Hoja ya Mkonge kuimaliza CCM Tanga - Zitto na Mnyika watikisa Korogwe

Sioni namna BEE policy ya Africa Kusini inavyoweza ku-fit kwenye mazingira yetu, BEE inafaa Afrika Kusini kwa sababu za kihistoria! Tanzania hatuna siasa za Whites and Blacks! Kwa hiyo hatuhitaji "Black Economic Empowerment, BEE"
Inawezekana part of the policy ikafaa kwa nchi kama yetu, sio lazima policy yote iwe feasible kwetu!
 
Zitto alivamia ajenda ya Wabunge wa Majimbo ya Korogwe, kwa vyovyote vile alitegemea wangempinga. Angetaka afanikishe ajenda yake, ambayo kimsingi ni nzuri, angewahusisha wenzake wenye dhamana na majimbo hayo. Tatizo lilikuwa ni njia na wala siyo malengo (kama kweli alikuwa nayo, na kama alikuwa na nia ya kizalendo ya kutaka mafanikio kwenye hili). Kama alikuwa anafanya siasa, kama inavyojidhihirisha sasa, matokeo ndiyo hayo - kukumbana na upinzani na ushindani mkali!

Mimi binafsi nimejifunza: Hoja yangu binafsi ya uchimbaji dhahabu Nzega nliyoiwasilisha kwenye zaidi ya mikutano 5 ya Bunge haijawahi kupatiwa nafasi kwa visingizio visivyo na maana kwa vile tu ni ya kipambanaji na mimi niliifanya ni yangu binafsi, sasa nimeamua kuunganisha wadau wengi zaidi ili tushirikiane kuiweka sawa na kuiwasilisha tena. Na sasa nimeamua kuwasilisha hoja binafsi bungeni kuhusiana na ajenda ya 'ajira kwa vijana' lakini nitawashirikisha wabunge wenzangu vijana kabla ya kufanya hivyo ili tufanikishe upatikanaji wa ufumbuzi wa pamoja wa tatizo hili...

Hkigwangwala, umeonyesha ni kwa kiasi gani rushwa imeharibu ubongo wa wana ccm wote, yaani una pendekeza premeeting na zito ili awalainishe ndiyo mfikirie kuiunga mkono hoja nzuri ya mkonge? hamna ufahamu binafsi kujua cha kuitendea nchi yenu? wabunge wa ccm mnaonekana hamjui wajibu wenu bungeni hadi majimboni, mnatia aibu!!!!!!!!d zito alichambua faida tarajiwa kwa zao la mkonge, kutoka mtu mmoja mmoja, vikundi hadi taifa kwa ujumla, utekelezaji wa muswada ungetupatia megawati za kutosha za umeme na wakulima kwa mara ya kwanza nchini wangekuwa wawekezaji wakuu kwenye nishati ya umeme, wasingetegemea mikopo pekee ya benki kuendeleza kilimo, kwangu mimi wewe siyo dokta. hustahili kuheshimiwa.
 
Sioni namna BEE policy ya Africa Kusini inavyoweza ku-fit kwenye mazingira yetu, BEE inafaa Afrika Kusini kwa sababu za kihistoria! Tanzania hatuna siasa za Whites and Blacks! Kwa hiyo hatuhitaji "Black Economic Empowerment, BEE"

Emmani,

Hapa key ni matabaka katika uchumi. Ni kweli matabaka ya RSA yamejikita katika ubaguzi wa rangi. Kutokuwepo (japo sina hakika kama ni kweli) kwa ubaguzi wa rangi haindoi hoja ya kuwepo kwa Matabaka. Katika matabaka yetu, vijana walio ndani ya Tabaka-linalonyonywa (deprived) ni muhimu wafanyiwe mpango wa kuwezeshwa kiuchumi (Economic Empowerment). Haipaswi kuwa "Copy-n-Paste" ya BEE bali ni case study ya kuchagiza hoja na kutengeneza sera na mpango unaoendena na mazingira, matatizo na haja ya vijana wa Tanzania.
 
