Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 573
- 2,553
Maandamano ya Jumatano, Januari 2024, yataanza Saa 3:00 asubuhi. Yatahusisha njia mbili kuanzia Mbezi Mwisho (Stand) na Buguruni, na yataishia Ofisi za UN, barabara ya Sam Nujoma, Dar es Salaam.
Nakala za barua za taarifa ya Maandamano haya zimepelekwa kwa makamanda wote wa Polisi Wilaya, pamoja na Mkuu wa kanda ya Polisi Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika, kumalizia maandamano ofisi za UN ni kwa sababu UN inao wajibu na nafasi ya kuchukua hatua kwa kadri itakavyoona inafaa.
Kuhusu suala la mjadala, Mnyika amesema tayari walifanya mdahalo na CCM kwa mwaka mzima na haoni mantiki ya kuendelea kupoteza muda zaidi hivyo wakutane barabarani.
Mnyika amefafanua pia majibu ya maswali ya CHADEMA yanapaswa kutolewa na viongozi wakubwa kama, amewaasa wananchi kutokukubali kuhamishwa kwenye hoja.
Pia, ameelezea kuwa CHADEMA ni chama kinachoamini katika kubana matumizi na kuwa na Serikali ndogo, hoja aliyoitoa kuhusu idadi ya wabunge wawili (Me na Ke) kila jimbo imetoka kwenye Rasimu ya Warioba ambayo ukiisoma utagundua kuwa idadi ya wabunge itapungua kwa kuwa watatokea kwenye Halmashauri za Wilaya (wabunge 278 tu) badala ya Sera ya sasa ya Majimbo ambapo kuna wabunge zaidi ya 370.
===
Pia soma: CHADEMA yatangaza Maandamano Kupinga Miswada ya Sheria za Uchaguzi iliyowasilishwa Bungeni