Nikupateje
JF-Expert Member
- Dec 22, 2009
- 1,334
- 988
Zitto alivamia ajenda ya Wabunge wa Majimbo ya Korogwe, kwa vyovyote vile alitegemea wangempinga. Angetaka afanikishe ajenda yake, ambayo kimsingi ni nzuri, angewahusisha wenzake wenye dhamana na majimbo hayo. Tatizo lilikuwa ni njia na wala siyo malengo (kama kweli alikuwa nayo, na kama alikuwa na nia ya kizalendo ya kutaka mafanikio kwenye hili). Kama alikuwa anafanya siasa, kama inavyojidhihirisha sasa, matokeo ndiyo hayo - kukumbana na upinzani na ushindani mkali!
Mimi binafsi nimejifunza: Hoja yangu binafsi ya uchimbaji dhahabu Nzega nliyoiwasilisha kwenye zaidi ya mikutano 5 ya Bunge haijawahi kupatiwa nafasi kwa visingizio visivyo na maana kwa vile tu ni ya kipambanaji na mimi niliifanya ni yangu binafsi, sasa nimeamua kuunganisha wadau wengi zaidi ili tushirikiane kuiweka sawa na kuiwasilisha tena. Na sasa nimeamua kuwasilisha hoja binafsi bungeni kuhusiana na ajenda ya 'ajira kwa vijana' lakini nitawashirikisha wabunge wenzangu vijana kabla ya kufanya hivyo ili tufanikishe upatikanaji wa ufumbuzi wa pamoja wa tatizo hili...
Mh. Kigwangalla,
Katika matamshi uliyowahi kunishangaza ni hili la leo. Kumbe tatizo kwako si ukweli wa hoja bali ni njia aliyotuia Zitto.
Kwa namna moja umewatukana Wabunge wa Korogowe na wana CCM wote kwamba wanachojali ni njia wanayoitaka wao hata kama jambo lenyewe ni la ukweli na manufaa.
Principle ya ukweli ni kwamba ukweli hauhitaji njia ya kuufikisha. Ukweli hauna wakati muafaka. Wakati wote ni wakati wa kuutoa ukweli.
Mwenye tatizo ni anayeambiwa ukweli na si ukweli wenyewe. Hivyo, hapa mwenye tatizo ni wewe na wote mlioukataa ukweli wa Zitto.
Kama Zitto akisema DSalaam itakumbwa na Tsunami basi Kigwangala unatuambia kuwa Zitto achague njia ya kutuambia ili wabunge wa CCM Dar wasimpinge.
Kingwangwala ninaamini wewe ni Doctor.
Kama Zitto akisema jimboni kwako kipindupindu kinawashambulia wapiga kura wako basi unatuambia kuwa afanye caucas na wewe na wana-Tabora ili mkubaliane na ukweli huo na ndipo muuunge mkono.
Ndugu yangu,
Hakuna siku uliyojiaibisha kama leo, ningekuwa wewe ningefuta kauli hii kwa njia yoyote.