Zitto alivamia ajenda ya Wabunge wa Majimbo ya Korogwe, kwa vyovyote vile alitegemea wangempinga. Angetaka afanikishe ajenda yake, ambayo kimsingi ni nzuri, angewahusisha wenzake wenye dhamana na majimbo hayo. Tatizo lilikuwa ni njia na wala siyo malengo (kama kweli alikuwa nayo, na kama alikuwa na nia ya kizalendo ya kutaka mafanikio kwenye hili). Kama alikuwa anafanya siasa, kama inavyojidhihirisha sasa, matokeo ndiyo hayo - kukumbana na upinzani na ushindani mkali!

Mimi binafsi nimejifunza: Hoja yangu binafsi ya uchimbaji dhahabu Nzega nliyoiwasilisha kwenye zaidi ya mikutano 5 ya Bunge haijawahi kupatiwa nafasi kwa visingizio visivyo na maana kwa vile tu ni ya kipambanaji na mimi niliifanya ni yangu binafsi, sasa nimeamua kuunganisha wadau wengi zaidi ili tushirikiane kuiweka sawa na kuiwasilisha tena. Na sasa nimeamua kuwasilisha hoja binafsi bungeni kuhusiana na ajenda ya 'ajira kwa vijana' lakini nitawashirikisha wabunge wenzangu vijana kabla ya kufanya hivyo ili tufanikishe upatikanaji wa ufumbuzi wa pamoja wa tatizo hili...

Hamis,

Kwenye signature yako unasema kuwa "Mabadiliko ya kweli yataletwa na sisi....!" Anyway, sijui una maana gani hapo sisi kama CCM au sisi kama Vijana?

Kwa jinsi ninavyokuona kutokana na maandishi yako na jinsi ulivyoshindwa kutetea hoja yako na kuhakikisha inaingia bungeni wakati ipo kwa manufaa ya wananchi unaowawakilisha. Nashindwa kuamini upiganaji wako unaodai nao. Hoja ya madini ni hoja ya msingi na ninaamini a lot of MPs wanauchungu nayo sasa sijui kwa nini mpaka uiunganishe na hoja ya vijana ndiyo ipite. Kama kweli unataka mabadiliko ya kweli kama unavyosema mwenyewe, kwa nini usipiganie kubadilisha utaratibu wa kuwasilisha hoja ili hoja za muhimu kama yako isizuiliwe kwa muda wa miaka 6 bila sababu za msingi.

Kwa hiyo unataka kutuambia umetumia miaka 5 kupata mbinu za kuwakilisha hoja ileile iliyokataliwa kwa miaka 6 kwa kuiunganisha na hoja ya vijana tu?? Nafikiri walioizuia nao wana akili na sidhani kama wataikubali kirahisi tu kwa vile imekuja kiaina. Lazima ilizuiliwa kwa vile ilikuwa inagusa maslahi ya watu au taasisi.......Kwa ushauri wangu, badala ya kutumia miaka 5 kupitisha hoja unatakiwa upiganie mabadiliko ya mfumo au utaratibu mzima ili hoja zikubaliwe kujadiliwa bila kufuuta maslahi binafsi bila kuangalia nani katoa hoja kwa vile ninyi wote ni waakilishi wa wananchi na siyo vyama kama ambavyo mmekuwa mkifikiria au kupigania nkiwa mjengoni.
 
Dr.kingwangala hiyo comment yako inadhihirisha ukutu wa mawazo.ata kama zitto alivamia hoja za wabunge wa ccm mkoa wa tanga yote ilikuwa n kwa nia nzur ya kuinua uchumi wa nchi na wakulima ma tanga pia.kulikuwa na ulazma gan wabumge kupinga hoja ile hasa wabunge wa tanga.dr.watanzania wa sasa sio kama unavyowafikiria huu ni usaliti kwa wananch wa tanga.wanaona hawana mtetez bungeni..NA NYIE WAKAZI WA TANGA MUACHE KUPOKEAPOKEA KANGA NA SUKAR KTK UCHAGUZI HAYA NDO MATUNDA YAKE.v
 
Inawezekana part of the policy ikafaa kwa nchi kama yetu, sio lazima policy yote iwe feasible kwetu!

Bigirita,

Ukiamua kugereza (plagiarize) jambo/kitu, ni vema basi walau ujaribu kulipa jambo/kitu unachogereza uhalisia. Kuna watu wakiamua kugereza wanafanya "On-to" na mimi sikumaanisha "On-to"

Asante sana Bigirita kuliona hilo.
 
Zitto alivamia ajenda ya Wabunge wa Majimbo ya Korogwe, kwa vyovyote vile alitegemea wangempinga. Angetaka afanikishe ajenda yake, ambayo kimsingi ni nzuri, angewahusisha wenzake wenye dhamana na majimbo hayo. Tatizo lilikuwa ni njia na wala siyo malengo (kama kweli alikuwa nayo, na kama alikuwa na nia ya kizalendo ya kutaka mafanikio kwenye hili). Kama alikuwa anafanya siasa, kama inavyojidhihirisha sasa, matokeo ndiyo hayo - kukumbana na upinzani na ushindani mkali!

Mimi binafsi nimejifunza: Hoja yangu binafsi ya uchimbaji dhahabu Nzega nliyoiwasilisha kwenye zaidi ya mikutano 5 ya Bunge haijawahi kupatiwa nafasi kwa visingizio visivyo na maana kwa vile tu ni ya kipambanaji na mimi niliifanya ni yangu binafsi, sasa nimeamua kuunganisha wadau wengi zaidi ili tushirikiane kuiweka sawa na kuiwasilisha tena. Na sasa nimeamua kuwasilisha hoja binafsi bungeni kuhusiana na ajenda ya 'ajira kwa vijana' lakini nitawashirikisha wabunge wenzangu vijana kabla ya kufanya hivyo ili tufanikishe upatikanaji wa ufumbuzi wa pamoja wa tatizo hili...

Mimi sioni shaka kabisa kwa hoja hiyo kupelekwa Bungeni na kuonekana ilivamiwa.......Tatizo Wabunge wa Tanzania hamjui nini cha kufanya bungeni sasa kwanini hamkuunga mkono hoja hiyo ili iwe na tija kwa Taifa. Tatizo lenu DR ninyi mnaamini Chadema wakianzisha hoja mnafikiri mtaonekana hamna maana kulikuwa kuna haja gani Mbunge wa Tanga kusimama na kupinga hoja ya mkonge angalia mashamba yalivyo serikali inasubiri nini?
Kwanini msitumie mawazo ya Zitto kwaajili ya kutatua matatizo hayo ya mkonge? Jaribuni kujali maslai ya Taifa. Unafakiri Watu wanaolima watamfikiriaje Mbunge yule aliyempinga zitto?
Dr kwani angeshilikisha wadau vipi kushirikisha si kuweka hoja mezani na wabunge kuchangia au mlitaka mpate kitu kidogo? Ndio mjue mmeshilikishwa kwani hoja hiyo alienda kuisoma kwenye Bunge la kenya? Mambo ya kukutana kwenye kahawa na kuwaambia watu waunge hoja mkono huo ni UTOTO na Si BUNGE.
Ebu Dr tuwekeni maslai ya Taifa Mbele tuache siasa na hoja imeletwa na nani Mbona hoja ya Muheshimiwa Mkamba ya Makazi iliungwa mkono na wote.
Nafikiri hata hoja yako ni nzuri na haitaji kumshilikisha mtu andaa na kuipeleka Bungeni kwa wabunge wenye akili bila kujali Umri watachangia na kuunga mkono hoja kwanini hoja hizo zishirikishwe nje ya vikao hayo ni majukungu na kuendeleza rushwa nchini weka hoja Mezani kila mtu afanye upembuzi yakinifu si kama ile ya zitto CCM kutaa na kuona Takataka
.
 
