KERO Stendi kuu ya mabasi ya Moshi (Kilimanjaro) imejaa ujinga, upuuzi, uchafu na ushamba uliopitiliza

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,129
35,152
Nikiwa katika pitapita zangu za kusafiri mwishoni mwa mwaka huu wa 2023 nikajikuta mikoa ya kaskazini, nikatua Stendi kuu ya mabasi ya mikoani pale Moshi mjini na hapo nikakutana na mambo ya ajabu, yaani uchafu, ushamba na ujinga wa kiwango cha juu kupitiliza tena mamlaka za serikali zikisimamia.

Hivi inakuwaje mji wenye sifa ya usafi kuliko miji yote hapa Tanzania na pilikapilika za kitalii kuwa katika hali ile. Kwa sifa za mkoa wa Kilimanjaro na asili ya kipekee ya wenyeji wake (maendeleo na ustaarabu) nisingetegemea kuyakuta haya.

Sote tunajua, kwa mgeni mji huanzia stendi na huishia stendi, na kwa kuwa watu wengi hupenda kujifunza au kutaka kuiga ya Kilimanjaro basi nimeyaweka wazi haya ili kuwananga wahusika yamkini labda watajirekebisha.

Na hapa JF nitachambua kwa kina kila kitu cha kijinga, ushamba, upumbavu na uchafu uliopitiliza nilichokutana nacho pale stendi kuu ya mabasi Moshi mjini(Kilimanjaro).

Kwanza nikiri wazi, japokuwa hii stendi ilijengwa zamani kidogo (zaidi ya miaka 20 iliyopita) tena katikati ya mji wa Moshi lakini ubunifu wake bado unaonekana uko kisasa sana (standard bus stand design) japokuwa matumizi yake bado yako kizamani mnoo kwa Moshi. Na haya ndio kwa haraka haraka niliyoyaona;

1. Hakuna eneo rasmi la abiria kusubiria (Passenger waiting area). Yaani eneo rasmi lililojengwa kusubiria abiria limejazwa meza za ovyo za walanguzi na mawakala wa kukatia tiketi za mabasi, biashara ndogo ndogo, milingoti ya bendera za CCM nk. Yaani pamekaa kitapeli kwa 100%.

2. Hakuna ofisi rasmi hata moja ya makampuni ya mabasi ndani ya stendi. Vyumba vyote vimepangishwa biashara zingine zisizohusiana na usafirishaji. (Baada ya kudodosa sana nikaelezwa fremu karibu zote za chini ndani ya hiyo stendi ni miradi rasmi binafsi ya wakubwa ndani ya Manispaa ya Moshi na baadhi ya vigogo wa CCM mkoa, wamejimilikisha hizo fremu kifisadi na kuwapangisha watu vile wanavyojisikia na ndio kikwazo cha kuzuia kukamilika ujenzi wa stendi mpya maeneo ya Majengo)

3. Stendi imegeuzwa kuwa ni soko rasmi la wamachinga. Kila biashara ya uchuuzi, ulanguzi mdogo mdogo, mama lishe, shoe shine, kupaka rangi kucha, utapeli, udangaji nk unaikuta ndani ya stendi. Yaani ile sio stendi bali ni soko holela.

4. Hakuna sehemu rasmi za kutupia takataka ndogo ndogo za mikononi, ni kama hakuna dustbin kabisa. Takataka unaweza kutupa popote na hakuna yoyote wa kukukataza.

5. Hakuna taa zinazowaka usiku eneo la parking za mabasi, kumebakia magofu ya milingoti ya chuma na mabaki ya taa chakavu zilizokufa.

6. Miundo mbinu ya kudumu imechakaa kupitiliza. Kingo za kuta kuzunguka stendi zimebomoka na kupauka, barabara za ndani zimejaa mashimo balaa. Ni kama mahandaki ya kule Gaza.

