Gharama zitazoongezeka endapo hoja ya CHADEMA kuongeza idadi ya wabunge itapita

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,224
22,305
Baada ya nchi nzima kushtushwa na hoja namba 5 kutoka kwenye hoja za CHADEMA kuhusu muswada wa sheria ya uchaguzi leo nimeona tukumbushane gharama tutazozilipa wananchi kwa ongezeko la wabunge wapya takribani 135. Kimsingi hoja namba 5 ni hoja yenye nia ovu.

Kwa sasa bunge zima la Tanzania lina wabunge wa kuchaguliwa na kuteuliwa 393 bunge zima. Wale wa kuchaguliwa ni 264. Kwa mujibu wa hoja namba 5 ni kuwa kila jimbo liwe na mbunge mwanamke na mwanaume, yaani wawili. Hii ina maana wabunge wa kuchaguliwa watakuwa 528. Hadi hapo kunakuwa na ongezeko la wabunge 135 kwa idadi ya 393 ya sasa. Kwa mshahara wa Tsh 16.5m kwa mwezi kutahitajika Bilioni 134 kuwalipa wabunge wapya 135 kwa miaka mitano. Kwa mafao ya Tsh 250m basi zitahitajika bilioni 34 kuwalipa. Ongezeko hili litaambatana na kuongezeka kwa ruzuku kwa vyama vya siasa kwasababu hupata ruzuku kulingana na idadi ya wabunge. Kimsingi tutapigika sana kutafuta pesa za kuhudumia wanasiasa badala ya maendeleo.

Mimi namtupia lawama Mbowe kwa kuingiza ujasiriamali kwenye siasa bila kujali kuwa ni hatari kwa wananchi. Endapo hoja yake itapita basi kutakuwa na ongezeko kubwa la ruzuku kwenye chama anachomiliki kupitia wabunge watakaochaguliwa. Hoja namba 5 haikuwa ya bahati mbaya. Mr DJ alishapiga hesabu za mbali sana.
 
wabunge wa viti maalm wanakuwa hawapo. Idadi ya viti maalum kwa sasa ni wangapi? tuanzie hapo
 
Wingi wa mikoa na wilaya hili hulioni,ukubwa wa cabinet yako sio tatizo kwako, ukubwa wa serikali yako sio tatizo, elewa kwenye SADC, Tanzania ndio nchi pekee yenye mikoa zaidi ya 20!
 
Wabunge wawili jimbo moja sio? Hiyo hoja imekaa kimtego na kuishiwa mbinu vipi majimbo yote yakichukuliwa na CCM?
 
umesoma maelezo lakini? mbona unauliza kitu kilichoandikwa tayari.
Kutakuwa na re organisation of majimbo according to wingi wa wapiga kura, siyo kama sasa. majimbo yatapungua........ nitardi kwako in the afternoon for more clarification.
 
Hoja za Chadema nyingi ni za kipumbavu kabisa, ikiwa ni hivyo basi nashauri ubunge iwe ni shughuli ya hiyari isiyo na malipo yoyote bali utu wa mgombeaji yenye nia ya kupigania maendeleo ya dhati kabisa na moyoni ya jimbo lake, yenye posho ya shilingi milioni moja tu kwa mwezi.
-UBUNGE IWE NI KAZI YA KIZALENDO!
-SI LAZIMA BUNGE LETU LIFANANE NA MABUNGE MENGINE DUNIANI KATIKA KUSHINDANA KULIPA MALIPO MAKUBWA, TUTENGENEZE BUNGE LETU LA KIAINA YAKE.
 
Umeona hoja hiyo,tu,, hoja muhimu zote hujaziona?. Kwani sukari huko Bei gani?
 
Baada ya nchi nzima kushtushwa na hoja namba 5 kutoka kwenye hoja za CHADEMA kuhusu muswada wa sheria ya uchaguzi leo nimeona tukumbushane gharama tutazozilipa wananchi kwa ongezeko la wabunge wapya takribani 135. Kimsingi hoja namba 5 ni hoja yenye nia ovu.

Kwa sasa bunge zima la Tanzania lina wabunge wa kuchaguliwa na kuteuliwa 393 bunge zima. Wale wa kuchaguliwa ni 264. Kwa mujibu wa hoja namba 5 ni kuwa kila jimbo liwe na mbunge mwanamke na mwanaume, yaani wawili. Hii ina maana wabunge wa kuchaguliwa watakuwa 528. Hadi hapo kunakuwa na ongezeko la wabunge 135 kwa idadi ya 393 ya sasa. Kwa mshahara wa Tsh 16.5m kwa mwezi kutahitajika Bilioni 134 kuwalipa wabunge wapya 135 kwa miaka mitano. Kwa mafao ya Tsh 250m basi zitahitajika bilioni 34 kuwalipa. Ongezeko hili litaambatana na kuongezeka kwa ruzuku kwa vyama vya siasa kwasababu hupata ruzuku kulingana na idadi ya wabunge. Kimsingi tutapigika sana kutafuta pesa za kuhudumia wanasiasa badala ya maendeleo.

Mimi namtupia lawama Mbowe kwa kuingiza ujasiriamali kwenye siasa bila kujali kuwa ni hatari kwa wananchi. Endapo hoja yake itapita basi kutakuwa na ongezeko kubwa la ruzuku kwenye chama anachomiliki kupitia wabunge watakaochaguliwa. Hoja namba 5 haikuwa ya bahati mbaya. Mr DJ alishapiga hesabu za mbali sana.
Jimama la hovyo na haribifu kwa nchi. Kufa.
 
Back
Top Bottom