Zitto alivamia ajenda ya Wabunge wa Majimbo ya Korogwe, kwa vyovyote vile alitegemea wangempinga. Angetaka afanikishe ajenda yake, ambayo kimsingi ni nzuri, angewahusisha wenzake wenye dhamana na majimbo hayo. Tatizo lilikuwa ni njia na wala siyo malengo (kama kweli alikuwa nayo, na kama alikuwa na nia ya kizalendo ya kutaka mafanikio kwenye hili). Kama alikuwa anafanya siasa, kama inavyojidhihirisha sasa, matokeo ndiyo hayo - kukumbana na upinzani na ushindani mkali!

Mimi binafsi nimejifunza: Hoja yangu binafsi ya uchimbaji dhahabu Nzega nliyoiwasilisha kwenye zaidi ya mikutano 5 ya Bunge haijawahi kupatiwa nafasi kwa visingizio visivyo na maana kwa vile tu ni ya kipambanaji na mimi niliifanya ni yangu binafsi, sasa nimeamua kuunganisha wadau wengi zaidi ili tushirikiane kuiweka sawa na kuiwasilisha tena. Na sasa nimeamua kuwasilisha hoja binafsi bungeni kuhusiana na ajenda ya 'ajira kwa vijana' lakini nitawashirikisha wabunge wenzangu vijana kabla ya kufanya hivyo ili tufanikishe upatikanaji wa ufumbuzi wa pamoja wa tatizo hili...

Toa picha yako hapa..wanaume wanapiga picha kama hizo? utalipiwa?? Zito kadandia hoja..huna aibu??
 
Ndugu, DR. Kigwangala tuna tatizo kubwa zaidi ya siasa za kujikweza ama kujitafutia umaarufu wa kisiasa kama ambavyo msamiati huu umekuwa ukitumika. Tatizo letu ni kuwa sehemu ya tatizo. Hatujitambui kwamba ni binadamu tulioumbwa kukabiliana na mazingira tunayoishi (ukifikiria kwa mtazamo wa sasa utaona niko very wrong). Tulio wengi hatuamini katika maneno yetu, matendo yetu na maisha yetu. Hali hii imepelekea kutojiamini katika mambo ya msingi ya maisha yetu. Viongozi wetu hamjiamini wenyewe na mbaya zaidi hamuamini kwamba miongoni mwa watanzania wapo wenye uwezo wa jambo fulani muhimu na wanaoaminika. Kwa udhaifu huo ndio tumegeuka taifa la vilio na malalamiko kila siku. Mifano ni mingi tu, ziara za JK kuomba misaada, Spika kudhani ugumu wa maisha ya Dodoma utatatuliwa kwa posho, kushindwa kutoa maamuzi hata kwa jambo lililo wazi kabisa EPA, Meremeta, Jairo.
Ushauri wangu ni kwamba ni bora uungane na wale waliotambua kuna tatizo wakaamua kulivalia njuga bila kusubiri agenda iliasisiwa na nani, bali utekelezaji wa ajenda hiyo ndilo hitaji la msingi. Jiondoe kwenye kundi la watu wanaoishi katika fikra za ajenda zetu ni bora kuliko zao, jiunge na kundi la wenye kuishi katika utekelezaji wa ajenda zetu wote. Bila hata kumung'unya maneno kupambana na matatizo ya wananchi kupitia CCM (sehemu ya tatizo) ni sawa na kuogelea kwenye bwawa la tope lenye kina kirefu. CCM ndio msingi wa tatizo la ajira, kuanguka kwa uchumi, kuongezeka kwa uhalifu, kuongezeka kwa maradhi, ujinga, umasikini, na ufisadi uliovuka mipaka. Bila kuing'oa CCM hakuna kitu kinachoitwa maendeleo kitashuhudiwa na watanzania kwa karne nyingi zijazo.
 
Homeboy Kingwangallah,

Alichofanya Zitto ni SIASA. Kama umeshacheza mchezo wa Chess au Draft, hiyo inaitwa unampa kwanza mtu ale ili mwishoni ajipange vizuri kwenye mstari na mwisho unammaliza kiurahisi.

Ukisoma historia ya Mtemi Mirambo, mzee ambaye nimetokea kumheshimu sana, alitumia mbinu hizi kwa kujifanya anamkimbia adui na adui akajileta kwenye msitu aliokuwa kajipanga vizuri na hapo alitembeza kipigo cha Mbwa mwizi.

Alichokifanya Zitto ni kuwatega CCM kitoto sana. Alileta mada ambayo alijua LAZIMA CCM ITAPINGA. Ila hamkujua kwamba kwa kufanya hivyo, mmeshampa nafasi ya kwenda Tanga kuwashitaki kwa wananchi. Na cha ajabu si kuwa aliwashtukiza kwani kabla ya vikao, huwa kila kitakachosomwa, kinawekwa hadharani kwenu. Sijui kwa nini hata mwana CCM mmoja mwenye kuona mbali, hakuliona hilo. Anyway, kama wabunge wa CCM kwenye mkutano walimtuma Wasira na akapiga kura kuwaondoa wasigombee NEC bila kujua na mwisho anamuuliza Kinana mpango umefikia wapi wakati mwenyewe alijifunga goli bila kujua, huwezi kushangaa.

Kuhusu kesi ya kuwatetea wananchi wa Nzega kuhusu migodi, nakubaliana na wewe kuwa ulifanya makosa makubwa. Kama kweli una nia ya dhati kulifanikisha swala hilo, kwa nini usiwaone wataalamu. Mie ningelikuwa mgonjwa, ningelikuja kwako unitibu. Kwenye swala la migodi, utatakiwa kumuona mtaalamu wa sheria maana huwezi kwenda kwa kutumia mabavu. Na inapokuja swala la SHERIA na kupigania haki za binadamu/wanyamwezi, tafadhali weka taifa mbele na chama nyuma. Wala usifikiri mara mbili mbili, wee nenda muone Mpiganaji, TUNDU LISU na nina imani atakusaidia sana sana. Hata watu kama Dr. Slaa inapokuja kwenye mambo ya sheria anaweza kuwa msaada mkubwa.

UDSM au sehemu nyingine nyingi tu, kuna Wanasheria waliobobea na wanaweka taifa mbele, watakusaidia sana. Hata kaka Samuel Sitta anaweza kukusaidia kama kweli una nia ya dhati. Ila katika hao wote, bado nina imani Tundu Lisu is the best.

Angalizo: Ninavyosema Tundu Lisu au Slaa, simaanishi CHADEMA. Ninavyosema Sitta simaanishi CCM.
 
duh!ama kweli mwenye shibe kamwe hamkumbuki mwenye njaa,kurukia hoja au kutodandia hoja si suluhisho la matatizo ya Watanzania,tatizo hapa ni caucus ya chama katika kuwaweka sawa wabunge wa CCM kupinga hoja za msingi zenye kutafuta suluhu ya matatizo ya wananchi, kisa zimewasilishwa na wapinzani.Tulikwisha sema wachumia tumbo utawajua tu,kama utakavyomjua mnafiki.Sifa za mnafiki zipo tatu,akiahaidi hatekelezi,hakitekeleza, kwa kiwango duni ili naye achumie tumbo lake na akisema usahau,kwa kuwa si dhamira yake ila amesukumwa na nguvu ya njaa yake.

Heshima uliyoanza kujijengea mh.Kigwangallah sasa unataka kuiharibu kwa mikono yako,hata vitabu vitakatifu vimezungumza kuwa wajinga tu ndo haribu kazi za mikono yao.Suala si kurukia hoja,ingekuwa kurukia basi wananchi hiyo ndo ilikuwa hoja yao,walilitegemea sana zao hilo katika kuinua uchumi wa mkoa huo,ila kutokana na sera chafu za chama chako,zao hilo lilikufa na mkoa huo kupoteza rasilimali watu ambao wengi wo walikimbilia mijini kutafuta riziki.

Tuna kuheshimu mkuu Kigwangallah,jitahidi usikurupuke,najaribu kuheshimu taaluma yako,kizuri kitunze ili kidumu daima dumu.Lazima tuwe wakali utakapoteleza kwani kuteleza si kuanguka.na hoja unatetea fikra mgando wa Wabunge vilaza ndani ya CCM,tuakuasa jaribu kuwa mzalendo kwanza chama baadae.
 
bana weye -ningejua huja biadaye- kwani huji kuwa kapilau ka siku moja na kipande cha khanga nacho ni kitu?
 
Zitto alivamia ajenda ya Wabunge wa Majimbo ya Korogwe, kwa vyovyote vile alitegemea wangempinga. Angetaka afanikishe ajenda yake, ambayo kimsingi ni nzuri, angewahusisha wenzake wenye dhamana na majimbo hayo. Tatizo lilikuwa ni njia na wala siyo malengo (kama kweli alikuwa nayo, na kama alikuwa na nia ya kizalendo ya kutaka mafanikio kwenye hili). Kama alikuwa anafanya siasa, kama inavyojidhihirisha sasa, matokeo ndiyo hayo - kukumbana na upinzani na ushindani mkali!

Mimi binafsi nimejifunza: Hoja yangu binafsi ya uchimbaji dhahabu Nzega nliyoiwasilisha kwenye zaidi ya mikutano 5 ya Bunge haijawahi kupatiwa nafasi kwa visingizio visivyo na maana kwa vile tu ni ya kipambanaji na mimi niliifanya ni yangu binafsi, sasa nimeamua kuunganisha wadau wengi zaidi ili tushirikiane kuiweka sawa na kuiwasilisha tena. Na sasa nimeamua kuwasilisha hoja binafsi bungeni kuhusiana na ajenda ya 'ajira kwa vijana' lakini nitawashirikisha wabunge wenzangu vijana kabla ya kufanya hivyo ili tufanikishe upatikanaji wa ufumbuzi wa pamoja wa tatizo hili...

Hapa CDM hawajadandia ajenda yeyote ya wabunge wa sisiem. Nyinyi mngewaunga mkono CDM kama wangepiga usingizi kama ilivyo formula ya CCM bungeni. Ninawapa hongera CDM kwa mapambano.

Juzi nilikuwa ninaongea na vijana wa boda boda pale Moshi walikuwa wanasikitika sana walivyofanyiwa ukatili, unyama wa kuuwa viwanda hapo moshi. Kijana mmoja akasema kama wasingekuwa na hizi boda boda sijui wangekuwa katika hali gani. Mmoja akasema wameua hivi viwanda ili wauze boda boda. Yaani wananchi wanamaswali mengi sana ambayo CCM inatakiwa kuyajibu kiundani na itoe faida waliyopata baada ya kuuwa vile viwanda vyetu. Tushirikiane pande zote kitaeleweka tu. Ingekuwa ni raha kuorodhesha viwanda vyote vilivyokufa na wakati na aliyekuwa mkurugenzi na bodi iliyokuwepo ili hata vizazi vyao vijue na wasipewe madaraka tena.
 
NADHANI DOKTA KACHEMSHA, Je ni tanga tu kwenye Mkonge? Ukisema wabunge wenye majimbo waongee ama washirikishwe ni kichekesho. Mtu mwenye upeo wa juu ataainisha mambo na kuyafanyia kazi sio kupelekewa. Hao wabunge wamekaa miaka mingapi kutoa huyo Mngoni wa Korogwe! Hao wabunge kuanzia Same Mpaka Challinze walishindwa nini kuongea.
Mheshimiwa tuaangalie mbele wale watakaonufaika moja kwa moja na taifa kwa ujumla. Acheni kusema jimbo langu jimbo langu" je mnamiliki watu pia?
 
Zitto alivamia ajenda ya Wabunge wa Majimbo ya Korogwe, kwa vyovyote vile alitegemea wangempinga. Angetaka afanikishe ajenda yake, ambayo kimsingi ni nzuri, (1)angewahusisha wenzake wenye dhamana na majimbo hayo. Tatizo lilikuwa ni njia na wala siyo malengo (2)(kama kweli alikuwa nayo, na kama alikuwa na nia ya kizalendo ya kutaka mafanikio kwenye hili). Kama alikuwa anafanya siasa, kama inavyojidhihirisha sasa, matokeo ndiyo hayo - kukumbana na upinzani na ushindani mkali!

