Fundisi Muhapa
JF-Expert Member
- Nov 25, 2013
- 4,422
- 2,110
Aisee umenikumbusha mbali sana enzi za born city Dar - Arusha,enzi hizo tunatoka Arusha saa 12 jioni tunafika dar saa 10 Usiku ,chakula tunakula mombo yaani mombo ukipita usiku ni kama mchana vile kumechangamka balaa,aisee daraja la wami tunapita saa 7 au 8 usiku mnaanza kuamshana daa long time na mpinzani wa born city alikuwa anaitwa SMAA ,enzi hizo za nissan diesel ,enzi za isuzu,leyland,leyland daf
SMAA nakumbuka lilikua limeandikwa WAMSEGEJU kwenye kioo cha mbele juu. Sjui hata walimaanisha nini!!
Kulikua pia na Machame Luxury na Bazuu (jeusiiii). Bazuu lilikuaga la kwanza kuingia stendi chugga safari zilipobadilishwa kuwa mchana na Lyatonga. Saa 7 washaingia. Kuna stori liliwahi kugeuza kurudi Dar baada ya kushusha. Ilikua msimu wa mafuriko. Luxury ya wakati huo FRESH YA SHAMBA. Baadae ikaja AIR CHALINZE.
falcon mombasa,
Kuna changamoto kwenye biashara ya luxury buses. Fresh ilijipotelea then Air Chalinze zikaungua zote moja hapohapo Chalinze!! Ikaja Scandinavia. Alipovamia tu ruti ya Ar-Dar haikupita miaka mitano na kampuni ikafa. Hao Tahmeed nao washaunguza limoja sijui hata la wapi. Section ya luxury kwa Ar-Dar mwachieni Dar Express na kwa sasa Kilimanjaro Express.
Hao Kilimanjaro jana nimeona wameingiza kifaa kimebebwa na semi trela. Sasa sijui ni jipya au ndo rangi? Ila linaonekana kama bodi tofauti japo Marcopolo. mocharles saidia hapa.
Hiyo michina yenu sjui TAH... nini nini huko pelekeni Mombasa na Tanga. Na ruti za huko kusini huwaambii kitu kwa michina. Kaa makambako uone. Alianza New Force basi wote huko fulu michina. Chugga luxury leta Scania bana!!