7. Eneo lote la stendi limezungukwa na utitiri wa vibanda holela, vya ovyo ovyo ambavyo kila mtu anajiwekea atakavyo.

8. Kwa zaidi ya asilimia 80 ya eneo la stendi kumejaa magari ya Noah, Hiace na Coaster za kwenda maeneo ya karibu karibu ndani ya Kilimanjaro na machache ya Arusha badala ya mabasi ya masafa marefu ndani na nje ya nchi.

9. Stendi imepakana na kuunganika na na dampo dogo la takataka. Yaani kunanuna na taka taka kuzagaa mara kwa mara huku baadhi ya watu wakienda haja ndogo za papo kwa papo.

10. Kuna vyoo vya kulipia vinavyotoa harufu kali kuelekea nje huku utitiri wa biashara zingine (zikiwemo za vyakula) zikizunguka maeneo hayo hayo. Huhitaji kuuliza vyoo viko wapi, harufu ya vyoo inakuelekeza vilipo.

11. Hakuna alama zozote au vibao vyenye kueleza na kuelekeza maeneo mbalimbali (ukiondoa vyooni). Yaani pamekaa kienyeji mnoo, utadhani watu wote ni wenyeji wanaoishi ndani ya stendi hiyo siku zote.

12. Hakuna eneo/ofisi ya maulizo (Customer enquiry). Ukipata shida au changamoto hujui uanzia wapi, uulize wapi, ulalamike wapi au umuulize nani.

13. Mazingira ya kiusalama ni sifuri. Emergency Assemble point hakuna, hakuna ofisi rasmi za polisi (kuna trafiki wanaokaa kaa njia ya kutokea mabasi muda fulani) nk.

14. Hakuna wabeba mizigo rasmi wala toroli rasmi za kubeba mizigo ya wasafiri. Kumejaa mateja na wapiga debe wanaomvamia msafiri yoyote mwenye mizigo na kumbabaisha.

15. Nyakati za usiku mara nyingi stendi hufungwa kabisa. Hivyo mabasi kulazimika kushushia abiria nje ya stendi.

16. Kumejaa kelele za muziki kutoka kwenye maduka, vibanda, baa uchwara na vispika vya matangazo ya biashara. Yaani pako vururu vururu.

17. Sehemu kubwa ya juu ghorofani ni kama haitumiki kabisa, sijui bado inajengwa! Ama imekosa wapangaji? Pamekaa kama gofu la kale.

18. Ndani ya jengo la stendi kuna vibanda umiza kwa ajili ya kuonyesha video, mpira, kuchoma CD, kudanga na kucheza kamari (betting).

19. Kumejaa takataka zilizozagaa balaa. Haijarishi ni muda gani, iwe asubuhi, mchana au usiku, ni machupa ya maji, vifungashio vya plastiki mpaka maganda ya matunda.

20. Parking ya magari binafsi na tax haileweki, kila mara huzaa migongano na mizozo. Hakuna tofauti kati ya tax rasmi, tax bubu na gari binafsi. Eneo la parking za magari lipo lakini utaratibu hauleweki na usalama ni duni. (Japokuwa kuwa kuna eneo rasmi, safi na bora la parking/stendi ya pikipiki).

21. Miundo mbinu ya kunawa mikono imebakia magofu ndani ya stendi, haifanyi kazi na bado ipo ndani ya stendi kama kumbukumbu ya kudumu!. Yaani usafi wa kunawa mikono uliletwa Moshi na Covid na ukafa baada ya covid kufifia.

Kwa leo niishie hapo, ni mengi nimejionea lakini kwa uhakika hayo ndio nimeweza kuandika, kama huamini siku moja pita pale na kushuhudia mwenyewe.
20240102_073848.jpg

20240102_073834.jpg

20240102_071442.jpg

20240102_072942.jpg

20240102_071714.jpg
 
Attachments

  • 20240102_071442.jpg
    20240102_071442.jpg
    862.9 KB · Views: 15
  • 20240102_072756.jpg
    20240102_072756.jpg
    1 MB · Views: 15
  • 20240102_072323.jpg
    20240102_072323.jpg
    597.3 KB · Views: 16
  • 20240102_073222.jpg
    20240102_073222.jpg
    889.2 KB · Views: 16
  • 20240102_072254.jpg
    20240102_072254.jpg
    857.1 KB · Views: 16
  • 20240102_073352.jpg
    20240102_073352.jpg
    1.5 MB · Views: 15
  • 20240102_073017.jpg
    20240102_073017.jpg
    840.9 KB · Views: 14
  • 20240102_073129.jpg
    20240102_073129.jpg
    935.7 KB · Views: 17
Nikweli nipahovyo sana Pana pollution zoote noise,air,land nk nilienda kula polisi mess pale pembeni kidogo wahudumu wazitooo,wazembeee,wajingaaa,Hawavutiii chakula kibayaaa,kimechachaaa,chabaridiii nlikula mtura kidogo nitapike yaani stand hupati chakula kizuri eti!!!
Watajitetea wanajenga ngangamfumuni LAKINI mkuu wa mkoa/wilaya,mbunge na mkurugenzi hawatoshi, wajipimee wanadhalilisha sana mkoa.
 
Nikiwa katika pitapita zangu za kusafiri mwishoni mwa mwaka huu wa 2023 nikajikuta mikoa ya kaskazini, nikatua Stendi kuu ya mabasi ya mikoani pale Moshi mjini na hapo nikakutana na mambo ya ajabu, yaani uchafu, ushamba na ujinga wa kiwango cha juu kupitiliza tena mamlaka za serikali zikisimamia.

Hivi inakuwaje mji wenye sifa ya usafi kuliko miji yote hapa Tanzania na pilikapilika za kitalii kuwa katika hali ile. Kwa sifa za mkoa wa Kilimanjaro na asili ya kipekee ya wenyeji wake (maendeleo na ustaarabu) nisingetegemea kuyakuta haya.

Sote tunajua, kwa mgeni mji huanzia stendi na huishia stendi, na kwa kuwa watu wengi hupenda kujifunza au kutaka kuiga ya Kilimanjaro basi nimeyaweka wazi haya ili kuwananga wahusika yamkini labda watajirekebisha.

Na hapa JF nitachambua kwa kina kila kitu cha kijinga, ushamba, upumbavu na uchafu uliopitiliza nilichokutana nacho pale stendi kuu ya mabasi Moshi mjini(Kilimanjaro).

Kwanza nikiri wazi, japokuwa hii stendi ilijengwa zamani kidogo (zaidi ya miaka 20 iliyopita) tena katikati ya mji wa Moshi lakini ubunifu wake bado unaonekana uko kisasa sana (standard bus stand design) japokuwa matumizi yake bado yako kizamani mnoo kwa Moshi. Na haya ndio kwa haraka haraka niliyoyaona;

1. Hakuna eneo rasmi la abiria kusubiria (Passenger waiting area). Yaani eneo rasmi lililojengwa kusubiria abiria limejazwa meza za ovyo za walanguzi na mawakala wa kukatia tiketi za mabasi, biashara ndogo ndogo, milingoti ya bendera za CCM nk. Yaani pamekaa kitapeli kwa 100%.

2. Hakuna ofisi rasmi hata moja ya makampuni ya mabasi ndani ya stendi. Vyumba vyote vimepangishwa biashara zingine zisizohusiana na usafirishaji. (Baada ya kudodosa sana nikaelezwa fremu karibu zote za chini ndani ya hiyo stendi ni miradi rasmi binafsi ya wakubwa ndani ya Manispaa ya Moshi na baadhi ya vigogo wa CCM mkoa, wamejimilikisha hizo fremu kifisadi na kuwapangisha watu vile wanavyojisikia na ndio kikwazo cha kuzuia kukamilika ujenzi wa stendi mpya maeneo ya Majengo)

3. Stendi imegeuzwa kuwa ni soko rasmi la wamachinga. Kila biashara ya uchuuzi, ulanguzi mdogo mdogo, mama lishe, shoe shine, kupaka rangi kucha, utapeli, udangaji nk unaikuta ndani ya stendi. Yaani ile sio stendi bali ni soko holela.

4. Hakuna sehemu rasmi za kutupia takataka ndogo ndogo za mikononi, ni kama hakuna dustbin kabisa. Takataka unaweza kutupa popote na hakuna yoyote wa kukukataza.

5. Hakuna taa zinazowaka usiku eneo la parking za mabasi, kumebakia magofu ya milingoti ya chuma na mabaki ya taa chakavu zilizokufa.

6. Miundo mbinu ya kudumu imechakaa kupitiliza. Kingo za kuta kuzunguka stendi zimebomoka na kupauka, barabara za ndani zimejaa mashimo balaa. Ni kama mahandaki ya kule Gaza.

7. Eneo lote la stendi limezungukwa na utitiri wa vibanda holela, vya ovyo ovyo ambavyo kila mtu anajiwekea atakavyo.

8. Kwa zaidi ya asilimia 80 ya eneo la stendi kumejaa magari ya Noah, Hiace na Coaster za kwenda maeneo ya karibu karibu ndani ya Kilimanjaro na machache ya Arusha badala ya mabasi ya masafa marefu ndani na nje ya nchi.

9. Stendi imepakana na kuunganika na na dampo dogo la takataka. Yaani kunanuna na taka taka kuzagaa mara kwa mara huku baadhi ya watu wakienda haja ndogo za papo kwa papo.

10. Kuna vyoo vya kulipia vinavyotoa harufu kali kuelekea nje huku utitiri wa biashara zingine (zikiwemo za vyakula) zikizunguka maeneo hayo hayo. Huhitaji kuuliza vyoo viko wapi, harufu ya vyoo inakuelekeza vilipo.

11. Hakuna alama zozote au vibao vyenye kueleza na kuelekeza maeneo mbalimbali (ukiondoa vyooni). Yaani pamekaa kienyeji mnoo, utadhani watu wote ni wenyeji wanaoishi ndani ya stendi hiyo siku zote.

12. Hakuna eneo/ofisi ya maulizo (Customer enquiry). Ukipata shida au changamoto hujui uanzia wapi, uulize wapi, ulalamike wapi au umuulize nani.

13. Mazingira ya kiusalama ni sifuri. Emergency Assemble point hakuna, hakuna ofisi rasmi za polisi (kuna trafiki wanaokaa kaa njia ya kutokea mabasi muda fulani) nk.

14. Hakuna wabeba mizigo rasmi wala toroli rasmi za kubeba mizigo ya wasafiri. Kumejaa mateja na wapiga debe wanaomvamia msafiri yoyote mwenye mizigo na kumbabaisha.

15. Nyakati za usiku mara nyingi stendi hufungwa kabisa. Hivyo mabasi kulazimika kushushia abiria nje ya stendi.

16. Kumejaa kelele za muziki kutoka kwenye maduka, vibanda, baa uchwara na vispika vya matangazo ya biashara. Yaani pako vururu vururu.

17. Sehemu kubwa ya juu ghorofani ni kama haitumiki kabisa, sijui bado inajengwa! Ama imekosa wapangaji? Pamekaa kama gofu la kale.

18. Ndani ya jengo la stendi kuna vibanda umiza kwa ajili ya kuonyesha video, mpira, kuchoma CD, kudanga na kucheza kamari (betting).

19. Kumejaa takataka zilizozagaa balaa. Haijarishi ni muda gani, iwe asubuhi, mchana au usiku, ni machupa ya maji, vifungashio vya plastiki mpaka maganda ya matunda.

20. Parking ya magari binafsi na tax haileweki, kila mara huzaa migongano na mizozo. Hakuna tofauti kati ya tax rasmi, tax bubu na gari binafsi. Eneo la parking za magari lipo lakini utaratibu hauleweki na usalama ni duni. (Japokuwa kuwa kuna eneo rasmi, safi na bora la parking/stendi ya pikipiki).

21. Miundo mbinu ya kunawa mikono imebakia magofu ndani ya stendi, haifanyi kazi na bado ipo ndani ya stendi kama kumbukumbu ya kudumu!. Yaani usafi wa kunawa mikono uliletwa Moshi na Covid na ukafa baada ya covid kufifia.

Kwa leo niishie hapo, ni mengi nimejionea lakini kwa uhakika hayo ndio nimeweza kuandika, kama huamini siku moja pita pale na kushuhudia mwenyewe.
"milingoti ya bendera za CCM nk. Yaani pamekaa kitapeli kwa 100%."

Shida inaanzia hapo

Sent from my TECNO W2 using JamiiForums mobile app
 
Nakushangaa uaneushangaa ujinga Tanzania. Niliwahi kuandika hivi:

Acha kelele. Tafuta hela uwe unaenda na wewe na ndinga yako kuhesabiwa kama kweka na shayo wazee wa mbege.
😂 :D :p
 
Ni kweli uliyoyasema mimi naishi Moshi.

Hii mikoa ya kaskazini hasa Moshi na Arusha stendi zao zilijengwa zamani kidogo, tofauti na mikoa mingine ambayo stendi zao zimejengwa juzi juzi. Sasa changamoto ni kwamba kipindi stendi hizi zinajengwa miaka ya 80 na 90 watu inaelekea walikua wachache so ndio maana ziko katikati ya mji na kwasasa zinaonekana ndogo.

Ila tatizo kubwa la mikoa mikubwa yote nchini ni hili la wafanyabiashara wadogowadogo kujiwekea vibanda/turubai/miavuli/meza sehemu yoyote wanayoona kuna nafasi, na kuanza kufanya biashara hapo! Hii ipo maeneo mengi nchini na ni changamoto kubwa kwasababu hawa ndio wanaovuruga muonekano mzima wa mji. Lakini pia ukisema uwafukuze, wanaenda wapi? Hakuna sehemu maalum zilizotengwa kwa ajili yao na kama zipo basi unakuta ama ziko nje kabisa ya mji ambapo biashara hamna, au zimeshajaa hakuna nafasi.

Inahitajika akili na ubunifu sana kutatua changamoto kama hizi.
 
Moshi na Arusha ndio mikoa maarufu yenye stand za hovyo!!

Lakini mkuu.
umejaribu kufika stand mpya ya Ngangamfumuni?

Nini kimekwamisha?
Pale Arusha hakuna stendi kabisa, pale pa sasa hapastahili kuitwa stand, pale ni choo cha vichaa.

Nimeambiwa Moshi walijenga hii stendi kama robo karne iliyopita, stendi ambayo design yake mpaka sasa bado ni bora mnoo, tatizo ni ujinga, ushamba na upuuzi wa wasimamizi wake.

Kuhusu hiyo stendi mpya huko Majengo (sijui ndio hiyo Ngangamfumuni), bado sijafika kuona (nikifika nitakuja na mrejesho hapa), lakini kwa habari za chini chini ni kuwa ile ni white Elephant project kwa sababu.
1. Wahusika (vigogo wa manispaa na CCM mkoa) wanakikisha haukamiliki siku za karibuni (ulipaswa uwe umekamilika na kuanza kutumika tangu 2017 lakini bado ni bila bila, na mara ya mwisho miaka mitatu iliyopita tuliambiwa ulikuwa umekamilika kwa zaidi ya 89% na ungekuwa tayari kutumika 2021) ili waendelee kuvuna pesa kupitia hii ya sasa.

2. Stendi mpya inajengwa karibu mnoo na katikati ya mji (ndani ya 4km kutoka stendi ya sasa ilipo) hivyo mantiki ya kujenga ili kupanua mji inakosekana.
 
Si tulikubaliana Kanda ya ziwa Victoria na Tanganyika ndy washamba alafu kaskazini ndy wajanja!
Vp mtoa mada kaskazini wanakuaje washamba tena
Kwa hichi ninachokiona stendi ya Moshi (ilivyokaa kishamba), kanda ya Ziwa (hususani Mwanza) wamewaacha mbali mnoo watu wa Moshi. Stand ya Mwanza imekaa kijanja sana, hii ya Moshi ni ushamba wa 100%
 
Back
Top Bottom