Mimi binafsi nimejifunza: Hoja yangu binafsi ya uchimbaji dhahabu Nzega nliyoiwasilisha kwenye zaidi ya mikutano 5 ya (3)Bunge haijawahi kupatiwa nafasi kwa visingizio visivyo na maana kwa vile tu ni ya kipambanaji na mimi niliifanya ni yangu binafsi, sasa nimeamua kuunganisha wadau wengi zaidi ili tushirikiane kuiweka sawa na kuiwasilisha tena. Na sasa nimeamua kuwasilisha hoja binafsi bungeni kuhusiana na ajenda ya 'ajira kwa vijana' lakini nitawashirikisha wabunge wenzangu vijana kabla ya kufanya hivyo ili tufanikishe upatikanaji wa ufumbuzi wa pamoja wa tatizo hili...

Majibu

(1) Usimwamshe aliyelala, ukimwamsha utalala wewe.
(2) Mwneye macho haambiwi tazama. Haja ya mja hunena, muungwana ni vitendo.
(3) Huwezi kutata tawi ulilolikalia.

Dr=Divai mpya kwenye buyu la zamani.
 
Zitto alivamia ajenda ya Wabunge wa Majimbo ya Korogwe, kwa vyovyote vile alitegemea wangempinga. Angetaka afanikishe ajenda yake, ambayo kimsingi ni nzuri, angewahusisha wenzake wenye dhamana na majimbo hayo. Tatizo lilikuwa ni njia na wala siyo malengo (kama kweli alikuwa nayo, na kama alikuwa na nia ya kizalendo ya kutaka mafanikio kwenye hili). Kama alikuwa anafanya siasa, kama inavyojidhihirisha sasa, matokeo ndiyo hayo - kukumbana na upinzani na ushindani mkali!

Mimi binafsi nimejifunza: Hoja yangu binafsi ya uchimbaji dhahabu Nzega nliyoiwasilisha kwenye zaidi ya mikutano 5 ya Bunge haijawahi kupatiwa nafasi kwa visingizio visivyo na maana kwa vile tu ni ya kipambanaji na mimi niliifanya ni yangu binafsi, sasa nimeamua kuunganisha wadau wengi zaidi ili tushirikiane kuiweka sawa na kuiwasilisha tena. Na sasa nimeamua kuwasilisha hoja binafsi bungeni kuhusiana na ajenda ya 'ajira kwa vijana' lakini nitawashirikisha wabunge wenzangu vijana kabla ya kufanya hivyo ili tufanikishe upatikanaji wa ufumbuzi wa pamoja wa tatizo hili...

Lugha uliyotumia hapo Mh. sio ya kiustaarabu kwa mtu kama wewe.... Suala la msingi hapo ni umuhimu wa hoja na sio kuwashirikisha wabunge wa maeneo hayo. Kama wao wanaona kuna umuhimu wa ku-support hoja wangetakiwa kufanya hivyo hata bila kushirikishwa individually. Mimi ninavyoelewa HOJA ikipelekwa bungeni manake wabunge mnakua mmeshirikishwa na hivyo kutoka hapo ni utashi wa mtu mmoja mmoja kushiriki au kutoshiriki. Tatizo la wabunge wa CCM ni kushikiwa ubongo na chama, maamuzi ya chama yanakua ndo maamuzi yako hata kama hayana maslahi kwa taifa. Mnajali sana maslahi ya chama kuliko maslahi ya wananchi wengi waliowachagua. Nakuhakikishia hiyo HOJA ya Mh. Zitto Kabwe itasimama hata bila ushiriki wa hao wabunge wa Tanga.
 
Zitto alivamia ajenda ya Wabunge wa Majimbo ya Korogwe, kwa vyovyote vile alitegemea wangempinga. Angetaka afanikishe ajenda yake, ambayo kimsingi ni nzuri, angewahusisha wenzake wenye dhamana na majimbo hayo. Tatizo lilikuwa ni njia na wala siyo malengo (kama kweli alikuwa nayo, na kama alikuwa na nia ya kizalendo ya kutaka mafanikio kwenye hili). Kama alikuwa anafanya siasa, kama inavyojidhihirisha sasa, matokeo ndiyo hayo - kukumbana na upinzani na ushindani mkali!

