibu haraka...hii ndio TZ ya JK
 
Hii muvi kali kweli ngoja nisogeze coke yangu na popkon!dah masteringi kibao ngoja tuone yupi atakufa ingawa steringi hafi hIi imekaa kaaa vp cjui!!
 
Hivi kwani kuna ugumu gani kusema nchi imewashinda?Serikali ya CCM imeshinda huo ndio ukweli wala hakuna lugha mbadala kwa jambo hili,haingii akili kama waziri mkuu anapishana na rais wake,nchi gani hii,kuwasiliana wao kwa wao tena supreme,tutegemee nini?
Siamini hiki kama kimetokea kweli,au hawa wamelogwa?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom