Kampuni ya mabasi ya sauli wapo juu ya sheria?

MLIMAWANYOKA

JF-Expert Member
Oct 25, 2019
487
1,633
Kwa route ya Mbeya - Dar ni hakika Sauli hana mpinzani mpaka sasa.. Nadhani hii ni kwa sababu ya kuwahi kufika...
WAtu wa Mbeya huwaambii kitu na Sauli yao.
Soma hapa

Leo Nmelazimika kuahirisha safari baada ya kuachwa na bus lao. Safari ya Dar - Mbeya.

Ilikuwa hivi.. Saa kumi na moja kamili nilikuwa nmeambiwa kuwa basi litapaki pale urafiki opposite na kituo cha mwendo kasi.. Mkono wa kushoto kutokea kariakoo.. Ambapo ndipo nilikatia tiketi.

Saa kumi na moja kamili.. Napiga namba ya konda, mbona sioni gari hapa, nkaambiwa vuka upande wa pili, nafika kule naambiwa gari ishaondoka..

Nkachukua boda kuanza kuifukizia konda kasema tukutane Mbezi..

Nkamuelekeza boda kuwa afike stand ya mabus ya Magufuli Mbezi.. Cha ajabu kufika pale.. Nampigia tena Wao wanapakilia stand ya mbezi kibanda cha mkaa.. Na hawaingii ndani. Kwa hiyo niwafuate kibaha. Daah..

Nikaona isiwe tabu. Nkamwambia konda basi auze hiyo ticket. Akasema sawa. Akanipa namba ya muhudumu wa ofisi za Shekilango.

0656911212 niwe nawasiliana naye kuhusu utaratibu wa ku top up ili nipangiwe safari nyingine ya kesho.. Ikabidi nirudi hapo shekilango. Nkakutana na dada mweupe kiasi na hijab yake kapendeza sana.. Majibu yake yakanitafakarisha na kujiuliza mengi.

Kasema
1.kwa leo tu wameacha abiria 6. Gari ilikatisha tiket 52 na 46 tu wamewahi bus. Kanionesha na mkeka..

2. Hakuna namna unaweza rudishiwa hela hata kama watauza hizo siti Morogoro au iringa, ukiachwa na gari ni furaha kubwa kwa dereva na kondakta wake.. Majibu ya konda kuwa wakipata mteja watakutunzia siti yalikuwa ya kuwapa moyo tu.

3. Kuhusu sauli kutoingia stand ya Magufuli kasema we hujiulizi kwanini wengine wanapigwa pini kuanzia Shekilango ila sauli inaanzia bila shida? Kasema hata kama hatuingii ila ushuru tunatoa.

4. Akanionesha tickets za abiria wengine walioachwa.. Kasema wamelipa upya.. So nilipe tu.. Nikazama mfukoni. Ukizingatia ni kweli kampuni zingine kama al saed hawaanzii safari Shekilango.

Mengi yana fikirisha ila cha kujiuliza hawa raia wapo juu ya sheria? Kwamba hata stand za kuingia wanajiamulia tu?

Naunga mkono mia kwa mia.. Kupanda mabus popote pale, ila stand kubwa yaingie aisee.. Siyo tu kutoa ushuru.
 
Yupo Golden Deer rangi ya blue ndie mpinzani wake uliza vizuri tafuta hilo hasa ukikutana dereva Linyama utaomba ushuke...
 
Pole, kubaliana na uhalisia tu mzee
Fresh mkuu... Kwa maana sina evidence kama siti imeuzwa.. Sina evidence kama aliyenikatia tiketi alisema saa kumi na moja niwe pale..
Evidence pekee ni kuwa huwa hawaingii stand ya Magufuli.

Ila wana customer care Mbovu saaana. Yule Dada mwenye Hijab kaniharibia siku.
 
Kwenye tickets mara nyingi huwa wanaandika muda wa ww kufika yaani dk 30 kabla ya gar kuondoka
 
Back
Top Bottom