Mimi binafsi nimejifunza: Hoja yangu binafsi ya uchimbaji dhahabu Nzega nliyoiwasilisha kwenye zaidi ya mikutano 5 ya Bunge haijawahi kupatiwa nafasi kwa visingizio visivyo na maana kwa vile tu ni ya kipambanaji na mimi niliifanya ni yangu binafsi, sasa nimeamua kuunganisha wadau wengi zaidi ili tushirikiane kuiweka sawa na kuiwasilisha tena. Na sasa nimeamua kuwasilisha hoja binafsi bungeni kuhusiana na ajenda ya 'ajira kwa vijana' lakini nitawashirikisha wabunge wenzangu vijana kabla ya kufanya hivyo ili tufanikishe upatikanaji wa ufumbuzi wa pamoja wa tatizo hili...
kwa mtindo huu watanzania bila kuiondoa CCM madarakani tusitegemee maendeleo yoyote kupatikana, yaani hoja ya msingi ya zitto inakwamishwa kwa kigezo hakuwashirikisha wabunge wa majimbo ya mwambao. Watanzania kokote mliko nisikilizeni mimi bila CCM kuondoka madarakani tusahau maendeleo. hali hii inasikitisha sana.

Uamuzi wa Zitto wa kulipeleka shauri hili kwa walengwa ni sahihi kabisa, wao (wabunge wa CCM) waache walikalie shauri hili lakini cha msingi CDM lazima itawafikia wananchi na kuwafumbua macho - mwitikio wa wana korogwe ni mzuri na kuna siku hawa watu watairudisha tu nchi hii kwa wananchi kupitia CDM. Mungu yuko nasi.
 
Zitto alivamia ajenda ya Wabunge wa Majimbo ya Korogwe, kwa vyovyote vile alitegemea wangempinga. Angetaka afanikishe ajenda yake, ambayo kimsingi ni nzuri, angewahusisha wenzake wenye dhamana na majimbo hayo. Tatizo lilikuwa ni njia na wala siyo malengo (kama kweli alikuwa nayo, na kama alikuwa na nia ya kizalendo ya kutaka mafanikio kwenye hili). Kama alikuwa anafanya siasa, kama inavyojidhihirisha sasa, matokeo ndiyo hayo - kukumbana na upinzani na ushindani mkali!

Mimi binafsi nimejifunza: Hoja yangu binafsi ya uchimbaji dhahabu Nzega nliyoiwasilisha kwenye zaidi ya mikutano 5 ya Bunge haijawahi kupatiwa nafasi kwa visingizio visivyo na maana kwa vile tu ni ya kipambanaji na mimi niliifanya ni yangu binafsi, sasa nimeamua kuunganisha wadau wengi zaidi ili tushirikiane kuiweka sawa na kuiwasilisha tena. Na sasa nimeamua kuwasilisha hoja binafsi bungeni kuhusiana na ajenda ya 'ajira kwa vijana' lakini nitawashirikisha wabunge wenzangu vijana kabla ya kufanya hivyo ili tufanikishe upatikanaji wa ufumbuzi wa pamoja wa tatizo hili...

Kwa hiyo mkuu unataka kutuambia kuwa nyinyi mko tayari kubisha lolote hata kama lina maslahi kwa wapiga kura wenu kwa sababu tu limeletwa na upinzani? Sasa kama ni hivyo unamuwakilisha nani hapo bungeni?
 
Mie sioni kam watu wa Tanga wanajijali kwani hawangeichagua CCm wakati wanajua ndiyo iliyowafikisha hapo na bila kuwahurumia. Kila kitu Tanga ni hovyo hovyo yuUvuvi zii, Mkonge ZII, Reli Ziii, Bandari ziii etc etct ziiiiiiiii lakini bado wako na majambazi wao tu leave them!!!!
 
Back
Top Bottom