Hongereni Mabasi ya Kilimanjaro Express

Hatimaye nimetimiza mpango. Ndani ya Tahmeed sasa, tumefika Korogwe. Safari ni ya kutoka Dar kwenda Nairobi!


Very comfortable sana hawa Jamaa!!


Sidhani kama ana mpinzani, kama yupo aseme..

Comfortable wapi mkuu acha kupiga promo, Haya mabasi yana shida moja siti zimebabanishwa mno, kiasi kwamba huwezi kunjua siti, labda mule watu wana enjoy AC basi ila siti zake sio kabisa,
Na hili ni tatizo la kampuni zote Tanzania, sit zinabananishwa mno, Panda Dar express, kilimanjaro ni the same, haya mabsi watu wana enjoye AC hakuna kingine cha maana mule, Labda kidogo Moderncoast hawa kidogo sit zao hazijabananishwa sana kama hao wengine
 
Umewajibu vizuri,mbona hawana subra katika kipindi cha.miaka 15 ndio tahmeed ya kwanza kuungua,kilimanjoro na dar express zimeungua mnoo ndani ya miaka mitatu hii
Pia kwenye tahmeed hakuna mzigo uliopotea wala alieumia lakin watu wameona ajali hiyo ndio sehemu ya kuhukumu na mkasahau hizo zinazoungua kila siku ndio zilipaswa zihukumiwe
Hawa jamaa ila Konda na Suka wao wana rugha ambazo sio kabisa, sijajua kama ni mabasi yote, ila kuna basi moja la Dar to Arusha kwa kweli konda sio kabisa plus Dereva wao
 
Sisi wa Moshi na Arusha hakuna mwingine bali KILIMANJARO EXPRESS.

Kilimanjaro ana nini cha ziada? kwa kifupi mabasi yote huduma zinafanana, Soda, maji, biskuti na kwa sasa AC, full stop, lugha za kondacta ni tatzio wana nata mno, Siti zimebananshwa mno huwezi kunjua sit, ukijaribu tu utasikia wa nyuma yako anapiga kelele.

Mabasi mengi ni tha same hakuna wenye utofauti w akutisha
 
Kwanza kabisa naomba nitoe pongezi kwa kampuni ya mabus ya kilimanjaro kwa kuona thread yangu wiki mbili zilizopita na kuamua kuifanyia kazi

Jumamosi hii ya juzi kilimanjaro express wameanza kufunga ac kwenye bus zao nne ambazo zitaanza kutumia ac siku ya jumatano kesho kutwa,i hope dar express nao watabadilika

Ila sasa nataka niwakosoe kilimajaro express,hivi ni ubahili kiasi gani mlio nao mkaamua kuongeza siti kwenye bus zenu zinazofungwa ac?yaani kwa kifupi haina tofauti na school bus tena za chekechea,mmebana siti ziwe ndogooo hakuna nafasi ya kuweka miguu,yaani ubahili huu umepitiliza,hii yote ni katika kushindana na tahmeed.

Sasa kilimanjaro mmebana siti ili waingie watu wengi,tv moja tu,hakuna wifi,siti sio za ngozi,charging system hakuna,fridge na disposer hakuna,halafu leo hii mnataka kushindana na TAHMEED

Ikumbukwe katika njia ya dar moshi arusha nairobi SUMATRA wamethibitisha ni TAHMEED pekee ndio bus la kifahari kwa kubandika sticker ya blue mlangoni kuthibitisha kuwa ni bus la daraja la juu sana

Mbaya zaidi TAHMEED imeleta mabus mapya zaidi ya 25 yapo yard kufikiria ziende route ipi ,hii imewaletea wamiliki wa mabus wa kaskazini waliozoea kufanya biashara kwa mazoea kitu kinachoitwa TAHMEED fever

Kigoma mbeya mwanza songea kahama singida jiandaeni

Mrejesho:
kilimanjaro express wamefanikiwa kufunga choo ambacho hakitumiki na ac wameghaili kuwawekea wateja wao ila wamekumbuka kuongeza siti kwenye bus zao

so sad

The best bus is Durlux
 
Mkuu unanikumbusha mbali sana, kipindi kile kuna ttbs, TBS, kamata, imam, lan'gata, Rombo safaris, Rombo mwelekeo, Rombo investment, masama cliff, njuweni, ngorika, hatco na mengine mengi.
...Fresh ya shamba
 
Yote tisa.....kumi ni kwamba kampuni ya BORN CITY iko njiani kuweka mabasi njia ya DAR/ARK.Wanaahidi huduma zilezile na hawatakuwa tayari kumuacha yoyote aliyekosa nauli kumrudisha home...kama zamani
BORN City ni habari nyingine kwa wajanja wa town wanaijua sana Enzi zile, warudi tujikumbushe
 
Aisee umenikumbusha mbali sana enzi za born city Dar - Arusha,enzi hizo tunatoka Arusha saa 12 jioni tunafika dar saa 10 Usiku ,chakula tunakula mombo yaani mombo ukipita usiku ni kama mchana vile kumechangamka balaa,aisee daraja la wami tunapita saa 7 au 8 usiku mnaanza kuamshana daa long time na mpinzani wa born city alikuwa anaitwa SMAA ,enzi hizo za nissan diesel ,enzi za isuzu,leyland,leyland daf
Umenikuna mjomba night chombo chatembea uzuri sana ati, madereva waraabu Uta wapenda, Moshi saa kumi jioni Dar esalaam saa 9.30/12.00am mko Kisutu.
 
Tahmeed hana ubavu wa kuleta luxury class kwenye route ndefu kama za mwanza,kigoma,kahama,mbeya,songea etc zitachoka kesho tu..hivi kuna watu bado wanapanda k'manjaro au dar exprec? Bora ukapanda BM coach au New force
Haa
 
Tahmeed hana ubavu wa kuleta luxury class kwenye route ndefu kama za mwanza,kigoma,kahama,mbeya,songea etc zitachoka kesho tu..hivi kuna watu bado wanapanda k'manjaro au dar exprec? Bora ukapanda BM coach au New force
Mm napanda new force songea dar masaa 15 ndani ya basi ruti ndefu hiii
 
Back
Top Bottom